Jumatatu, 15 Januari 2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I | A. Adamu na Hawa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia,
Amri ya Mungu kwa Adamu

A. Adamu na Hawa

1. Amri ya Mungu kwa Adamu

(Mwa 2:15-17) BWANA Mungu akamchukua huyo mtu, na akamweka katika bustani ya Edeni ili ailime na kuitunza. BWANA Mungu akamwamuru huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani unaweza kula: Lakini ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, usiyale: kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo hakika utakufa.

Mwenyezi Mungu alisema,Je, mlielewa chochote kutoka kwenye mistari hii? Je, ni vipi ambavyo sehemu hii ya maandiko inavyo wafanya kuhisi? Kwa nini “Amri ya Mungu kwa Adamu” ilidondolewa kutoka kwa maandiko? Je, kila mmoja wenu sasa anayo picha ya Mungu na Adamu katika akili yenu? Mnaweza kujaribu kufikiria: Kama ni nyinyi mliokuwa katika tukio hilo, je, Mungu katika moyo wenu angekuwa vipi? Ni hisia gani ambazo picha hii zinafanya mhisi? Hii ni picha ya kusisimua na ya kutuliza moyo. Ingawaje kunaye Mungu tu na binadamu ndani yake, ule ukaribu kati yao unastahili kuonewa wivu: Upendo mwingi wa Mungu amepewa binadamu kwa ukarimu, unamzunguka binadamu; binadamu ni mnyofu na asiye na hatia, aliye huru kabisa na asiyejali chochote, anayeishi kwa furaha kwa uangalizi wa jicho la Mungu; Mungu anaonyesha hali ya kujali binadamu huku naye binadamu anaishi katika ulinzi na baraka za Mungu; kila kitu binadamu anachofanya na kusema kinaunganishwa kwa karibu na Mungu na hakiwezi kutofautishwa.
Mnaweza kusema kwamba hii ndiyo amri ya kwanza ya Mungu aliyoitoa kwa binadamu tangu kumuumba yeye. Je, amri hii ina nini? Amri hii inayo mapenzi ya Mungu, lakini pia inayo wasiwasi Wake kwa wanadamu. Hii ndiyo amri ya kwanza ya Mungu na pia ndio mara ya kwanza Mungu anakuwa na wasiwasi kuhusu binadamu. Hivi ni kusema, Mungu analo jukumu kwa binadamu tangu ule wakati alipomuumba yeye. Jukumu Lake ni lipi? Lazima amlinde binadamu, kumwangalia binadamu. Anatumai kwamba binadamu anaweza kuamini na kutii maneno Yake. Hili pia ndilo tarajio la kwanza la Mungu kwa binadamu. Na ni kwa tarajio hili kwamba Mungu anasema yafuatayo: “Matunda ya kila mti wa bustani unaweza kula: Lakini ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, usiyale: kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo hakika utakufa.” Maneno haya rahisi yanawakilisha mapenzi ya Mungu. Yanafichua pia kwamba moyo wa Mungu tayari umeanza kuonyesha hali ya kujali binadamu. Miongoni mwa mambo yote, ni Adamu pekee aliyeumbwa kwa taswira ya Mungu; Adamu alikuwa kiumbe wa pekee aliye hai aliye na pumzi ya uhai ya Mungu; angeweza kutembea na Mungu, kuzungumza na Mungu. Na ndiyo maana Mungu alimpa amri kama hiyo. Mungu aliweka wazi katika amri hii kile binadamu anaweza kufanya, na vilevile akaweka wazi kile asichoweza kufanya.
