Jumamosi, 13 Julai 2019

Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake Sehemu ya Tano


Majaliwa ya Binadamu Yanaamuliwa na Mwelekeo Wake Kwa Mungu
Mungu ni Mungu aliye hai, na kama vile tu watu wanavyotenda tofauti katika hali tofauti, ndivyo mwelekeo wa Mungu ulivyo katika utendakazi huu na unavyotofautiana kwa sababu Yeye si kikaragosi, wala Yeye si hewa tupu. Kupata kuujua mwelekeo wa Mungu ni jambo lenye thamani kwa wanadamu. Watu wanafaa kujifunza vipi, kwa kuujua mwelekeo wa Mungu, wanaweza kuijua tabia ya Mungu na kuuelewa moyo Wake kidogo kidogo. Unapouelewa moyo wa Mungu kidogo kidogo hutahisi kwamba kumcha Mungu na kujiepusha na maovu ni jambo gumu la kutimiza. Kilicho zaidi ni kwamba, unapomwelewa Mungu, hakuna uwezekano wa wewe kufanya hitimisho kuhusu Yeye. Unapoacha kufanya hitimisho kuhusu Mungu, hakuna uwezekano wa wewe kumkosea Yeye, na bila kujua Mungu atakuongoza kuwa na maarifa Yake, na hivyo basi utamcha Mungu katika moyo wako. Utaacha kumfafanua Mungu kwa kutumia falsafa, zile barua, na nadharia ambazo umejifunza. Badala yake, kwa kutafuta nia za Mungu katika mambo yote na siku zote utaweza bila kufahamu kuwa mtu anayefuata moyo wa Mungu.
Kazi ya Mungu haionekani wala kugusika na wanadamu, lakini kulingana na Mungu, hatua za kila mmoja, pamoja na mwelekeo wake kwake Yeye—haya hayatambuliki tu na Mungu, lakini pia kuonekana vilevile. Hili ni jambo ambalo kila mmoja anafaa kutambua na kuwa wazi kulihusu. Unaweza kuwa ukijiuliza siku zote: "Je, Mungu anajua kile ninachofanya hapa? Je, Mungu anajua kile ninachofikiria sasa hivi? "Pengine Anajua, pengine Hajui." Kama utakuwa na aina hii ya mtazamo, kufuata na kusadiki Mungu ilhali unatia shaka katika kazi Yake na uwepo Wake, basi hivi karibuni au baadaye siku itawadia ambapo utamghadhabisha, kwa sababu tayari unayumbayumba pembezoni pa jabali hatari. Nimewaona watu ambao wamesadiki katika Mungu kwa miaka mingi lakini bado hawajapata uhalisia wa ukweli, wala hawaelewi hata mapenzi ya Mungu. Kimo cha maisha yao hakipigi hatua yoyote, ukitii tu falsafa zile za kiwango cha chini zaidi. Hii ni kwa sababu watu hawa hawajawahi kuchukulia neno la Mungu kama maisha yao binafsi, na hawajawahi kukabiliana na kukubali uwepo Wake. Je, unafikiri kwamba Mungu huwaona watu kama hawa na kujawa na furaha? Je, wanamtuliza Yeye? Katika jinsi hiyo, ni mbinu ya imani ya watu katika Mungu ambayo inaamua majaliwa yao. Iwe ni swali la namna unavyotafuta Mungu au namna unavyomshughulikia Mungu, ni mwelekeo wako binafsi ambao ni jambo muhimu zaidi. Usikose kumjali Mungu ni kana kwamba Yeye ni hewa tupu nyuma ya kichwa chako. Siku zote fikiria kuhusu Mungu wa imani yako kama Mungu hai, Mungu halisi. Yeye hayupo kule juu kwenye mbingu ya tatu bila chochote cha kufanya. Badala yake, siku zote bila kusita Anaangalia kwenye mioyo ya kila mmoja, Akiangalia ni nini unachofanya, akichunguza kila neno dogo na kila tukio dogo, akiangalia mwenendo wako na mwelekeo wako kwa Mungu. Kama uko radhi kujitolea kwa Mungu au la, tabia yako yote na fikira zako na mawazo yako ya ndani zaidi ziko mbele ya Mungu, na yanaangaliwa na Yeye. Ni kulingana na tabia yako, kulingana na vitendo vyako, na kulingana na mwelekeo wako kwa Mungu, ambapo maoni Yake kwako, na mwenendo Wake kwako, vinaendelea vikibadilika. Ningependa kutoa ushauri fulani kwa wale ambao wangeweza kujiwekelea kwenye mikono ya Mungu kama mtoto mchanga, kana kwamba Yeye Anapaswa kukupenda sana, kana kwamba Asingewahi kukuacha, kana kwamba mwelekeo Wake kwako ni ule ule