Jumatatu, 24 Septemba 2018

Kuzaliwa Upya Kupitia Neno la Mungu(II)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, maombi

Kuzaliwa Upya Kupitia Neno la Mungu(II)

Wang Gang Mkoa wa Shandong
Baada ya kurudi kwa kile chumba kidogo, nilichubuliwa na kugongwagongwa sana, maumivu yalikuwa yasiyovumilika. Moyo wangu haukuweza kujizuia kuzalisha hisia ya huzuni na udhaifu: Kwa nini waumini wanapaswa kuteseka jinsi hii? Nilihubiri Injili na nia njema za kuwaruhusu watu kuutafuta ukweli na kuokolewa, na bila kutarajia nimepitia mateso haya. Katika kufikiri juu ya hili, nilihisi zaidi kuwa nilikuwa nimekosewa. Katika maumivu yangu, nilifikiria maneno ya Mungu: “Kama binadamu, unapaswa kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu na kuvumilia kila mateso. Unapaswa kukubali kwa furaha na kwa hakika mateso kidogo unayopitia leo na kuishi maisha yenye maana, kama Ayubu, kama Petro. Katika ulimwengu huu, mwanadamu huvaa mavazi ya ibilisi, hula chakula kinachotolewa na ibilisi, na hufanya kazi na kutumika chini ya Shetani, na kukanyagiwa ndani ya uchafu wake. Usipoelewa maana ya maisha au njia ya kweli, basi ni nini maana ya maisha yako? Ninyi ni watu mnaofuatilia njia sahihi, wale wanaotafuta maendeleo. Ninyi ni watu ambao huinuka katika nchi ya joka kuu jekundu, wale ambao Mungu huwaita wenye haki. Je, hayo si maisha yenye maana zaidi?” (“Utendaji (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mwenyezi Mungu yalivutia hisia kubwa kutoka kwa wangu. Ndio, Mungu alininyunyizia na kunipa maneno Yake makarimu ya uzima, Ameniruhusu kufurahia neema Yake nyingi bure na kuniruhusu kujua siri za ukweli ambazo hakuna mtu yeyote tangu vizazi vya zamani amezielewa. Hii ni baraka maalum ambayo Mungu amenipa. Napaswa kushuhudia kwa Mungu na kuvumilia maumivu yote kwa ajili ya Mungu. Kiasi chochote cha maumivu ni cha kufaa, kwa sababu ni jambo la thamani na la maana sana! Leo, ninateswa kwa kuhubiri injili na siko tayari kupitia maumivu yoyote ya kimwili kwa ajili ya injili; ninahisi kukosewa na kutokuwa tayari. Si nimemhuzunisha Mungu kwa kufanya hivi? Si nimekosa dhamiri? Ningewezaje kustahili baraka za huruma za Mungu na utolewaji wa maisha? Vizazi vya watakatifu wamebeba ushuhuda wa nguvu na mkubwa kwa Mungu kwa sababu walifuata njia ya Mungu; waliishi maisha yenye maana. Leo nina maneno haya yote kutoka kwa Mungu, kwa hiyo mimi si ni lazima hata zaidi nitoe ushuhuda mzuri kwa ajili ya Mungu? Kwa kutafakari jambo hili, mwili wangu haukujihisi kama mchungu, nilijua sana kuwa ni neno la Mwenyezi Mungu ambalo lilinipa uwezo wa uzima, likiniruhusu kuushinda udhaifu wa mwili.
Siku iliyofuata, hao polisi waovu hawakuwa na mkakati mwingine ulioachwa kujaribu. Walinitishia wakisema: "Hutasema chochote? Basi tutakufunga gerezani!" Baadaye, walinipeleka kwa kituo cha kizuizi. Katika kituo cha kizuizi, hao polisi waovu waliendelea kutumia njia zote za mateso kwangu na mara nyingi waliwahimiza wafungwa kunipiga. Katika baridi kali ya majira ya baridi, waliwaagiza wafungwa kunimwagilia ndoo za maji baridi na kunilazimisha kuoga na maji baridi. Nilikuwa nikitetemeka kwa baridi kutoka utosini hadi kidoleni. Hapa, wafungwa walikuwa mashine ya kutengeneza pesa kwa serikali na hawakuwa na haki yoyote ya kisheria. Hawakuwa na chaguo jingine ila kuvumilia kuminywa na kutumiwa na wengine kwa faida yao kama watumwa. Gereza lilinilazimisha kuchapisha pesa za karatasi zilizotumika kama sadaka za kuteketezwa kwa wafu mchana kutwa na kunilazimisha nifanye kazi ya ziada usiku. Kama ningesimama ili kupumzika, basi mtu fulani angekuja na kunipiga sana. Mara ya kwanza, waliweka sheria kwamba nilipaswa kuchapisha vipande 2,000 vya karatasi kwa siku, kisha wakaongeza viwe vipande 2,800 kwa siku, na hatimaye hadi vipande 3,000. Kiasi hiki kilikuwa hakiwezekani kwa mtu mwenye ujuzi kukamilisha sembuse mtu asiye na ujuzi kama mimi kukamilisha. Kwa kweli, walipanga hivyo kwa makusudi ili nisiweze kukamilisha yote ili waweze kuwa na udhuru wa kunitesa na kunidhuru. Alimradi sikuweza kufikia kiasi hicho, hao polisi waovu wangeniwekea pingu za miguu kwa miguu yangu ambazo zilikuwa na uzito wa zaidi ya kilo 5, na kuifunga mikono na miguu pamoja kwa pingu. Yote niliyoweza kufanya ni kuketi pale, kuinamisha kichwa changu na kugeuza kiuno changu, vinginevyo sikuweza kusonga. Aidha, hawa polisi wakatili na wasio na hisia hawakuuliza au kujali kuhusu mahitaji yangu ya msingi. Ingawa choo kilikuwa ndani ya seli ya gereza, sikuweza kabisa kutembea na kukitumia; niliweza tu kuwaomba wenzangu katika seli kuniinua na kuniwekelea kwa choo. Kama walikuwa wafungwa bora zaidi kidogo, basi wangeweza kuniinua; kama hakuna mtu aliyenisaidia, basi singekuwa na chaguo jingine ila kujinyia katika suruali yangu. Wakati wa maumivu mno ulikuwa wakati wa chakula, kwa sababu mikono na miguu yangu ilikuwa imefungwa pamoja. Niliweza tu kuteremsha kichwa changu kwa nguvu zangu zote na kuinua mikono na miguu yangu. Ni kwa njia hii tu nilivyoweza kuiweka skonsi kinywani mwangu. Nilitumia nguvu nyingi sana kwa kila umo. Pingu zilisugua mikono na miguu yangu na zikisababisha maumivu makubwa. Baada ya muda mrefu, vifundo vya mikono yangu na vya miguu vilikuwa vimekuza sagamba nyeusi na ngumu zilizong'aa. Mara nyingi sikuweza kula wakati nilipokuwa nimefungiwa, na mara chache, wafungwa wangenipa skonsi mbili ndogo. Mara nyingi wangekula sehemu yangu na yote niliyopata ilikuwa tumbo tupu. Nilipokea hata kinywaji kidogo zaidi; awali, kila mmoja alipewa tu bakuli mbili za maji kwa siku, lakini nilikuwa nimefungiwa na sikuweza kusogea, hivyo ni kwa nadra sana niliweza kunywa maji yoyote. Mateso hayo ya kinyama yalikuwa yasiyosemeka. Kwa ujumla, niliteseka hivi mara nne na kila mara nilikuwa nimefungiwa kwa siku zisizopungua tatu na zisizozidi nane. Kila wakati ambapo njaa haikuvumilika, ningefikiria maneno ambayo Mungu aliyasema zamani: “Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu” (Mathayo 4:4). Hatua kwa hatua nilianza kutambua kwamba Mungu anataka kutimiliza ukweli kwamba “Neno Lake lakuwa uhai wa mwanadamu” kwangu kupitia mateso ya Shetani. Katika kuelewa mapenzi ya Mungu, moyo wangu uliokolewa na nikamwomba Mungu kwa amani na kujaribu kuyaelewa maneno ya Mungu. Pasipo kujua, sikuhisi uchungu sana tena au njaa. Hili kwa hakika lilinifanya nisihisi kuwa neno la Mungu ni ukweli, njia, na uzima na bila shaka ni msingi ambao napaswa kutegemea ili kuishi. Kwa hiyo, imani yangu kwa Mungu iliongezeka bila kujua. Nakumbuka wakati mmoja polisi wa gerezani kwa makusudi walinitesa na kunifunga pingu. Kwa siku tatu mchana na usiku sikunywa hata tone la maji. Mfungwa aliyekuwa amefungwa pingu karibu na mimi akasema: "Kulikuwa na mtu fulani wa umri mdogo kabla ambaye alifungwa pingu na kunyimwa chakula jinsi hii hadi kufa. Naona kuwa hujala chochote kwa siku kadhaa na bado una uchangamfu." Katika kusikia maneno yake, nilifikiri kwamba ingawa sikuwa nimekula au kunywa chochote kwa siku tatu mchana na usiku, sikuhisi kero ya njaa. Nilihisi sana kwamba hii ilikuwa ni nguvu ya uzima katika maneno ya Mungu ikinisaidia na kunisababisha kwa hakika kuona Mungu akionekana kwangu katika maneno Yake. Moyo wangu ulikuwa na msisimko daima; katika mazingira haya ya mateso niliweza kwa kweli kupitia uhalisi wa ukweli kwamba “Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu.” Huu kwa kweli ni utajiri wa thamani zaidi wa maisha ambao Mungu ameniridhia, na pia ni zawadi yangu ya pekee. Aidha, singeweza kamwe kuupata katika mazingira ambayo sikuhitaji kuwa na wasiwasi juu ya chakula au nguo. Sasa, mateso yangu yalikuwa na maana nyingi sana na thamani! Wakati huu, sikuweza kujizuia kufikiria maneno ya Mungu: “Kile ambacho umerithi wakati huu, kimepiku walichorithi mitume na manabii na ni kikuu zaidi kuliko alichopokea Musa na Petro. Baraka haziwezi zikapokewa kwa siku moja au mbili; sharti zipatikane kwa kujitolea kwingi. Yaani, lazima uwe na upendo uliosafishwa, imani kuu, na ukweli mwingi ambao Mungu Anakuagiza uufikie; zaidi ya hayo, sharti uelekeze uso wako kwa haki wala usikubali kushindwa, na lazima uwe na upendo usiofikia kikomo kwa Mungu. Azimio linahitajika kutoka kwako, na vilevile mabadiliko katika tabia ya maisha yako. Upotovu wako lazima utibiwe, na lazima ukubali mipango ya Mungu pasipo kulalamika, na hata uwe mtiifu hadi kifo. Hicho ndicho unachopaswa kutimiza. Hili ndilo lengo la Mungu la mwisho, na matakwa ya Mungu kwa watu wa kundi hili. Anapokukarimia mengi, anakutaka wewe badala yake na kukufanyia matakwa yanayokufaa” (“Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Katika kujaribu kuyaelewa maneno ya Mungu, nilitambua kwamba baada ya mateso na majaribu baraka huja kutoka kwa Mungu, na huu ndio ugavi wa mahitaji na umwagiliwaji wa maji kwangu kutoka kwa Mungu. Sasa, ingawa maneno ambayo Mungu amenipa yamepita vizazi vya watakatifu, bado nahitaji kuwa na imani na uvumilivu ili kuwa na uwezo wa kutokukubali kushindwa wakati wa majaribu na mateso yangu, kuitii mipango ya Mungu, na kupokea wokovu wa Mungu. Kisha nitaweza kuuingia uhalisi wa neno la Mungu na kuweza kuona matendo ya ajabu ya Mungu. Kama haingekuwa kwa gharama ya shida hii, singestahili kupokea ahadi na baraka za Mungu. Kupokea nuru ya Mungu kulinielekeza kuwa na udhabiti na nguvu zaidi ndani; niliweka azimio: Shirikiana na Mungu kwa bidii na kuyaridhisha mahitaji ya Mungu katikati ya mazingira haya machungu, kumshuhudia Mungu ili niweze kuwa na mavuno makubwa mno.
Mwezi mmoja baadaye, polisi wa CCP walinishtaki na "kushukiwa kuvuruga utaratibu wa jamii na kuharibu utekelezaji wa sheria"; nilihukumiwa mwaka mmoja wa mageuzi kupitia kazi. Nilipoingia kambi ya kazi, wale polisi waovu walieneza uvumi na upuuzi miongoni mwa wafungwa, wakisema kuwa nilikuwa muumini katika Mwenyezi Mungu, jambo ambalo ni baya kuliko mauaji na wizi, na waliwachochea wafungwa kunitesa. Kwa hiyo mara nyingi nilipigwa na kuwekwa katika hali ngumu na wafungwa bila sababu yoyote. Hili lilinifanya nione kweli kwamba China ni nchi ya mateso na maumivu inayoongozwa kwa uthabiti na Shetani, pepo. Kuna giza kutoka kila pembe, na hakuna mwanga unaoruhusiwa kuwepo; hakuna mahali kabisa pa waumini wa Mwenyezi Mungu kuishi. Wakati wa mchana, hao polisi waovu walinilazimisha kufanya kazi katika karakana. Kama sikufikia kiasi nilichopaswa kufikia, wangewaacha wafungwa wanipige wakati niliporudi kwa seli yangu gerezani na kutangaza "mfanyeni mfano ili kuwaogofya wengine." Nilipokuwa katika karakana nikihesabu mifuko, ningehesabu mifuko 100 na kisha kuifunga pamoja. Wafungwa wangekuja daima na kutoa mfuko moja au kadhaa kutoka kwa ile niliyokuwa nimehesabu, kisha wangesema kwamba sikuhesabu vizuri na kuchukua hiyo kama fursa ya kunipiga ngumi na mateke. Wakati msimamizi huyo aliponiona nikipigwa, angekuja na kuniuliza kwa unafiki kilichokuwa kikiendelea na wafungwa wangewasilisha ushahidi wa uongo kwamba sikuwa nimehesabu mifuko ya kutosha. Kisha ningelazimika kustahimili mfululizo wa ukosoaji mkali kutoka kwa msimamizi. Aidha, wangeniamuru nikariri "amri za maadili mema" kila asubuhi, na kama sikuzikariri, ningepigwa; pia wangenilazimisha kuimba nyimbo zilizokisifu chama cha Kikomunisti. Kama waliona kwamba sikuwa nikiimba au kwamba midomo yangu haikuwa ikisonga, basi usiku bila shaka ningepigwa. Pia waliniadhibu kwa kunifanya nipanguse sakafu, na kama sikupangusa kwa matarajio yao, basi ningepigwa kwa nguvu nyingi. Wakati mmoja, kwa ghafla wafungwa fulani walianza kunigonga na kunipiga mateke. Baada ya kunipiga, waliniuliza: "Kijana, unajua kwa nini unapigwa? Ni kwa sababu hukusimama na kumsalimu msimamizi wakati alipokuja!" Baada ya kila wakati nilipopigwa, nilikuwa na hasira lakini sikuthubutu kusema chochote; niliweza kulia tu na kumwomba Mungu kimyakimya, nikimwambia Yeye juu ya chuki na malalamiko moyoni mwangu kwa sababu ya mahali hapa palipo na utovu wa sheria, na kukosa mantiki. Hapakuwa na busara hapa, palikuwa na vurugu tu. Kulikuwa hakuna watu hapa, kulikuwa na pepo wenye wazimu na nge tu! Nilihisi maumivu mengi sana na shinikizo nikiishi katika shida hii; sikuwa tayari kukaa hata dakika moja zaidi. Kila wakati nilipotumbukia katika hali ya udhaifu na maumivu, ningefikiri juu ya maneno ya Mwenyezi Mungu: “Mmewahi kuzikubali baraka mlizopewa? Mmewahi kutatufa ahadi mlizopewa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza, katikati ya giza. Hakika mtakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika mtakuwa washindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, mtasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika mtakuwa shujaa na imara katika nchi ya Sinimu. Kupitia mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, hakika mtaangaza ndani ya ulimwengu wote kwa utukufu Wangu” ("Tamko la Kumi na Tisa" la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinitia moyo. Bila kujali kama kile Mungu alichokuwa akinifanyia kilikuwa neema na baraka au majaribu na usafishwaji, yote ilikuwa ili kunikimu na kuniokoa; ilikuwa ni kuweka ukweli ndani yangu na kufanya ukweli kuwa maisha yangu. Leo, Mungu aliruhusu mateso haya na taabu zinijie. Ingawa jambo hili lilisababishia mateso mengi, liliniruhusu kuweza kwa kweli kuwa na uzoefu kwamba Mungu yu pamoja nami; lilinifanya kwa kweli nifurahie maneno ya Mungu kuwa mkate wa maisha yangu na taa ya miguu yangu na mwanga kwa njia yangu, likiniongoza hatua kwa hatua kupitia mahali hapa padhalimu na pasipovumilika. Huu ndio upendo na ulinzi wa Mungu ambao nilifurahia na kupata wakati wa mchakato wa mateso yangu. Wakati huu, niliweza kuona kwamba nilikuwa kipofu sana na wa ubinafsi na nilikuwa mwenye uroho mno. Katika kumwamini Mungu, nilijua tu jinsi ya kufurahia neema na baraka za Mungu na sikutafuta ukweli na uhai kwa kiwango hata kidogo. Mara mwili wangu uliopitia shida kidogo, ningenung'unika bila kukoma; sikufuata kabisa mapenzi ya Mungu na sikutafuta kuielewa kazi ya Mungu. Daima ningemfanya Mungu ahisi huzuni na maumivu juu yangu. Kwa kweli nilikuwa bila dhamiri! Kwa majuto na kujilaumu, niliomba kimya kimya kwa Mungu: "Ewe Mwenyezi Mungu, naweza kuona kwamba kila kitu unachokifanya ni kuniokoa na kunipata. Ninachukia tu kwamba mimi ni mkaidi sana, ni kipofu na sina ubinadamu. Daima nimekuelewa visivyo na sijakuwa wa kufikiria mapenzi Yako. Ee Mungu, leo neno Lako limeuamsha moyo wangu wenye ganzi na roho yangu na limenisababisha kuyaelewa mapenzi Yako. Siko tayari tena kuwa na tamaa na mahitaji yangu mwenyewe; nitatii tu mipango Yako. Hata kama ni lazima nipitie matatizo yote, bado nitaendelea kushirikiana na Wewe kwa bidii na nitatoa ushahidi mkubwa sana Kwako muda wote wa mateso ya Shetani. Nitatafuta kujitenga na ushawishi wa Shetani na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu halisi ili kukuridhisha." Baada ya kuomba, nilielewa nia njema za Mungu, na nilijua kwamba kila mazingira ambayo Mungu aliniruhusu kupitia yalikuwa ni upendo na wokovu mkubwa wa Mungu kwangu. Kwa hiyo, singefikiria tena kujikunyata au kumwelewa Mungu visivyo. Ingawa hali ilikuwa bado ni ile ile, moyo wangu kwa kweli ulijaa furaha na ridhaa; nilihisi kuwa ni heshima na fahari kuweza kupitia shida na mateso kwa sababu ya imani yangu kwa Mwenyezi Mungu, na ilikuwa ni zawadi ya pekee kwangu, mtu mpotovu; ilikuwa baraka maalumu na neema za Mungu kwangu.
Baada ya kuwa na uzoefu wa mwaka mmoja wa shida katika jela, naona kwamba mimi ni mdogo sana wa kimo na kwamba nakosa ukweli mwingi sana. Mwenyezi Mungu kwa kweli amefidia upungufu wangu kupitia mazingira haya ya kipekee na ameniruhusu kukua. Katika dhiki yangu, Amenifanya kupata utajiri wa thamani mno katika maisha na kuelewa ukweli mwingi ambao sikuufahamu katika siku za nyuma na kuona kwa dhahiri sura mbaya kwa Shetani, pepo, na kiini cha kupinga maendeleo cha upinzani wake kwa Mungu. Nilitambua uhalifu wake muovu wa kumtesa Mwenyezi Mungu na kuwaua Wakristo. Nilipitia kwa dhati wokovu na huruma kubwa Mwenyezi Mungu aliyokuwa nayo kwangu, mtu mpotovu, na nimehisi kwamba nguvu na maisha katika maneno ya Mwenyezi Mungu yanaweza kunipa mwanga na kuwa maisha yangu na kunielekeza kumshinda Shetani na kwa ushupavu kutoka nje ya bonde la uvuli wa mauti. Vivyo hivyo, pia niligundua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anayeniongoza kwenye njia sahihi ya uzima. Ni njia ng'avu ya kupata ukweli na uzima! Kuanzia sasa na kwendelea, bila kujali ni mateso yapi, dhiki au majaribu hatari yanayonikabili, niko tayari kutafuta ukweli kwa bidii na kupata njia ya uzima wa milele ambayo Mwenyezi Mungu amenipa.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Tazama zaidi: ushuhuda wa Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni