Jumapili, 23 Septemba 2018

Hukumu Ni Mwanga (I)

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Hukumu

📖📖Hukumu Ni Mwanga (I)

Zhao Xia Mkoa wa Shandong
Jina langu ni Zhao Xia. Nilizaliwa katika familia ya kawaida. Kutokana na ushawishi wa misemo kama “Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo,” na “Kama vile mti huishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” sifa na heshima zikawa muhimu sana kwangu. Kila kitu nilichofanya kilikuwa ili kupata sifa, pongezi, na upendezwaji wa watu wengine. Baada ya kuolewa, malengo niliyojiwekea yalikuwa: Nitaishi maisha ya kitajiri zaidi kuliko wengine; Ni lazima nisiruhusu mtu yeyote kusema mambo hasi kuhusu jinsi ninavyowatendea wazee au kuhusu tabia na mwenendo wangu; na nitahakikishia mtoto wangu ataingia katika chuo kikuu cha kifahari na ana matarajio mazuri, ili kuongeza fahari zaidi katika heshima yangu. Kwa hivyo, sikuwahi kugombana na wakwe wangu. Mara nyingine, wakati walisema maneno makali kwangu, ningehisi nimekerwa mno mpaka ningejificha na kulia badala ya kuwapa uhasi. Wakati niliona wengine wakiwanunulia wazazi wao nguo wakati wa Mwaka Mpya wa Kichina na sikukuu zingine, ningeenda mara moja kumnunulia mama mkwe wangu baadhi, na ingekua pia ya ubora wa hali ya juu. Wakati jamaa walikuja kunitembelea, ningesaidia kununua vyakula na kupika. Hata wakati ilikuwa ngumu na ya kuchosha kiasi bado ningekuwa radhi kabisa. Nikihofia kuwa ningekuwa na utajiri kiasi kuliko wengine, niliacha mtoto wangu wa kike nyuma mwezi mmoja baada ya kumzaa na kurudi mara moja kazini. Matokeo yake yakawa, binti yangu alipata maumivu ya utapiamlo na akawa tu ngozi na mifupa kwa sababu hangeweza kunywa maziwa ya matiti yangu. Hali yake iliimarika tu baada ya sindano 100 za lishe, ilhali nilikuwa nimechoka sana kiasi kwamba nilikuwa na maumivu ya mgongo kila siku. Ingawa ilikuwa ngumu na yenye kuchokesha, nilivumilia shida hizo na nilijitolea kwa bidii kwa ajili ya kupata sifa nzuri. Katika miaka michache tu, nikawa mkwe maarufu katika kijiji, na familia yangu ikawa tajiri na kuonewa kijicho na watu walio karibu nasi. Matokeo yake yakawa, wakwe zangu, majirani, jamaa na marafiki wote walinisifu sana. Katika kukabiliwa na sifa na taadhimu kutoka kwa wale walio karibu nami, kiburi changu kilitoshelezwa sana. Nilihisi shida zangu wakati wa kipindi cha miaka michache iliyopita hazikuwa za bure, na nilikuwa nimefurahishwa sana kindani. Hata hivyo, maisha yangu ya utulivu yalikatishwa baada ya shemeji wangu kuolewa. Mke wake alinena nami kwa kejeli daima, akisema kuwa nilikuwa na nia fiche kwa kumtendea mama mkwe wetu vyema kwa sababu nilikuwa nataka tu mali yake. Yeye alikuwa akisema kila mara kuwa mama mkwe wetu alikuwa na upendeleo kwani alitupa sisi vitu vingi zaidi kuliko alivyowapa wao, na mara nyingi tulikuwa tukigombana kwa sababu ya haya. Nilihisi kuudhika mno na nilitaka kubishana naye hadharani ili kulalamika kutokuwa na hatia kwangu, lakini ingeweza kuharibu picha nzuri niliyokuwa nimejenga ndani ya mioyo ya watu. Kwa hivyo, ningejizuia kwa lazima, na wakati singeweza kuvumilia tena ningekuwa na kilio kikubwa kwa faragha. Baadaye, wifi huyo alisukuma bahati yake kwa kumiliki ardhi iliyosambazwa kwa upande wangu wa familia, iliyonifanya nitingike kwa hasira na nisikule au kunywa kwa masiku. Nilitaka hata pia kupambana naye hadi suluhu ipatikane. Hata hivyo, nikifikiria kwamba ingeweza kunifanya kupoteza heshima, kuharibu sifa yangu, na kufanya wale walio karibu nami kunidharau, nilimeza hayo yote, lakini ndani nilihisi nimekazwa mno kiasi kwamba nilikuwa na maumivu. Nilionekana mwenye majonzi na nilitanafusi siku nzima, nikihisi kama ilikuwa chungu sana na ya kuchosha kuishi na kutojua wakati kungekuwa na mwisho kwa maisha kama hayo.