Katika maneno haya machache rahisi, tunauona moyo wa Mungu. Lakini ni aina gani ya moyo tunaouona? Je, kunao upendo katika moyo wa Mungu? Je, upendo huo unao hali yoyote ya kujali ndani yake? Upendo wa Mungu na kujali kwake katika mistari hii hakuwezi kutambulika na kuthaminiwa tu na watu, lakini unaweza pia kuhisiwa vizuri na kwa kweli. Hayo ni kweli? Kwa vile nimesema tayari mambo haya, bado mnafikiria kwamba haya ni maneno machache tu rahisi? Si rahisi hivyo, kweli? Mngeweze kuona hivi awali? Kama Mungu mwenyewe angekuambia maneno hayo machache ungehisi vipi ndani yenu? Kama wewe si mtu mwenye utu, kama moyo wako ni baridi kama barafu, basi usingehisi chochote, usingethamani upendo wa Mungu, na usingejaribu kuuelewa moyo wa Mungu. Lakini kama wewe ni mtu mwenye dhamiri, mwenye ubinadamu, basi utahisi tofauti. Utahisi joto, utahisi kuwa umetunzwa na umependwa, na utahisi furaha. Je, hayo ni kweli? Unapohisi mambo haya, utatenda vipi kwa Mungu? Utahisi ukiwa umeunganishwa kwa Mungu? Utampenda na kumheshimu Mungu kutoka kwenye sakafu ya moyo wako? Moyo wako utakuwa karibu zaidi na Mungu? Unaweza kuona kutoka kwa haya namna ambavyo upendo wa Mungu ulivyo muhimu kwa binadamu. Lakini kile kilicho muhimu zaidi ni kuthamini na kufahamu kwa binadamu upendo huu wa Mungu. Kwa hakika, Mungu hasemi mambo mengi yanayofanana kwenye awamu hii ya kazi Yake? Lakini je, watu wa leo wanauthamini moyo wa Mungu? Je, mnaweza kung'amua mapenzi ya Mungu Niliyoyazungumzia muda mfupi uliopita? Hamwezi hata kutambua mapenzi ya Mungu wakati yanaonekana waziwazi, yanaweza kushikika na ni ya kihalisia. Na ndiyo maana Nasema hamna maarifa na uelewa halisi wa Mungu. Je, haya si kweli? Hayo tu ndiyo yote tutakayowasiliana nanyi kwenye sehemu hii.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli,
Adamu aitwaye mnyama

2. Mungu Amuumba Hawa

(Mwa 2:18-20) BWANA Mungu akasema, Si vizuri kwamba huyo mtu awe peke yake; Nitamfanyia msaidizi wa kupatana naye. Na kutoka katika ardhi BWANA Mungu akaumba kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani; akamletea Adamu ili aone atawaitaje: na kila ambacho Adamu alikiita kiumbe hai, likawa ndilo jina lake kuanzia siku hiyo. Adamu akawapa majina kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakupatikana wa kumsaidia Adamu aliyefanana.
(Mwa 2:22-23) Na ule ubavu, ambao BWANA Mungu aliuchukua kutoka kwa Adamu, yeye akaufanya mwanamke, na akamleta kwa Adamu. Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa wa mifupa yangu, na nyama ya nyama zangu: basi ataitwa Mwanamke, kwa maana ametwaliwa kutoka kwa Mwanamume.
Kunazo kauli kuu chache kwenye sehemu hii ya maandiko. Tafadhali zichoree mstari chini: “na kila ambacho Adamu alikiita kiumbe hai, likawa ndilo jina lake kuanzia siku hiyo.” Kwa hivyo ni nani aliyepatia viumbe wote haya majina yao? Alikuwa Adamu, si Mungu. Kauli hii inamwambia mwanadamu ukweli: Mungu alimpa binadamu werevu alipomuumba Yeye. Hivi ni kusema kwamba, werevu wa binadamu ulitoka kwa Mungu. Hili ni kweli. Lakini kwa nini? Baada ya Mungu kumuumba Adamu, Adamu alienda shuleni? Je, alijua namna ya kusoma? Baada ya Mungu kuwaumba viumbe hai mbalimbali, je Adamu aliwatambua wanyama hawa wote? Je, Mungu alimwambia majina ya viumbe hao? Bila shaka, Mungu pia hakumfunza namna ya kutunga yale majina ya viumbe hawa. Huo ndio ukweli! Basi alijua vipi namna ya kupatia viumbe hawa hai majina yao na aina gani ya majina ya kuwapatia? Haya yote yanahusiana na swali kuhusu ni nini ambacho Mungu aliongezea kwa Adamu alipomuumba yeye. Ukweli unathibitisha kwamba wakati Mungu alipomuumba binadamu Alikuwa ameongezea werevukwake. Huu ni ukweli muhimu sana. Je, nyinyi nyote mmesikiliza kwa makini? Kunao ukweli mwingine muhimu ambao unafaa kuwa wazi kwenu? Baada ya Adamu kuwapatia viumbe hai majina yao, majina haya yalipangwa kwenye msamiati wa Mungu. Kwa nini Ninasema hivyo? Hii pia inahusisha tabia ya Mungu, na lazima Niielezee.
