Jumanne, 20 Machi 2018

Umeme wa Mashariki | Kazi na Kuingia (6)

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, siku za mwisho,
Kazi na Kuingia (6)

Umeme wa Mashariki | Kazi na Kuingia (6)

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi na kuingia kwa uhalisia ni vya kiutendaji na vinarejelea kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu. Mwanadamu kukosa kabisa uelewa juu ya sura halisi ya Mungu na kazi ya Mungu kumesababisha shida kubwa katika kuingia kwake. Leo hii, watu wengi bado hawajui kazi ambayo Mungu anatimiza katika siku za mwisho, au kwa nini Mungu Anastahimili fedheha kubwa kupita kiasi kuja katika mwili na kusimama na mwanadamu katika makovu na majonzi. Mwanadamu hajui chochote kuhusu lengo la kazi ya Mungu, wala kusudi la mpango wa Mungu kwa ajili ya siku za mwisho.

Jumatatu, 19 Machi 2018

"Vunja Pingu na Ukimbie" (2) - Je, Kila Kitu Kilicho Katika Biblia ni Neno la Mungu?


"Vunja Pingu na Ukimbie" (2) - Je, Kila Kitu Kilicho Katika Biblia ni Neno la Mungu?


Utambulisho


Kama watu wengi wa kidini wenye imani katika Bwana, Mzee Li daima amehisi kwamba "kila kitu kilicho katika Biblia kilitiwa msukumo na Mungu," "Biblia ni neno la Mungu," na "Biblia humwakilisha Mungu." Dhana hizi zilikuwa kwa muda mrefu zimeunda msingi wa imani yake. Zilikuwa zimekita mizizi ndani ya moyo wake na zilikuwa zimekuwa kikwazo kwa kujifunza kwake njia ya kweli na pia utumwa uliomzuia kukubali njia ya kweli. Wahubiri wa Kanisa la Mwenyezi Mungu waliposoma kwa subira kwa Mzee Li kuhusu neno la Mungu na kufanya ushirika naye kuhusu ukweli, hatimaye alielewa kuwa si Biblia yote iliyotiwa msukumo na Mungu, lakini ina maneno ya Mungu na maneno ya mwanadamu . Mzee Li sasa alikuwa huru kutoka kwa utumwa na pingu za dhana hizi za kidini.

"Vunja Pingu na Ukimbie" (1) - Legeza Pingu na Ujifunze Njia ya Kweli


Utambulisho

    Mzee wa kanisa Li, kutokana na imani pofu katika maneno ya wachungaji wa kidini, alihisi kwamba kazi na maneno yote ya Mungu yaliandikwa katika Biblia na kwamba chochote nje ya Biblia hakingeweza kuwa kazi na neno la Mungu. Li alifikiri kwamba yote aliyohitaji kufanya ni kushika Biblia na wakati Bwana angekuja tena, angenyakuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kwa hiyo, Li hakuipa fikira kazi ya Mwenyezi Mungukatika siku za mwisho. Wakati mmoja, Mzee Li alipata kujua kwamba mfanyakazi mwenza, Mzee Lin, alikuwa akichunguza Umeme wa Mashariki kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Jumapili, 18 Machi 2018

Umeme wa Mashariki | Kazi na Kuingia (8)

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, wokovu,

Umeme wa Mashariki | Kazi na Kuingia (8)


Mwenyezi Mungu alisema, Nimezungumza mara nyingi sana kwamba kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kwa ajili ya kubadilisha roho ya kila mtu, kubadilisha nafsi ya kila mtu, ili kwamba moyo wake, ambao umeteseka sana na kiwewe, uwe umebadilishwa, hivyo kuokoa nafsi yake, ambayo imeumizwa kwa kina zaidi na Shetani; ni kwa sababu ya kuamsha roho za watu, kuyeyusha mioyo yao baridi, na kuwaruhusu kurudisha nguvu za ujana. Haya ndiyo mapenzi makubwa ya Mungu. Weka pembeni mazungumzo ya ni namna gani maisha na uzoefu wa mwanadamu ni ya kiburi au ya kina; mioyo ya watu itakapokuwa imeamshwa, wanapokuwa wameamshwa kutoka kwa ndoto zao na kujua kikamilifu madhara yaliyoletwa na joka kuu jekundu, kazi ya huduma ya Mungu itakuwa imekamilika. Siku ambayo kazi ya Mungu itakuwa imekamilika ni wakati ambapo mwanadamu ataanza rasmi njia ya imani sahihi kwa Mungu.

Umeme wa Mashariki | Kazi na Kuingia (7)

Umeme wa Mashariki, kumjua Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu,

Umeme wa Mashariki | Kazi na Kuingia (7)


Mwenyezi Mungu alisema, Imemchukua mwanadamu mpaka siku hii kutambua kwamba kile mtu anachokosa si tu kuruzukiwa maisha ya kiroho na uzoefu wa kumjua Mungu, lakini, muhimu zaidi, mabadiliko katika tabia yake. Kutokana na ujinga kamili wa mwanadamu wa historia na utamaduni wa kale wa wanadamu, hana ujuzi wa kazi ya Mungu hata kidogo. Mwanadamu hutumaini kuwa ndani kabisa ya moyo, mwanadamu anaweza kumpenda Mungu sana, lakini kwa sababu ya upotovu mkubwa mno wa mwili wa mwanadamu, pamoja na kutojali na upumbavu, mwanadamu ameshushwa kuwa asiye na ufahamu wa Mungu hata kidogo. Mungu Anakuja miongoni mwa wanadamu siku ya leo kwa kusudi la kubadilisha mawazo na roho zao, na taswira ya Mungu katika mioyo yao ambayo wamekuwa nayo kwa maelfu ya miaka.

Jumamosi, 17 Machi 2018

Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu,
Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja


Mwenyezi Mungu alisema, Mwanzoni, Mungu alikuwa anapumzika. Hakukuwa na binadamu ama kitu chochote kingine duniani wakati huo, na Mungu hakuwa amefanya kazi yoyote ile. Mungu alianza tu kazi Yake ya usimamizi baada ya binadamu kuwepo na baada ya binadamu kupotoshwa. Kutoka hapa kuendelea, Mungu hakupumzika tena lakini badala yake Alianza kufanya kazi miongoni mwa binadamu. Ilikuwa kwa sababu ya upotovu wa binadamu ndipo Mungu alichukuliwa kutoka kwa pumziko Lake, na ilikuwa pia kwa sababu ya uasi wa malaika mkuu ndipo Mungu alichukuliwa kutoka kwa pumziko Lake.

Umeme wa Mashariki | Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, hukumu,

Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Mwenyezi Mungu alisema, Mwanadamu anaelewa sehemu ndogo ya kazi ya leo na kazi ya baadaye, lakini hafahamu hatima ambapo mwanadamu ataingia. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutekeleza wajibu wa kiumbe: Mwanadamu anapaswa kumfuata Mungu kwa lolote afanyalo, na mnapaswa muendelee mbele kwa njia yoyote ambayo Nitawaambia. Wewe huna mbinu ya kufanya mipango yako mwenyewe, na huna uwezo wa kujitawala mwenyewe; yote ni lazima yaachwe kwa rehema za Mungu, na kila kitu kinadhibitiwa na mikono Yake. Kama kazi ya Mungu ilimkimu mwanadamu kwa kumpa hatima, hatima ya ajabu, kabla ya wakati, na kama Mungu alitumia hii kumshawishi mwanadamu na kusababisha mwanadamu kumfuata Yeye—kama Yeye alifanya mpango na mwanadamu—basi huu haungekuwa ni ushindi, wala haingekuwa kufanya kazi katika maisha ya binadamu.