Jumatatu, 8 Januari 2018

Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Neno Laonekana katika Mwili

Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

    Mwenyezi Mungu alisema,Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii kabisa kwamba mwili wa mwanadamu umeharibiwa ndio maana Mungu akamfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake; aidha, kwa sababu mwanadamu ni mhusika wa uharibifu, Amemfanya mwanadamu kuwa mlengwa wa kazi Yake katika hatua zote za kazi Yake ya wokovu.

Jumapili, 7 Januari 2018

Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,  Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,
Neno Laonekana katika Mwili

Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu

Mwenyezi Mungu alisema,Enzi ya zama ishaenda, na enzi mpya imefika. Mwaka baada ya mwaka na siku baada ya siku, Mungu amefanya kazi nyingi. Alikuja duniani, kisha Akaondoka. Mzunguko kama huu umeendelea kwa vizazi vingi. Siku ya leo, Mungu anaendelea kama mbeleni kufanya kazi Anayopaswa kufanya, kazi ambayo bado Hajaikamilisha, kwani hadi leo, bado Hajaingia mapumzikoni. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo, Mungu amefanya kazi nyingi, lakini ulijua kwamba kazi anayoifanya Mungu leo ni nyingi kuliko awali na kipimo ni kikubwa zaidi? Hii ndiyo maana Nasema Mungu amefanya jambo kubwa miongoni mwa wanadamu. Kazi zote za Mungu ni muhimu sana, iwe kwa mwanadamu ama Mungu, kwani kila kitu cha kazi Yake kina uhusiano na mwanadamu.

Jumamosi, 6 Januari 2018

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu,
Neno Laonekana Katika Mwili

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Mwenyezi Mungu alisema,Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kusikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje, kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu na dada wanaomfuata Yesu wangependa kumpa Yesu makaribisho mazuri. Lakini Je, mmewaza iwapo utamjua Yesu Atakaporejea? Je, mtaelewa kila kitu Atakachosema? Je, mtakubali bila masharti, kila kazi ambayo Anafanya? Wale wote ambao wamesoma Biblia wanajua kuhusu kurudi kwa Yesu, na wale wote ambao wamesoma Biblia wanangoja kwa makini kuja Kwake.

Alhamisi, 4 Januari 2018

Umeme wa Mashariki | Kanuni Zangu za Maisha Ziliniacha Nikiwa Nimeharibika | kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu,  Kanisa,
Kanuni Zangu za Maisha Ziliniacha Nikiwa Nimeharibika

45.Umeme wa Mashariki | Kanuni Zangu za Maisha Ziliniacha Nikiwa Nimeharibika

Changkai Mji wa Benxi, mkoa wa Liaoning
Maneno ya kawaida "Watu wazuri humaliza wakiwa wa mwisho" ni ambayo mimi binafsi ninayafahamu sana. Mimi na mume wangu sote tulikuwa hasa watu wasio na hatia: Wakati wa masuala yaliyohusisha faida au hasara yetu binafsi, hatukuwa aina ya watu wa kubishana na kusumbuana na wengine. Pale ambapo tuliweza kuwa wavumilivu tulikuwa wavumilivu, pale ambapo tungeweza kuwa na fadhila tulifanya tulivyoweza kuwa na fadhila. Kama matokeo yake, mara nyingi tulijipata tukiwa tumedanganywa na kudhulumiwa na wengine. Kwa hakika ilionekana kuwa katika maisha, "Watu wazuri humaliza wakiwa wa mwisho"—iwapo una huruma nyingi sana katika moyo wako, iwapo una fadhila nyingi sana na mwenye staha katika mambo yako, uko katika hatari kuu ya kudanganywa.

Kukubali Ukweli kwa Hakika Ni Nini? | kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Ukweli,
Kukubali Ukweli kwa Hakika Ni Nini

53.Kukubali Ukweli kwa Hakika Ni Nini?

Xiaohe Mji wa Puyang, Mkoa wa Henan
Hapo awali, kila wakati niliposoma maneno yaliyofichuliwa na Mungu kuhusu jinsi watu hawakubali ukweli, sikuamini kwamba maneno hayo yangetumika kwangu. Nilifurahia kula na kunywa neno la Mungu na kuwasiliana kuhusu neno la Mungu, na niliweza kukubali na kukiri kila kitu ambacho Mungu amesema kuwa ukweli—bila kujali jinsi kilivyoumiza moyo wangu au jinsi hakikuambatana na mawazo yangu. Aidha, bila kujali kiwango cha dosari kaka na dada zangu wangeonyesha, ningekikiri na kukikubali. Sikutafuta kujitetea mwenyewe, hivyo nilidhani kwamba nilikuwa mtu ambaye kwa hakika alikubali ukweli.

Jumatano, 3 Januari 2018

Umeme wa Mashariki | Ni Nini Husababisha Uongo | kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, ukweli,
Umeme wa Mashariki | Ni Nini Husababisha Uongo

27. Umeme wa Mashariki | Ni Nini Husababisha Uongo

Xiaojing Jijini Heze, Mkoani Shandong
Kila mara nilipoona neno la Mungu likituomba kuwa watu waaminifu na kuzungumza kwa usahihi, niliwaza, “Sina tatizo na kuzungumza kwa usahihi. Si ni kusema tu kitu jinsi kilivyo na kusema mambo jinsi yalivyo? Je, hiyo si rahisi? Kilichokuwa kimenikera zaidi daima katika dunia hii walikuwa watu waliotia chumvi walipozungumza.” Kwa sababu ya hili, nilihisi imani kuu, nikifikiri kwamba sikuwa na shida katika hali hii. Lakini kupitia tu kwa ufunuo wa Mungu ndio niligundua kwamba, bila kuingia katika ukweli au kubadili tabia ya mtu, mtu hawezi kwa vyovyote kuzungumza kwa usahihi.

Umeme wa Mashariki | Ufahamu wa Kuokolewa | kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, ukombozi,
Umeme wa Mashariki | Ufahamu wa Kuokolewa

23. Umeme wa Mashariki | Ufahamu wa Kuokolewa

Lin Qing Jijini Qingzhou, Mkoa wa Shandong
Kwa miaka hii mingi ya kumfuata Mungu, nimeacha furaha ya familia yangu na mwili, na nimekuwa na shughuli nyingi siku nzima nikitimiza wajibu wangu kanisani. Kwa hiyo niliamini: Mradi tu nisiache kazi katika kanisa ambayo nimeaminiwa, nisimsaliti Mungu, nisiache kanisa, na kumfuata Mungu hadi mwisho, nitahurumiwa na kuokolewa na Mungu. Niliamini pia kuwa nilikuwa nikitembea katika njia ya wokovu na Mungu, na yote niliyokuwa niyafanye ni kumfuata Yeye mpaka mwisho.