![]() |
| Neno la Mungu lilimjia Yona kwa mara ya kwanza |
(II) Ubinadamu Hupata Kibali cha Huruma na Uvumilivu wa Mungu Kupitia kwa Toba ya dhati
Kinachofuata ni hadithi ya biblia ya “Wokovu wa Mungu kwa Ninawi.”
(Yona 1:1-2) Basi neno la BWANA lilimjia Yona mwana wa Amitai, likisema, Inuka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, upige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.
(Yona 3) Neno la BWANA likamjia Yona mara ya pili, likisema, Inuka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, uhubiri habari Ninayokuamuru. Basi Yona akainuka, akaenda Ninawi, kulingana na amri ya BWANA. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu. Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti, akasema, Baada ya siku arobaini mji wa Ninawi utaangamizwa. Basi watu wa Ninawi wakamwamini Mungu, wakatangaza kufunga, wakavaa nguo za magunia, kutoka Yule aliye mkubwa hadi aliye mdogo.
