Mungu ananuia kuangamiza ulimwengu kwa gharika, anamwagiza Nuhu kuijenga safina. |
B. Nuhu
1. Mungu ananuia kuangamiza ulimwengu kwa gharika, anamwagiza Nuhu kuijenga safina.
(Mwa 6:9-14) Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu: Nuhu alikuwa mtu wa haki na mkamilifu katika vizazi vyake, na Nuhu alitembea pamoja na Mungu. Nuhu akazaa wana watatu wa kiume, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Dunia pia ilikuwa potovu mbele za Mungu, dunia ilijaa dhuluma. Mungu akaingalia dunia, na, tazama, ilikuwa imepotoka; maana kila mwenye mwili alikuwa amejiharibia njia yake duniani. Na Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu dunia imejawa na dhuluma kupitia kwao; na, tazama, Nitawaharibu pamoja na dunia. Ujitengenezee safina ya mti wa mvinje; utatengeneza vyumba ndani ya safina, na uifunike ndani na nje kwa lami.
(Mwa 6:18-22) Lakini nawe Nitalifanya agano langu kuwa thabiti; nawe utakuja katika safina, wewe, na wanao, na mkeo, na wake za wanao pamoja nawe. Na katika kila kilicho hai chenye mwili, wawili wa kila namna utawaleta ndani ya safina, kuwaweka hai pamoja nawe; watakuwa mume na mke. Katika vyote virukavyo kwa jinsi yake, na kila namna ya mnyama kwa jinsi yake, kila kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake, wawili wa kila namna watakuja kwako, ili uwaweke hai. Na ujichukulie chakula cha kila namna kinacholika, ukikusanye kwako; nacho kitakuwa ni chakula chenu, na chao. Ndivyo alivyofanya Nuhu; kulingana na vyote ambavyo Mungu alimwamuru, hivyo ndivyo alivyofanya.
Mwenyezi Mungu alisema,Je sasa mnaelewa kwa jumla Nuhu ni nani baada ya kuzisoma fahamu hizi? Nuhu ni mtu wa aina gani? Maandishi asilia ni: “Nuhu alikuwa mtu wa haki na mkamilifu katika vizazi vyake. Kulingana na uelewa wa watu wa kisasa, mtu mwenye haki wakati huo wa nyuma alikuwa mtu wa aina gani? Mtu mwenye haki anafaa kuwa mtu mtimilifu. Je, mnajua kama mtu huyu mtimilifu ni mtimilifu machoni mwa binadamu au ni mtimilifu machoni mwa Mungu? Bila shaka mtu huyu mtimilifu ni mtu mtimilifu machoni mwa Mungu na wala si machoni mwa binadamu.. Haya yote ni kweli! Hii ni kwa sababu binadamu ni kipofu na hawezi kuona, na Mungu tu ndiye anayeiangalia nchi nzima na kila mmoja wetu, Mungu pekee ndiye anayejua Nuhu ni mtu mtimilifu. Hivyo basi, mpango wa Mungu wa kuuangamiza ulimwengu kwa gharika ulianza pindi tu Alipomuita Nuhu.
Katika enzi hiyo, Mungu alinuia kumuita Nuhu ili kufanya kitu muhimu sana. Kwa nini ilikuwa lazima Afanye hivyo? Kwa sababu Mungu alikuwa na mpango kwa moyo Wake wakati huo. Mpango Wake ulikuwa kuangamiza ulimwengu kwa gharika. Kwa nini auangamize ulimwengu? Maandiko yanasema hivi: “Dunia pia ilikuwa potovu mbele za Mungu, dunia ilijaa dhuluma.” Mnaona nini kutoka kwenye kauli “dunia ilijaa dhuluma”? Ni ajabu duniani wakati ulimwengu na watu wake wanapotoka kwa kupindukia, na ni hivi: “dunia ilijaa dhuluma.” Katika lugha ya leo, “ikajaa dhuluma” inamaanisha kila kitu kimechanganyika. Kwa binadamu, inamaanisha kwamba katika nyanja zote za maisha hakuna mpangilio, na mambo yamejaa fujo kweli na ni magumu kudhibiti. Katika macho ya Mungu, inamaanisha watu wa ulimwengu wamepotoka sana. Wamepotoka hadi kiwango gani? Wamepotoka hadi kiwango ambacho Mungu hawezi tena kuvumilia kuangalia na hawezi tena kuwa na subira kuhusu hali hiyo. Wamepotoka hadi kiwango ambacho Mungu anaamua kuwaangamiza. Wakati Mungu alipoamua kuuangamiza ulimwengu, Alipanga kupata mtu wa kuijenga safina. Kisha Mungu akamchagua Nuhu kufanya kitu hicho, ambacho ni kumruhusu Nuhu kuijenga safina. Kwa nini Mungu alimchagua Nuhu? Katika macho ya Mungu, Nuhu ni mtu mwenye haki na haijalishi kile ambacho Mungu atamwagiza yeye kufanya, atafanya vivyohivyo. Hii inamaanisha atafanya chochote anachoambiwa kufanya na Mungu. Mungu alitaka kumtafuta mtu kama huyu ili afanye kazi na Yeye, kukamilisha kile alichokuwa amemwminia kufanya, kuikamilisha kazi Yake hapa duniani. Hapo nyuma, kulikuwa na mtu mwengine kando na Nuhu ambaye angekamilisha kazi hiyo? Bila shaka la! Nuhu ndiye aliyekuwa mtu wa pekee ambaye angeweza kukamilisha kile ambacho Mungu alikuwa amemwaminia kufanya, na hivyo Mungu alimchagua yeye. Lakini je upana na viwango vya Mungu vya kuwaokoa watu hapo nyuma vilikuwa sawa na vile vya sasa? Jibu ni bila shaka kunao utofauti! Kwa nini Nauliza hivi? Nuhu alikuwa ndiye mwanaume pekee mwenye haki katika macho ya Mungu wakati huo, kwa dokezo watoto wake wa kiume na mke na wakwe wake wote hawakukuwa watu wenye haki, lakini Mungu aliwalinda watu hawa kwa sababu ya Nuhu. Mungu hakuwataka wao kufanya kile anachowataka watu kufanya leo, na badala yake Aliwaweka hai wanachama wote wanane wa familia ya Nuhu . Walipata baraka za Mungu kwa sababu ya Nuhu kuwa mwenye haki. Kama Nuhu asingekuwepo, hakuna yeyote kati yao ambaye angekamilisha kile ambacho Mungu alikuwa amemwaminia kufanya. Hivyo basi Nuhu alikuwa ndiye mtu wa pekee ambaye alitakikana kubakia hai baada ya ulimwengu kuangamizwa wakati huo, na wale wengine walikuwa tu wafadhiliwa wa ziada. Hii inaonyesha kwamba, katika enzi kabla ya Mungu kuanza rasmi kazi Yake ya usimamizi, kanuni na viwango ambavyo Alishughulikia watu na kuwadai mahitaji vilikuwa vimelegezwa kidogo. Kwa watu wa leo, namna ambavyo Mungu alivyoshughulikia familia ya Nuhu ya watu wanane yaonekana kukosa haki. Lakini tukilinganisha na wingi wa kazi ambayo Yeye Anafanya kwa watu na kiwango cha neno Lake Analopitisha, namna Mungu alivyoshughulikia familia ya Nuhu ya watu wanane ilikuwa tu ni kanuni ya kazi Yake aliyoifanyia katika usuli wa kazi Yake wakati huu. Kwa kulinganisha, familia ya Nuhu ya watu wanane ndio ilipokea mengi zaidi kutoka kwa Mungu au ni watu wa Mungu ndio waliopokea?
Kwamba Nuhu alihitajika ni ukweli mdogo, lakini hoja kuu ya kile tunachozungumzia sasa—tabia ya Mungu, mapenzi Yake kiini Chake halisi katika rekodi hii—si rahisi. Ili kuelewa dhana hizi mbalimbali za Mungu lazima kwanza tuelewe ni mtu wa aina gani ambaye Mungu hutamani kuita, nakupitia hii, tuweze kuelewa tabia yake, mapenzi yake na kiini chake halisi. Kufanya hivi ni muhimu. Hivyo katika macho ya Mungu, mtu huyu ni wa aina gani ambaye yeye humwita? Huyu lazima awe ni mtu anayeweza kuyasikiza maneno Yake. Wakati huohuo, lazima mtu huyu awe yule wa kuwajibika, mtu atakayetekeleza neno la Mungu kwa kuliona kuwa jukumu na wajibu ambao anahitajika kukamilisha. Basi mtu huyu anahitajika kuwa mtu anayemjua Mungu? La. Hapo nyuma, Nuhu hakuwa ameyasikia sana mafundisho ya Mungu wala kupitia kazi yoyote ile ya Mungu. Hivyo basi, maarifa ya Nuhu kumhusu Mungu yalikuwa madogo mno. Ingawaje imerekodiwa hapa kwamba Nuhu alitembea na Mungu, aliwahi kuuona ubinafsi wa Mungu ? Jibu ni bila shaka la! Kwa sababu katika siku hizo, wajumbe wa Mungu tu ndio waliowaendea watu. Ingawa waliweza kuawakilisha Mungu katika kusema na kufanya mambo, walikuwa wakipitisha tu mapenzi na nia Zake. Ubinafsi wa Mungu haukufichuliwa kwa binadamu uso-kwa- macho. Kwenye sehemu hii ya maandiko, chote tunachoona tu ni kile ambacho mtu huyu Nuhu alilazimika kufanya na maagizo ya Mungu kwake yalikuwa gani. Hivyo basi ni kiini kipi kilichoonyeshwa na Mungu hapa? Kila kitu anachofanya Mungu kimepangiliwa kwa uhakika. Anapoona jambo au hali ikitokea, kutakuwa na kiwango cha kulipima jambo hilo katika macho Yake, na kiwango hiki kitaamua kama Ataanza mpango wa kulishughulikia au namna ya kuchukulia jambo na hali hii. Yeye anajali na ana hisia kwa kila kitu. Kwa hakika ni kinyume kabisa cha mambo. Kunao mstari hapa ambao Mungu alimwambia Nuhu: “Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu dunia imejawa na dhuluma kupitia kwao; na, tazama, Nitawaharibu pamoja na dunia.” Katika maneno ya Mungu wakati huu, Alisema kwamba Angeangamiza binadamu tu? La! Mungu Alisema kwamba Angeangamiza viumbe wote hai wenye mwili. Kwa nini Mungu alitaka kuangamiza? Kunao ufunuo mwingine wa tabia ya Mungu hapa: Katika macho ya Mungu, kunayo mipaka ya subira yake kwa kupotoka kwa binadamu, kwa uchafu, vurugu, na kutotii kwa mwili wote. Mipaka Yake ni ipi? Ni kama vile alivyosema Mungu: “Mungu akaingalia dunia, na, tazama, ilikuwa imepotoka; maana kila mwenye mwili alikuwa amejiharibia njia yake duniani.” Kauli hii “maana kila mwenye mwili alikuwa amejiharibia njia yake duniani” inamaanisha nini? Inamaanisha kiumbe yeyote hai, wakiwemo wale waliofuata Mungu, wale walioita jina la Mungu,wale waliowahi kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Mungu, wale waliomtambua Mungu kwa vinywa vyao na hata kumsifia Mungu—pindi tabia yao ilipojaa upotovu na kufikia macho ya Mungu, basi ingemlazimu kuwaangamiza. Hiyo ndiyo ilikuwa mipaka ya Mungu. Hivyo basi ni hadi kiwango kipi Mungu alibakia kuwa mwenye subira kwa binadamu na upotovu wa mwili wote? Hadi katika kiwango ambacho watu wote, wawe wafuasi wa Mungu au wasioaminii, walikuwa hawatembelei njia sahihi. Hadi kiwango ambacho binadamu alikuwa hajapotoshwa tu katika maadili na mwenye wingi wa maovu, lakini pia pale ambapo hakukuwa na mtu aliyesadiki uwepo wa Mungu, tupilia mbali yeyote aliyesadiki kuwa ulimwengu unatawaliwa na Mungu na kwamba Mungu anaweza kuwaletea watu nuru na njia sahihi. Hadi kiwango ambacho binadamu aliudharau uwepo wa Mungu, na hakumruhusu Mungu kuwepo. Pindi upotovu wa mwanadamu ulipofikia kiwango hiki, Mungu asingeweza tena kuwa na subira Ni nini kingechukua nafasi yake? Kuja kwa hasira ya Mungu na adhabu ya Mungu. Huu haukuwa ufunuo kiasi wa tabia ya Mungu? Katika enzi hii ya sasa, yupo bado binadamu mwenye haki katika macho ya Mungu? Yupo bado binadamu mtimilifu katika macho ya Mungu? Enzi hii ndiyo ile ambayo tabia ya miili yote duniani imepotoka mbele ya macho ya Mungu? Katika siku na enzi hii, mbali na wale Mungu anataka kuwafanya kuwa kamili, wale wanaoweza kumfuata Mungu na kuukubali wokovu Wake, huoni kwamba watu wote wa mwili wanapatia changamoto ile mipaka ya subira ya Mungu? Si kila kitu kinachofanyika kando yenu, kila mnachoona kwa macho yenu, na kusikia kwa masikio yenu, na kupitia ninyi binafsi kila siku katika ulimwengu huu kimejaa vurugu? Katika macho ya Mungu, si ulimwengu kama huu, enzi kama hii, inafaa kukomeshwa? Ingawaje usuli wa enzi ya sasa ni tofauti kabisa na usuli wa enzi ya Nuhu, hisia na hasira Alizo nazo Mungu kwa kupotoka kwa binadamu inabakia ileile sawa na ilivyokuwa wakati huo. Mungu anaweza kuwa mwenye subira kwa sababu ya kazi Yake, lakini kulingana na hali na masharti ya aina yote, ulimwengu huu unafaa kuwa uliangamizwa kitambo katika macho ya Mungu. Hali imepita na kupitiliza ile iliyokuwa hapo nyuma wakati ulimwengu uliangamizwa na gharika. Lakini tofauti ni nini? Hili ndilo jambo jingine linalohuzunisha moyo wa Mungu zaidi, na pengine kitu ambacho hakuna yeyote kati yenu anaweza kutambua.
Mungu ananuia kuangamiza ulimwengu kwa gharika, anamwagiza Nuhu kuijenga safina. |
Alipokuwa akiuangamiza ulimwengu kwa gharika, Mungu angemwita Nuhu ili kuijenga safina na kufanya baadhi ya kazi ya matayarisho. Mungu angemwita binadamu mmoja—Nuhu—kumfanyia misururu hii ya mambo. Lakini kwenye enzi ya sasa, Mungu hana mtu yeyote wa kumuita. Kwa nini hivyo? Kila mmoja aliyeketi hapa pengine anaelewa na kujua sababu vizuri sana. Je, mngependa Mimi niweze kuiweka wazi? Kuitaja kwa sauti huenda kukawaaibisha na kufanya kila mmoja kukasirika. Baadhi ya watu wanaweza kusema: “Ingawaje sisi si watu wenye haki na wala sisi si watu watimilifu kwenye macho ya Mungu, kama Mungu atatuelekeza sisi kufanya kitu, bado tutaweza kukifanya. Kabla, Aliposema janga kuu lilikuwa likija, tulianza kutayarisha chakula na vitu ambavyo tungehitaji wakati wa janga hilo. Si haya yote yalifanywa kulingana na mahitaji ya Mungu? Si tulikuwa tukishirikiana kwa hakika na kazi ya Mungu? Mambo haya tuliyofanya hayawezi kulinganishwa na kile Nuhu alifanya? Kwani kufanya kile tulichofanya si utiifu wa kweli? Kwani hatukuwa tunafuata maagizo ya Mungu? Kwani hatukufanya kile Mungu alichosema kwa sababu tunayo imani katika maneno ya Mungu? Basi kwa nini Mungu angali na huzuni? Kwa nini Mungu anasema Hana mtu wa kumwita?” Kunao tofauti wowote kati ya vitendo vyenu na vile za Nuhu? Tofauti ni nini? (Kutayarisha chakula leo kwa minajili ya janga kulikuwa nia yetu binafsi.) (Matendo yetu hayawezi kufikia yale ya “haki,” ilhali Nuhu ni mtu mwenye haki mbele ya macho ya Mungu.) Kile mlichosema hakiko mbali sana na ukweli. Kile alichofanya Nuhu ni tofauti sana kulingana na kile watu wanafanya sasa. Wakati Nuhu alipofanya kama vile Mungu alivyomwaagiza hakujua nia za Mungu zilikuwa nini. Hakujua ni nini ambacho Mungu Alitaka kukamilisha. Mungu alikuwa amempa tu amri, Akamwagiza afanye kitu, lakini bila ya maelezo mengi, na akaendelea mbele na kukifanya. Hakujaribu kuelewa kwa siri nia za Mungu zilikuwa nini, wala hakumpinga Mungu au kuwa na fikira mbili kuhusu jambo hilo. Alienda tu na kuifanya vilivyo kwa moyo safi na rahisi. Chochote ambacho Mungu alimruhusu kufanya alifanya, na kutii na kusikiliza neno la Mungu vyote vilikuwa ni imani yake ya kufanya mambo. Hivyo ndivyo alivyokuwa myofu na mwepesi wa kushughulikia kile ambacho Mungu alimwaminia kufanya. Kiini chake —kiini cha vitendo vyake kilikuwa ni utiifu, sio kutarajia kwa kukisia, sio kupinga, na zaidi; kutofikiria kuhusu maslahi yake binafsi na faida zake na hasara zake. Zaidi ya hayo, wakati Mungu Aliposema angeuangamiza ulimwengu kwa mafuriko, hakuuliza ni lini au kujaribu kulielewa jambo hilo kwa ujumla, na bila shaka hakumuuliza Mungu namna hasa alivyopanga kuangamiza ulimwengu. Alifanya tu kama Mungu alivyomwagiza. Njia yoyote ile aliyotaka Mungu, safina hiyo iweze kujengwa na hasa kujengwa na nini, alifanya tu vile ambavyo Mungu alimwomba na pia akaanza kazi mara moja. Alifanya hivyo kwa mwelekeo wa kutaka kutosheleza Mungu. Je, alikuwa akifanya hivyo kujisaidia yeye kuepuka janga? La. Je, alimwuliza Mungu ni baada ya muda gani zaidi kabla ulimwengu ungeangamizwa? Hakuuliza. Je, alimwuliza Mungu au alijua ingechukuwa muda gani kuijenga safina? Hakujua hilo pia. Alitii tu, akasikiliza, na kufanya hivyo inavyohitajika. Watu wa sasa si sawa: Pindi tu taarifa fulani inapojitokeza kupitia kwa neno la Mungu, pindi tu watu wanapohisi ishara ya kutatizwa au matatizo, wote watachukua hatua mara moja, haijalisha ni nini, au gharama husika, ili kutayarisha kile ambacho watakula, kunywa, na kutumia athari za baadaye, hata kupanga njia za wao kutoroka wakati janga litakapovamia. Hata ya kuvutia zaidi ni kwamba, wakati huu muhimu, akili za binadamu zinakuwa zenye “manufaa sana.” Katika hali ambazo Mungu hajanipa maagizo yoyote, binadamu anaweza kupanga kila kitu kwa njia inayofaa Mngeweza kutumia neno “sahihi” ili kuielezea. Na kuhusiana na kile Mungu anachosema, nia za Mungu ni nini, au kile Mungu anataka ni nini, hakuna anayejali na hakuna anayejaribu kukitambua. Je, huo sio utofauti mkubwa zaidi kati ya watu wa leo na Nuhu?
Katika rekodi hii ya hadithi ya Nuhu, mnaona sehemu ya tabia ya Mungu? Kunacho mpaka kwa subira ya Mungu kwa upotovu, uchafu, na vurugu la binadamu. Anapofikia ile mpaka, Hatawahi tena kuwa na subira na badala yake Ataanza usimamizi Wake mpya na mpango mpya, kuanza kufanya kile ambacho lazima Afanye, kufichua matendo Yake na upande ule mwingine wa tabia Yake. Kitendo hiki Chake si cha kuonyesha kwamba lazima Asiwahi kukosewa na binadamu au kwamba Yeye amejaa mamlaka na hasira, na wala si kuonyesha kwamba Anaweza kuangamiza ubinadamu. Ni kwamba tabia Yake na kiini chake takatifu ambacho hakiwezi tena kuruhusu, hakina tena subira kwa aina hii ya ubinadamu kuishi mbele Yake, kuishi chini ya utawala Wake. Hivyo ni kusema, wakati wanadamu wote uko dhidi Yake, wakati hakuna mtu yeyote Anayeweza kuokoa katika ulimwengu mzima, Hatakuwa tena na subira kwa ubinadamu kama huu, na Ataweza, bila ya utundu wowote, tekeleza mpango Wake—kuangamiza ubinadamu wa aina hii. Kitendo kama hicho cha Mungu kinaamuliwa na tabia Yake. Hii ni athari inayohitajika, na athari ambayo kila kiumbe aliyeoumbwa chini ya utawala wa Mungu lazima ashuhudie. Je, haya hayaonyeshi kwamba katika enzi ya sasa, Mungu hawezi kusubiri kukamilisha mpango Wake na kuokoa watu Anaotaka kuokoa? Katika hali hizi, Mungu anajali kuhusu nini zaidi? Si vile wale wasiomfuata Yeye kabisa au wale wanaompinga Yeye kwa vyovyote vile wanamshughulikia Yeye au kumpinga Yeye, au namna ambavyo mwanadamu anamdanganya Yeye. Anajali tu kuhusu kama wale wanaomfuata Yeye, walengwa wa wokovu Wake katika mpango Wake wa usimamizi, wamewekwa kamili na Yeye, na kama wametimiza utoshelezi Wake. Kuhusiana na watu wale wengine bali na wale wanaomfuata Yeye, Anawatolea tu adhabu kidogo mara kwa mara ili kuonyesha ghadhabu Yake. Kwa mfano tsunami, mitetemeko ya ardhi, kuibuka kwa volkano na kadhalika. Wakati huohuo, Anawalinda kwa dhati na kuwashughulikia wale wanaomfuata Yeye na karibu wanaokolewa na Yeye. Tabia ya Mungu ni hii: Kwa mkono mmoja, Anaweza kuwapatia watu Anaonuia kutekeleza subira na ustahimilivu kamili wa kupindukia na kuwasubiria wao kwa muda mrefu Anavyoweza; kwa mkono mwingine, Mungu anachukia na kuchukizwa kwa dhati na watu wa aina ya Shetani wasiomfuata Yeye na wanaompinga Yeye. Ingawaje Hajali kama hawa watu wa aina ya Shetani wanamfuata au wanamwabudu Yeye, bado Anawachukia wao huku akiwa na subira na wao katika moyo Wake, na Anapoamua mwisho wa hawa watu wa aina ya Shetani, Yeye pia anasubiria kufika kwa hatua za mpango Wake wa usimamizi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni