Kazi ya mwanadamu ina mipaka na kadiri inavyoweza kufika. Mtu mmoja anaweza kufanya kazi ya wakati fulani na hawezi kufanya kazi ya enzi nzima—vinginevyo anaweza kuwaongoza watu katika kanuni. Kazi ya mwanadamu inaweza kufaa tu katika kipindi au awamu fulani. Hii ni kwa sababu uzoefu wa mwanadamu una mipaka. Mtu hawezi kulinganisha kazi ya mwanadamu na kazi ya Mungu. Namna mwanadamu anavyofanya mambo na maarifa yake ya ukweli yote yanatumika tu katika mawanda fulani. Huwezi kusema kwamba njia ambayo mwanadamu anaiendea ni matakwa ya Roho Mtakatifu kabisa, kwa sababu mwanadamu anaweza kupewa nuru na Roho Mtakatifu tu na hawezi kujazwa kikamilifu na Roho Mtakatifu.
Vitu ambavyo mwanadamu anaweza kuvipitia vyote vipo ndani ya mawanda ya ubinadamu na haviwezi kuzidi mawanda ya fikra katika akili ya kawaida ya mwanadamu. Wale wote wenye udhihirisho halisi wanapitia uzoefu ndani ya mawanda haya. Wanapoupitia ukweli, siku zote ni uzoefu wa maisha ya kawaida ya mwanadamu chini ya nuru ya Roho Mtakatifu, sio kupitia uzoefu kwa namna ambayo inakengeuka kutoka kwa maisha ya kawaida ya mwanadamu. Wanapitia uzoefu wa ukweli ambao unatiwa nuru na Roho Mtakatifu katika msingi wa kuishi maisha yao ya kibinadamu. Aidha, ukweli huu unatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, na kina chake kinahusiana na hali ya mtu huyo. Mtu anaweza kusema kwamba njia wanayoipitia ni maisha ya kawaida ya kibinadamu ya mwanadamu kuutafuta ukweli na kwamba hiyo ndiyo njia ambayo mtu wa kawaida ambaye amepata nuru ya Roho Mtakatifu anaipita. Huwezi kusema kwamba njia wanayoipitia ni njia ambayo imechukuliwa na Roho Mtakatifu. Katika uzoefu wa kawaida wa kibinadamu, kwa sababu watu wanaoutafuta ukweli hawafanani, kazi ya Roho Mtakatifu pia haifanani. Aidha, kwa sababu mazingira wanayoyapitia na kiwango cha uzoefu wao havifanani, kwa sababu ya mchanganyiko wa akili na mawazo yao, uzoefu wao pia umechanganyika kwa kiwango tofauti. Kila mtu anaelewa ukweli kulingana na hali yake tofauti ya kibinafsi. Uelewa wao wa maana halisi ya ukweli hauko kamili, na ni kipengele chake kimoja tu au vichache. Mawanda ambayo ukweli unaeleweka kwa mwanadamu siku zote umejikita katika hali tofauti tofauti za watu, na hivyo hazifanani. Kwa njia hii, maarifa yanayodhihirisha ukweli ule ule na watu tofauti hayafanani. Hii ni sawa na kusema, uzoefu wa mwanadamu siku zote una mipaka, na hauwezi kuwakilisha kikamilifu matakwa ya Roho Mtakatifu, na kazi ya mwanadamu haiwezi kuchukuliwa kama kazi ya Mungu, hata kama kile kinachodhihirishwa na mwanadamu kinafanana kwa karibu sana na mapenzi ya Mungu, hata kama uzoefu wa mwanadamu unakaribiana sana na kazi ya ukamilifu itakayofanywa na Roho Mtakatifu. Mwanadamu anaweza kuwa tu mtumishi wa Mungu, akifanya kazi ambayo Mungu amemkabidhi. Mwanadamu anaweza kudhihirisha maarifa tu chini ya nuru ya Roho Mtakatifu na ukweli alioupata kutokana na uzoefu wake binafsi. Mwanadamu hana sifa na hana vigezo vya kuwa njia ya Roho Mtakatifu. Hana uwezo wa kusema kuwa kazi ya mwanadamu ni kazi ya Mungu. Mwanadamu ana kanuni za kufanya kazi za mwanadamu, na wanadamu wote wana uzoefu tofauti na wana hali zinazotofautiana. Kazi ya