![]() |
| Kanuni Zangu za Maisha Ziliniacha Nikiwa Nimeharibika |
45.Umeme wa Mashariki | Kanuni Zangu za Maisha Ziliniacha Nikiwa Nimeharibika
Changkai Mji wa Benxi, mkoa wa Liaoning
Maneno ya kawaida "Watu wazuri humaliza wakiwa wa mwisho" ni ambayo mimi binafsi ninayafahamu sana. Mimi na mume wangu sote tulikuwa hasa watu wasio na hatia: Wakati wa masuala yaliyohusisha faida au hasara yetu binafsi, hatukuwa aina ya watu wa kubishana na kusumbuana na wengine. Pale ambapo tuliweza kuwa wavumilivu tulikuwa wavumilivu, pale ambapo tungeweza kuwa na fadhila tulifanya tulivyoweza kuwa na fadhila. Kama matokeo yake, mara nyingi tulijipata tukiwa tumedanganywa na kudhulumiwa na wengine. Kwa hakika ilionekana kuwa katika maisha, "Watu wazuri humaliza wakiwa wa mwisho"—iwapo una huruma nyingi sana katika moyo wako, iwapo una fadhila nyingi sana na mwenye staha katika mambo yako, uko katika hatari kuu ya kudanganywa.




