Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Huruma-na-uvumilivu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Huruma-na-uvumilivu. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 14 Julai 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza”



Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza”

Mwenyezi Mungu anasema, “Wanadamu, walioacha ruzuku ya uzima kutoka kwa mwenye Uweza, hawajui kwa nini wanaishi, na bado wanaogopa kifo. Hukuna usaidizi, hakuna msaada, lakini bado wanadamu wanasita kufumba macho yao, wakiyakabili yote bila woga, wanaendeleza kwa muda mrefu kuishi kwa aibu ulimwenguni humu katika miili isiyokuwa na utambuzi wa nafsi. Unaishi hivyo, pasipo matumaini; anaishi hivyo, pasipo kuwa na lengo. Kuna aliye Mtakatifu tu katika hekaya atakayekuja kuwaokoa wale wanaoomboleza kwa maumivu na wanatamani sana majilio Yake.

Jumatatu, 5 Februari 2018

Tabia ya Haki ya Mungu | (II)Ubinadamu Hupata Kibali cha Huruma na Uvumilivu wa Mungu Kupitia kwa Toba ya dhati

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia,
Neno la Mungu lilimjia Yona kwa mara ya kwanza

(II) Ubinadamu Hupata Kibali cha Huruma na Uvumilivu wa Mungu Kupitia kwa Toba ya dhati

Kinachofuata ni hadithi ya biblia ya “Wokovu wa Mungu kwa Ninawi.”

(Yona 1:1-2) Basi neno la BWANA lilimjia Yona mwana wa Amitai, likisema, Inuka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, upige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.
(Yona 3) Neno la BWANA likamjia Yona mara ya pili, likisema, Inuka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, uhubiri habari Ninayokuamuru. Basi Yona akainuka, akaenda Ninawi, kulingana na amri ya BWANA. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu. Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti, akasema, Baada ya siku arobaini mji wa Ninawi utaangamizwa. Basi watu wa Ninawi wakamwamini Mungu, wakatangaza kufunga, wakavaa nguo za magunia, kutoka Yule aliye mkubwa hadi aliye mdogo.