Mungu alimuumba binadamu, Akapumua maisha ndani yake, na pia Akampa baadhi ya werevu Wake, uwezo Wake, na kile Anacho na alicho. Baada ya Mungu kumpa binadamu mambo haya yote, binadamu aliweza kufanya baadhi ya mambo haya kwa uhuru na kufikiria pekee yake. Kama kile binadamu anaunda na kufanya ni kizuri machoni mwa Mungu, basi Mungu anakikubali na haingilii kati. Kama kile binadamu anafanya ni sahihi, basi Mungu atakiacha tu kiwe hivyo milele Kwa hivyo kauli hii “na kila ambacho Adamu alikiita kiumbe hai, likawa ndilo jina lake kuanzia siku hiyo” inaonyesha nini? Inaopendekeza kwamba Mungu hakufanya marekebisho yoyote kwa majina ya wale viumbe mbalimbali hai. Jina lolote lile ambalo Adamu alimwita, Mungu alisema “Ndiyo” na akasajili jina hilo hivyo. Je, Mungu alionyesha maoni yoyote? La, hilo ni hakika. Kwa hivyo, mnaona nini hapa? Mungu Alimpa binadamu werevu naye binadamu akautumia werevu wake aliopewa na Mungu kufanya mambo. Kama kile binadamu anafanya ni kizuri machoni mwa Mungu, basi kinathibitishwa, kutambulika, na kukubalika na Mungu bila ya utathmini au upinzani wowote. Hili ni jambo ambalo hakuna mtu wala roho wa maovu, wala Shetani, anaweza kufanya. Je, mnauona ufunuo wa tabia ya Mungu hapa. Je, mwanadamu, mwanadamu aliyepotoshwa, au Shetani anaweza kuwakubali wengine kuwawakilisha katika kufanya mambo huku wakitazama? Bila shaka la! Je, wanaweza kupigania cheo na yule mtu mwengine au nguvu nyingine ambayo ni tofauti na wao? Bila shaka wangefanya hivyo! Na kwa muda huo, kama angekuwa ni mtu aliyepotoshwa au Shetani aliyekuwa na Adamu, bila shaka wangekataa kile ambacho Adamu alikuwa akifanya. Ili kuthibitisha kwamba wanao uwezo wa kufikiria kwa uhuru na wanayo maono yao binafsi na ya kipekee, wangekataa kabisa kila kitu alichofanya Adamu: Unataka kukiita hivyo? Kwa kweli, sitakiita hivyo, nitakiita hivi; ulikiita Tom lakini mimi nitakiita Harry. Lazima nionyeshe ustadi wangu. Haya ni aina gani ya asili? Hii ni asili ya kiburi kisicho na mipaka? Lakini Mungu anayo tabia kama hii? Je, Mungu alikuwa na upinzani wowote usiokuwa wa kawaida kwa mambo haya ambayo Adamu alifanya? Jibu ni bila shaka la! Kati ya tabia ambayo Mungu anafichua, hakuna hata chembe ya ubishi, ya kiburi, au kujigamba kwa nafsi. Hilo liko wazi kabisa hapa. Hili ni jambo dogo tu, lakini kama huelewi kiini cha Mungu, kama moyo wako hautajaribu kujua namna ambavyo Mungu anatenda na mwelekeo wa Mungu ni ipi, basi hutajua tabia ya Mungu au kuyaona maonyesho na ufunuo wa tabia ya Mungu. Je, hayo si kweli? Je, unakubali kile Nimetoka tu kukuelezea? Kwa kujibu matendo ya Adamu, Mungu hakutangaza kwa sauti kwamba, “Umefanya vyema. Umefanya sahihi Ninakubali.” Katika Moyo Wake, hata hivyo, Mungu aliidhinisha, akathamini, akashangilia kile Adamu alikuwa amefanya. Hili ndilo jambo la kwanza tangu uumbaji ambalo binadamu alikuwa amemfanyia Mungu akifuata maagizo Yake. Ni jambo ambalo binadamu alifanya badala ya Mungu na kwa niaba ya Mungu. Mbele ya macho yake, hili lilitokana na werevu Aliokuwa amempa binadamu. Mungu aliliona kama jambo zuri, kitu kizuri. Kile ambacho Adamu alifanya wakati huo kilikuwa maonyesho ya kwanza ya werevu wa Mungu kwa binadamu. Hili lilikuwa onyesho zuri kutoka kwa maoni ya Mungu. Kile Ninachotaka kukuambia nyinyi hapa ni kwamba nia ya Mungu katika kuongezea sehemu ya kile Anacho na alicho na werevu wake kwa binadamu ilikuwa ili mwanadamu aweze kuwa kiumbe hai anayemwonyesha Yeye. Kwa kiumbe hai kama huyo kufanya mambo hayo kwa niaba yake, ilikuwa ndicho hasa kile Mungu alikuwa akitamani kuona.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, neema,
Adamu na Hawa
3. (Mwa 3:20-21) Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa mama ya wote walio hai. Pia BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi; na akawavisha.
Hebu tuangalie kifungu hiki ya tatu, kiachosema kwamba, kunayo maana katika jina Adamu alimpa Hawa, kweli? Hii inaonyesha kwamba baada ya kuumbwa, Adamu alikuwa na fikira zake na alielewa mambo mengi. Lakini kwa sasa, hatutasoma na kuchunguza kile alichoelewa au kwa kiwango kipi alielewa kwa sababu hiyo si hoja kuu Ninayotaka kuzungumzia kwenye kifungu hiki ya tatu. Hivyo hoja kuu katika kifungu cha tatu ni gani? Hebu na tuuangalie mstari huo, “Pia BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi; na akawavisha.” Kama hatutakuwa na ushirika kuhusu mstari huu wa maandiko leo, huenda hamtawahi kutambua uzito ulio katika maneno haya. Kwanza, hebu niwape vidokezo fulani. Panua kufikiria kwenu na kuona picha ya bustani ya Edeni, huku Adamu na Hawa wakiishi ndani. Mungu anaenda kuwatembelea lakini wanajificha kwa sababu wako uchi. Mungu hawezi kuwaona, na baada ya kunawaita wao, wanasema, “Hatuwezi kudhubutu Kuwaona kwa sababu tuko uchi.” Hawathubutu kumwona Mungu kwa sababu wako uchi. Kwa hivyo Yehova Mungu anawafanya nini? Mandishi asilia yanasema: “Pia BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi; na akawavisha.” Sasa mnajua kile Mungu alitumia kutengeneza nguo zao? Mungu alitumia ngozi za wanyama kutengeneza nguo zao. Hivyo ni kusema, nguo ambazo Mungu alitengenezea binadamu zilikuwa za koti la manyoya. Hiki ndicho kilichokuwa kipande cha kwanza cha nguo ambacho Mungu alitengenezea binadamu. Koti la manyoya ni mavazi ya soko la vitu vya bei ghali kwa viwango vya leo, kitu ambacho si kila mtu anaweza kumudu kuvaa. Kama mtu atakuuliza: Kipande cha kwanza cha nguo kilichovaliwa na wazee wa wanadamu kilikuwa kipi? Unaweza kujibu: Kilikuwa ni koti la manyoya. Nani aliyekitengeneza hicho koti la manyoya? Unaweza kujibu zaidi: Mungu alikitengeneza! Hiyo ndiyo hoja kuu: Nguo hii ilitengenezwa na Mungu. Je, hilo ni jambo la kutilia maanani, sivyo? Kwa vile sasa nimetoka kukifafanua, picha imeibuka katika akili zenu ? Kunafaa kuwa angaa na mpangilio wa juu kukihusu. Hoja ya kuwaambia haya leo si kuwafahamisha kuhusu kipande cha kwanza cha nguo cha binadamu kilikuwa nini. Hivyo hoja ni gani? Hoja si lile koti la manyoya, lakini namna ya kujua tabia na uwepo na milika zilizofichuliwa na Mungu alipokuwa Akifanya hivi.
Katika picha hii ya ““Pia BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi; na akawavisha,” ni wajibu gani ambao Mungu anatekeleza anapokuwa na Adamu na Hawa? Na ni katika aina gani ya uajibu ambao Mungu anajitokeza katika uliwengu akiwa tu na wanadamu wawili? Kutekeleza wajibu wa Mungu? Kaka na dada kutoka Hong Kong, tafadhali jibuni. (Kutekeleza wajibu wa mzazi.) Kaka na dada kutoka Korea Kusini, ni wajibu wa aina gani mnafikiria Mungu anatekeleza hapa? (Kiongozi wa familia.) Kaka na dada kutoka Taiwan, mnafikiria nini? (Wajibu wa mtu katika familia ya Adamu na Hawa, wajibu wa mwanafamilia.) Baadhi yenu mnafikiria kuwa Mungu anajitokeza kama mwanafamilia wa Adamu na Hawa, huku baadhi wakisema kwamba Mungu anajitokeza kama kiongozi wa familia na wengine wanasema kwamba Anajitokeza kama mzazi. Haya yote yanafaa sana. Lakini ni nini hasa Ninachotilia mkazo hapa? Mungu aliwaumba watu hawa wawili na kuwashughulikia kama mtu na mwandani Wake. Akiwa ndiye mwanafamilia pekee wao, Mungu aliangalia kuishi kwao na pia akakidhi mahitaji yao ya kimsingi. Hapa, Mungu anajitokeza kama mzazi wa Adamu na Hawa. Huku Mungu akifanya haya, binadamu haoni namna ambavyo Mungu alivyo mkuu; haoni mamlaka ya juu zaidi ya Mungu, hali Yake ya mafumbo, na hasa haoni hasira au adhama Yake. Kile anachoona tu ni unyenyekevu wa Mungu, upendo Wake, kujali Kwake binadamu na jukumu Lake na utunzaji Wake kwake yeye. Mwelekeo na njia ambayo Mungu alishughulikia Adamu na Hawa ni sawa na namna ambavyo wazazi wa kibinadamu wanavyoonyesha hali ya kuwajali watoto wao binafsi. Ni kama pia namna ambavyo wazazi wa kibinadamu wanavyopenda, kuangalia, na kutunza watoto wao binafsi wa kiume na kike—halisia, namna ya kuonekana, na kushikika. Badala ya kujiweka Yeye Mwenyewe katika cheo cha juu na cha utukufu, Mungu mwenyewe alitumia ngozi kutengeneza nguo za binadamu. Haijalishi kama koti hili la manyoya lilitumika kufunika uchi wao au wao kujikinga dhidi ya baridi. Kwa ufupi, nguo hii iliyotumika kuufunika mwili wa binadamu ilitengenezwa na Mungu mwenyewe kwa mikono Yake mwenyewe. Badala ya kuitengeneza tu kupitia kwa fikira au kwa mbinu za kimiujiza kama watu wanavyofikiria, Mungu alikuwa amefanya kitu cha halali kwa binadamu ambacho binadamu anafikiria Mungu hawezi na hafai kufanya. Kitu hiki kinaweza kuwa rahisi ambacho baadhi huenda hata wasifikirie kwamba kinastahili kutajwa, lakini kinawaruhusu pia wale wote wanaomfuata Mungu lakini awali walikuwa na mawazo yasiyoeleweka kuhusu Yeye kuweza kupata maono kuhusu ukweli na uzuri Wake, na kuuona uaminfu Wake na asili Yake ya unyenyekevu. Kinawafanya watu wenye kiburi kisicho na kifani wanaofikiria kwamba wako juu na wanao utukufu kuinamisha vichwa vyao kwa aibu mbele ya ukweli na unyenyekevu wa Mungu. Hapa, ukweli na unyenyekevu wa Mungu unawezesha zaidi watu kuona namna ambavyo Anapendeka. Kwa kinyume cha mambo, yule Mungu mkubwa sana, Mungu anayependeka na yule Mwenyezi Mungu katika mioyo ya watu ni mdogo sana, asiyevutia, na asiyeweza kuhimiliwa hata mara moja. Unapouona mstari huu na kuisikia hadithi hii, unamkasirikia Mungu kwa sababu Alifanya kitu kama hiki? Baadhi ya watu wanaweza kufanya hivyo, lakini kwa wengine itakuwa ni tofauti kabisa. Watafikiri Mungu ni mkweli na anapendeka, na hasa ni ule ukweli na uzuri wa Mungu ndiyo unaowafurahisha. Kwa kadri wanavyoona ule upande wa kweli wa Mungu, ndipo wanapothamini uwepo wa kweli wa upendo wa Mungu, umuhimu wa Mungu katika mioyo yao, na namna anavyosimama kando yao kila muda.