Mwisho wa binadamu kweli ndio mwanzo wa Mungu. Pindi wakati nilikuwa na maumivu na kuhisi mnyonge, Mwenyezi Mungu alinyoosha mikono Yake ya wokovu kwangu. Siku moja, jirani yangu aliniuliza: "Unaamini katika uwepo wa Mungu?" Nilijibu: "Nani asiye? Ninaamini Mungu yupo." Kisha akasema kwamba Mungu anayeamini ndiye Mungu pekee na wa kweli aliyeumba ulimwengu na vitu vyote, na kwamba mwanzoni, binadamu waliishi katika baraka za Mungu kwa sababu walimwabudu Mungu, lakini baada ya wao kupotoshwa na Shetani, hawaabudu tena Mungu na ndivyo basi wanaishi chini ya laana na maumivu kwa Mungu. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho alikuja kuwapa watu ukweli na kuwaokoa kutoka kwenye lindi kuu la taabu. Kwa kuongezea, pia aliwasiliana uzoefu wake mwenyewe wa kumwamini Mungu. Baada ya kusikiza mawasiliano yake, nilihisi kuwa nimepata msiri wangu wa karibu sana, na singeweza kujizuia kuelezea maumivu yote moyoni mwangu. Baadaye, alinisomea kifungu cha neno la Mungu:“Unapokuwa umechoka na unapoanza kuona huzuni katika ulimwengu huu, usifadhaike, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote. Yupo pembeni mwako Anakuangalia, anakusubiri uweze kumrudia. Anasubiri siku ambayo kumbukumbu zako zitarejea: kuwa na utambuzi wa ukweli kwamba ulitoka kwa Mungu, kwa namna fulani na mahala fulani umepotea, umeanguka barabarani ukiwa hujitambui, halafu pasipo kujua unakuwa na 'baba.' Halafu tena unatambua kuwa Mwenye Uweza amekuwa akiangalia, akisubiri kurejea kwako muda huu wote” (“Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalitiririka ndani ya moyo wangu kama mkondo wenye joto, yakituliza moyo wangu wenye uchungu na huzuni, na singeweza kuzuia machozi yangu kumwagika. Wakati huo huo, nilihisi kama mtoto aliye na mateso aliyepotea na aliyerudi kwa ghafla katika kumbatio la mama yake. Kulikuwa na msisimko usioweza kusemeka na mhemuko katika moyo wangu. Niliendelea kumshukuru Mungu, kwa sababu alinichukua katika nyumba Yake na kunijalia wakati sikuwa na pengine pa kwenda. Nitafuata Mungu kwa moyo na roho yangu! Tangu wakati huo, nilisoma maneno ya Mungu, nikamwomba Mungu, na niliimba nyimbo za kumsifu Mungu kila siku, mambo yalilonifanya kutulia hasa katika moyo wangu. Kwa kuhudhuria mikutano, niliona kuwa ndugu walikuwa kama familia kubwa, ingawa wao hawana uhusiano wa damu. Uingiliano wao ulikuwa wa kawaida na wazi, ulikuwa umejaa uelewa, ustahamilivu, na uvumilivu, na haukuwa na wivu, mgongano na kupanga njama au kisingizio na unafiki. Hawakuwadhulumu maskini ilhali wakipenda matajiri, na wote waliweza kutendea kila mtu na unyofu na usawa. Moyo wangu ungehisi huru hasa wakati tuliimba nyimbo za kumsifu Mungu pamoja. Kwa sababu hiyo nilipendezwa na maisha haya ya kanisa yenye upendo na ukunjufu, ya haki na yenye furaha. Nilisadiki kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu pekee wa kweli na nilifanya uamuzi wangu kuwa ningemfuata hadi mwisho.
