Kuzaliwa Upya Kupitia Neno la Mungu(I)
Wang Gang Mkoa wa Shandong
Mimi ni mkulima na kwa sababu familia yangu ni maskini, daima ilinibidi nisafiri kwenda kote kutafuta kazi za muda ili kupata pesa; nilidhani kuwa ningeweza kujipatia maisha mazuri kupitia kazi yangu ya kimwili. Hata hivyo, kwa uhalisi, niliona kuwa hapakuwa na hakikisho la haki za kisheria za wafanyakazi wahamiaji kama mimi; mshahara wangu mara nyingi ulizuiliwa bila sababu yoyote. Mara kwa mara nilidanganywa na kutumiwa na wengine kwa faida yao.
Baada ya kazi ngumu ya mwaka mmoja, sikupokea kile nilichopaswa kupokea. Nilihisi kwamba ulimwengu huu kwa kweli ulikuwa wa giza! Watu hutendeana kama wanyama ambapo wenye nguvu huwawinda walio dhaifu; wao hushindana wenyewe kwa wenyewe, kupigana kwa kukaribiana sana, na sikuwa na mahali pa usalama kwendelea kuishi jinsi hii. Katika maumivu mno na mfadhaiko wa roho yangu, na wakati nilipokuwa nimepoteza imani katika maisha, rafiki yangu alishirikiana wokovu wa Mwenyezi Mungu nami. Tangu wakati huo, nilikutana mara kwa mara, kusali na kuimba pamoja na ndugu wa kiume na wa kike; tuliwasiliana ukweli, na tulitumia uwezo wetu ili kufidia udhaifu wa mwingine. Nilijihisi mwenye furaha sana na aliyekombolewa. Katika Kanisa la Mwenyezi Mungu, niliona kwamba ndugu wa kiume na wa kike hawakujaribu kushindana kwa akili au kufanya utofautishaji wa kijamii; wote walikuwa wazi kabisa na walipatana wenyewe kwa wenyewe. Kila mtu alikuwa hapo kutafuta ukweli kwa bidii ili kuziacha tabia zao potovu, na kuishi kama wanadamu na kupata wokovu. Hili liliniwezesha kupitia furaha katika maisha na kuelewa umuhimu na thamani ya maisha. Kwa hiyo, niliamua kuwa ni lazima nieneze injili na kuwaruhusu watu zaidi wanaoishi gizani kuja kwa Mungu ili kupokea wokovu Wake na kuona mwanga tena. Kwa hiyo, nilijiunga na wale wa kutangaza injili na kumshuhudia Mungu. Lakini bila kutarajia, nilikamatwa na serikali ya CCP kwa kuhubiri injili na kupitia unyama mno wa mateso, utendewaji wa kikatili na kifungo cha jela.
Ilikuwa wakati wa alasiri katika majira ya baridi ya mwaka wa 2008, wakati dada wawili na mimi tulipokuwa tukiishuhudia kazi ya Mungu katika siku za mwisho kwa mlengwa wa injili, tuliripotiwa na watu waovu. Maafisa sita wa polisi walitumia udhuru wa haja ya kuangalia vibali vya makazi yetu ili kuingia kwa nguvu katika nyumba ya mlengwa wa injili. Walipokuwa wakiingia mlangoni, walisema kwa sauti kubwa: "Msisonge!" Wawili wa wale polisi waovu walionekana kuwa wazimu kabisa waliponirukia; mmoja wao alikamata kwa nguvu nguo juu ya kifua changu na mwingine akamata mikono yangu kwa nguvu na kutumia nguvu zake zote ili kuikaza nyuma yangu, kisha akaniuliza kwa ukali: "Unafanya nini? Unatoka wapi? Jina lako ni nani?" Nikauliza kwa kujibu: "Unafanya nini? Unanikamatia nini?" Waliposikia nikisema hivi, walikasirika kweli na wakasema kwa ukali: "Haijalishi sababu ni nini, wewe ndiwe tunayetafuta na unakuja nasi!" Baadaye, wale polisi waovu wakanichukua pamoja na wale dada wawili, wakatusukuma ndani ya gari la polisi na kutupeleka kwa kituo cha polisi cha mahali pale pale.
Baada ya kufika kwa kituo cha polisi, wale polisi waovu walinichukua na kunifungia ndani ya chumba kidogo; waliniamuru nichutame sakafuni na kunipangia watu wanne wanichunge. Kwa sababu nilikuwa nimechuchumaa kwa muda mrefu, nikawa nimechoka sana kiasi kwamba sikuweza kustahimili. Papo hapo nilijaribu kusimama, wale polisi waovu walinijia mbio mbio na kugandamiza kichwa changu chini ili kunizuia kusimama. Ilikuwa tu hadi wakati wa usiku walipokuja kunipekua na kuniruhusu kusimama; walipokosa kupata chochote katika utafutaji wao, wote waliondoka. Muda mfupi baadaye, nikasikia mayowe yenye kutia hofu ya mtu aliyekuwa akiteswa katika chumba cha pili, na wakati huo, niliogopa sana: Sijui ni mateso gani na matendo katili watakayotumia kwangu baadaye! Nilianza kumwomba Mungu kwa moyo wangu kwa dharura: "Ee Mwenyezi Mungu, ninaogopa sana hivi sasa, naomba Unipe imani na nguvu, nifanye imara na jasiri ili niweze kuwa shahidi Kwako. Kama siwezi kuvumilia mateso yao na matendo ya ukatili, kama itanilazimu kujiua kwa kuuma ulimi wangu, sitawahi kukusaliti Wewe kama Yuda!" Baada ya kuomba, niliyafikiria maneno ya Mungu, "Usiogope, Mwenyezi Mungu wa majeshi kwa hakika atakuwa pamoja nawe; Yuko tayari kukukinga na Yeye ni Ngao yako" ("Tamko la Ishirini na Sita" katika Neno Laonekana Katika Mwili). Naam, Mwenyezi Mungu ndiye tegemeo langu na Yeye yu pamoja nami; ni nini kingine cha kuogopwa? Ninahitaji kumtegemea Mungu ili kupigana na Shetani. Maneno ya Mungu yaliondoa woga kutoka moyoni mwangu, na moyo wangu uliwekwa huru.
Usiku huo, polisi wanne wa kishetani walinijia na mmoja wao akanielekeza na kuguta: "Bila shaka tulishika samaki mkubwa! Ninyi waumini wa Mwenyezi Mungu mnavuruga utaratibu wa jamii, na mnavunja sheria za kitaifa ….” Aliguta alipokuwa akinisukuma ndani ya chumba cha mateso kwa ghorofa ya pili, akiniamuru nichuchumae. Chumba cha mateso kiliandaliwa na aina zote za vyombo vya mateso kama vile kamba, vijiti vya mbao, virungu, mijeledi, bunduki, nk. Vilikuwa vimepangwa kwa machafuko. Akiwa na uso uliojikunja na macho yaliyowaka kwa hasira, polisi mmoja mwovu alizishika nywele zangu kwa mkono mmoja, na kirungu cha umeme, ambacho kilitoa sauti za dhoruba za "kushambulia na kuzibua" kwa ule mkono mwingine, na akafanya madai ya kuitishia habari: "Ni watu wangapi walio katika kanisa lenu? Eneo la mkutano wenu liko wapi? Ni nani anayesimamia? Ni watu wangapi walio katika sehemu hiyo wakihubiri Injili? Ongea! Vinginevyo, utapata kinachokuja!" Nikaangalia hatari iliyotisha ya kirungu cha umeme na nikaangalia tena kwa chumba kilichojaa vyombo vya mateso; sikuweza kujizuia kuhisi fadhaa na kuogopa. Sikujua kama ningeweza kuyashinda mateso haya. Katika tu wakati huu muhimu, nilifikiria maneno ya Mwenyezi Mungu yakisema: “Lazima pia unywe kutoka kwenye kikombe kikali nilichonywea Mimi (hili ndilo alilomwambia baada ya kufufuka), lazima utembee njia niliyotembea Mimi …” (“Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Nilitambua kwamba hiki kilikuwa kitu ambacho Mungu alituaminia na ilikuwa ni njia ya maisha ambayo Mungu binafsi alituanzishia. Katika kuitembea njia ya kumwamini Mungu na kutafuta ukweli, bila shaka ni lazima mtu apitie mateso na kuvunjika moyo. Hili ni jambo lisiloepukika, na mwishowe, shida hizi huleta baraka kutoka kwa Mungu. Ni kwa njia ya mateso tu watu wanapoweza kupokea njia ya ukweli iliyotolewa na Mungu, na ukweli huu ni uzima wa milele, ambao hutolewa na Mungu. Napaswa kutembea katika nyayo za Mungu na kukabiliana na jambo hili kwa ujasiri; sipaswi kuwa na woga au hofu. Katika kufikiria jambo hili, moyo wangu mara moja ulizalisha aina fulani ya nguvu na nikasema kwa sauti kubwa: "Ninaamini tu katika Mwenyezi Mungu, sijui chochote kingine!" Wakati polisi muovu aliposikia jambo hili, alivurugika na kunidukua kwa nguvu kwa upande wa kushoto wa kifua changu na kirungu hicho cha umeme. Alinishtua kwa karibu dakika moja. Mara moja nilisikia kama damu katika mwili wangu ilikuwa imechemshwa; nilikuwa na maumivu yasiyovumilika kutoka kwa kichwa hadi kwa mguu na nikabiringika nikipiga mayowe sakafuni. Bado hakutaka kuniacha na ghafla akaanza kunivuta na akatumia kirungu kuniinua kwa kidevu changu, akiguta: "Sema! Hutakiri chochote?" Aliguta na kunidukua upande wa kulia wa kifua changu na kirungu cha umeme, nilichomwa na umeme vibaya sana kiasi kwamba nilikuwa nikitetemeka kutoka kichwa hadi mguu. Baadaye mwili uliuma vibaya sana kiasi kwamba nilizirai kama nimelala sakafuni bila kujongea. Sikujua ni muda gani uliokuwa umepita, lakini niliamka yule polisi muovu akisema: "Je! Unajifanya kuwa mfu? Unajifanya! Endelea kujifanya! "Walinidukua tena na kirungu kwa uso na kunipiga teke kwa paja. Baadaye, waliniburuta na kuniuliza kwa ukali: "Je, utaniambia!?" Bado sikujibu. Kisha hao polisi waovu walinipiga kikatili kwa uso wangu kwa ngumi zao na jino langu moja liling'olewa, jino jingine liligongwa hadi likalegea. Mara moja mdomo wangu ulianza kuvuja damu. Katika kukabiliwa na mateso ya kichaa ya pepo hawa, niliogopa tu kwamba ningemsaliti Mungu kwa sababu ya kutoweza kuyahimili mateso yao. Wakati huu, nilifikiri tena juu ya maneno ya Mungu, "Kutoka kwa nje, wale wenye mamlaka wanaonekana kuwa waovu, lakini huhitaji kuogopa—hiyo ni kwa sababu una ujasiri kidogo. Almradi unaweza kuujenga ujasiri wako, hakuna kitu kitakachokuwa kigumu mno" ("Tamko la Sabini na Tano" katika Neno Laonekana Katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinipa imani na nguvu tena, na niligundua kuwa ingawa hawa polisi waovu mbele yangu walikuwa na kichaa na bila nidhamu, walipangwa na mkono wa Mungu. Wakati huo, Mungu alikuwa akiwatumia kupima imani yangu. Alimradi niliegemea imani na kumtegemea Mungu na sikukubali kushindwa nao, bila kuzuilika wangeshindwa kwa aibu. Katika kufikiri juu ya hili, nilikusanya nguvu zangu zote za mwili wangu na nikajibu kwa sauti kuu: "Kwa nini mmenileta hapa? Kwa nini mnanishtua kwa umeme kwa kirungu cha umeme? Ni kosa gani nimelifanya?" Yule polisi muovu kwa ghafla akawa mtu aliyeshtuka kiasi cha kutowaza na kukandamizwa sana na dhamiri ya hatia. Alianza kugugumiza: "Mimi … mimi … Sikupaswa kukuletea hapa?" Kisha akaondoka kwa aibu. Katika kuona hali ya aibu ya mtanziko wa Shetani, niliguswa hadi nikalia. Katika mashaka haya, kwa kweli nilipitia nguvu na mamlaka ya maneno ya Mwenyezi Mungu. Alimradi neno la Mungu linawekwa katika vitendo na kufuatwa, basi Mungu atakutunza na kukukinga na nguvu za Mungu zitaandamana nawe. Wakati huo huo, nilijihisi ninawiwa na Mungu kwa sababu ya jinsi nilivyokuwa na imani kidogo. Baadaye, afisa mmoja mrefu wa polisi aliingia na kunijia na akasema: "Unapaswa tu kutuambia ni wapi familia yako huishi na ni watu wangapi walio katika familia yako, na tutakuachilia mara moja." Alipoona kwamba singesema chochote, alivurugika na kukamata mkono wangu kwa nguvu na kuulazimisha mkono wangu kutia alama kwa ungamo la mdomo walilokuwa wameandika. Niliona kwamba huo ungamo la mdomo halikuwa vile niliyowaambia, lilikuwa ni ushahidi ghushi na wa bandia. Nilijawa na hasira ya haki na kulishika na kulirarua vipande vipande. Yule polisi muovu mara moja aliingiwa na hasira na kunipiga na ngumi yake upande wa kushoto wa uso wangu. Kisha akanipiga makofi mara mbili katika uso kwa nguvu sana kiasi kwamba nilishikwa na kizunguzungu. Baadaye, walinipeleka kwa chumba kidogo nilichokuwemo awali.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni