Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii kabisa kwamba mwili wa mwanadamu umeharibiwa ndio maana Mungu akamfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake; aidha, kwa sababu mwanadamu ni mhusika wa uharibifu, Amemfanya mwanadamu kuwa mlengwa wa kazi Yake katika hatua zote za kazi Yake ya wokovu. Mwanadamu ni kiumbe anayekufa, ni wa mwili na damu, na Mungu ndiye tu Anayeweza kumwokoa mwanadamu.
Jumamosi, 7 Septemba 2019
Ijumaa, 6 Septemba 2019
Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Pili)
Kazi ya Mungu Mwenyewe ni maono ambayo mwanadamu lazima afahamu, kwa kuwa kazi ya Mungu haiwezi kutekelezwa na mwanadamu, wala haimilikiwi na mwanadamu. Hatua tatu za kazi ndizo ukamilifu wa usimamizi wa Mungu, na hakuna ono kuu kuliko hili linalopaswa kufahamika kwa mwanadamu. Kama mwanadamu hafahamu maono haya makuu, basi si rahisi kumjua Mungu, na si rahisi kujua mapenzi ya Mungu, na, zaidi ya hayo, njia ambayo mwanadamu anapitia inazidi kuwa ngumu. Bila maono, mwanadamu hangeweza kufika umbali huu. Ni maono ambayo yamemlinda mwanadamu hadi leo, na ambayo yamempa mwanadamu ulinzi mkuu.
Alhamisi, 5 Septemba 2019
Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Kwanza)
Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu.
Jumatano, 4 Septemba 2019
Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Pili
Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Pili
Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu aliwaumba watu hawa wawili na kuwashughulikia kama mtu na mwandani Wake. Akiwa ndiye mwanafamilia pekee wao, Mungu aliangalia kuishi kwao na pia akakidhi mahitaji yao ya kimsingi. Hapa, Mungu anajitokeza kama mzazi wa Adamu na Hawa. Huku Mungu akifanya haya, binadamu haoni namna ambavyo Mungu alivyo mkuu; haoni mamlaka ya juu zaidi ya Mungu, hali Yake ya mafumbo, na hasa haoni hasira au adhama Yake. Kile anachoona tu ni unyenyekevu wa Mungu, upendo Wake, kujali Kwake binadamu na jukumu Lake na utunzaji Wake kwake yeye. Mwelekeo na njia ambayo Mungu alishughulikia Adamu na Hawa ni sawa na namna ambavyo wazazi wa kibinadamu wanavyoonyesha hali ya kuwajali watoto wao binafsi. Ni kama pia namna ambavyo wazazi wa kibinadamu wanavyopenda, kuangalia, na kutunza watoto wao binafsi wa kiume na kike—halisia, namna ya kuonekana, na kushikika.”
Tazama Zaidi: Neno la Mungu | "Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya"
Jumanne, 3 Septemba 2019
Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Pili)
Kazi ya mwanadamu ina mipaka na kadiri inavyoweza kufika. Mtu mmoja anaweza kufanya kazi ya wakati fulani na hawezi kufanya kazi ya enzi nzima—vinginevyo anaweza kuwaongoza watu katika kanuni. Kazi ya mwanadamu inaweza kufaa tu katika kipindi au awamu fulani. Hii ni kwa sababu uzoefu wa mwanadamu una mipaka. Mtu hawezi kulinganisha kazi ya mwanadamu na kazi ya Mungu. Namna mwanadamu anavyofanya mambo na maarifa yake ya ukweli yote yanatumika tu katika mawanda fulani. Huwezi kusema kwamba njia ambayo mwanadamu anaiendea ni matakwa ya Roho Mtakatifu kabisa, kwa sababu mwanadamu anaweza kupewa nuru na Roho Mtakatifu tu na hawezi kujazwa kikamilifu na Roho Mtakatifu.
Jumatatu, 2 Septemba 2019
Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza)
Ni kiasi gani cha kazi ya mwanadamu ni kazi ya Roho Mtakatifu na uzoefu wa mwanadamu ni kiasi gani? Hata sasa, tunaweza kusema kuwa watu bado hawayaelewi maswali haya, ambayo yote ni kwa sababu watu hawaelewi kanuni za utendaji kazi wa Roho Mtakatifu. Kazi ya mwanadamu Ninayoizungumzia, kimsingi, ni kwa kurejelea kazi za wale ambao wana kazi ya Roho Mtakatifu au wale ambao wanatumiwa na Roho Mtakatifu. Sizungumzii kazi ambayo inatokana na matakwa ya mwanadamu bali kazi ya mitume, watendaji kazi au kaka na dada wa kawaida waliopo katika mawanda ya kazi ya Roho Mtakatifu.
Jumapili, 1 Septemba 2019
Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Pili)
Petro alifanywa mkamilifu kwa kupitia ushughulishaji na usafishaji. Alisema, “Mimi ni lazima nikidhi mapenzi ya Mungu wakati wote. Kwa yote nifanyayo mimi natafuta tu kukidhi mapenzi ya Mungu, na kama mimi ninaadibiwa, au kuhukumiwa, bado nina furaha kufanya hivyo.” Petro alimpa Mungu kila kitu chake, na kazi yake, maneno, na maisha yote yalikuwa yote kwa ajili ya kumpenda Mungu. Alikuwa mtu ambaye alitafuta utakatifu, na alipopitia zaidi, ndivyo upendo wake wa Mungu ndani ya moyo wake ulikuwa mkubwa zaidi. Paulo, wakati huo huo, alifanya tu kazi ya nje, na ingawa alitia bidii katika kazi yake, juhudi zake zilikuwa kwa ajili ya kufanya kazi yake vizuri na hivyo kupata tuzo.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)