mwanadamu inajumuisha uzoefu wake wote chini ya nuru ya Roho Mtakatifu. Uzoefu huu unaweza tu kuwakilisha asili ya mwanadamu na hauwakilishi asili ya Mungu, au mapenzi ya Roho Mtakatifu. Kwa hivyo, njia anayoipita mwanadamu haiwezi kusemwa kuwa njia anayoipita Roho Mtakatifu, kwa sababu kazi ya mwanadamu haiwezi kuwakilisha kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu na uzoefu wa mwanadamu sio matakwa ya Roho Mtakatifu. Kazi ya mwanadamu ina hatari ya kuangukia katika kanuni, na mbinu za kazi yake zimefinywa katika uelewa wake finyu na hawezi kuwaongoza watu katika njia huru. Wafuasi wengi wanaishi ndani ya mawanda finyu, na uzoefu wao pia unakuwa ni finyu. Uzoefu wa mwanadamu siku zote ni finyu; mbinu ya kazi yake pia ni finyu na haiwezi kulinganishwa na kazi ya Roho Mtakatifu au kazi ya Mungu mwenyewe—hii ni kwa sababu uzoefu wa mwanadamu, hatimaye, ni finyu. Hata hivyo Mungu anafanya kazi Yake, hakuna kanuni kwa kazi yake; vyovyote vile inavyofanywa, haifungwi na njia moja. Hakuna kanuni za aina yoyote ile katika kazi ya Mungu, kazi Yake yote inatolewa kwa uhuru. Haijalishi ni muda kiasi gani mwanadamu anatumia kumfuata Yeye, hawawezi kutengeneza sheria zozote za njia anavyofanya kazi. Ingawaje kazi Yake inaongozwa na kanuni, siku zote inafanywa katika njia mpya na siku zote inakuwa na maendeleo mapya ambayo ni nje ya uwezo wa mwanadamu. Katika kipindi fulani, Mungu anaweza kuwa na njia nyingi tofauti tofauti za kazi na njia tofauti za kuongoza, akiruhusu watu siku zote kuwa na kuingia kupya na mabadiliko mapya. Huwezi kuelewa sheria za kazi Yake kwa sababu siku zote anafanya kazi katika njia mpya. Ni kwa njia hii tu ndiyo wafuasi wa Mungu hawawezi kuanguka katika kanuni. Kazi ya Mungu Mwenyewe siku zote inaepuka mitazamo ya watu na kupinga mitazamo yao. Ni wale tu ambao wanamfuata Yeye kwa moyo wote ndio wanaoweza kubadilishwa tabia zao na wanaweza kuishi kwa uhuru bila kuwa chini ya kanuni zozote au kufungwa na mitazamo yoyote ya kidini. Madai ambayo kazi ya mwanadamu inawawekea watu yamejikita katika uzoefu wake mwenyewe na kile ambacho yeye mwenyewe anaweza kutimiza. Kiwango cha matakwa haya kimejifunga ndani ya mawanda fulani, na mbinu za kutenda pia ni finyu sana. Kwa hivyo wafuasi bila kutambua huishi ndani ya matakwa finyu; kadri muda unavyokwenda, yanakuwa kanuni na taratibu za kidini. Ikiwa kazi ya kipindi fulani kinaongozwa na mtu ambaye hajapitia kukamilishwa na Mungu na hakupokea hukumu, wafuasi wake wote watakuwa wadini na wataalamu wa kumpinga Mungu. Kwa hivyo, ikiwa mtu fulani ni kiongozi aliyehitimu, mtu huyo anapaswa kuwa amepitia hukumu na kukubali kukamilishwa. Wale ambao hawajapitia mchakato wa hukumu, hata kama wanaweza kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, wanadhihirisha vitu ambavyo havieleweki na visivyokuwa halisi. Kadri muda unavyozidi kwenda, watawaongoza watu katika kanuni zisizoeleweka vizuri na za kimuujiza. Kazi ambayo Mungu anaifanya haiambatani na mwili wa mwanadamu; haiambatani na mawazo ya mwanadamu bali inapinga mitazamo ya mwanadamu; haijachanganywa na mitazamo ya kidini isiyoeleweka vizuri. Matokeo ya kazi Yake hayawezi kupatikana kwa mwanadamu ambaye hajakamilishwa Naye na yapo nje ya uwezo wa fikira za mwanadamu.