Kwa wakati huu, tunafaa kuunganisha mazungumzo yetu na sasa. Kama Mungu angeweza kufanya mambo haya madogo mbalimbali kwa binadamu Aliowaumba hapo mwanzo kabisa, hata vitu vingine ambavyo watu hawangethubutu kufikiria ama kutarajia, basi naye Mungu angewafanyia watu leo mambo kama hayo? Baadhi ya watu husema, “Ndiyo!” Kwa nini hivyo? Kwa sababu kiini cha Mungu si bandia, uzuri Wake si bandia. Kwa sababu kiini cha Mungu kwa kweli kipo, na si kitu kilichoongezewa tu na wengine na bila shaka si kitu ambacho kinabadilika na mabadiliko ya muda, mahali, na enzi. Ukweli na uzuri wa Mungu unaweza kwa kweli kuonyeshwa kupitia kufanya jambo ambalo watu wanafikiria si la kipekee na ni dogo, jambo ambalo ni dogo sana kiasi cha kwamba watu hata hawafikirii angeweza kufanya. Mungu si mnafiki. Hakuna kupiga chuku, kufunika ukweli, majivuno au kiburi katika tabia na kiini Chake. Siku zote Hajigambi, lakini badala yake Anapenda, Anaonyesha hali ya kujali, Anaangalia, na kuwaongoza wanadamu Aliowaumba kwa uaminifu na dhati. Haijalishi ni kiwango kipi ambacho watu wanaweza kuthamini, kuhisi, au kuona, Mungu kwa hakika anafanya mambo haya. Je, kujua kwamba Mungu anacho kiini kama hicho kunaweza kuathiri upendo wa watu kwake Yeye? Kutaweza kushawishi namna wanavyomcha Mungu? Ninatumai utakapoelewa upande halisi wa Mungu utaweza kuwa hata karibu zaidi na Yeye na kuweza kuthamini hata zaidi na kwa kweli upendo Wake na utunzaji Wake kwa wanadamu, huku wakati huohuo pia kumpa moyo wako na kutowahi tena kuwa na shaka au wasiwasi wowote kwake Yeye. Mungu anafanya kimyakimya kila kitu Alicho nacho kwa ajili ya binadamu, akifanya kimyakimya kupitia ukweli, uaminifu, na upendo Wake. Lakini siku zote Hana hofu au majuto yoyote kwa yale yote Anayofanya, wala hahitaji mtu yeyote kumlipa Yeye kwa njia yoyote au kuwa na nia za kuwahi kupokea kitu kutoka kwa wanadamu. Kusudio tu la kila kitu Alichowahi kufanya ni ili Aweze kupokea imani na upendo wa kweli kutoka kwa wanadamu. Hebu tuhitimishe mada hii ya kwanza hapa.
Je, mazungumzo haya yamewasaidia? Yamewasaidia kwa kiasi kipi? (Uelewa na maarifa zaidi kuhusu upendo wa Mungu.) (Mbinu hii ya mawasiliano inaweza kutusaidia katika siku za mbele ili kuweza kuthamini zaidi neno la Mungu, kufahamu hisia alizokuwa nazo na maana ya mambo Aliyoyasema Alipoyasema, na kuhisi namna Alivyohisi wakati huo.) Je, yupo yeyote kati yenu anayehisi hata zaidi uwepo halisi wa Mungu baada ya kuyasoma maneno haya? Je, mnahisi uwepo wa Mungu si mtupu wala wa kutiliwa mashaka tena? Pindi mnapokuwa na hisia hii, mnahisi kwamba Mungu yupo tu kando yenu? Pengine hisia hiyo si ya dhahiri kwa sasa hivi au hamtaweza kuihisi sasa hivi bado. Lakini siku moja, mtakapokuwa na shukrani ya kina na ya kweli na maarifa halisi kuhusu tabia na kiini cha Mungu ndani ya moyo wako, utahisi kwamba Mungu yupo tu kando yako—ni vile tu kwamba haujawahi kumkubali kwa kweli Mungu ndani ya moyo wako. Haya ni halisi.
Mnafikiria vipi kuhusu mbinu hii ya mawasiliano? Mnaweza kuiendeleza? Mnafikiria aina hii ya ushirika kuhusu mada ya kazi ya Mungu na tabia ya Mungu ni nzito? Mnahisi vipi? (Vizuri sana, kuchangamka.) Ni nini kilichowafanya kuhisi vizuri? Kwa nini mlichangamka? (Ilikuwa sawa na kurudi kwenye Bustani ya Edeni, kurudi kuwa kando ya Mungu.) “Tabia ya Mungu” kwa kweli ni mada ambayo haijazoeleka sana na kila mmoja, kwa sababu kile ambacho unafikiria kwa kawaida, kile unachosoma kwenye vitabu au hapa kwenye ushirika, siku zote hukufanya kuhisi kama mtu asiyeona akimgusa ndovu—unahisi tu kila pahali kwa kutumia mikono yako, lakini kwa hakika huoni chochote kwa macho yako. Mguso wa mkono hauwezi tu kukupa mpangilio wa kimsingi wa maarifa ya Mungu, wacha hata dhana iliyo wazi. Kile ambacho mguso wa mkono unakupatia ni kufikiria zaidi, kiasi kwamba huwezi kufafanua kwa uhakika tabia ya Mungu na kiini halisi. Badala yake, masuala haya ya kutokuwa na uhakika yanayotokana na kufikiria kwako huwa siku zote yanaonekana kujaza moyo wako na shaka. Wakati ambapo huwezi kuwa na uhakika kuhusu kitu na ilhali bado unajaribu kukielewa, ndani ya moyo wako bado siku zote kutaendelea kuwa na mambo yanayopingana na ukinzana, na wakati mwingine huenda hata yakabadilika na kuwa shida, na kukufanya kuhisi ni kana kwamba umepoteza kitu. Je, si jambo la kusikitisha sana unapotaka kumtafuta Mungu, kumjua Mungu, na kumwona Yeye waziwazi, lakini siku zote kutoweza kupata majibu? Bila shaka, maneno haya yanalengwa kwa wale wanaotamani kutafuta uwezo wa kumuheshimu sana Mungu na kuridhisha Mungu. Kwa wale watu ambao hawatilii maanani mambo kama haya, hili kwa hakika si muhimu kwa sababu wanatumaini kwamba ni bora zaidi kwamba uhalisi na uwepo wa Mungu uwe ni ngano ya kale au ndoto, ili waweze kufanya chochote wanachotaka, ili waweze kuwa wale wakubwa zaidi na wenye umuhimu zaidi, na kuweza kutenda vitendo vya maovu bila ya kujali athari zake, na hivyo basi kutoweza kukabiliana na adhabu au kulazimika kuwajibika , ili hata mambo ambayo Mungu anasema kuwahusu watendaji maovu hayataweza kuwahusu wao. Watu hawa hawako radhi kufahamu tabia ya Mungu, wamechoshwa na kujaribu kujua Mungu na kila kitu kuhusu Yeye. Wangependelea kwamba Mungu asiwepo. Watu hawa wanampinga Mungu na wao ndio watakaoondolewa.
                 kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi:  Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni