Jumapili, 7 Aprili 2019

Wimbo wa kuabudu | Shetani Hawezi Kubadili Chochote Chini ya Mamlaka ya Mungu

Wimbo wa kuabudu Shetani Hawezi Kubadili Chochote Chini ya Mamlaka ya Mungu

I
Ni kwa miaka ngapi, maelfu ya miaka,
Shetani amekuwa akimpotosha mwanadamu, akifanya mabaya mengi sana.
Vizazi, kimoja baada ya kingine vimedanganywa naye.
Oh, ni uhalifu kiasi kipi, uhalifu wa kuogofya
ambao Shetani amefanya katika dunia hii yote.
Alimchangamsha mwanadamu kupigana na Mungu, akamnyanyasa, na kumdanganya mwanadamu,
akatafuta kuuharibu mpango wa usimamizi wa Mungu.

Jumamosi, 6 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Tatu



Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu anasema, “Wakati Mungu alipofanya kazi katika ubinadamu, mbinu, maneno, na ukweli Wake mwingi vyote vilionyeshwa kwa njia ya kibinadamu. Lakini wakati uo huo tabia ya Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, na mapenzi Yake vyote vilionyeshwa kwa watu kuweza kujua na kuvielewa. Kile walichojua na kuelewa kilikuwa hasa kiini Chake na Alicho nacho na kile Alicho, vyote ambavyo vinawakilisha utambulisho na hadhi ya asili ya Mungu Mwenyewe.

Ijumaa, 5 Aprili 2019

Wimbo wa kuabudu | 79. Kazi na Maonyesho Huamua Kiini Chake


Wimbo wa kuabudu | 79. Kazi na Maonyesho Huamua Kiini Chake

I


Kiini cha Kriso kinaamuliwa na kazi Yake na maonyesho.

Na moyo ulio wa kweli, Anatimiza kile ambacho ameaminiwa nacho,

Anamwabudu Mungu aliye mbinguni na anatafuta mapenzi ya Baba Yake.

Haya yote yanaamuliwa na kiini Chake, na hivyo pia ufunuo Wake wa asili.

Alhamisi, 4 Aprili 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII” Sehemu ya Pili
Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu ni Bwana wa kanuni zinazoudhibiti ulimwengu, Anadhibiti kanuni zinazoongoza kuishi kwa vitu vyote, na pia Anadhibiti ulimwengu na vitu vyote kiasi kwamba vinaweza kuishi pamoja; Anaifanya ili kwamba visikwishe au kutoweka ili kwamba binadamu aendelee kuishi, binadamu anaweza kuishi katika mazingira hayo kupitia uongozi wa Mungu. Kanuni hizi zinazoongoza vitu vyote zipo chini ya utawala wa Mungu, na binadamu hawawezi kuingilia na hawawezi kuzibadilisha; ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anajua kanuni hizi na ni Yeye pekee ndiye anazisimamia.”

Tazama zaidi: Maonyesho ya Mungu | "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu"




Jumatano, 3 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)” Sehemu ya Kwanza



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)” Sehemu ya Kwanza
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Kwenye Siku ya Kwanza, Mchana na Usiku wa Mwanadamu Vinazaliwa na Kujitokeza Waziwazi kwa Msaada wa Mamlaka ya Mungu Kwenye Siku ya Pili, Mamlaka ya Mungu Yalipangilia Maji, na Kufanya Mbingu, na Anga za Mbinu za Kimsingi Zaidi za Kuishi kwa Binadamu Kuonekana

Jumanne, 2 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 38

Matamshi ya Mwenyezi MunguSura ya 38

Si kwamba imani yako ni nzuri au safi, lakini badala yake, kazi Yangu ni ya ajabu! Kila kitu ni kwa sababu ya rehema Zangu! Hupaswi kuwa na tabia potovu ya ubinafsi au kiburi hata kidogo, vinginevyo kazi Yangu kwako haitaendelea. Lazima uelewe wazi kwamba iwapo watu wanaanguka au kusimama imara si kwa sababu yao, ni kwa sababu Yangu. Leo, kama huelewi vizuri hatua hii, hutaweza kuingia katika ufalme! 

Jumatatu, 1 Aprili 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku”



Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku”

Mwenyezi Mungu anasema, “Kuanzia leo, Mungu ataweza kuwafanya watu wasiokuwa na fikira za kidini kuwa watimilifu kwa njia rasmi, ambao wako tayari kuweka pembeni nafsi zao za kale, na ambao wanamtii tu Mungu, pamoja na kuwafanya kuwa watimilifu wale wanaotamani neno la Mungu. Watu hawa wanafaa kusimama na kumhudumia Mungu. Kwake Mungu kunayo na hekima nyingi na isiyoisha. Kazi yake ya kustaajabisha na matamshi yake yenye thamani ni vitu ambavyo vipo ili watu wengi zaidi kuweza kufurahia.