Kazi katika akili ya mwanadamu inafikiwa kwa urahisi sana na mwanadamu. Wachungaji na viongozi katika ulimwengu wa kidini, kwa mfano, wanategemea karama zao na nafasi zao katika kufanya kazi zao. Watu wanaowafuata kwa muda mrefu wataambukizwa na karama zao na kuvutwa na vile walivyo. Wanalenga karama za watu, uwezo na maarifa ya watu, na wanamakinikia mambo ya kimiujiza na mafundisho mengi yasiyokuwa na uhalisi (kimsingi, haya mafundisho hayawezi kutekelezeka). Hawalengi mabadiliko ya tabia za watu, badala yake wanalenga kuwafundisha watu uwezo wao wa kuhubiri na kufanya kazi, kuboresha maarifa ya watu na mafundisho makuu ya kidini. Hawalengi kuona ni kwa kiasi gani tabia ya watu imebadilika au ni kwa kiasi gani watu wanauelewa ukweli. Wala hawajali utu wa watu, wala kujua hali za watu za kawaida na zisizo za kawaida. Hawapingi mitazamo ya watu au kufunua mitazamo yao, achilia mbali kurekebisha hali yao ya dhambi. Watu wengi wanaowafuata wanahudumia kwa karama zao za asili, na kile wanachokidhihirisha ni maarifa na ukweli wa kidini usioeleweka, ambayo ni nje ya mguso wa uhalisia na kuwapatia watu uzima. Kimsingi, kiini cha kazi yao ni kulea talanta, kumlea mtu kuwa mhitimu mwenye talanta aliyemaliza mafunzo ya kidini ambaye baadaye anakwenda kufanya kazi na kuongoza. Kwa miaka elfu sita ya kazi ya Mungu unaweza kupata sheria zozote kuihusu? Kuna kanuni na mibano mingi katika kazi ambayo mwanadamu hufanya, na ubongo wa mwanadamu umejazwa na mafundisho mengi ya kidini. Hivyo mwanadamu anachokidhihirisha ni kiasi cha maarifa na utambuzi ndani ya uzoefu wake wote. Mwanadamu hawezi kudhihirisha kitu chochote zaidi ya hiki. Uzoefu au maarifa ya mwanadamu hayaibuki kutoka ndani ya karama zake za ndani au tabia yake; vinaibuka kwa sababu ya uongozi wa Mungu na uchungaji wa moja kwa moja wa Mungu. Mwanadamu ana ogani tu ya kupokea uongozi huu na sio ogani ya kudhihirisha moja kwa moja uungu. Mwanadamu hana uwezo wa kuwa chanzo, anaweza kuwa tu chombo ambacho hupokea maji kutoka kwa chanzo; hii ndiyo tabia ya mwanadamu, ogani ambayo mtu anapaswa kuwa nayo kama mwanadamu. Ikiwa mtu anapoteza ogani ya kukubali neno la Mungu na kupoteza tabia ya kibinadamu, mtu huyo anapoteza pia kile ambacho ni cha thamani sana, na anapoteza wajibu wa mwanadamu aliyeumbwa. Ikiwa mtu hana maarifa au uzoefu wa neno la Mungu au kazi Yake, mtu huyo anapoteza wajibu wake, wajibu anaopaswa kuutimiza kama kiumbe aliyeumbwa, na kupoteza heshima ya kiumbe aliyeumbwa. Ni tabia ya Mungu kudhihirisha uungu ni nini, kama unadhihirishwa katika mwili au moja kwa moja na Roho Mtakatifu; hii ni huduma ya Mungu. Mwanadamu anadhihirisha uzoefu wake mwenyewe au maarifa (yaani, anadhihirisha kile alicho) wakati wa kazi ya Mungu au baada yake; hii ndiyo tabia ya mwanadamu na wajibu wa mwanadamu, ndicho kitu ambacho mwanadamu anapaswa kukifikia. Ingawa udhihirishaji wa mwanadamu ni duni sana kuliko kile ambacho Mungu anadhihirisha, na kuna kanuni nyingi katika kile ambacho mwanadamu hudhihirisha, mwanadamu anapaswa kutimiza wajibu anaopaswa kutimiza na kufanya kile anachopaswa kufanya. Mwanadamu anapaswa kufanya kitu chochote kinachowezekana kwa mwanadamu kufanya ili kutimiza wajibu wake, na hapaswi kuacha kitu hata kidogo.
Baada ya kufanya kazi kwa miaka mingi, mwanadamu atakuwa na uzoefu wa miaka hii yote, vile vile atakuwa na hekima na kanuni alizozipata. Mtu anayefanya kwa muda mrefu anajua jinsi ya kuelewa mizunguko ya Roho Mtakatifu, anajua ni wakati gani Roho Mtakatifu anafanya kazi na wakati gani Hafanyi; anajua jinsi ya kufanya ushirika akiwa amebeba mzigo, anaitambua hali ya kawaida ya kazi ya Roho Mtakatifu na hali ya kawaida ya ukuaji wa watu katika uzima. Huyo ni mtu ambaye amefanya kazi kwa miaka mingi na anaijua kazi ya Roho Mtakatifu. Wale ambao wamefanya kazi kwa muda mrefu wanazungumza kwa uhakika na bila haraka; hata wakati ambapo hawana kitu cha kusema wanakuwa watulivu. Kwa ndani, wanaweza kuendelea kuomba ili kupata kazi ya Roho Mtakatifu bila wasiwasi au dukuduku; wana uzoefu katika kufanya kazi. Mtu ambaye amefanya kazi kwa muda mrefu na ana masomo na uzoefu mkubwa ana vitu vingi ndani ambavyo vinazuia kazi ya Roho Mtakatifu; hii ni dosari ya kufanya kazi kwa muda mrefu. Mtu ambaye ndio anaanza tu kufanya kazi hajaleta katika kazi masomo au uzoefu wa kibinadamu, hususan kuhusu jinsi ambavyo Roho Mtakatifu anafanya kazi. Hata hivyo, wakati wa kufanya kazi, taratibu anaanza kuelewa jinsi ambavyo Roho Mtakatifu anafanya kazi na anakuwa na utambuzi wa jinsi ya kufanya ili kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu na jinsi ya kufanya ili kugusa sehemu muhimu za wengine. Anakuja kuwa na uelewa wa kawaida ambao wale wanaofanya kazi wanapaswa kuwa nao. Kadri muda unavyokwenda, anapata kujua hekima hiyo na maarifa ya kawaida kuhusu kufanya kazi kwa ufasaha mkubwa sana, na anaonekana kuyatumia kwa urahisi anapofanya kazi. Hata hivyo, Roho Mtakatifu anapobadilisha namna Anavyofanya kazi, bado anakuwa amejikita katika maarifa yake ya zamani ya kufanya kazi na kanuni zake za zamani za kufanya kazi na anajua kidogo sana kuhusu harakati mpya za kufanya kazi. Miaka mingi ya kufanya kazi na kuwa katika uongozi na uwepo kamili wa Roho Mtakatifu kunampatia masomo mengi zaidi ya kufanya kazi na uzoefu mwingi. Vitu hivyo vinamjaza kujiamini ambako sio kiburi. Kwa maneno mengine, anafurahishwa kabisa na kazi yake mwenyewe na kuridhika sana na maarifa ya kawaida aliyoyapata kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa umahususi, vitu vile ambavyo watu wengine hawakuvipata au kuvitambua vinampatia kujiamini zaidi kwa nafsi yake; inaonesha kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ndani yake haiwezi kuzimwa kamwe, na wengine hawana sifa ya kutendewa hivi. Watu wa aina hii ambao wamefanya kazi kwa miaka mingi na ambao wameitumia thamani ndio wana sifa ya kuifurahia. Vitu hivi vinakuwa ni kikwazo kikubwa katika kukubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu. Hata kama anaweza kuikubali kazi mpya, si kitu cha kuibuka mara moja. Kwa uhakika atapitia michakato kadhaa kabla ya kuikubali. Hali hii inaweza kugeuka taratibu baada ya mitazamo yake ya zamani kushughulikiwa na tabia yake ya zamani kuhukumiwa. Bila ya kupitia hatua hizi, habadiliki na kukubali kwa urahisi mafundisho mapya na kazi ambayo haikubaliani na mitazamo yake ya zamani. Hii ndiyo sehemu ngumu sana ya kushughulika nayo katika mwanadamu, na sio rahisi kuibadilisha. Ikiwa, kama mtenda kazi, ana uwezo wa kupata na kuielewa kazi ya roho Mtakatifu na kuutambua mchakato wake, vile vile ana uwezo wa kutozuiwa na uwezo wake wa kufanya kazi na kuwa na uwezo wa kuikubali kazi mpya katika mwanga wa kazi ya zamani, ni mtu mwenye hekima na mtenda kazi mwenye sifa. Wanadamu mara nyingi wanafanya kazi kwa miaka mingi bila kutafakari uwezo wao wa kufanya kazi, au wanashindwa kukubali kazi mpya baada ya kutafakari uzoefu wao wa kufanya kazi na hekima na hawawezi kuelewa kwa usahihi au kuishughulikia kwa usahihi kazi ya zamani na mpya. Wanadamu hakika ni wagumu kuwaongoza! Wengi wenu mko hivi. Wale ambao wamepitia uzoefu wa miaka katika kazi ya Roho Mtakatifu wanaona vigumu kuikubali kazi mpya, mara nyingi wanakuwa wamejazwa mitazamo ambayo wanaona ni vigumu kuiacha, ilhali mtu ambaye ndio ameanza tu kazi anakosa maarifa ya kawaida ya kufanya kazi na hajui hata jinsi ya kushughulikia masuala rahisi kabisa. Nyinyi watu ni wagumu kweli kweli! Wale wenye vyeo fulani nyuma yao wana kiburi na majivuno kweli kiasi kwamba wamesahau kule walikotoka. Siku zote wanawadharau wadogo, ila bado hawawezi kukubali kazi mpya na hawawezi kuachana na mitazamo waliyoikusanya na kuiweka kwa miaka mingi sana. Ingawa hao watu wadogo wasiokuwa na maarifa wanaweza kukubali kiasi kidogo cha kazi ya Roho Mtakatifu na wana shauku kubwa, mara zote wanakuwa wanatatanika na hawajui cha kufanya wanapokutana na matatizo. Ingawa wana shauku, wao ni wajinga mno. Wana uelewa mdogo tu wa kazi ya Roho Mtakatifu na hawawezi kuutumia katika maisha yao; huwa ni mafundisho tu ambayo hayana maana kabisa. Kuna watu wengi kama wewe; ni wangapi wanafaa kwa ajili ya kutumika? Ni wangapi wanaoweza kufanya kile kinachofaa kwa ajili ya Roho Mtakatifu? Inaonekana kwamba mmekuwa watiifu sana hadi sasa, lakini kwa kweli, hamjaachana na mitazamo yenu, bado mnatafuta kwenye Biblia, mkiamini mambo yasiyo dhahiri, au kuhangaika katika mitazamo. Hakuna yeyote ambaye huchunguza kazi halisi ya leo au kuzama ndani yake. Mnaikubali njia ya leo kwa mitazamo yenu ya zamani. Mtafaidika vipi na imani kama hiyo? Ingeweza kusemwa kuwa ndani yenu mmefichwa mitazamo mingi ambayo haijafunuliwa, na kwamba mnafanya tu jitihada kubwa kuificha na msiweze kuifunua kwa urahisi. Hamkubali kazi mpya kwa uaminifu na hampangi kuachana na mitazamo yenu ya zamani; mna falsafa nyingi sana za maisha za kusikitisha. Hamuachi mitazamo yenu ya zamani na kwa shingo upande mnashughulika na kazi mpya. Mioyo yenu ni miovu sana, na hamchukui hatua ya kazi mpya katika moyo. Mtu mzembe kama nyinyi anaweza kufanya kazi ya kueneza injili? Mnaweza kuchukua kazi mpya ya kueneza injili katika ulimwengu mzima? Matendo yenu haya yanawazuia kubadilisha tabia yenu na kumjua Mungu. Ikiwa mtaendelea hivi, mwisho wake mtaondolewa.
Mnapaswa kujua jinsi ya kutofautisha kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Unaweza kuona nini katika kazi ya mwanadamu? Kuna vitu vingi ambavyo ni uzoefu wa mwanadamu katika kazi ya mwanadamu; kile ambacho mwanadamu anakidhihirisha ndivyo hivyo alivyo. Kazi ya Mungu pia inadhihirisha vile Alivyo, lakini vile Alivyo ni tofauti na mwanadamu alivyo. Kile mwanadamu alicho ni kiwakilishi cha uzoefu na maisha ya mwanadamu (kile ambacho mwanadamu anakipitia au kukabiliana nacho katika maisha yake, au falsafa za maisha alizo nazo), na watu wanaoishi katika mazingira tofauti hudhihirisha utu tofauti. Kama una uzoefu wa kijamii au la na jinsi ambavyo unaishi na kupitia uzoefu katika familia yako inaweza kuonekana katika kile unachokidhihirisha, wakati ambapo huwezi kuona kutoka kwa kazi ya Mungu mwenye mwili kama Ana uzoefu wa maisha ya kijamii au Hana. Anatambua vizuri asili ya mwanadamu, Anaweza kufunua aina ya matendo yote yanayohusiana na kila aina ya watu. Ni mzuri pia katika kufunua tabia ya dhambi ya mwanadamu na tabia yake ya uasi. Haishi miongoni mwa watu wa kidunia, lakini Anatambua asili ya watu wenye mwili wa kufa na upotovu wote wa watu wa duniani. Hivi ndivyo Alivyo. Ingawa Hashughuliki na dunia, Anajua kanuni za kushughulika na dunia, kwa sababu Anaielewa vizuri asili ya mwanadamu. Anajua kuhusu kazi ya Roho ambayo jicho la mwanadamu haliwezi kuiona na kwamba masikio ya mwanadamu hayawezi kusikia, wanadamu wa leo na wanadamu wa enzi zote. Hii inajumuisha hekima ambayo sio falsafa ya maisha na makuu ambayo watu hupata ugumu kuelewa. Hiki ndicho Alicho, kuwa wazi kwa watu na pia kufichika kwa watu. Kile anachokidhihirisha sio kile ambacho mwanadamu asiye wa kawaida alivyo, bali ni tabia za asili na uungu wa Roho. Hasafiri ulimwengu mzima lakini anajua kila kitu kuhusu ulimwengu. Anawasiliana na "sokwe" ambao hawana maarifa au akili, lakini Anadhihirisha maneno ambayo ni ya kiwango cha juu kuliko maarifa na juu ya watu wakubwa duniani. Anaishi miongoni mwa kundi la wanadamu wapumbavu na wasiojali ambao hawana utu na ambao hawaelewi mila na desturi za ubinadamu na maisha, lakini Anaweza kumwambia mwanadamu kuishi maisha ya kawaida, na kwa wakati uo huo kufichua msingi na uduni wa utu wa mwanadamu. Haya yote ndiyo Alivyo, mkuu kuliko vile ambavyo mwanadamu yeyote wa damu na nyama alivyo. Kwake Yeye, si lazima kupitia uzoefu wa maisha ya kijamii magumu na changamani, ili Aweze kufanya kazi Anayotaka kufanya na kwa kina kufichua asili ya mwanadamu aliyepotoka. Maisha duni ya kijamii ambayo ni machafu hayauadilishi mwili Wake. Kazi Yake na maneno Yake hufichua tu kutotii kwa mwanadamu na hayampatii mwanadamu uzoefu na masomo kwa ajili ya kushughulika na ulimwengu. Hahitaji kuipeleleza jamii au familia ya mwanadamu wakati Anapompatia mwanadamu uzima. Kumweka wazi na kumhukumu wanadamu sio udhihirisho wa uzoefu wa mwili Wake; ni kufunua vile mwanadamu asivyokuwa na haki baada ya kufahamu kutotii kwa mwanadamu na kuchukia upotovu wa mwanadamu. Kazi yote Anayoifanya ni kufunua tabia Yake kwa mwanadamu na kudhihirisha asili Yake. Ni Yeye tu ndiye anayeweza kuifanya kazi hii, sio kitu ambacho mtu mwenye mwili na damu anaweza kukipata. Kwa kuangalia kazi Yake, mwanadamu hawezi kuelezea Yeye ni mtu wa aina gani. Mwanadamu hawezi kumwainisha kama mtu aliyeumbwa kwa misingi ya kazi Yake. Kile Alicho pia kinamfanya Asiweze kuainishwa kama mtu aliyeumbwa. Mwanadamu anaweza kumwona tu kama Asiye mwanadamu, lakini hajui amuainishe kwa kundi gani, kwa hivyo mwanadamu analazimika kumuainisha katika kundi la Mungu. Inaleta maana kwa mwanadamu kufanya hivi, kwa sababu Amefanya kazi kubwa miongoni mwa watu, ambayo mwanadamu hawezi kufanya.
Kazi ambayo Mungu anafanya haiwakilishi uzoefu wa mwili Wake; kazi ambayo mwanadamu anafanya inawakalisha uzoefu wa mwanadamu. Kila mtu anazungumza juu ya uzoefu wake binafsi. Mungu Anaweza kuonyesha ukweli moja kwa moja, wakati mwanadamu anaweza tu kuonyesha uzoefu unaolingana na huo baada ya kupata uzoefu wa ukweli. Kazi ya Mungu haina masharti na haifungwi na muda au mipaka ya kijiografia. Anaweza kudhihirisha kile Alicho wakati wowote, mahali popote. Anafanya kazi vile Anavyopenda. Kazi ya mwanadamu ina masharti na muktadha; vinginevyo hana uwezo wa kufanya kazi na hawezi kudhihirisha uelewa wake wa Mungu au uzoefu wake wa ukweli. Unatakiwa tu kulinganisha tofauti baina yao ili kuonyesha kama ni kazi ya Mungu mwenyewe au kazi ya mwanadamu. Kama hakuna kazi inayofanywa na Mungu Mwenyewe, na kuna kazi tu ya mwanadamu, utajua kwamba mafundisho ya mwanadamu ni makuu, zaidi ya uwezo wa mtu yeyote yule; toni yao ya kuzungumza, kanuni zao katika kushughulikia mambo na uwezo wao katika kufanya kazi ni zaidi ya uwezo wa wengine. Nyinyi wote mnawatamani watu hawa wenye ubinadamu wa juu, lakini huwezi kuona kutoka katika kazi na maneno ya Mungu jinsi ubinadamu Wake ulivyo wa juu. Badala yake, Yeye ni wa kawaida, na Anapofanya kazi, Yeye ni wa kawaida na halisi lakini pia hapimiki kwa watu wenye mwili wa kufa, kitu ambacho kinawafanya watu wahisi kumheshimu sana. Pengine uzoefu wa mtu katika kazi yake ni mkubwa sana, au dhana na fikra zake ni za juu sana, na ubinadamu wake ni mzuri hasa; hivi vinaweza kutamaniwa na watu tu, lakini visiamshe kicho na hofu yao. Watu wote wanawatamani wale ambao wana uwezo wa kufanya kazi na ambao wana uzoefu wa kina na wanaweza kuutenda ukweli, lakini hawawezi kuvuta kicho, bali kutamani na kijicho. Lakini watu ambao wamepitia uzoefu wa kazi ya Mungu hawamtamani Mungu, badala yake wanahisi kwamba kazi Yake haiwezi kufikiwa na mwanadamu na haiwezi kueleweka na mwanadamu, na kwamba ni nzuri na ya kushangaza. Watu wanapopitia uzoefu wa kazi ya Mungu, uelewa wao wa kwanza kuhusu Yeye ni kwamba Hawezi kueleweka, ni mwenye hekima na wa ajabu na wanamheshimu bila kujitambua na kuihisi siri ya kazi Anayoifanya, ambayo inapita akili ya mwanadamu. Watu wanataka tu kuwa na uwezo wa kukidhi matakwa Yake, kuridhisha matamanio Yake; hawatamani kumpita Yeye, kwa sababu kazi anayoifanya inakwenda zaidi ya fikra za mwanadamu na haiwezi kufanywa na mwanadamu kama mbadala. Hata mwanadamu mwenyewe hayajui mapungufu yake, wakati Amefungua njia mpya na kumleta mwanadamu katika dunia mpya zaidi na nzuri zaidi, ili mwanadamu awe na mwendelezo mpya na kuwa na mwanzo mpya. Kile ambacho mwanadamu anakihisi kwa ajili Yake, sio matamanio, au sio matamanio tu. Uzoefu wao wa kina ni kicho na upendo, hisia zao ni kwamba Mungu kweli ni wa ajabu sana. Anafanya kazi ambayo mwanadamu hawezi kufanya, Husema vitu ambavyo mwanadamu hawezi kuvisema. Watu ambao wamepitia uzoefu wa kazi Yake siku zote hupitia uzoefu wa hisia isiyoweza kuelezeka. Watu wenye uzoefu wa kina hasa wanampenda Mungu. Siku zote wanahisi upendo Wake, wanahisi kwamba kazi Yake ni ya hekima sana, ni ya kushangaza sana, na hivyo hii inazalisha nguvu isiyokoma ndani yao. Si woga au upendo wa mara moja moja na heshima, bali hisia za ndani za upendo wa Mungu na uvumilivu kwa mwanadamu. Hata hivyo, watu ambao wamepata uzoefu wa kuadibu Kwake na hukumu wanamhisi Yeye kuwa mtukufu na wa heshima. Hata watu ambao wamepitia uzoefu mkubwa wa kazi Yake pia hawawezi kumwelewa; watu wote wanaomheshimu wanajua kwamba kazi Yake hailingani na mitazamo ya watu lakini siku zote inakwenda kinyume na mitazamo yao. Haihitaji watu kumtamani kabisa au kuwa na mwonekano wa kujikabidhi Kwake, badala yake anataka wawe na heshima ya kweli na kujikabidhi kikamilifu. Katika nyingi ya kazi Yake, mtu yeyote mwenye uzoefu wa kweli anahisi heshima Kwake, ambayo ni ya juu kuliko matamanio. Watu wameiona tabia Yake kwa sababu ya kazi Yake ya kuadibu na hukumu, na kwa hiyo wanamcha mioyoni mwao. Mungu anapaswa kuchiwa na kutiiwa, kwa sababu uungu Wake na tabia Yake havifanani kama ule wa watu walioumbwa na vikuu juu ya vile vya watu walioumbwa. Mungu sio kiumbe Aliyeumbwa, na ni Yeye tu anayestahili kuchiwa na heshima na taadhima; mwanadamu hana sifa ya kupewa hivi. Hivyo, watu wote waliopitia uzoefu wa kazi Yake na kweli wanamjua wanampatia heshima. Hata hivyo, wale ambao hawaachani na mitazamo yao kuhusu Yeye, yaani, wale ambao hawamwoni Yeye kuwa Mungu, hawana uchaji wowote Kwake, na hata kama wanamfuata hawajashindwa; ni watu wasiotii kwa asili yao. Anafanya kazi hii ili kupata matokeo kwamba viumbe vyote vilivyoumbwa vinaweza kumcha Muumbaji, vimwabudu Yeye, na kujikabidhi katika utawala Wake bila masharti. Haya ni matokeo ya mwisho ambayo kazi Yake yote inalenga kuyapata. Ikiwa watu ambao wamepitia kazi hiyo hawamheshimu Mungu, hata kidogo, kama kutotii kwao kwa zamani hakutabadilika kabisa, basi watu hawa ni hakika wataondolewa. Kama mtazamo wa mwanadamu kwa Mungu ni kumtamani au kuonyesha heshima kwa mbali na sio kumpenda, hata kidogo, hivi ndivyo mtu bila moyo wa kumpenda Mungu anapofikia, na mtu wa aina hiyo anakosa hali za kumwezesha kukamilishwa. Ikiwa kazi kubwa sana hivi inashindwa kupata upendo wa kweli wa mtu, hii ina maana kwamba mtu huyo hajampata Mungu na kwa uhalisia hatafuti kuujua ukweli. Mtu ambaye hampendi Mungu hapendi ukweli na hivyo hawezi kumpata Mungu, achilia mbali kupata ukubali wa Mungu. Watu kama hao, bila kujali ni kwa kiasi gani wanapata uzoefu wa Roho Mtakatifu, na bila kujali jinsi gani wanapitia uzoefu wa hukumu, bado hawawezi kumcha Mungu. Hawa ni watu ambao asili yao haiwezi kubadilishwa, ambao wana tabia ya uovu uliokithiri. Wale wote ambao hawamchi Mungu wataondolewa, na kuwa walengwa wa hukumu, na kuadhibiwa kama tu wale ambao wanafanya uovu, watateseka hata zaidi ya wale ambao wamefanya matendo ambayo si ya haki.
Tufuate: Kanisa la Mwenyezi Mungu Lilikujaje Kuwepo?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni