Ni kiasi gani cha kazi ya mwanadamu ni kazi ya Roho Mtakatifu na uzoefu wa mwanadamu ni kiasi gani? Hata sasa, tunaweza kusema kuwa watu bado hawayaelewi maswali haya, ambayo yote ni kwa sababu watu hawaelewi kanuni za utendaji kazi wa Roho Mtakatifu. Kazi ya mwanadamu Ninayoizungumzia, kimsingi, ni kwa kurejelea kazi za wale ambao wana kazi ya Roho Mtakatifu au wale ambao wanatumiwa na Roho Mtakatifu. Sizungumzii kazi ambayo inatokana na matakwa ya mwanadamu bali kazi ya mitume, watendaji kazi au kaka na dada wa kawaida waliopo katika mawanda ya kazi ya Roho Mtakatifu.
Hapa, kazi ya mwanadamu hairejelei kazi ya Mungu mwenye mwili bali mawanda na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu kwa watu. Ingawa kanuni hizi ni kanuni na mawanda ya kazi ya Roho Mtakatifu, hazifanani na kanuni na mawanda ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Kazi za mwanadamu zina kiini na kanuni za mwanadamu, na kazi za Mungu zina kiini na kanuni za Mungu.
Kazi katika mkondo wa Roho Mtakatifu, bila kujali ni kazi ya Mungu Mwenyewe au ni kazi ya watu wanaotumiwa, ni kazi ya Roho Mtakatifu. Kiini cha Mungu Mwenyewe ni Roho, ambaye anaweza kuitwa Roho Mtakatifu au Roho mwenye nguvu mara saba. Kwa vyovyote, ni Roho wa Mungu. Ni kwamba tu Roho wa Mungu anaitwa majina tofauti katika enzi tofauti tofauti. Lakini nafsi Yao bado ni moja. Hivyo, kazi ya Mungu mwenyewe ni kazi ya Roho Mtakatifu; kazi za Mungu mwenye mwili hazitofautiani na kazi za Roho Mtakatifu. Kazi ya wanadamu wanaotumiwa pia ni kazi ya Roho Mtakatifu. Ni kwamba tu kazi ya Mungu ni dhihirisho kamili la Roho Mtakatifu, na hakuna tofauti, ilhali kazi ya wanadamu wanaotumiwa inachanganyika na mambo mengi ya kibinadamu, na wala sio udhihirishaji wa moja kwa moja wa Roho Mtakatifu, wala udhihirishaji kamili. Kazi ya Roho Mtakatifu ina mawanda mapana na wala haizuiliwi na hali yoyote ile. Kazi hiyo inatofautiana kwa watu tofauti tofauti, na kutoa dutu tofauti tofauti zifanyazo kazi. Kazi pia inatofautiana katika enzi mbali mbali, kama pia ilivyo kazi tofauti katika nchi mbalimbali. Bila shaka ingawa Roho Mtakatifu hufanya kazi katika njia nyingi tofauti tofauti na kulingana na kanuni nyingi, haijalishi kazi imefanyikaje au kwa watu wa aina gani, kiini ni tofauti daima, na kazi Anazofanya kwa watu tofauti zote zina kanuni na zote zinaweza kuwakilisha kiini cha mhusika anayefanyiwa kazi. Hii ni kwa sababu kazi ya Roho Mtakatifu ni mahususi kabisa kwa mapana yake na inapimika. Kazi inayofanywa katika mwili uliopatikana si sawa na kazi inayofanywa kwa watu, na kazi hii pia inatofautiana kulingana na tabia mbalimbali za watu. Kazi inayofanywa katika mwili uliopatikana si sawa na kazi inayofanywa kwa watu, na katika mwili uliopatikana Hafanyi kazi ile ile kama aliyoifanya kwa watu. Kwa ufupi, haijalishi Anafanya kazi jinsi gani, kazi katika vitu mbalimbali haifanani, na kanuni ambazo Anazitumia kufanya kazi zinatofautiana kulingana na hali na asili ya watu mbalimbali. Roho Mtakatifu Anafanya kazi kwa watu tofautitofauti kulingana na kiini chao cha asili na haweki mahitaji ambayo ni zaidi ya kiini chao cha asili, na wala Hafanyi kazi zaidi ya tabia yao halisi. Kwa hivyo, kazi ya Roho Mtakatifu kwa mwanadamu inawaruhusu watu kuona dutu ya mtu anayefanyiwa kazi. Utu wa asili wa mwanadamu haubadiliki; tabia halisi ya mwanadamu ina mipaka. Kama Roho Mtakatifu huwatumia watu au anawafanyia watu kazi, kazi hiyo siku zote inafanywa kulingana na tabia za watu ili waweze kunufaika kutoka kwayo. Roho Mtakatifu anapofanya kazi kwa wanadamu wanaotumika, karama zao na tabia zao halisi zinatumiwa pia na wala haziachwi. Tabia zao halisi zinatumiwa zote kwa ajili ya kutoa huduma kwa kazi. Tunaweza kusema kuwa Anafanya kazi kwa kutumia sehemu zilizopo za wanadamu ili kupata matokeo yatendayo kazi. Kinyume chake, kazi inayofanyika katika mwili uliopatikana ni kumdhihirisha moja kwa moja Roho na wala haichanganywi na akili na mawazo ya mwanadamu, haifikiwi na karama za mwanadamu, uzoefu wa mwanadamu au hali ya ndani ya mwanadamu. Kazi nyingi mno ya Roho Mtakatifu yote inalenga kumnufaisha na kumwadilisha mwanadamu. Lakini baadhi ya watu wanaweza kukamilishwa wakati wengine hawana vigezo vya kuweza kukamilishwa, ni sawa na kusema, hawawezi kukamilishwa na ni vigumu sana kuokolewa, na ingawa wanaweza kuwa walishakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, mwishowe wanaondolewa. Hii ni sawa na kusema kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwaadilisha watu, hii haimaanishi kwamba wale wote waliokwisha kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu wanapaswa kukamilishwa kikamilifu, kwa sababu njia wanayoiendea watu wengi si njia ya kukamilishwa. Wana kazi moja tu ya Roho Mtakatifu, na wala si ushirikiano wa kibinafsi wa binadamu au njia sahihi za kibinadamu. Kwa njia hii, kazi ya Roho Mtakatifu kwa watu hawa inakuwa kazi katika huduma ya wale ambao wanakamilishwa. Kazi ya Roho Mtakatifu haiwezi kuonwa moja kwa moja na watu au kuguswa moja kwa moja na watu wenyewe. Inaweza kudhihirishwa tu kwa njia ya msaada wa watu wenye karama ya kufanya kazi, ikiwa na maana kwamba kazi ya Roho Mtakatifu inatolewa kwa wafuasi Wake kwa njia ya udhihirisho wa wanadamu.
Kazi ya Roho Mtakatifu inakamilishwa na kukamilika kupitia watu wa aina nyingi na hali nyingi tofauti tofauti. Ingawa kazi ya Mungu mwenye mwili inaweza kuwakilisha kazi ya enzi zote, na inaweza kuwakilisha uingiaji wa watu katika enzi nzima, kazi kwa watu wengi bado inahitajika kufanywa na watu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu na sio Mungu mwenye mwili. Kwa hivyo, kazi ya Mungu, au huduma ya Mungu mwenyewe, ni kazi ya Mungu mwenye mwili na haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kazi ya Roho Mtakatifu imekamilishwa kupitia watu wa aina mbalimbali na haiwezi kukamilishwa na mtu mahususi mmoja tu, au kufafanuliwa kikamilifu kupitia mtu mmoja mahususi. Wale ambao wanaongoza kanisa pia hawawezi kuiwakilisha kazi ya Roho Mtakatifu kikamilifu; wanaweza kufanya tu kazi fulani ya kuongoza. Kwa njia hii, kazi ya Roho Mtakatifu inaweza kugawanywa katika sehemu tatu: Kazi ya Mungu mwenyewe, kazi ya wanadamu wanaotumiwa, na kazi kwa wale wote walioko katika mkondo wa Roho Mtakatifu. Miongoni mwa hizo tatu, kazi ya Mungu ni kuongoza enzi nzima; kazi ya wanadamu wanatumiwa ni kuwaongoza wafuasi wote wa Mungu kwa kutumwa au kupokea maagizo kwa ajili ya kazi ya Mungu mwenyewe; na wanadamu hawa ndio wanaoshirikiana na kazi ya Mungu; kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu kwa wale waliopo katika mkondo wake ni kudumisha kazi Yake yote, yaani, kudumisha usimamizi wote na kudumisha ushuhuda Wake, na wakati uo huo kuwakamilisha wale wanaoweza kukamilishwa. Sehemu tatu hizi ni kazi kamili ya Roho Mtakatifu, lakini bila kazi ya Mungu Mwenyewe, kazi yote ya usimamizi inaweza kutuama. Kazi ya Mungu Mwenyewe inahusisha kazi ya wanadamu wote, na pia inawakilisha kazi ya enzi nzima. Hii ni kusema kwamba, kazi ya Mungu mwenyewe inawakilisha harakati na mwelekeo wa kazi yote ya Roho Mtakatifu, ilhali kazi ya mitume inafuata kazi ya Mungu na wala haiongozi enzi, na wala haiwakilishi mwelekeo unaofanya kazi wa Roho Mtakatifu katika enzi nzima. Huwa wanafanya tu kazi ambayo mwanadamu anapaswa kufanya, ambayo haihusishi kabisa kazi ya usimamizi. Kazi ya Mungu ni mradi ndani ya kazi ya usimamizi. Kazi ya mwanadamu ni wajibu tu wa wanadamu kuweza kutumika na wala haina uhusiano na kazi ya usimamizi. Kwa sababu ya utambulisho na uwakilishaji tofauti wa kazi hii, licha ya ukweli kwamba zote ni kazi za Roho Mtakatifu, kuna tofauti za wazi na bainifu kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Aidha, kiwango cha kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu kwa watu wenye tambulisho tofauti inatofautiana. Hizi ni kanuni na mawanda ya kazi ya Roho Mtakatifu.
Kazi ya mwanadamu inawakilisha uzoefu wake na ubinadamu wake. Kile ambacho mwanadamu anatoa na kazi ambayo anafanya vinamwakilisha yeye. Mwanadamu kuona, mwanadamu kufikiri, mantiki ya mwanadamu na uwezo mkubwa wa kufikiri vyote vinajumuishwa katika kazi yake. Kimsingi, uzoefu wa mwanadamu, unaweza zaidi kuwakilisha kazi yake na kile ambacho mtu amekipitia kitakuwa ni sehemu ya kazi yake. Kazi ya mwanadamu inaweza kudhihirisha uzoefu wake. Pale ambapo baadhi ya watu wanakuwa katika hali ya kukaa tu bila kufanya kujishughulisha, sehemu kubwa ya ushirika wao inakuwa na mambo ya uasi. Kama uzoefu wao ni mzuri na wanapita katika njia ya upande mzuri, kile wanachoshiriki kinatia moyo sana, na watu wanaweza kupokea mambo mazuri kutoka kwao. Ikiwa mfanyakazi atakuwa katika hali ya kukaa tu wakati huu, ushirika wake siku zote utakuwa na mambo ya uasi. Aina hii ya ushirika ni ya kuvunja moyo, na wengine watavunjika mioyo bila kujua kwa kufuata ushirika wa yule mfanyakazi. Hali ya wafuasi inabadilika kutegemea na hali ya kiongozi. Vile ambavyo mfanyakazi alivyo ndani, ndivyo hivyo anavyojidhihirisha, na kazi ya Roho Mtakatifu mara nyingi inabadilika kulingana hali ya mwanadamu. Anafanya kazi kulingana na uzoefu wa mwanadamu na wala hamshurutishi mwanadamu bali anamsihi mwanadamu kulinga na hali yake ya kawaida ya uzoefu wake. Hii ni kusema kwamba ushirika wa mwanadamu unatofautiana na neno la Mungu. Ushirika wa mwanadamu hueleza vile anavyotazama mambo na uzoefu wake, ukidhihirisha kile wanachokiona na kupitia uzoefu wao juu ya msingi wa kazi ya Mungu. Wajibu wao ni kutafuta, kazi au maneno ya Mungu, kile wanachopaswa kufanya au kuingia kwacho, halafu kukiwasilisha kwa wafuasi. Hivyo, kazi ya mwanadamu inawakilisha kuingia au matendo yake. Kazi hiyo imechanganyikana na masomo ya kibinadamu na uzoefu au mawazo ya kibinadamu. Haijalishi namna ambavyo Roho Mtakatifu Anafanya kazi, ama Anavyomfanyia kazi mwanadamu au Mungu mwenye mwili, siku zote watenda kazi ndio wanaodhihirisha vile walivyo. Ingawa ni Roho Mtakatifu ambaye hufanya kazi, kazi hiyo imejengwa katika msingi wa mwanadamu alivyo kwa asili, kwa sababu Roho Mtakatifu hafanyi kazi pasipo msingi. Kwa maneno mengine, kazi haifanyiki pasipokuwa na kitu, lakini siku zote hufanyika kulingana na mazingira halisi na hali halisi. Ni kwa njia hii pekee ndio tabia ya mwanadamu inaweza kubadilishwa, kwamba mitazamo yake ya zamani na mawazo yake ya zamani yanaweza kubadilishwa. Kile ambacho mwanadamu hukidhihirisha ni kile anachokiona, kupitia uzoefu na kukitafakari. Hata kama ni mafundisho au mitazamo, haya yote hufikiwa na fikra za mwanadamu. Bila kujali ukubwa wa kazi ya mwanadamu, haiwezi kuzidi mawanda ya uzoefu wa mwanadamu, kile ambacho mwanadamu huona, au kile ambacho mwanadamu anaweza kukitafakari au kuingia akilini mwake. Kile ambacho Mungu anadhihirisha ndivyo hivyo Mungu Mwenyewe alivyo, na hii ni nje ya uwezo wa mwanadamu, yaani, nje ya uwezo wa kufikiri kwa mwanadamu. Anadhihirisha kazi Yake ya kuwaongoza wanadamu wote, na hii hauhusiani na undani wa uzoefu wa mwanadamu, badala yake inahusu usimamizi Wake. Mwanadamu anadhihirisha uzoefu wake wakati Mungu akidhihirisha hali Yake—hali hii ni tabia Yake ya asili na uko nje ya uwezo wa mwanadamu. Uzoefu wa mwanadamu ni kuona kwake na kupata maarifa kulingana na udhihirishaji wa Mungu wa hali Yake. Kuona huko na maarifa vinaitwa asili ya mwanadamu. Vinadhihirishwa kwa msingi wa tabia ya asili ya mwanadamu na tabia yake halisi; hivyo pia vinaitwa asili ya mwanadamu. Mwanadamu anaweza kushiriki kile anachokipitia na kukiona. Kile ambacho hajawahi kukipitia au kukiona au akili yake haiwezi kukifikia, yaani, vitu ambavyo havipo ndani yake, hawezi kuvishiriki. Ikiwa kile ambacho mwanadamu anakidhihirisha sio uzoefu wake, basi ni kile anachokitafakari au mafundisho ya kidini. Kwa ufupi, hakuna ukweli wowote katika maneno yake. Kama hujawahi kukutana na maswala ya jamii, huwezi kushiriki kwa uwazi kwenye mahusiano changamani katika jamii. Kama huna familia na watu wengine wanazungumza juu ya masuala ya familia, huwezi kuelewa kiasi kikubwa cha kile walichokuwa wakisema. Kwa hivyo, kile ambacho mwanadamu anakifanyia ushirika na kazi anayofanya vinawakilisha hali yake ya ndani. Ikiwa mtu anafanya ushirika kuhusu uelewa wake wa kuadibu na hukumu, lakini huna uzoefu wake, usithubutu kukana maarifa yake, badala yake kuwa na uhakika wa anachokisema kwa asilimia mia moja. Hii ni kwa sababu kile anachokifanyia ushirika ni kitu ambacho hujawahi kupata uzoefu wake, kitu ambacho hujawahi kukifahamu, na akili yako haiwezi kukitafakari. Unaweza tu kujifunza kutoka kwa ufahamu wake njia za maisha yajayo yanayohusiana na kuadibu na hukumu. Lakini njia hii inaweza kufanya kazi tu kama uelewa uliojikita katika fundisho na haiwezi kuchukua nafasi ya ufahamu wako, na zaidi sana uzoefu wako. Pengine unafikiri kwamba kile anachokisema ni sahihi, lakini unapokipitia, unagundua kwamba hakitekelezeki katika mambo mengi. Pengine unahisi kwamba maarifa fulani unayoyasikia hayatekelezeki kabisa; unakuwa na mtazamo kuhusu maarifa hayo kwa wakati fulani, na ingawa unayakubali, unafanya hivyo shingo upande. Lakini unapopata uzoefu, maarifa yanayokupatia mtazamo ndiyo yanayoongoza matendo yako. Na kadri unavyotenda, ndivyo unavyozidi kuelewa thamani halisi na maana ya maneno yake. Baada ya kuwa na uzoefu, sasa unaweza kuzungumza juu ya maarifa unayopaswa kuwa nayo kuhusu vitu ulivyovipitia. Aidha, unaweza pia kutofautisha kati ya wale ambao maarifa yao ni halisi na yanayotekelezeka na wale ambao maarifa yao yamejikita katika mafundisho ya kidini na hayana thamani. Kwa hivyo, kama maarifa ambayo unayazungumzia yanapatana na ukweli basi kwa kiasi kikubwa yanategemea na iwapo una uzoefu wa kivitendo. Pale palipo na ukweli katika uzoefu wako, maarifa yako yatakuwa yanatekelezeka na yenye thamani. Kupitia uzoefu wako, pia unaweza kupata utambuzi na umaizi, kukuza maarifa yako, na kuongeza hekima yako na akili ya kuzaliwa katika kujiongoza. Maarifa yanayozungumzwa na watu ambao hawana ukweli ni fundisho la kidini tu, bila kujali yana nguvu kiasi gani. Mtu wa aina hii anaweza kuwa mwenye akili sana yanapokuja masuala ya kimwili lakini hawezi kutofautisha yanapokuja masuala ya kiroho. Hii ni kwa sababu watu kama hao hawana uzoefu wowote katika masuala ya kiroho. Kuna watu ambao hawajapata nuru katika masuala ya kiroho na kwa hivyo hawaielewi roho. Bila kujali unazungumzia kipengele gani cha maarifa, ilimradi ni asili yako, basi ni uzoefu wako binafsi, maarifa yako halisi. Kile ambacho watu wenye mafundisho tu huzungumzia, yaani, wale ambao hawana ukweli au uhalisi, huzungumzia yaweza kusemwa kuwa ni asili yao, kwa sababu mafundisho yao yamefikiwa kwa njia ya kutafakari sana na ni matokeo ya akili yao kutafakari kwa kina, lakini ni mafundisho tu, si kitu chochote zaidi ya fikra dhahania. Uzoefu wa aina tofauti za watu unawakilisha vitu vilivyomo ndani yao. Wale wote ambao hawana uzoefu wa kiroho hawawezi kuzungumza juu ya maarifa ya ukweli, maarifa sahihi kuhusu aina mbalimbali za masuala ya kiroho. Kile ambacho mtu anakidhihirisha ndivyo alivyo ndani—hii ni hakika. Ikiwa mtu anatamani kuwa na maarifa ya masuala ya kiroho na ukweli, anapaswa kuwa na uzoefu halisi. Ikiwa huwezi kuzungumza kwa usahihi juu ya masuala ya kawaida yanayohusiana na maisha ya mwanadamu, basi utawezaje kuzungumzia masuala ya kiroho? Wale wanaoweza kuliongoza kanisa, kurutubisha maisha ya watu, na kuwa mtume kwa watu, wanapaswa kuwa na uzoefu halisi, uelewa sahihi wa masuala ya kiroho, kuukubali kuliko sahihi na kuwa na uzoefu wa ukweli. Watu wa namna hiyo tu ndio waliofuzu kuwa watenda kazi au mitume wanaoyaongoza makanisa. Vinginevyo, wanaweza kuwa wafuasi kama wadogo na hawawezi kuongoza, wala kuwa mtume mwenye uwezo wa kuwapatia watu uhai. Hii ni kwa sababu kazi ya mitume siyo kukimbia au kupigana; ni kutoa huduma ya maisha na kuongoza mabadiliko katika tabia ya mwanadamu. Ni kazi ambayo inafanywa na wale ambao wameagizwa kubeba majukumu mazito na sio kitu ambacho kila mtu anaweza kukifanya. Aina hii ya kazi inaweza tu kufanywa na wale ambao wana maisha ya uwepo, yaani, wale ambao wana uzoefu wa ukweli. Haiwezi kufanywa na kila mtu ambaye anaweza kukata tamaa, anaweza kukimbia au yupo tayari kutumia pesa; watu ambao hawana uzoefu wa ukweli, wale ambao hawajawahi kupogolewa au kuhukumiwa, hawawezi kufanya aina hii ya kazi. Watu ambao hawana uzoefu, yaani, watu wasio na ukweli, hawawezi kuona ukweli kwa uwazi kwa kuwa wao wenyewe hawako katika hali hii. Hivyo, mtu wa aina hii si kwamba anaweza tu kufanya kazi ya kuongoza bali atakuwa mtu wa kuondolewa ikiwa hatakuwa na ukweli kwa muda mrefu. Kuona unakokuzungumzia kunaweza kuthibitisha ugumu ulioupitia maishani, katika suala ambalo umefanyiwa kuadibu na katika jambo ambalo umehukumiwa kwalo. Hii pia ni kweli katika majaribu: Vitu ambavyo mtu anasafishwa kwavyo, vitu ambavyo kwavyo mtu yupo mdhaifu, hivi ni vitu ambavyo mtu ana uzoefu navyo, vitu ambavyo mtu anaelewa njia zake. Kwa mfano, ikiwa mtu amekatishwa tamaa katika ndoa, muda mwingi atakuwa anafanya ushirika, "Asante Mungu, Mungu asifiwe, ni lazima nitimize matakwa ya Mungu, na kuyatoa maisha yangu yote, kuikabidhi ndoa yangu kikamilifu katika mikono ya Mungu. Niko radhi kuyatoa maisha yangu yote kwa Mungu." Kupitia ushirika, kila kitu ndani ya mwanadamu, kile alicho, kinaweza kuwakilishwa. Mwendo wa hotuba ya mtu, kama anazungumza kwa sauti kubwa au kwa sauti ya chini, masuala kama hayo ambayo si masuala ya uzoefu hayawezi kuwakilisha kile alichonacho na kile alicho. Yanaweza kueleza tu iwapo tabia yake ni nzuri au mbaya, au kama asili yake ni nzuri au mbaya lakini haiwezi kulinganishwa na kama ana uzoefu. Uwezo wa mtu kujidhihirisha anapozungumza, ama ujuzi au kasi ya kuzungumza, ni suala tu la mazoezi na haliwezi kuchukua nafasi ya uzoefu wake. Unapozungumza juu ya uzoefu wako binafsi, unafanya ushirika wa kile ambacho unakipatia umuhimu na vitu vyote ndani yako. Usemi Wangu unawakilisha asili Yangu, lakini kile Ninachokisema kiko nje ya uwezo wa mwanadamu. Kile Nikisemacho sio kile ambacho mwanadamu anakipitia, na sio kitu ambacho mwanadamu anaweza kukiona, pia si kitu ambacho mwanadamu anaweza kukigusa, lakini ndivyo Nilivyo. Baadhi ya watu wanakiri tu kwamba kile Ninachokifanyia ushirika ndicho kile Nimekipitia, lakini hawatambui kwamba ni udhihirishaji wa moja kwa moja wa Roho. Ni kweli, kile Ninachokisema ndicho kile Nimekipitia. Ni Mimi Ndiye Niliyefanya kazi ya usimamizi kwa kipindi cha zaidi ya miaka elfu sita. Nimeshuhudia kila kitu kuanzia mwanzo wa uumbaji wa mwanadamu hadi leo; Nitashindwaje kukizungumzia? Linapokuja suala la asili ya mwanadamu, Nimeiona waziwazi, na Nimeiangalia toka zamani; sasa Nitashindwaje kuiongelea? Kwa kuwa nimeiona asili ya mwanadamu kwa uwazi, Nina sifa za kumrudi mwanadamu na kumhukumu, kwa sababu mwanadamu mzima ametoka Kwangu lakini ameharibiwa na Shetani. Kwa ukweli, Nimehitimu kutathmini kazi ambayo Nimeifanya. Ingawa kazi hii haijafanywa na mwili Wangu, ni udhihirishaji wa moja kwa moja wa Roho, na hiki ndicho Nilicho nacho na kile Nilicho. Kwa hivyo, Ninaweza kudhihirisha na kufanya kazi ambayo Napaswa kufanya. Kile ambacho mwanadamu anakisema ni kile alichokipitia. Ni kile ambacho wamekiona, kile ambacho akili zao zinaweza kukifikia, na kile ambacho milango yao ya fahamu inaweza kuhisi. Hicho ndicho wanachoweza kukifanyia ushirika. Maneno yaliyosemwa na mwili wa Mungu ni udhihirishaji wa moja kwa moja wa Roho na kudhihirisha kazi ambayo imefanywa na Roho. Mwili haujaipitia au kuiona, lakini bado Anaonyesha asili Yake kwa sababu kiini cha mwili ni Roho, na Anadhihirisha kazi ya Roho. Ingawa mwili hauwezi kuifikia, ni kazi ambayo tayari imefanywa na Roho. Baada ya kufanyika mwili, kupitia udhihirishaji wa mwili, Anawasaidia watu kujua asili ya Mungu na kuwafanya watu kuiona tabia ya Mungu na kazi ambayo ameifanya. Kazi ya mwanadamu inawawezesha watu kuelewa kwa uwazi kuhusu kile wanachopaswa kuingia kwacho na wanachopaswa kukielewa; kunahusisha kuwaongoza watu kupata uelewa na kuujua ukweli. Kazi ya mwanadamu ni kuwaendeleza watu; kazi ya Mungu ni kufungua njia mpya na kufungua enzi mpya kwa ajili ya wanadamu, na kuwafunulia watu kile ambacho hakijafahamika kwa watu wenye mwili wa kufa, akiwasaidia kuelewa tabia Yake. Kazi ya Mungu ni kuwaongoza wanadamu wote.
Kazi ya Roho Mtakatifu ni kuhusu kuwasaidia watu kupata faida; ni kuwaadilisha watu; hakuna kazi ambayo haiwanufaishi watu. Haijalishi kama ukweli ni wa kina au usio wa kina, na haijalishi tabia ya wale wanaopokea ukweli huo ilivyo, chochote ambacho Roho Mtakatifu Anafanya, yote hayo huwanufaisha watu. Lakini kazi ya Roho Mtakatifu haiwezi kufanywa moja kwa moja; ni lazima ifanywe na wanadamu wanaoshirikiana Naye. Ni kwa njia hii pekee ndiyo matokeo ya kazi ya Roho Mtakatifu yanaweza kupatikana. Bila shaka, inapokuwa ni kazi ya moja kwa moja ya Roho Mtakatifu, haijachanganywa na kitu chochote kabisa; lakini inapotumia mwanadamu kama chombo, inakuwa imechanganywa sana na sio kazi halisi ya Roho Mtakatifu. Kwa njia hii, ukweli hubadilika katika viwango tofauti. Wafuasi hawapokei maana halisi ya Roho Mtakatifu bali wanapokea muungano wa kazi ya Roho Mtakatifu na uzoefu na maarifa ya mwanadamu. Sehemu ya kazi ya Roho Mtakatifu inayopokelewa na wafuasi ni sahihi. Uzoefu na maarifa ya mwanadamu yanayopokewa yanatofautiana kwa sababu watenda kazi ni tofauti. Watenda kazi wanapokuwa na nuru na uongozi wa Roho Mtakatifu, wanakuwa wanapata uzoefu kulingana na nuru na uongozi huu. Ndani ya uzoefu huu kuna akili ya mwanadamu na uzoefu, vile vile asili ya ubinadamu, ambapo wanapata maarifa na kuona vile walivyopaswa kuona. Hivi ndivyo inavyokuwa baada ya mwanadamu kuujua ukweli. Namna hii ya kutenda siku zote haifanani kwa sababu watu wana uzoefu tofauti na vitu ambavyo watu wanavipitia ni tofauti. Kwa njia hii, nuru ile ile ya Roho Mtakatifu inaleta maarifa tofauti na desturi kwa sababu wale wanaopokea nuru hiyo ni tofauti. Baadhi ya watu hufanya makosa madogo wakati wa utendaji ilhali wengine hufanya makosa makubwa, na baadhi hawafanyi chochote ila ni makosa tu. Hii ni kwa sababu uwezo wa kuelewa mambo unatofautiana na kwa sababu tabia zao halisi pia zinatofautiana. Baadhi ya watu wanaelewa hivi baada ya kuusikia ujumbe, na baadhi ya watu wanauelewa vile baada ya kuusikia ukweli. Baadhi ya watu wanapotoka kidogo; na baadhi hawaelewi kabisa maana ya ukweli. Kwa hiyo, kwa jinsi yoyote mtu aelewavyo ndivyo atakavyowaongoza wengine; hii ni kweli kabisa, kwa sababu kazi yake inadhihirisha asili yake tu. Watu wanaoongozwa na watu wenye uelewa sahihi wa ukweli pia watakuwa na uelewa sahihi wa ukweli. Hata kama kuna watu ambao uelewa wao una makosa, ni wachache sana, na sio watu wote watakuwa na makosa. Watu wanaoongozwa na watu ambao wana makosa katika kuuelewa ukweli bila shaka watakuwa wenye makosa. Watu hawa watakuwa na makosa katika kila njia. Kiwango cha kuuelewa ukweli miongoni mwa wafuasi kinategemea kwa kiasi kikubwa watenda kazi. Bila shaka, ukweli kutoka kwa Mungu ni sahihi na hauna makosa, na ni hakika. Lakini, watenda kazi hawako sahihi kikamilifu na hatuwezi kusema kwamba ni wa kutegemewa kabisa. Ikiwa watenda kazi wana njia ya kuuweka ukweli katika njia ya matendo, basi wafuasi pia watakuwa na njia ya kuutenda. Ikiwa watenda kazi hawawezi kuuweka ukweli katika matendo bali wanashikilia mafundisho tu, wafuasi hawatakuwa na uhalisia wowote. Tabia na asili ya wafuasi vinaukiliwa na kuzaliwa na havihusiani na watenda kazi. Lakini kiwango ambacho kwacho wafuasi wanauelewa ukweli na kumfahamu Mungu kinategemeana na watenda kazi (hii ni kwa baadhi ya watu tu). Vyovyote alivyo mtenda kazi, hivyo ndivyo wafuasi anaowaongoza watakavyokuwa. Kile ambacho mtenda kazi anakidhihirisha ni asili yake mwenyewe, bila kuacha chochote. Yale anayowaambia wafuasi wake watende ndiyo yeye mwenyewe yuko radhi kuyafikia au ni yale anayoweza kutimiza. Watenda kazi wengi huwaambia wafuasi wao kufuata mambo fulani kulingana na yale wao wenyewe wanayoyafanya, licha ya kuwepo mengi ambayo watu hawawezi kuyafikia kabisa. Kile ambacho watu hawawezi kufanikisha kinakuwa kizuizi katika kuingia kwao.
Kuna makosa machache zaidi katika kazi ya wale ambao wamepitia uzoefu wa kupogolewa na hukumu. Udhihirishaji wa kazi zao ni sahihi zaidi. Wale wanaotegemea asili yao katika kufanya kazi wanafanya makosa makubwa sana. Kuna uasili mwingi sana katika kazi ya watu ambao si wakamilifu, kitu ambacho kinaweka kizuizi kikubwa katika kazi ya Roho Mtakatifu. Hata wale ambao kwa asili wana vigezo vya kuwawezesha kufanya kazi pia wanapaswa kupitia uzoefu kwa kupogolewa na hukumu ili waweze kufanya kazi ya Mungu. Kama hawajapitia hukumu kama hiyo, kwa namna yoyote nzuri ile watakavyofanya, haiwezi kuambatana na kanuni za ukweli na ni uasili kabisa na uzuri wa mwanadamu. Katika kufanya kazi ya Mungu, kazi ya wale ambao wamepitia uzoefu wa kupogolewa na hukumu ni sahihi zaidi kuliko kazi ya wale ambao hawajahukumiwa. Wale ambao hawajapitia hukumu hawadhihirishi chochote isipokuwa mawazo ya kibinadamu, yakiwa yamechanganyika na uelewa wa kibinadamu na talanta za ndani. Sio udhihirisho sahihi wa mwanadamu wa kazi ya Mungu. Watu wanaowafuata wanaletwa mbele yao kwa tabia yao ya ndani. Kwa sababu wanadhihirisha vitu vingi vya kuona na uzoefu wa mwanadamu, ambavyo takribani havina muungano na maana ya asili ya Mungu, na hutofautiana sana nayo, kazi ya mtu wa aina hii haiwezi kuwaleta watu mbele ya Mungu, lakini wataletwa kwake. Hivyo wale ambao hawakupitia hukumu na kuadibu, hawana sifa za kufanya kazi ya Mungu. Kazi ya mtenda kazi mwenye sifa inaweza kuwaleta watu katika njia sahihi na kuwaruhusu kuzama kwa kina katika ukweli. Kazi anayofanya inaweza kuwaleta watu mbele ya Mungu. Aidha, kazi anayofanya inaweza kutofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu mwingine na wala haifungwi na kanuni, inawapatia watu uhuru. Aidha, wanaweza kukua katika uzima kwa taratibu, wakiendelea kukua na kuzama ndani kabisa katika ukweli. Kazi ya mtenda kazi asiyehitimu haifikii kiwango hiki; kazi yake ni ya kipumbavu. Anaweza kuwaleta watu katika kanuni; kile anachowataka watu kufanya hakitofautiani kati ya mtu na mtu; hafanyi kazi kulingana na mahitaji halisi ya watu. Katika aina hii ya kazi kunakuwa na kanuni nyingi sana na mafundisho mengi sana, na haiwezi kuwaleta watu katika uhalisia au katika hali ya kawaida ya kukua katika uzima. Inaweza kuwawezesha watu tu kusimama kwa kanuni chache zisizokuwa na maana. Uongozaji wa namna hii unaweza tu kuwapotosha watu. Anakuongoza ili uwe kama yeye; anaweza kukuleta katika kile anacho na kile alicho. Kwa wafuasi kutambua endapo viongozi wana sifa, jambo la muhimu ni kuangalia njia wanayoiongoza na matokeo ya kazi yao, na kuangalia iwapo wafuasi wanapokea kanuni kulingana na ukweli, na kama wanapokea namna ya kufanya kunakowafaa wao ili waweze kubadilishwa. Unapaswa kutofautisha kati ya kazi tofauti za aina tofauti za watu; haupaswi kuwa mfuasi mpumbavu. Hili linaathiri suala la kuingia kwako. Ikiwa huwezi kutofautisha uongozi wa mtu yupi una njia na upi hauna, utadanganywa kwa urahisi. Haya yote yana athari ya moja kwa moja katika maisha yako. Kuna mambo mengi ya asili katika kazi ya mtu ambaye hajakamilishwa; matakwa mengi ya kibinadamu yamechanganywa humo. Hali yao ni ya asili, kile walichozaliwa nacho, si maisha baada ya kupitia kushughulikiwa au uhalisia baada ya kubadilishwa. Ni kwa namna gani aina hii ya mtu anaweza kuunga mkono utafutaji wa uzima? Maisha halisi ya mwanadamu ni akili au talanta yake ya ndani. Aina hii ya akili au talanta ni kinyume cha kile hasa ambacho Mungu anamtaka mwanadamu kufanya. Ikiwa mwanadamu hajakamilishwa na tabia yake ya upotovu haijapogolewa na kushughulikiwa, kutakuwa na pengo kubwa kati ya kile anachokidhihirisha na ukweli; utachanganywa na vitu visivyoeleweka vizuri kama vile tafakari zake na uzoefu wa upande mmoja, n.k. Aidha, bila kujali jinsi anavyofanya kazi , watu wanahisi kwamba hakuna lengo la jumla na hakuna ukweli ambao unafaa kwa kuingia watu wote. Matakwa mengi yanawekwa kwa watu wakitakiwa kufanya kile ambacho ni nje ya uwezo wao, kumwingiza bata katika kitulio cha ndege. Hii ni kazi ya matakwa ya binadamu. Tabia ya upotovu ya mwanadamu, mawazo yake na mitazamo vinaenea katika sehemu zote za mwili wake. Mwanadamu hakuzaliwa na tabia ya kutenda ukweli, na wala hana tabia ya kuuelewa ukweli moja kwa moja. Vikiwekwa pamoja na tabia potovu ya mwanadamu, aina hii ya mtu asili inapofanya kazi, je, si huu ni mvurugano? Lakini mwanadamu ambaye amekamilishwa ana uzoefu wa ukweli ambao watu wanapaswa kuuelewa, na maarifa ya tabia yao ya dhambi, ili kwamba vitu visivyoeleweka vizuri na visivyokuwa halisi vipotee kwa taratibu, ikiwa na maana kwamba ukweli alioudhihirisha unakuwa sahihi zaidi na halisi. Mawazo katika akili ya mwanadamu yanazuia kazi ya Roho Mtakatifu. Mwanadamu ana dhana nzuri, mantiki ya maana na uzoefu mkongwe katika kukabiliana na mambo. Kama haya yote hayatapitia kupogolewa na kusahihishwa, yote yanakuwa vizuizi katika kazi. Hivyo kazi ya mwanadamu haiwezi kufikia kiwango cha juu cha usahihi, hususan kazi ya watu ambao hawajakamilishwa.
Zaidi: Kwa Nini Umeme wa Mashariki Unaenda Mbele Kwa Mwendo Usioweza Kukomeshwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni