Jumanne, 18 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu III Sehemu ya Pili


Neno la Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu III Sehemu ya Pili

Tumetoka tu kuongea kuhusu jinsi Shetani hutumia maarifa kumpotosha mwanadamu, basi kinachofuata wacha tushiriki kuhusu jinsi Shetani hutumia sayansi kumpotosha mwanadamu. Kwanza, Shetani hutumia jina la sayansi kuridhisha kutaka kujua kwa mwanadamu, kuridhisha hamu ya mwanadamu[a] kutafiti sayansi na kuchunguza siri. Pia, katika jina la sayansi, Shetani huridhisha haja ya mwili na mahitaji ya mwanadamu kuendelea kuinua ubora wao wa maisha. Shetani hivyo, katika jina hili, hutumia njia ya sayansi kumpotosha mwanadamu. Je, ni kufikiria tu kwa mwanadamu ama akili za mwanadamu ambazo Shetani anapotosha kwa kutumia njia hii ya sayansi? Miongoni mwa watu, matukio na mambo katika mazingira yetu ambayo tunaweza kuona na ambayo tunakutana nayo, ni yapi mengine ambayo Shetani anatumia sayansi kupotosha? (Mazingira ya kiasili.) Mko sahihi. Inaonekana kwamba mmedhuriwa sana na hili, na pia mmeathirika sana na yeye. Mbali na kutumia matokeo yote ya utafiti na mahitimisho mbalimbali ya sayansi kumdanganya mwanadamu, Shetani pia hutumia sayansi kama mbinu ya kutekeleza uangamizi na unyonyaji tele wa mazingira ya kuishi aliyopewa mwanadamu na Mungu. Anafanya hivi chini ya kisingizio kwamba iwapo mwanadamu anatekeleza utafiti wa kisayansi, mazingira ya kuishi ya mwanadamu yatakuwa bora na bora zaidi na viwango vya kuishi vya mwanadamu daima vitaboreka, na zaidi ya hayo kwamba maendeleo ya kisayansi yanafanywa ili kuhudumia mahitaji ya mwili ya mwanadamu yanayozidi kila siku na haja yao ya kuendelea kupandisha ubora wao wa maisha. Kama sio kwa sababu hizi, basi mbona sayansi iendelezwe?. Huu ni msingi wa kidhahania wa maendeleo ya Shetani ya sayansi. Hata hivyo, sayansi imemletea binadamu nini? Mazingira yetu ya karibu kabisa yana nini? Si hewa ambayo binadamu hupumua imechafuliwa? Maji tunayoyanywa kweli bado ni safi? (La.) Basi, je, chakula tunachokula, kingi chake ni cha kiasili? (La.) Basi ni nini tena? Kinakuzwa kwa kutumia mbolea na kupaliliwa kwa kutumia vinasaba, na pia kuna mabadiliko yanayozalishwa kwa kutumia mbinu mbalimbali za sayansi, ili kwamba hata mboga na matunda tunayoyala sio ya kiasili tena. Si rahisi sasa kwa watu kupata yai la asili kula. Na mayai hayaonji yalivyokuwa yakionja awali, baada ya kusindikwa na inayoitwa sayansi na Shetani. Kwa kuangalia taswira kubwa, anga nzima imeharibika na kuchafuliwa; milima, maziwa, misitu, mito, bahari, na kila kitu juu na chini ya ardhi vyote vimeharibiwa na inayoitwa mafanikio ya kisayansi. Kwa maneno mengine, ikolojia nzima, mazingira yote ya kuishi yaliyopewa mwanadamu na Mungu yameangamizwa na kuharibiwa na inayodaiwa kuwa sayansi. Ingawa kuna watu wengi waliopata walichotarajia katika suala la ubora wa maisha wanaotafuta, kuridhisha tamaa na miili yao, mazingira ambayo mwanadamu anaishi kimsingi yameharibiwa na kuangamizwa na "mafanikio" mbalimbali yaliyoletwa na sayansi. Hata nje ama katika nyumba zetu hatuna tena haki ya kupumua pumzi moja ya hewa safi. Hii ni huzuni ya mwanadamu? Bado kuna furaha yoyote ya kuzungumzia kwa mwanadamu kuishi katika nafasi hii ya kuishi? Mwanadamu anaishi katika nafasi hii ya kuishi na, kutoka mwanzoni, haya mazingira ya kuishi yaliumbwa na Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Maji ambayo watu hunywa, hewa ambayo watu hupumua, chakula ambacho watu hula, mimea, miti, na bahari—haya mazingira ya kuishi yote yalipewa mwanadamu na Mungu; ni asili, na hutekeleza kulingana na amri asili iliyotolewa na Mungu. Kama hakungekuwa na sayansi, watu wangekuwa na furaha na wangefurahia kila kitu kikiwa cha asili kabisa kulingana na njia ya Mungu na kulingana na kile Mungu amewapa wafurahie. Sasa, hata hivyo, haya yote yameangamizwa na kuharibiwa na Shetani; nafasi ya kimsingi ya kuishi ya mwanadamu haipo tena katika hali yake asili zaidi. Lakini hakuna anayeweza kutambua kilichosababisha matokeo ya aina hii ama jinsi haya yalikuja kuwa, na zaidi ya hapo hata watu zaidi wanaelewa na kukaribia sayansi kwa kutumia mawazo waliyoingiziwa na Shetani Je, hii si ya kuchukiza sana na ya kusikitisha? Kwa kuwa Shetani sasa amechukua nafasi ambamo wanadamu wapo na mazingira yao ya kuishi na kuwapotosha kuwa katika hali hii, na kwa kuwa wanadamu wanaendelea kwa njia hii, kuna haja yoyote ya mkono wa Mungu kuwaangamiza wanadamu hawa duniani? Kuna haja ya mkono wa Mungu kuwaangamiza wanadamu? (La.) Iwapo wanadamu watazidi kuendelea kwa njia hii, watachukua mwelekeo upi? (Uharibifu.) Wanadamu wataharibiwa vipi? Zaidi ya mwanadamu kutafuta kwa tamaa umaarufu na faida, daima anaendelea kutekeleza uchunguzi wa sayansi na utafiti wa kina, kisha bila kikomo huridhisha mahitaji yake ya mwili na tamaa; yapi tena ni matokeo ya mwanadamu? Kwanza kabisa hakuna tena usawa wa ikolojia na, pamoja na hili, miili ya wanadamu yote imetiwa doa na kuharibiwa na mazingira ya hali hii, na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza na mapigo kusambaa kila mahali. Hii ni hali ambayo mwanadamu sasa hawezi kudhibiti, sivyo? (Ndiyo.) Sasa kwa sababu mnaelewa hili, iwapo wanadamu hawamfuati Mungu, lakini daima wanamfuata Shetani kwa njia hii—kutumia maarifa daima kujitajirisha, kutumia sayansi kuchunguza bila kikomo siku za baadaye za maisha ya binadamu, kutumia mbinu ya aina hii kuendelea kuishi—mnaweza kutambua hitimisho ya asili ya wanadamu itakuwa vipi? Matokeo ya mwisho asilia yatakuwa yapi? (Uharibifu.) Itakuwa uharibifu: kukaribia uharibifu hatua moja kwa wakati. Kukaribia uharibifu kwa hatua moja kwa wakati! Inaonekana sasa kama sayansi ni aina ya ushombwe ambao Shetani amemwandalia mwanadamu, ili wakati mnapojaribu kupambanua mambo mnafanya hivyo katika hali ya ukungu; haijalishi mnaangalia kwa ugumu aje, hamwezi kuona mambo kwa wazi, na haijalishi mnajaribu sana vipi, hamwezi kuyatambua. Shetani, hata hivyo, bado anatumia jina la sayansi kuzidisha hamu yako na kukuongoza kwa pua, mguu mmoja mbele ya mwingine, kuelekea shimo na kuelekea kifo. Sivyo? (Ndiyo.) Hii ndiyo njia ya pili.
Njia ya tatu ni ipi? Ni jinsi Shetani hutumia desturi ya kitamaduni kumpotosha mwanadamu. Kuna usawa mwingi kati ya desturi ya kitamaduni na ushirikina, ni tu kuwa desturi ya kitamaduni ina hadithi fulani, vidokezo, na vyanzo fulani. Shetani ametunga na kuunda ngano ama hadithi nyingi katika vitabu vya historia, na kuacha watu na hisia za kina za desturi ya kitamaduni ama watu wa kishirikina. Chukua kwa mfano Watu Wanane Wasiokufa Wanaovuka Bahari, Safari ya kwenda Magharibi, Mfalme Mkuu Jade, Nezha Anamshinda Joka Mfalme, na Uchunguzi wa Miungu, zote za Uchina. Haya hayajakita mizizi katika akili za mwanadamu? Hata iwapo baadhi yenu hawajui maelezo yote, bado mnajua hadithi za jumla, na yaliyomo kwa jumla ndiyo yanayokwama katika moyo wako na yanakwama katika akili yako, na huwezi kuyasahau. Haya ni mambo ambayo Shetani alimwekea mwanadamu kitambo sana, baada ya kusambaza katika nyakati tofauti mawazo yake au hekaya. Haya mambo yanadhuru moja kwa moja na kumomonyoa nafsi za watu na kuweka watu chini ya fingo moja baada ya jingine. Hiyo ni kusema kwamba baada ya wewe kukubali mambo haya yanayotoka kwa desturi ya kitamaduni, hadithi ama ushirikina, baada ya mambo haya kuwekwa kwa akili yako, baada ya hayo kukwama katika moyo wako, ni kama tu apizo—unakamatwa na kushawishika na hizi tamaduni, haya mawazo na hadithi za kitamaduni. Yanashawishi maisha yako, mtazamo wako wa maisha na pia yanashawishi maoni yako ya mambo. Hata zaidi yanashawishi ufuataji wako wa njia sahihi ya maisha: Hii bila shaka ni apizo. Unajaribu lakini huwezi kuyatupilia mbali; unayakatakata lakini huwezi kuyakata chini; unayapiga lakini huwezi kuyapiga chini. Sivyo? (Ndiyo.) Zaidi ya hayo, baada ya mwanadamu bila kujua kuwekwa chini ya aina hii ya apizo, bila kujua, anaanza kumwabudu Shetani, kukuza taswira ya Shetani katika moyo wake. Kwa maneno mengine, anamweka Shetani kama sanamu, kifaa cha yeye kuabudu na kutazamia, hata kwenda mbali kiasi cha kumchukulia kama Mungu. Bila kujua, mambo haya yako katika mioyo ya watu yakidhibiti maneno na matendo yao. Aidha, kwanza unachukulia hadithi na hekaya hizi kuwa uongo, na kisha bila kujua unakubali kuwepo kwa hadithi hizi, kuzitengenezea sanamu halisi na kuzibadili kuwa mambo halisi yaliyopo. Katika kutojua, unapokea haya mawazo bila kufahamu na kuwepo kwa vitu hivi. Pia unapokea bila kufahamu mashetani, Shetani na sanamu ndani ya nyumba yako na ndani ya moyo wako—hii bila shaka ni apizo. Je, mnahisi sawa? (Ndiyo.) Kuna yeyote miongoni mwenu ambao wamechoma ubani na kuabudu Budha? (Ndiyo.) Kwa hivyo madhumuni ya kuchoma ubani na kumwabudu Budha yalikuwa yapi? (Kuombea amani.) Kwa kuifikiria sasa, ni ujinga kuombea amani kutoka kwa Shetani? Shetani analeta amani? (La.) Je, mlikuwa wajinga hapo nyuma? (Ndiyo.) Namna ya aina hiyo ni ya upuuzi, jinga na nyofu, siyo? Shetani anafikiria tu jinsi ya kukupotosha na hawezi kukupa amani; anaweza tu kukupa nafasi ya kupumua ya muda mfupi. Lakini lazima uchukue kiapo na ukivunja ahadi yako ama ukivunja kiapo ulichofanya, basi utaona jinsi anavyokuadhibu. Kwa kukufanya uchukue kiapo, kwa kweli anataka kukudhibiti. Wakati mlipoombea amani, mlipata amani? (La.) Hamkupata amani, lakini kinyume na hayo alileta bahati mbaya, majanga yasiyoisha kweli bahari isiyo na mipaka ya uchungu. Amani haiko miongoni mwa miliki ya Shetani, na hili ni ukweli. Haya ndiyo matokeo kwa wanadamu ya ushirikina wa kikabila na desturi ya kitamaduni.
Suala la mwisho ni jinsi Shetani kutumia kwa manufaa yake mienendo ya kijamii kumpotosha mwanadamu. Hii mienendo ya kijamii ina mambo mengi. Watu wengine husema: "Je, ni kuhusu nguo tunazovaa? Je, ni kuhusu mtindo wa karibuni, vipodozi, kutengeneza nywele na chakula cha kidomo?" Je, ni kuhusu mambo haya? Hii ni sehemu ya mienendo, lakini hatutaki kuzungumzia haya hapa. Tunataka tu kuzungumza kuhusu mawazo ambayo mienendo ya kijamii inaleta kwa watu, jinsi inasababisha watu kutenda duniani, malengo ya maisha na mtazamo ambao inaleta kwa watu. Hii ni muhimu sana: inaweza kudhibiti na kushawishi hali ya akili ya mwanadamu. Moja baada ya nyingine, hii mienendo yote inabeba ushawishi mwovu unaoendelea kumpotosha mwanadamu, kumfanya kuendelea kupoteza dhamiri, ubinadamu na mantiki, na unaoshukisha maadili yao na ubora wao wa tabia zaidi na zaidi, hadi kwa kiwango ambamo tunaweza hata kusema wengi wa watu sasa hawana uadilifu, hawana ubinadamu, wala hawana dhamiri yoyote, wala akili yoyote. Hivyo mienendo hii ni ipi? Huwezi kuona mienendo hii kwa macho. Wakati upepo wa mwenendo unavuma, pengine ni idadi ndogo ya watu tu watakuwa waanzisha mitindo. Wanaanza kwa kufanya jambo la aina hii, kukubali wazo la aina hii ama mtazamo wa aina hii. Wengi wa watu, hata hivyo, katikati ya kutojua kwao, bado watazidi kuambukizwa, kufanywa wenyeji na kuvutia na aina hii ya mwenendo, hadi wote bila kujua na bila kujitolea wanamkubali, na wote wanazama na kudhibitiwa na yeye. Kwa mwanadamu ambaye si wa mwili na akili timamu, ambaye kamwe hajui ukweli, ambaye hawezi kusema tofauti kati ya vitu vyema na hasi, mienendo ya aina hii moja baada ya nyingine inawafanya wote wawe radhi kukubali mienendo hii, mtazamo wa maisha, na maadili yatokayo kwa Shetani. Wanakubali anachowaambia Shetani juu ya jinsi ya kukaribia maisha na jinsi ya kuishi ambayo Shetani "amewapa." Hawana nguvu, wala hawana uwezo, wala ufahamu wa kupinga. Kwa hivyo hii mienendo hasa ni nini? Nimechukua mfano rahisi ambao mnaweza kuja kuelewa. Kwa mfano, watu wa kale waliendesha biashara zao kwa njia ambayo haikudanganya wazee wala vijana, na ambayo iliuza bidhaa kwa bei sawa bila kujali aliyekuwa akinunua. Je, dokezo la dhamiri na ubinadamu haliwasilishwi hapa? Wakati watu walitumia aina hii ya imani walipokuwa wakifanya biashara zao, inaonyesha kwamba bado walikuwa na baadhi ya dhamiri, baadhi ya ubinadamu wakati huo. Lakini na mahitaji ya mwanadamu ya kiasi kinachopanda daima cha pesa, watu bila kujua walikuja kupenda pesa, hupenda faida na hupenda raha zaidi na zaidi. Kwa hivyo watu walikuja kuona pesa kuwa muhimu zaidi? Wakati watu wanaona pesa kuwa muhimu zaidi, bila kujua wanapuuza sifa, umashuhuri wao, ufahari, na uadilifu wao; wanapuuza mambo haya yote, sivyo? Unapojihusisha katika biashara, unaona mtu mwingine akichukua mbinu tofauti na kutumia njia mbalimbali kuibia watu na kuwa tajiri. Ingawa pesa iliyopatwa ni faida iliyopatwa vibaya, wanakuwa tajiri zaidi na zaidi. Wanajihusisha na biashara sawa na wewe, lakini familia yao yote inafurahia maisha kukuliko, na unahisi vibaya, ukisema: "Mbona siwezi kufanya hivyo? Mbona siwezi kupata kama wapatavyo? Ni lazima nifikirie njia ya kupata pesa zaidi, kufanya biashara yangu kufanikiwa." Kisha unafikiria hili. Kulingana na mbinu ya kawaida ya kutengeneza pesa, kutodanganya wazee wala vijana na kuuza vitu kwa bei sawa kwa wote, pesa unayotengeneza ni kwa dhamiri nzuri, lakini haiwezi kukufanya kuwa tajiri haraka. Hata hivyo, chini ya tamaa ya kutengeneza faida, kufikiria kwako kunapitia mabadiliko taratibu. Katika mabadiliko haya, kanuni zako za tabia pia zinaanza kubadilika. Wakati unamdanganya mtu kwa mara ya kwanza, unapomlaghai mtu kwa mara ya kwanza, una mashaka, ukisema "Hii ni mara ya mwisho namdanganya mtu na sitafanya hivyo tena. Siwezi kudanganya watu. Kudanganya watu kutapata tu adhabu na kutaleta majanga kwangu! Hii ni mara ya mwisho namdanganya mtu na sitafanya hivyo tena." Unapomdanganya mtu kwa mara ya kwanza, moyo wako una aibu kiasi; hii ndiyo kazi ya dhamiri ya mwanadamu—kuwa na aibu na kukushutumu, ili ihisi kuwa siyo asili wakati unamdanganya mtu. Lakini baada ya wewe kufanikiwa kumdanganya mtu unaona kwamba sasa una pesa zaidi kuliko awali, na unafikiria mbinu hii inaweza kuwa ya manufaa sana kwako. Licha ya maumivu madogo ndani ya moyo wako, bado unahisi kujipongeza kwa mafanikio yako, na unahisi kuridhishwa kidogo na wewe mwenyewe. Kwa mara ya kwanza, unakubali tabia yako mwenyewe na unakubali uwongo wako mwenyewe. Baadaye, wakati mwanadamu amechafuliwa na kudanganywa huku, ni sawa na mtu ambaye anahusika na kamari na kisha anakuwa mchezaji kamari. Katika kutoelewa, anapenda tabia yake ya kudanganya na anaikubali. Katika kutoelewa, anachukua kudanganya kuwa tabia halali ya kibiashara, na anachukua kudanganya kuwa mbinu ya manufaa zaidi ya kusalimika kwake na maisha yake; anafikiria kwamba kwa kufanya hivi anaweza kuwa tajiri haraka. Mwanzoni mwa mchakato huu watu hawawezi kukubali tabia ya aina hii, wanadharau tabia hii na njia hii ya kufanya mambo, kisha wanajaribu tabia hii wao wenyewe, na kuijaribu kwa njia yao wenyewe, na kisha mioyo yao inaanza kubadilika polepole. Kwa hivyo mabadiliko haya ni yapi? Ni kukubali na kukiri mwenendo huu, kukiri na kukubali wazo hili lililoingizwa kwako na mwenendo wa jamii. Katika kutoelewa, unahisi kwamba usipodanganya katika biashara basi utapata hasara, kwamba usipodanganya basi utakuwa umepoteza kitu. Bila kujua, kudanganya huku kunakuwa nafsi yako, tegemeo kuu lako, na pia kunakuwa aina ya tabia ambayo ni kanuni isiyoweza kutupiliwa mbali katika maisha yako. Baada ya mwanadamu kukubali tabia hii na kufikiria huku, je, moyo wa mwanadamu unapitia mabadiliko? Moyo wako umebadilika, basi uadilifu wako umebadilika? Ubinadamu wako umebadilika? (Ndiyo.) Basi dhamiri yako imebadilika? (Ndiyo.) Uwepo wote wa mwanadamu unapitia mabadiliko bora, kutoka kwa mioyo yao hadi kwa mawazo yao, hadi kwa kiwango ambapo wanabadilika kutoka ndani hadi nje. Mabadiliko haya yanakuweka mbali na mbali zaidi kutoka kwa Mungu, na unakuwa na uafikiano zaidi na zaidi na Shetani, unakuwa sawa zaidi na zaidi na yeye.
Sasa mienendo hii ya kijamii ni rahisi kwako kuelewa. Nilichagua tu mfano rahisi, mfano unaoonekana kawaida ambao watu watakuwa wanajua. Hii mienendo ya kijamii ina ushawishi mkubwa kwa watu? (Ndiyo.) Kwa hivyo hii mienendo ya kijamii ina athari inayodhuru kwa kina kwa watu? (Ndiyo.) Athari ya kudhuru kwa kina kwa watu. Shetani hutumia moja ya mienendo hii ya kijamii baada ya nyingine kupotosha nini ya mwanadamu? (Dhamiri, akili, ubinadamu, maadili.) Nini tena? (Mtazamo wa mwanadamu wa maisha.) Je, inasababisha kuzorota polepole ndani ya watu? (Ndiyo.) Shetani hutumia hii mienendo ya kijamii kuvuta watu hatua moja baada ya nyingine hadi katika kiota cha mashetani, ili watu walionaswa katika mienendo ya kijamii bila kujua wanatetea pesa na tamaa za mwili, na pia kutetea uovu na ukatili. Punde mambo haya yameingia moyoni mwa mwanadamu, ni nini basi mwanadamu anakuwa? Mwanadamu anakuwa ibilisi Shetani! Hii ni kwa sababu ya mwelekeo kisaikolojia upi katika moyo wa mwanadamu? Ni kipi ambacho mwanadamu anatetea? Mwanadamu huanza kupenda uovu na ukatili. Hawapendi uzuri ama wema, wala hata amani. Watu hawako radhi kuishi maisha rahisi ya ubinadamu wa kawaida, lakini badala yake wanataka kufurahia hadhi ya juu na utajiri mkubwa, kufurahia raha za mwili, na kutumia juhudi zote kuridhisha miili yao, bila vizuizi, hakuna vifungo vya kuwashikilia nyuma, kwa maneno mengine kufanya chochote wanachotaka. Hivyo wakati mwanadamu ametumbukizwa katika mienendo ya aina hii, maarifa ambayo mmefunzwa yanaweza kuwasaidia kuwa huru? Je, desturi ya kitamaduni na ushirikina mnayojua yanaweza kuwasaidia kutupilia mbali hii hatari ya kutisha? Je, maadili ya desturi na sherehe za desturi ambazo mwanadamu huelewa zinaweza kumsaidia kujizuia? Chukua Fasihi Bora ya Herufi Tatu, kwa mfano. Inaweza kusaidia watu kutoa miguu yao katika mchanga unaomeza wa[b] mienendo hii? (La, haiwezi.) Kwa njia hii, mwanadamu anakuwa mwovu zaidi na zaidi, mwenye kiburi, mwenye kushusha hadhi, mwenye ubinafsi, na mwenye kijicho. Hakuna tena upendo kati ya watu, hakuna tena upendo wowote kati ya wanafamilia, hakuna tena uelewa wowote kati ya jamaa na marafiki; mahusiano ya binadamu yamejawa ukatili. Kila mtu anataka kutumia mbinu katili kuishi miongoni mwa wanadamu wenzake; wanakamata riziki zao kwa kutumia ukatili; wanashinda vyeo vyao na kupata faida zao wenyewe kwa kutumia ukatili na wanafanya chochote watakacho kwa kutumia njia mbovu na katili. Si ubinadamu huu unatisha? (Ndiyo.) Baada ya kunisikia Nikiongea kuhusu vitu hivi sasa, hamfikiri kwamba inatisha kuishi miongoni mwa aina hii ya umati, katika dunia hii na katika mazingira, yote ambayo Shetani amepotosha? (Ndiyo.) Kwa hivyo mmewahi kujihisi kuwa wenye kusikitisha? Lazima mnaihisi kiasi sasa, siyo? (Ndiyo.) Kwa kusikiza sauti zenu, inaonekana kana kwamba mnafikiria "Shetani hutumia njia nyingi mbalimbali kumpotosha mwanadamu. Anakamata kila fursa na yupo kila mahali tunageukia. Mwanadamu bado anaweza kuokolewa?" Mwanadamu bado anaweza kuokolewa? Wanadamu wanaweza kujiokoa? (La.) Je, Mfalme Mkuu wa Jade anaweza kumwokoa mwanadamu? Je, Confucius anaweza kumwokoa mwanadamu? Je, Guanyin Bodhisattva anaweza kumwokoa mwanadamu? (La.) Kwa hivyo ni nani anayeweza kumwokoa mwanadamu? (Mungu.) Watu wengine, hata hivyo, wataibua katika mioyo yao maswali kama: "Shetani anatudhuru kwa kiasi kikubwa sana, kwa hasira sana basi hatuna matumaini ya kuishi, wala imani katika kuishi. Sote tunaishi miongoni mwa upotovu na kila mtu anampinga Mungu hata hivyo, na sasa mioyo yetu imezama chini kadri iwezavyo. Kwa hivyo wakati Shetani anatupotosha, Mungu yuko wapi? Mungu anafanya nini? Chochote Mungu anatufanyia kamwe hatukihisi!" Watu wengine bila kuepukika wanahisi kuhuzunika na bila kuepukika wanahisi kuvunjika moyo kiasi. Kwenu, hisia hii ni ya kina sana kwa sababu vyote ambavyo Nimekuwa nikisema vimekuwa kuwafanya watu kuja kuelewa polepole, kuhisi zaidi na zaidi kwamba hawana matumaini, kuhisi zaidi na zaidi kwamba wameachwa na Mungu. Lakini usijali. Mada yetu ya kushiriki leo, "uovu wa Shetani," siyo dhamira yetu ya kweli. Kuongea kuhusu kiini cha utakatifu wa Mungu, hata hivyo, lazima kwanza tuongee kuhusu jinsi Shetani anampotosha mwanadamu na uovu wa Shetani ili kuifanya kuwa wazi zaidi kwa watu mwanadamu sasa yuko katika hali ya aina gani. Lengo moja la kuongea juu ya hili ni kuruhusu watu kujua uovu wa Shetani, ilhali jingine ni kuwaruhusu watu kuelewa kwa kina zaidi utakatifu ni nini.
Je, haya mambo ambayo Nimeongea kuhusu hivi karibuni ni ya kina zaidi kuliko ya wakati uliopita? (Ndiyo.) Hivyo uelewa wenu sasa basi ni wa kina zaidi? (Ndiyo.)





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni