Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kuondoa-Ukungu-ili-kuona-Mwanga-wa-Kweli. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kuondoa-Ukungu-ili-kuona-Mwanga-wa-Kweli. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 27 Desemba 2019

Sura ya 21

Mwanadamu huanguka katikati ya mwanga Wangu, na anasimama imara kwa sababu ya wokovu Wangu. Niletapo wokovu ulimwenguni kote, mwanadamu hujaribu kutafuta njia za kuingia miongoni mwa mtiririko wa urejesho Wangu, ilhali kuna watu wengi ambao huoshwa wasijulikane waliko na gharika hili la urejesho; kuna watu wengi ambao wamezama na kumezwa na mafuriko haya ya maji; na kuna watu wengi pia ambao husimama imara huku kukiwa na mafuriko, ambao hawajawahi kupoteza hisia zao za mwelekeo, na ambao basi wamefuata mafuriko mpaka sasa. Ninaenda hatua kwa hatua na mwanadamu, lakini yeye hajawahi kunitambua; yeye anajua tu nguo Ninazovaa kwa nje, na hajui utajiri uliofichika ndani Mwangu. Ingawa Mimi humruzuku mwanadamu na kumpa kila siku, hana uwezo wa kukubali kwa kweli, hana uwezo wa kupokea utajiri wote niliompa. Hakuna jambo lolote kuhusu upotovu wa mwanadamu ambalo huniepuka;