na usingeweza kubadilika: Acha kuota ndoto! Mungu ni mwenye haki katika kutendea kila mtu. Anakabiliana na kazi ya ushindi wa wanadamu na wokovu kwa bidii. Huo ndio usimamizi Wake. Anashughulikia kila mmoja kwa umakinifu, na wala si kama kiumbe cha kufugwa cha kucheza nacho. Upendo wa Mungu kwa binadamu si ule wa kudekeza au kupotosha; rehema na uvumilivu Wake kwa wanadamu si dokezi au ya kutotilia maanani. Kinyume cha mambo, upendo wa Mungu kwa wanadamu ni wa kutunza, kusikitikia, na kuheshimu maisha; rehema na uvumilivu Wake vyote vinaonyesha matarajio Yake kwa binadamu; rehema na uvumilivu Wake ndivyo ambavyo binadamu anahitaji ili kuishi. Mungu yuko hai, na kwa hakika Mungu yupo; mwelekeo Wake kwa wanadamu unafuata kanuni, si yenye kutangazwa kama imani ya dini, na unaweza kubadilika. Mapenzi Yake kwa binadamu yanabadilika kwa utaratibu na kurekebishwa kwa muda, hali na mwelekeo wa kila mtu. Hivyo basi unafaa kuwa wazi kabisa katika hili na kuelewa kwamba kiini halisi cha Mungu hakibadiliki na tabia Yake itajitokeza katika nyakati tofauti na muktadha tofauti. Huenda usifikirie kwamba hili si suala muhimu, na wewe unatumia dhana zako za kibinafsi katika kufikiria namna ambavyo Mungu anafaa kufanya mambo. Lakini zipo nyakati ambapo kinyume kabisa cha mtazamo wako ni kweli, na kwa kutumia dhana zako za kibinafsi katika kujaribu na kumpima Mungu, tayari umemghadhabisha. Hii ni kwa sababu Mungu hafanyi kazi kama unavyofikiria wewe, Naye Mungu hatalishughulikia suala hili kama vile unavyosema Atalishughulikia. Na hivyo basi Nakukumbusha kuwa makini na mwenye hekima katika mtazamo wako katika kila kitu, na ujifunze namna ya kufuata kanuni ya kutembea kwenye njia ya Mungu katika mambo yote—kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Lazima uimarishe uelewa dhabiti katika masuala ya mapenzi ya Mungu na mwelekeo wa Mungu; kutafuta watu walio na nuru kuuwasilisha kwako, na kutafuta kwa dhati. Usimwone Mungu wa imani yako kama kikaragosi—kuhukumu kiholela, kufikia hitimisho kiholela, kutomshughulikia Mungu kwa heshima Anayostahili. Katika mchakato wa wokovu wa Mungu Anapofafanua matokeo yako, bila kujali kama Yeye atakupa rehema, au uvumilivu, au hukumu na kuadibu, mwelekeo Wake kwako wewe unabadilika. Inategemea na mwelekeo wako kwa Mungu, na uelewa wako wa Mungu. Usiache dhana moja ya kupita ya maarifa au uelewa wako katika Mungu kumfafanua Yeye daima. Usisadiki katika Mungu aliyekufa; amini kwa yule aliye hai. Kumbuka hili! Ingawa Nimezungumzia ukweli fulani hapa, ukweli mliohitaji kusikia, kwa mujibu wa hali yenu ya sasa na kimo chenu cha sasa, Sitatoa mahitaji yoyote makubwa zaidi ili nisije nikaiondoa shauku yenu. Kufanya hivyo kutajaza mioyo yenu na huzuni na simanzi, na kuwafanya nyinyi kuhisi masikitiko mengi mno kwa Mungu. Badala yake Natumai kwamba mnaweza kutumia upendo wa Mungu katika mioyo yenu, na kutumia mwelekeo ambao ni wa heshima kwa Mungu wakati mnapotembea kwenye njia iliyo hapo mbele. Usimalizie suala la jinsi ya kushughulikia imani ya Mungu kwa kubahatisha. Lishughulikie kama mojawapo ya maswali makubwa zaidi yaliyopo. Liwekeni kwenye mioyo yenu, litieni kwenye matendo, unganeni nalo kupitia kwa maisha halisi—msikubaliane nalo kwa maneno pekee. Kwani hili ni suala la uzima na mauti, na ndilo ambalo litaamua hatima yako. Usilichukulie kama mzaha, kama mchezo wa mtoto! Baada ya kuwaambia maneno haya leo, Najiuliza mavuno ya uelewa yamekuwa nini katika akili zenu? Kunayo maswali yoyote ambayo ungependa kuuliza kuhusu kile Nilichokisema leo?
Ingawa mada hizi ni mpya kidogo, na zimeondolewa kidogo kutoka kwenye mitazamo yenu na kile ambacho kwa kawaida mnafuatilia na kutilia maanani, Nafikiria kwamba baada ya mada hizi kuwasilishwa kwa kipindi cha muda, mtaimarisha uelewa mzuri wa kila kitu Nilichosema hapa. Kwa sababu hizi ni mada mpya, mada ambazo hujawahi kufikiria awali, Ninatumai kwamba hazitaongezea mzigo kwako. Ninaongea maneno haya leo si kwa sababu ya kuwatishia nyinyi, wala Sijaribu kukushughulikia wewe; badala yake, nia Yangu ni kukusaidia kuelewa ukweli wa hoja. Kwa vyovyote vile, kunao umbali kati ya wanadamu na Mungu. Ingawa binadamu anaamini katika Mungu, hajawahi kumwelewa Mungu; hajawahi kujua mitazamo ya Mungu. Binadamu pia hajawahi kuwa na shauku katika kuujali mwelekeo wa Mungu. Badala yake, amesadiki kwa kutojua, ameendelea mbele kwa kutojua na amekosa kumakinika katika maarifa na uelewa wake wa Mungu. Hivyo basi Nahisi mshawasha wa kuyafumbua masuala haya kwa niaba yenu na kuwasaidia kuelewa huyu Mungu unayemsadiki hasa ni Mungu wa aina gani; kile Anachofikiria; mwelekeo Wake ni nini katika kushughulikia Kwake kwa watu wa aina tofauti; uko mbali kiasi gani kukamilisha mahitaji Yake; na tofauti iliopo kati ya hatua zako na kiwango anachohitaji Yeye. Shabaha katika kujua kwako haya ni kuwapa kigezo cha kupimia kwenye mioyo yenu ambacho mtaweza kupimia dhidi ya na kujua barabara mnayotembelea imewaelekeza katika mavuno aina gani, kile ambacho hamjapata kwenye barabara hii, na sehemu zile ambazo hamjajihusisha kwazo. Wakati mnawasiliana miongoni mwa nyinyi wenyewe, kwa kawaida mnazungumzia mada chache zinazungumziwa kwa kawaida; upana huo wa kazi ni mwembamba, na maudhui ni ya juujuu sana. Kunao umbali, nafasi, kati ya kile ambacho mnazungumzia na nia za Mungu, katikati ya mazungumzo yenu na upana na kiwango cha mahitaji ya Mungu. Kuendelea hivi baada ya muda kutawafanya kupotoka zaidi na zaidi kutoka kwenye njia ya Mungu. Mnayachukua tu maneno yaliyopo kutoka kwa Mungu na kuyageuza kuwa vifaa vya kuabudu, kuwa kaida za dini na utaratibu. Hayo tu ndiyo maana yake! Kwa hakika, Mungu hana nafasi kamwe katika mioyo yenu, na Mungu hajawahi kuipata mioyo yenu. Baadhi ya watu hufikiria kwamba kumjua Mungu ni vigumu sana—huu ndio ukweli. Ni vigumu! Kama watu wataambiwa kutekeleza wajibu wao na kuhakikisha kwamba mambo yanatendeka kwa nje, kama wataulizwa kutia bidii, basi watu watafikiria kwamba kusadiki Mungu ni jambo rahisi sana, kwa sababu haya yote yanapatikana katika ule upana wa uwezo wa binadamu. Ilhali punde tu mada hizo zinaposonga kuelekea kwenye maeneo ya nia za Mungu na mwelekeo wa Mungu kwa binadamu, basi mambo yanapata kuwa magumu zaidi kwa watu wote. Hiyo ni kwa sababu yote haya yanahusisha uelewa wa ukweli na kuingia kwao katika uhalisia; bila shaka kuna kiwango cha ugumu. Lakini baada ya wewe kuingia kupitia mlango wa kwanza, baada ya wewe kuanza kuingia ndani yake, mambo yanaanza kuwa rahisi na rahisi kwa utaratibu.
Sehemu ya Mwanzo ya Kumcha Mungu ni Kumtendea Kama Mungu
Mtu fulani amelizua swali hivi punde: Inakuwaje kwamba tunajua zaidi kuhusu Mungu kuliko alivyojua Ayubu, ilhali bado hatuwezi kumcha Mungu? Tuliligusia suala hili hapo awali kidogo, sivyo? Kwa hakika, kiini halisi cha swali hili kimeweza pia kuzungumziwa awali kwamba ingawa Ayubu hakumjua Mungu wakati huo, alimshughulikia Yeye kama Mungu, na kumchukulia Yeye kama Bwana wa mambo yote mbinguni na nchini. Ayubu hakumchukulia Mungu kuwa adui. Badala yake, alimwabudu Yeye kama Muumba wa viumbe vyote. Watu siku hizi wanampinga Mungu sana kwa nini? Kwa nini hawawezi kumcha Mungu? Sababu moja ni kwamba wamepotoshwa pakubwa na Shetani. Wakiwa na asili yao ya kishetani ikiwa imekita mizizi ndani, watu wanageuka na kuwa adui wa Mungu. Hivyo basi, hata ingawa wanasadiki katika Mungu na kumtambua Mungu, bado wanaweza kumpinga Mungu na kujiweka katika nafasi ya upinzani na Yeye. Hili linaamuliwa na asili ya binadamu. Sababu nyingine ni kwamba ingawa watu wanasadiki Mungu, hawamchukulii Yeye tu kama Mungu. Badala yake, wanamchukulia Mungu kuwa ndiye anayempinga binadamu, wakimwona Yeye kuwa adui wa binadamu, na hawawezi kupatanishwa na Mungu. Ni rahisi hivyo. Je, jambo hili halikuzungumziwa kwenye kikao cha awali? Hebu fikiria: Hiyo ndiyo sababu? Ingawa unayo maarifa kidogo ya Mungu, maarifa haya hasa ni nini? Haya siyo yale kila mtu anazungumzia? Haya si yale ambayo Mungu alikuambia? Unajua tu zile dhana za kinadharia na kifalsafa; umewahi kupitia dhana halisi ya Mungu? Je, unayo maarifa ya kibinafsi? Je, unayo maarifa na uzoefu wa kimatendo? Kama Mungu asingekuambia, ungelijua hili? Maarifa yako katika nadharia hayawakilishi maarifa halisi. Kwa ufupi, bila kujali ni kiwango kipi unachojua na ni vipi ulivyokijua hatimaye, kabla ya wewe kufikia uelewa halisi wa Mungu, Mungu ndiye adui wako, na kabla ya wewe kumshughulikia Mungu hivyo, Amewekwa kuwa mpinzani wako, kwani wewe ni mfano halisi wa Shetani.
Unapokuwa pamoja na Kristo, pengine unaweza kumhudumia kwa milo mitatu kwa siku, pengine kumhudumia Yeye kwa chai, kuyashughulikia mahitaji Yake ya maisha, ni kana kwamba unamshughulikia Kristo kama Mungu. Kila wakati jambo linapofanyika, mitazamo ya watu siku zote inakuwa kinyume cha mtazamo wa Mungu. Siku zote wanashindwa kuelewa mtazamo wa Mungu, na wanashindwa kuukubali. Ingawa watu wanaweza kupatana na Mungu juujuu, hii haimaanishi kwamba wanalingana na Yeye. Punde tu jambo linapofanyika, ukweli wa kutotii kwa binadamu unaibuka, na kuthibitisha ukatili uliopo kati ya binadamu na Mungu. Ukatili huu si wa Mungu kumpinga binadamu; si Mungu kutaka kuwa katili kwa binadamu, na si Mungu kumweka binadamu katika upinzani na kumshughulikia binadamu hivyo. Badala yake, ni hali ya upinzani huu wa kiini halisi kwa Mungu ambao unajificha katika mapenzi ya kibinafsi ya binadamu, na katika akili ya kutofahamu ya binadamu. Kwa sababu binadamu anachukulia kila kitu kinachotoka kwa Mungu kama kifaa cha utafiti wake, mwitikio wake kwa hiki ambacho kinatoka kwa Mungu na kile ambacho kinamhusisha Mungu ni, zaidi ya yote, kukisia, na kushuku, na kisha haraka sana kuingia katika mwelekeo ambao unakinzana na Mungu, na unapingana na Mungu. Baada ya hapo, binadamu atachukua hali hizi za moyo za kimyakimya na kuzua mjadala na Mungu au kushindana na Mungu hadi kufikia kiwango ambacho atatia shaka kama Mungu wa aina hii anastahili kufuatwa. Licha ya hoja kwamba urazini wa binadamu unamwambia asiendelee hivi, bado atachagua kufanya hivyo licha ya kutotaka kufanya hivyo, kiasi kwamba ataendelea bila kusita hadi mwisho. Kwa mfano, ni nini mwitikio wa kwanza kwa baadhi ya watu wanaposikia uvumi fulani au matusi fulani kumhusu Mungu? Mwitikio wa kwanza ni: Sijui kama uvumi huu ni kweli au la, kama upo ama haupo, hivyo basi nitasubiri na kuona. Kisha wanaanza kutafakari: Hakuna njia ya kuthibitisha haya; ipo kweli? Uvumi huu ni kweli au la? Ingawa mtu huyu haonyeshi juujuu, moyo wake tayari umeanza kutia shaka, tayari umeanza kumkataa Mungu. Ni nini kiini halisi cha aina hii ya mwelekeo, aina hii ya mtazamo? Je huu si usaliti? Kabla ya wao kukumbwa na suala, huwezi kuona mtazamo wa mtu huyu ni nini—yaonekana ni kana kwamba wao hawakinzani na Mungu, ni kama hawamchukulii Mungu kuwa adui. Hata hivyo, punde wanapokumbwa na suala hilo, wanasimama mara moja na Shetani na kumpinga Mungu. Hali hii inapendekeza nini? Inapendekeza kwamba binadamu na Mungu wanapingana! Si kwamba Mungu anamchukulia binadamu kama adui, lakini kwamba kile kiini halisi chenyewe cha binadamu ni kikatili kwa Mungu. Haijalishi ni kwa muda mrefu vipi ambapo mtu humfuata Mungu, ni kiwango kipi anacholipia; haijalishi vipi ambavyo mtu anamsifu Mungu, anavyojihifadhi dhidi ya kumpinga Mungu, hata akijisihi kumpenda Mungu, hatawahi kufaulu kumshughulikia Mungu kama Mungu. Si hali hii inaamuliwa na kiini halisi cha mwanadamu? Kama Utamshughulikia kama Mungu, unaweza kwa kweli kusadiki kwamba Yeye ni Mungu, unaweza bado kuwa na shaka lolote kwake Yeye? Bado kunaweza kuwa na maswali yoyote yanayomhusu Yeye katika moyo wako? Hakuwezi. Mitindo ya ulimwengu huu ni miovu kweli, kizazi hiki cha wanadamu kina uovu kweli—inakuwaje kwamba huna hata dhana zozote kuyahusu? Wewe mwenyewe umejaa uovu—inakuwaje kwamba huna dhana zozote kuhusu hayo? Ilhali uvumi mchache tu, matusi fulani yanaweza kusababisha dhana kubwa mno kumhusu Mungu, zinaweza kuleta mawazo mengi mno, hali inayoonyesha vile ambavyo kimo chako kilivyo bado kichanga! "Mnong’ono" tu wa mbu wachache, nzi wachache wabaya, hilo tu ndilo linalokupotosha? Huyu ni mtu wa aina gani? Je, unajua anachofikiria Mungu kuhusu mtu wa aina hii? Mwelekeo wa Mungu kwa hakika uko wazi sana kuhusiana na ni vipi Anavyowashughulikia watu hawa. Ni kwa sababu tu kwamba ushughulikiaji wa Mungu kwa watu hawa ni kuwapuuza—mwelekeo Wake ni kutowatilia maanani, na kutomakinikia watu hawa wasiojua. Kwa nini hivyo? Kwa sababu katika moyo Wake Hakuwahi kupangilia kuhusu kupata watu hao ambao wameahidi kuwa wakatili kwake Yeye hadi mwisho, na ambao hawajawahi kupangilia kutafuta njia ya uwiano na Yeye. Pengine maneno haya Niliyoyaongea yamewaumiza watu wachache. Kwa kweli, mko radhi kuniruhusu Mimi kuwadhuru siku zote namna hii? Bila kujali kama mko radhi au la, kila kitu Ninachosema ni ukweli! Kama siku zote Ninawadhuru namna hii, siku zote Nafichua makovu yenu, je, itaathiri taswira za majivuno kuhusu Mungu katika mioyo yenu? (Haitaathiri.) Ninakubali kwamba haitaathiri kwani kwa ufupi hakuna Mungu katika mioyo yenu. Yule Mungu wa majivuno anayepatikana ndani ya mioyo yenu, yule mnayemtetea kwa dhati na kulinda, kwa ufupi si Mungu. Badala yake ni ndoto ya kufikiria kwa binadamu; kwa ufupi haipo. Hivyo basi ni bora zaidi kama Nitafichua jibu la kitendawili hiki. Je, huu si ukweli wote? Mungu halisi hatokani na kufikiria kwa binadamu. Natumai kwamba nyote mnaweza kukabiliana na uhalisia huu, na utawasaidia katika maarifa yenu ya Mungu.
Wale Watu Wasiotambuliwa na Mungu
Kunao baadhi ya watu ambao imani yao haijawahi kutambuliwa katika moyo wa Mungu. Kwa maneno mengine, Mungu hatambui kwamba watu hawa ni wafuasi Wake, kwa sababu Mungu haisifu imani yao. Kwa watu hawa, haijalishi wamemfuata Mungu kwa miaka mingapi, mawazo na mitazamo yao haijawahi kubadilika. Wao ni kama wasioamini, wanatii kanuni na njia ambayo wasioamini wanafanya mambo yao, kutii sheria zao za kusalia na imani. Hawakuwahi kukubali neno la Mungu kama maisha yao, hawakuwahi kusadiki kwamba neno la Mungu ni ukweli, hawakuwahi kunuia kukubali wokovu wa Mungu, na hawakuwahi kutambua Mungu kama Mungu wao. Wanachukulia kusadiki Mungu kuwa uraibu fulani wa wanagenzi, wakishughulikia Mungu kama riziki ya kiroho, hivyo basi hawafikirii kwamba ipo thamani ya kujaribu na kuelewa tabia ya Mungu, au kiini halisi cha Mungu. Unaweza kusema kwamba kila kitu kinacholingana na Mungu wa kweli hakihusiani kwa vyovyote vile na watu hawa. Hawana hamu yoyote, na hawawezi kusumbuliwa ili kuitikia. Hii ni kwa sababu ndani kabisa ya mioyo yao kunayo sauti ya nguvu ambayo siku zote inawaambia: Mungu haonekani na hagusiki, na Mungu hayupo. Wanasadiki kwamba kujaribu kumwelewa Mungu wa aina hii hakutastahili jitihada zao; itakuwa sawa na wao kujidanganya. Wanamtambua Mungu kwa maneno tu, na hawachukui msimamo wowote halisi. Pia hawafanyi chochote katika hali ya kimatendo, wakifikiri kwamba wao ni werevu sana. Mungu anachukulia vipi watu kama hawa? Anawachukulia kuwa wasioamini. Baadhi ya watu huuliza: "Je, wasioamini wanaweza kulisoma neno la Mungu? Je, wanaweza kutekeleza wajibu wao? Je, wanaweza kuyasema maneno haya: "Nitaishi kwa ajili ya Mungu"? Kile ambacho binadamu huona mara nyingi ni maonyesho ya juujuu tu ya watu, na wala si kiini chao halisi. Ilhali Mungu haangalii maonyesho haya ya juujuu; Yeye huona tu kiini chao halisi cha ndani. Hivyo basi, Mungu anao mwelekeo wa aina hii, ufafanuzi wa aina hii, kwa watu kama hawa. Kuhusiana na kile ambacho watu hawa husema: "Kwa nini Mungu hufanya hivi? Kwa nini Mungu hufanya vile? Siwezi kuelewa haya; siwezi kuelewa yale; haya hayaingiliani na fikira za binadamu; Lazima unielezee haya; ..." Jibu langu ni: Inahitajika kuelezea suala hili kwako? Je, suala hili lina chochote kuhusiana na wewe? Unafikiria wewe ni nani? Ulitokea wapi? Umefuzu kumwelekeza Mungu? Je, unamwamini Yeye? Je, Anatambua imani yako? Kwa sababu imani yako haina chochote kuhusiana na Mungu, matendo Yake yana uhusiano gani na wewe? Hujui pale ulipo katika moyo wa Mungu, ilhali umefuzu kuzungumza na Mungu?
Maneno ya Maonyo
Hamhisi vibaya baada ya kusikia matamshi haya? Ingawa huenda msiwe radhi kusikiliza maneno haya, au msiwe radhi kuyakubali, yote ni uhakika. Kwa sababu awamu hii ya kazi ni ya Mungu kutenda, kama hujali nia za Mungu, hujali mwelekeo wa Mungu na huelewi kiini halisi na tabia ya Mungu, basi hatimaye wewe ndiwe utakayekosa kufaidi. Msiyalaumu maneno yangu kwa kuwa magumu kusikiliza, na msiyalaumu kwa kupunguza majivuno ya shauku yenu. Mimi naongea ukweli; na wala Sinuii kuwavunja moyo. Haijalishi ni nini Ninachowauliza ninyi, na haijalishi ni vipi mnavyohitajika kukifanya, Ninatumai kwamba mtatembelea njia sahihi, na ninatumai kwamba mtafuata njia ya Mungu na wala msipotoke katika njia hii. Kama hutaendelea kulingana na neno la Mungu, na hufuati njia Yake, basi hakutakuwa na shaka kwamba unaasi dhidi ya Mungu na umepotea kutoka kwa njia sahihi. Hivyo basi Nahisi kwamba yapo masuala fulani ambayo lazima Niwabainishie, na kuwafanya kusadiki dhahiri shairi, waziwazi, bila ya tone la mashaka na kuwasaidia waziwazi kujua mwelekeo wa Mungu, nia za Mungu, namna Mungu anavyomfanya binadamu kuwa mtimilifu, na ni kwa njia gani Yeye Hupanga matokeo ya binadamu. Endapo kutakuwa na siku ambayo hutaweza kuanza katika njia hii, basi Sitahitajika kuwajibika kwa vyovyote vile kwa sababu maneno haya tayari yamezungumzwa kwako waziwazi. Na kuhusu vile unavyoshughulikia matokeo yako binafsi—suala hili lote umeachiwa wewe. Mungu Anayo mielekeo tofauti kuhusiana na matokeo ya watu aina tofauti. Anazo njia Zake binafsi za kuwapima binadamu, na kiwango Chake binafsi cha mahitaji. Kiwango chake cha kuwapima watu ni kile ambacho ni cha haki kwa kila mmoja—hakuna shaka kuhusu hilo. Hivyo basi, woga wa watu fulani hauhitajiki. Je, umepata tulizo la moyo sasa? Ndivyo hivyo kwa leo. Kwaheri!

Oktoba 17, 2013

Chanzo: Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake Sehemu ya Tano

Kuhusu Sisi:  Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni