Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 21
Machoni pa Mungu, watu ni kama wanyama katika ulimwengu wa wanyama. Wao hupigana, huchinjana, na huwa na ushirikiano wa pekee mmoja kwa mwingine. Machoni pa Mungu, wao pia ni kama sokwe, wakipangiana hila bila kujali umri au jinsia. Kwa hivyo, yote ambayo wanadamu wote hufanya na kuonyesha hayajawahi kuupendeza moyo wa Mungu.