Kwa kupitia kusoma maneno ya Mungu, nilielewa hamu ya haraka ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu kwa kiwango kikubwa kiwezekanavyo, na kuona kwamba ndugu wengi walikuwa wakifanya kila liwezekanalo kujitoa na kujitumia kwa ajili ya kueneza injili ya ufalme. Hivyo basi pia nikajihusisha kikamilifu katika kuhubiri injili. Kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kuokoa na kubadili wanadamu. Ili kunitakasa na kunibadili mimi, Mungu alilenga asili yangu mbovu na alitekeleza adabu na hukumu Yake pamoja na rehema na wokovu juu yangu mara kwa mara. Wakati mmoja, nilikwenda kuhubiri injili kwa aliyeweza kuwa mwaminifu. Nilipogundua kuwa yeye alikuwa kiongozi, niliamua kuratibu na Mungu kumleta mbele Yake kwa vyovyote vile. Ilikuwa msimu wa kilimo wenye shughuli nyingi wakati huo. Baada ya kuona jinsi alivyokuwa na shughuli nyingi za kilimo, nilienda kufanya kazi pamoja naye huku nikimpa ushuhuda wa kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Nani angejua ya kwamba baada ya kuzungumza naye kwa siku tatu mtawalia angekuwa hana nia ya kuukubali tu na badala yake angenikaripia: "Wewe huna haya hata! Mimi tayari nilisema siyaamini haya, na bado huachi kuhubiri." Maneno yake yaliniumiza sana. Uso wangu ulichomeka ni kama nilikuwa nimechapwa makofi mara kadhaa hadharani, wakati moyo wangu uliuma na wimbi baada ya wimbi la maumivu hafifu yasiyo makali. Nilifikiria: Nilikuja kukuhubiria kwa nia njema na nilijichokesha nilipokusaidia na kazi yako hadi mgongo wangu ulipata maumivu, na bado badala ya kukubali hayo, ulinitendea hivi. Wewe ni katili kweli! Nilihisi nimeaibishwa mno na sikutaka kuzungumza naye tena, lakini pia nilihisi kuwa hii haikuwa inaambatana na nia za Mungu, kwa hivyo niliomba kwa ukimya moyoni mwangu na nilizuia maumivu yangu ya kindani ili kuendelea kuongea naye nilipokuwa nikimsaidia na kazi yake. Hata hivyo, haidhuru kwa bidii gani niliwasiliana sikuweza bado kumfikia. Niliporomoka kama mpira uliotolewa upepo niliporudi nyumbani. Maneno ya mlengwa wa mahubiri yangu yaliendelea kujitokeza kichwani mwangu. Nilivyofikiria zaidi kuhusu hayo ndivyo nilivyoteseka zaidi: Mbona ninajisumbua? Yote niliyoyapata kama malipo ya nia yangu njema yalikuwaa kuzomewa, kukashifiwa, na kunyanyaswa. Kwa kweli hii sio haki kabisa! Hakuna mtu aliyewahi kunitenda namna hii. Kueneza injili ni uchungu na ngumu kabisa! Hapana, siwezi kwenda nje kuhubiri injili tena! Ikiwa nitaendelea kuhubiri sitabaki na heshima yoyote ya kuona mtu yeyote. Wakati tu nilipohisi nimekosewa sana na mwenye maumivu kiasi kwamba sikuwa na hiari tena ya kuhubiri injili, maneno ya Mungu yalinipatia nuru: “Je, unajua mzigo ulio begani mwako, kazi yako na majukumu yako? Hisia yako ya kihistoria ya mwito iko wapi? … Wao ni masikini, wa kuhurumiwa, vipofu na waliopotea na wanalia gizani, ‘Njia iko wapi?’ Jinsi gani wanatamani mwangaza, kama nyota iangukayo kutoka angani, ianguke ghafla na kutawanya nguvu za giza zilizowakandamiza wanadamu kwa miaka mingi. Ni nani anayeweza kujua jinsi wanavyotumaini kwa hamu, na wanavyotamani hili usiku na mchana? Wanadamu hawa wanaoteseka mno wamebaki wafungwa katika jela za giza, bila tumaini la kuwachiliwa huru, hata ile siku ambayo mwanga utaonekana; ni lini hawatalia kwa uchungu tena? Roho hawa dhaifu ambao kamwe hawajapewa pumziko kwa hakika wanateseka na bahati hii mbaya. Kwa muda mrefu wamefungiwa nje na kamba zisizo na huruma na historia iliyokwama katika wakati. Ni nani amewahi kusikia sauti ya vilio vyao? Ni nani amewahi kuona nyuso zao zenye taabu? Umewahi kufikiria jinsi moyo wa Mungu ulivyosononeka na ulivyo na wasiwasi? Anawezaje kustahimili kuona mwanadamu asiye na hatia, Aliyemuumba kwa mikono Yake Mwenyewe akiteswa na makali? Mwishowe, wanadamu ndio wasio na bahati na waliopewa sumu. Hata ingawa wamenusurika mpaka siku hii, ni nani angefikiri kuwa wamepewa sumu na yule mwovu kwa muda mrefu? Je, umesahau kuwa wewe ni mmoja wa waathiriwa? Kwa ajili ya upendo wako kwa Mungu, una nia ya kufanya kila uwezalo kuwaokoa walionusurika? Je, huna nia , ya kutumia nguvu zako zote kulipiza Mungu anayempenda binadamu kama nyama na damu Yake Mwenyewe?” (“Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Mistari katikati ya maneno ya Mungu yote yalifichua hangaiko Lake na huzuni Yake yenye masikitiko na ya kuwajali watu wasio na hatia. Mungu hawezi kuvumilia kuona watu walioumbwa kwa mikono Yake mwenyewe wakidanganyika na kuumizwa na Shetani. Mungu anaendelea kusubiri kwa hamu sana kwa wanadamu kurudi katika nyumba Yake hivi karibuni ili wapokee wokovu mkubwa amewafadhili. Ilhali wakati nilipopatwa na maneno machache makali kutoka kwa mlengwa wangu wa mahubiri, nilihisi nimekosewa na kuteswa na nililalamika kuhusu shida na mateso hayo. Nilikuwa hata tena sina radhi ya kushirikiana kwa sababu nilikuwa nimefedheheka. Dhamiri na mantiki yangu ilikuwa wapi? Ili kutuokoa sisi watu potovu katika siku za mwisho, Mungu ameendelea kuwindwa na kuteswa na serikali kwa kila mara, kutelekezwa, kushutumiwa, kukufuriwa na kukashifiwa na jamii ya dini, na kuelewa visivyo na kupingwa na sisi wafuasi wa Mungu. Yale machungu na aibu Mungu amepitia ni mengi sana, ni mengi kabisa! Hata hivyo, Mungu hakuachana na wokovu Wake wa wanadamu, na aliendelea kutoa mahitaji ya wanadamu katika utulivu. Upendo wa Mungu ni mkubwa sana! Nafsi yake ni nzuri sana na yenye ukarimu! Taabu zangu leo ​​haziwezi kulinganishwa na mateso ambayo Mungu amepitia kwa ajili ya kuokoa mwanadamu! Nilikumbuka kuwa mimi nilikuwa pia mwathiriwa, mtu yule aliyekuwa amedhuruiwa na Shetani kwa miaka. Kama Mungu hangekuwa amenyoosha mikono Yake ya wokovu kwangu, ningekuwa bado ninan’gan’gana kwa uchungu katika giza, nisiweze kupata mwanga na matumaini ya kuishi. Kwa kufurahia wokovu wa Mungu, ninapaswa kuubeba aibu na maumivu ili kufanya lote liwezekanalo kushirikiana na Mungu, kutekeleza wajibu wangu vizuri, na kuleta watu wale wasio na hatia na bado wanadhuruiwa na Shetani mbele za Mungu. Hii ni ya thamani na ya maana zaidi kuliko kazi yoyote duniani, na ni ya kufaa haijalishi ni mateso ngapi yanapaswa kuvumiliwa! Nilipofikiria juu ya haya, sikuhisi tena kwamba kuhubiri kwa injili ni kitu chenye uchungu, na badala yake nilihisi mwenye bahati kuwa na uwezo wa kuratibu na injili ya ufalme. Huu ulikuwa heshima yangu na pia kuinuliwa na Mungu. Nilifanya uamuzi wangu: Bila kujali aina gani ya shida nitakayopatana nayo katika kazi yangu ya injili, nitajitolea yangu yote na kuwaleta watu zaidi na zaidi wenye shauku ya Mungu mbele Yake ili kufariji moyo Wake! Baadaye, nilijirusha mwenyewe tena katika kazi ya injili tena.
Kufuatia kipindi cha mafunzo, kila nilipokutana na mlengwa wa mahubiri ambaye alikuwa na mtazamo mbaya au aliyeninenea maneno makali wakati wa kutekeleza wajibu wangu, ningekuwa na uwezo wa kukabiliana na hilo kwa njia sahihi na kuendelea kushirikiana na moyo wa upendo. Kwa sababu ya haya, nilihisi nilikuwa nimebadilika na sikuwa ninajali tena kuhusu heshima na hadhi. Lakini wakati Mungu aliweka mazingira mengine ya kunijaribu kulingana na kile nilichohitaji katika maisha, nilifichuliwa kabisa tena. Siku moja, kiongozi wa kanisa alinijulia hali hivi karibuni na pia alizungumzia nia za Mungu za wakati uliopo na njia ya utendaji. Wakati niligundua wakati wa mazungumzo kuwa alikuwa anahamishwa katika kanisa lingine ili kutimiza wajibu wake, singeweza kujisaidia kuhisi wimbi la msisimko: Kuna uwezekano kuwa nitafanywa kuwa kiongozi wa kanisa baada ya yeye kuondoka. Ikiwa ndivyo, ni lazima kabisa nishirikiane vizuri! Wakati tu nilipokuwa ninahisi furaha kisiri, dada huyo alisema kuwa dada mwingine katika kijiji changu angetutembelea kesho. Nilikuwa na wasiwasi mara tu niliposikia hayo: Anakujia nini? Yeye ndiye atafanywa kuwa kiongozi mpya wa kanisa? Singeweza kujizuia kuwa na wasiwasi: Hajakuwa akimwamini Mungu kwa muda mrefu kama vile nimefanya, na pia anakuja kutoka kijiji hicho kama mimi. Ikiwa yeye atafanywa kiongozi, basi heshima yangu itakuwa aje? Ndugu wataniona namna gani? Kwa hakika watasema kuwa mimi huwa sifuatilii ukweli kwa kiwango chake. Sikuweza kuacha kufikiria juu ya hayo. Niligaagaa na kugeuka kitandani usiku, nisiweze kulala. Wakati wa mkutano siku iliyofuata, nilitia makini mara kwa mara sauti na mtazamo wa kile kiongozi alikuwa akisema kwa sababu nilitaka kujua kwa hamu ni nani angechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa kanisa. Kila wakati kiongozi huyo aliniangalia alipozungumza, nilihisi tumaini la kufanywa kuwa kiongozi. Sura yangu ingejawa na furaha na ningekubali kwa kichwa na kukubaliana na chochote alichosema. Kwa upande huo mwingine, wakati wowote kiongozi huyo alitazama dada huyo mwingine alipokuwa akizungumza, ningekuwa na uhakika kuwa dada huyo angetajwa kama kiongozi, na ningehisi huzuni na kuwa na masumbuko makali kwa sababu ya hilo. Wakati wa siku hizo chache, nilikuwa nimeteseka kwa ajili ya heshima na hadhi sana hadi nikawa na wasiwasi na kuchanganyikiwa. Nilipoteza hamu yangu ya kula na hata nikahisi kama muda ulikuwa unapita hasa polepole, ni kama ulikuwa umeganda. Kiongozi wa kanisa aliweza kuona hali niliyokuwa katika, kwa hivyo alipata kifungu cha neno la Mungu niweze kusoma: “Sasa nyinyi ni wafuasi, na mna ufahamu fulani wa hatua hii ya kazi. Hata hivyo, bado hamjaweka kando tamaa yenu ya hadhi. Wakati hadhi yenu iko juu mnatafuta vizuri, lakini wakati hadhi yenu iko chini hamtafuti tena. Baraka za hadhi daima ziko katika fikira zenu.” “Ingawa mmefikia hatua hii leo, bado hamjaiacha hadhi, lakini daima mnapambana kuuliza kuihusu na kila siku mnaichunguza…. Kadiri unavyotafuta zaidi kwa njia hii ndivyo utavyovuna kidogo zaidi. Kadiri ilivyo kubwa zaidi tamaa ya mtu ya hadhi, ndivyo itabidi washughulikiwe kwa uzito zaidi na ndivyo zaidi lazima wapitie usafishaji mkubwa. Mtu wa aina hiyo hana thamani kabisa! Lazima ashughulikiwe na ahukumiwe vya kutosha ili aache hilo kabisa. Mkifuatilia kwa njia hii mpaka mwisho, hamtavuna chochote. Wale ambao hawafuatilii maisha hawawezi kubadilishwa; wale ambao hawana kiu ya ukweli hawawezi kupata ukweli. Hulengi kufuatilia mabadiliko ya kibinafsi na kuingia ndani; daima wewe hulenga tamaa zile badhirifu na vitu vinavyozuia upendo wako kwa Mungu na kukuzuia kufika karibu na Yeye. Je, vitu hivyo vinaweza kukubadili? Je, vinaweza kukuleta katika ufalme?” (“Mbona Huko Tayari Kuwa Foili[a]?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kila mstari wa maneno ya Mungu uligonga moyo mwangu, ukinifanya nihisi kuwa Mungu alikuwa kando yangu, akifuatia kila neno na mwenendo wangu. Singeweza kujizia ila kujitafakari kwa mawazo na utendaji wangu siku hizi mbili zilizopita. Niligundua kuwa mtazamo wangu wa ufuatiliaji ulikuwa mbovu sana na uliathiriwa na misemo kama "Kama vile mti unavyoishi kwa sababu ya gome lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake," na "Mtu huacha jina lake nyuma mahali popote anapoishi, kama vile bata bukini hunena kilio chake popote anapoburuka." Siku zote nilitaka hadhi ili nipate kushinda sifa zaidi kutoka kwa wengine, kilichosababisha mimi kuteseka kwa ajili ya heshima na hadhi kiasi kwamba nilikuwa na wasiwasi na kuchanganyikiwa, nilipoteza hamu yangu ya kula na singeweza kulala, na nilijifanya kuonekana mpumbavu. Hali kama hiyo ilitengenezwa na Mungu kulingana na hali yangu. Ilikuwa upendo wa Mungu ukiniangukia. Kazi ya Mungu leo ​​ilikuwa ya kuniokoa, kunisaidia kuepuka ushawishi wa giza wa Shetani ili nipate kupata wokovu. Njia niliyokuwa nikitafutilia ilikinzana na kazi na mahitaji ya Mungu. Singekuwa na uwezo wa kupokea idhini ya Mungu hata kama ningemwamini hadi mwisho. Ningeachwa bila chochote! Kwa hivyo nilimwomba Mungu kwa ukimya: "Ewe Mungu! Niko radhi kutii kazi Yako, kutembea katika njia sahihi ya kuamini Mungu kwa mujibu wa mahitaji Yako, na kutia juhudi kwa neno Lako ili kufikia kuelewa ukweli na kuachana na tabia yangu mbovu. Bila kujali kama nimefanywa kiongozi, nitafuatilia ukweli na kutia makini kwa kubadili mambo yangu ambayo hayakidhi malengo Yako." Baada ya kuelewa makusudi ya Mungu, nilihisi hasa utulivu moyoni mwangu na nilifurahia kuwasiliana bila kujali maudhui yalikuwa gani. Baada ya mkutano, kiongozi wa kanisa alisema kuwa, kulingana na mapendekezo ya wengi wa ndugu, dada huyo angekuwa kiongozi mpya wa kanisa, na kuwa ningeweza kuratibu na kazi yake. Nilikuwa na utulivu sana ndani na kukubali bila kusita, kukubali kufanya kazi kwa upatanifu na dada huyo ili kutimiza wajibu wetu.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Tazama zaidi: Umeme wa Mashariki | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni