Mwanadamu anaishi katikati ya mwanga, ilhali hana habari kuhusu thamani ya mwanga huo. Hana ufahamu kuhusu kiini cha mwanga huo, na chanzo cha mwanga huo, na, zaidi ya hayo, hajui mmiliki wake ni nani. Ninapotuza mwanga huo miongoni mwa binadamu, papo hapo Ninachunguza hali ilivyo miongoni mwa wanadamu: Kwa sababu ya mwanga huo, watu wote wanabadilika, na wanakua, na wametoka gizani. Ninaangalia kila pembe ya ulimwengu, na Ninaona kuwa milima yote imefunikwa na ukungu, kwamba maji yameganda kwa ajili ya baridi, na kwamba, kwa sababu ya kuja kwa mwanga, watu wanatazama Mashariki ili wapate kuona kitu kilicho na thamani zaidi—ilhali mwanadamu bado hana uwezo wa kutambua njia ya wazi kwenye ukungu huo. Kwa sababu dunia nzima imefunikwa kwa ukungu, Ninapotazama kutoka mawinguni, kuwepo Kwangu hakujawahi kutambuliwa na mwanadamu;
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kuijua-Sauti-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kuijua-Sauti-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Jumapili, 29 Desemba 2019
Ijumaa, 27 Desemba 2019
Sura ya 21
Mwanadamu huanguka katikati ya mwanga Wangu, na anasimama imara kwa sababu ya wokovu Wangu. Niletapo wokovu ulimwenguni kote, mwanadamu hujaribu kutafuta njia za kuingia miongoni mwa mtiririko wa urejesho Wangu, ilhali kuna watu wengi ambao huoshwa wasijulikane waliko na gharika hili la urejesho; kuna watu wengi ambao wamezama na kumezwa na mafuriko haya ya maji; na kuna watu wengi pia ambao husimama imara huku kukiwa na mafuriko, ambao hawajawahi kupoteza hisia zao za mwelekeo, na ambao basi wamefuata mafuriko mpaka sasa. Ninaenda hatua kwa hatua na mwanadamu, lakini yeye hajawahi kunitambua; yeye anajua tu nguo Ninazovaa kwa nje, na hajui utajiri uliofichika ndani Mwangu. Ingawa Mimi humruzuku mwanadamu na kumpa kila siku, hana uwezo wa kukubali kwa kweli, hana uwezo wa kupokea utajiri wote niliompa. Hakuna jambo lolote kuhusu upotovu wa mwanadamu ambalo huniepuka;
Ijumaa, 20 Desemba 2019
Jinsi ya kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu. Hivyo ndivyo alivyokuwa mwanzoni na Mungu” (Yohana 1:1-2).
“Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, aliyejawa neema na ukweli” (Yohana 1:14).
“Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu” (Yohana 14:6).
“Maneno ninayoongea kwenu ni roho, na ni uhai” (Yohana 6:63).
Jumatatu, 16 Desemba 2019
Sura ya 18
Katika mwako wa umeme, kila mnyama hufichuliwa katika hali yake halisi. Hivyo pia, kama wameangaziwa na mwanga Wangu, wanadamu wamepata tena utakatifu waliokuwa nao wakati mmoja. Oo, ya kwamba dunia potovu ya zamani mwishowe imeanguka na kutumbukia ndani ya maji ya taka na, kuzama chini ya maji, na kuyeyuka na kuwa tope! Ah, ya kwamba binadamu wote Niliouumba hatimaye umerudiwa na uhai tena katika mwanga, kupata msingi wa kuwepo, na kuacha kupambana katika tope! Ah, Mambo mengi ya uumbaji Ninayoyashikilia mikononi Mwangu! Wanawezaje, kukosa kufanywa upya, kupitia maneno Yangu?
Jumatatu, 9 Desemba 2019
Sura ya 17
Sauti Yangu inatoka kama radi, ikitia nuru roboduara zote nne na dunia nzima, na katikati ya radi na umeme, binadamu wanaangushwa chini. Hakuna mwanadamu aliyewahi kusimama imara katikati ya radi na umeme: Wanadamu wengi wanaogopa sana kuja kwa mwangaza Wangu na hawajui cha kufanya. Wakati mwangaza hafifu unaanza kuonekana Mashariki, watu wengi, wakiongozwa na huu mng’ao dhaifu, wanaamshwa mara moja kutoka kwa njozi zao. Lakini, hakuna aliyewahi kutambua kwamba siku imewadia mwangaza Wangu unaposhuka duniani.
Jumamosi, 7 Desemba 2019
Sura ya 16
Kuna mengi ambayo Natamani kumwambia mwanadamu, mambo mengi sana ambayo lazima Nimwambie. Lakini uwezo wa mwanadamu wa kukubali una upungufu mwingi: Hana uwezo wa kuyaelewa kabisa maneno Yangu kulingana na kile Ninachokitoa, na anaelewa kipengele kimoja tu lakini haelewi vingine. Lakini Simwangamizi mwanadamu kwa ajili ya ukosefu wake wa nguvu, wala Siudhiki na udhaifu wake. Naifanya kazi Yangu tu, na kuongea jinsi ambavyo Nimefanya, hata kama mwanadamu haelewi matakwa Yangu; siku itakapokuja, watu watanijua ndani kabisa ya nyoyo zao, na watanikumbuka katika mawazo yao.
Jumapili, 1 Desemba 2019
Wimbo wa Maneno ya Mungu Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote
I
Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia,
unaanza kutenda wajibu wako.
Katika mpango na utaratibu wa Mungu,
unachukua nafasi yako,
na unaanza safari ya maisha.
Vyovyote vilivyo msingi wako
ama safari iliyo mbele yako,
hakuna anayeweza kuepuka utaratibu
na mpango ambao Mbingu imeweka,
na hakuna aliye na amri juu ya hatima yake,
kwani ni Yule tu anayetawala juu ya vitu vyote
ndiye ana uwezo wa kazi kama hii.
Alhamisi, 28 Novemba 2019
Sura ya 13
Dhamira Zangu kadhaa zimefichwa ndani ya matamshi ya sauti Yangu. Ila mwanadamu hajui na hafahamu chochote kuhusu haya, huku akiendelea kuyapokea na kuyafuata maneno Yangu kutoka nje, bila kung’amua roho Yangu na kuelewa mapenzi Yangu kutoka ndani ya maneno Yangu. Hata ingawa Nimeyaweka maneno Yangu wazi, kuna yeyote aliyeelewa? Nilitoka Sayuni Nikaja miongoni mwa wanadamu.
Jumatano, 27 Novemba 2019
Wimbo wa Maneno ya Mungu Mungu Hutumaini Mtu Anaweza Kumjua na Kumwelewa
I
Tangu uhusiano wa kwanza wa Mungu na mwanadamu,
Amekuwa akifichua kwao
Kiini Chake na vile Alivyo na Alicho nacho,
bila kukoma, kila wakati.
Kama watu katika enzi wanaweza kuona au kuelewa,
Mungu huzungumza na kufanya kazi
ili kuonyesha tabia Yake na kiini.
Ijumaa, 8 Novemba 2019
“Kutoka kwa Kiti cha Enzi Hububujika Maji ya Uzima” – Jinsi ya Kupata Njia ya Uzima wa Milele | Swahili Gospel Movie Clip 8/9
“Kutoka kwa Kiti cha Enzi Hububujika Maji ya Uzima” – Jinsi ya Kupata Njia ya Uzima wa Milele | Swahili Gospel Movie Clip 8/9
Kwa maelfu ya miaka waumini wa Bwana wametaka kupata uzima wa milele, lakini hakuna mtu ambaye ameweza kutimiza matamanio haya. Sasa, umechanganyikiwa kuhusu kama kweli kuna njia ya uzima wa milele au la au umechanganyikiwa juu ya jinsi unavyoweza kufuatilia hili kwa njia ambayo utapata njia ya uzima wa milele? Hii video fupi itakuambia jinsi ya kupata njia ya uzima wa milele.
Jumanne, 5 Novemba 2019
Sura ya 6
Kwa masuala ya ndani ya roho, unapaswa kuwa makini kwa utaratibu; kwa maneno Yangu, unapaswa kuwa msikivu kwa makini. Unapaswa kulenga hali ambayo unaona Roho Yangu na nafsi Yangu ya mwili, maneno Yangu na nafsi Yangu ya mwili, kama kitu kimoja kizima kisichogawanyika, na kufanya kuwa binadamu wote wataweza kuniridhisha mbele Yangu.
Jumamosi, 26 Oktoba 2019
Kwa Nini Mungu Hutajwa Majina, na Jina Moja Linaweza Kuwakilisha Uzima wa Mungu?
Sura ya 2 Ukweli wa Majina ya Mungu
1. Kwa Nini Mungu Hutajwa Majina, na Jina Moja Linaweza Kuwakilisha Uzima wa Mungu?
Maneno Husika ya Mungu:
Je, Jina la Yesu “Mungu pamoja nasi,” linaweza kuwakilisha tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake? Je, linaweza kueleza Mungu kwa ukamilifu? Kama mwanadamu atasema ya kwamba Mungu Ataitwa tu Yesu, na hawezi kuwa na jina lingine kwa sababu Mungu hawezi kubadilisha tabia yake, basi maneno hayo ni kufuru! Je, unaamini kwamba jina la Yesu, Mungu pamoja nasi, linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu?
Ijumaa, 25 Oktoba 2019
Wimbo Mpya wa Kusifu na Kuabudu 2019 | “Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu” | MV
Wimbo Mpya wa Kusifu na Kuabudu 2019 | “Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu” | MV
Mandhari iliyochorwa katika Biblia “Amri ya Mungu kwa Adamu”
ni ya kugusa na yenye kutia moyo.
Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu,
uhusiano kati ya hao wawili ni wa ndani sana tunaanza kuhisi mshangao.
Upendo wa Mungu unaofurika umepewa mwanadamu bure;
Mwanadamu, maasumu na safi, bila ya wajibu wa kumnyima uhuru,
huishi kwa furaha kamili machoni mwa Mungu.
Mungu humtunza mtu, na mtu huishi chini ya mabawa Yake.
Yote ambayo mtu hufanya, maneno yake yote na matendo,
yamefungwa pamoja na Mungu, hayawezi kujitenga.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)






