Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Hatua-Tatu-za-Kazi-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Hatua-Tatu-za-Kazi-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 28 Desemba 2019

Kujua madhumuni na Umuhimu wa Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu

(1) Lengo na umuhimu wa kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake. Israeli ni mahali ambapo Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka katika mavumbi ya mahali hapo Yehova alimuumba mwanadamu; mahali hapa pakawa kituo cha kazi Yake duniani. Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa ukoo wa Adamu, walikuwa msingi wa kibinadamu wa kazi ya Yehova duniani.

Jumanne, 24 Desemba 2019

Jua madhumuni ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu

Maneno Husika ya Mungu:

Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.

Ijumaa, 13 Desemba 2019

Wimbo wa Maneno ya Mungu Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi

Kanisa la Mwenyezi Mungu

I
Mungu ana mpango wa usimamizi wa miaka 6,000,
uliyogawanywa katika hatua tatu,
kila moja inaitwa enzi.
Kwanza ni Enzi ya Sheria, kisha Enzi ya Neema,
na Enzi ya Ufalme ni awamu ya mwisho.
Ingawa kazi ya Mungu ni tofauti katika kila moja,
yote inalingana na kile ambacho binadamu wanahitaji,
ama hasa inalingana na ujanja ambao Shetani anatumia,
anapopigana na Yeye.

Jumamosi, 19 Oktoba 2019

Ni jinsi gani hatua tatu za kazi ya Mungu kwa pole pole huongeza uketo ili watu waokolewe na kukamilishwa?

4. Ni jinsi gani hatua tatu za kazi ya Mungu kwa pole pole huongeza uketo ili watu waokolewe na kukamilishwa?

Maneno Husika ya Mungu:
Usimamizi mzima wa Mungu umegawika katika hatua tatu, na katika kila hatua, mahitaji yanayofaa yanatakiwa kutoka kwa mwanadamu. Aidha, kadri enzi zinavyopita na kuendelea, mahitaji ya Mungu kwa wanadamu wote huwa ya juu hata zaidi. Kwa hiyo, hatua kwa hatua, kazi hii ya usimamizi wa Mungu hufikia kilele chake, hadi mwanadamu aamini ukweli wa “kuonekana kwa Neno katika mwili,”