Ijumaa, 20 Desemba 2019

Jinsi ya kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima?


Aya za Biblia za Kurejelea:

“Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu. Hivyo ndivyo alivyokuwa mwanzoni na Mungu” (Yohana 1:1-2).

“Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, aliyejawa neema na ukweli” (Yohana 1:14).

“Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu” (Yohana 14:6).

“Maneno ninayoongea kwenu ni roho, na ni uhai” (Yohana 6:63).

Maneno Husika ya Mungu:

Ukweli unatoka katika ulimwengu wa mwanadamu, na bado ukweli katika mwanadamu unapitishwa na Kristo. Unaanzia kwa Kristo, yaani, kutoka kwa Mungu mwenyewe, na hauwezi kufikiwa na mwanadamu.

kutoka katika “Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna jinsi ya kutumia maneno ili kuueleza ukweli kikamilifu, ukweli ukiwekwa kwa lugha ya binadamu ni methali kwa mwanadamu; ubinadamu hauwezi kupata uzoefu wake kikamilifu, na ubinadamu lazima uishi kwa kuutegemea. Kipande cha ukweli kinaweza kuufanya ubinadamu mzima kuishi kwa maelfu ya miaka.

Ukweli ni maisha ya Mungu Mwenyewe, ukiiwakilisha tabia Yake binafsi, ukiwakilisha dutu Yake binafsi, ukiwakilisha kila kitu ndani Yake.

kutoka katika “Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

“Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu, na Neno likawa mwili.” Hii (kazi ya kuonekana kwa Neno katika mwili) ni kazi ambayo Mungu atatimiza katika siku za mwisho, na ni sura ya mwisho ya mpango Wake mzima wa uongozi, kwa hivyo Mungu lazima Aje duniani na kudhihirisha maneno Yake katika mwili.

kutoka katika “Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Wakati huu, Mungu haji kufanya kazi kwa mwili wa kiroho ila kwa ule wa kawaida sana. Sio tu mwili wa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, lakini pia mwili ambao Mungu anarudia. Ni mwili wa kawaida sana. Ndani Yake, huwezi kuona chochote kilicho tofauti na cha wengine, lakini unaweza kupokea kutoka Kwake ukweli ambao hujawahi kusikia mbeleni. Mwili huu usio na umuhimu ni mfano halisi wa maneno yote ya kweli kutoka kwa Mungu, ambao hufanya kazi ya Mungu siku za mwisho, na maonyesho ya tabia nzima ya Mungu kwa mwanadamu kuja kujua. Je, hukutamani sana kumwona Mungu aliye mbinguni? Je, hukutamani sana kumwelewa Mungu aliye mbinguni? Je, hukutamani sana kuona hatima ya mwanadamu? Atakueleza hizi siri zote ambazo hakuna mwanadamu ameweza kukuambia, na hata Atakuelezea kuhusu ukweli usioelewa. Yeye ndiye lango la kuingia katika ufalme, na mwongozo wako katika enzi mpya. Mwili wa kawaida kama huu una siri nyingi zisizoeleweka. Matendo Yake labda hayaeleweki kwako, lakini lengo la kazi yote Anayoifanya limekutosha kuona kuwa Yeye si mwili wa kawaida anavyoamini mwanadamu. Kwani Anawakilisha mapenzi ya Mungu na pia utunzaji anaoonyesha Mungu kwa mwanadamu siku za mwisho. Ingawa huwezi kuyasikia maneno Anayozungumza yanayoonekana kutingisha mbingu na dunia wala kuona macho Yake kama moto mkali, na ingawa huwezi kuhisi nidhamu ya fimbo Yake ya chuma, unaweza kusikia kupitia maneno Yake ghadhabu ya Mungu na kujua kwamba Mungu Anaonyesha huruma kwa mwanadamu; unaweza kuona tabia ya haki ya Mungu na hekima Yake, na zaidi ya hayo, kutambua wasiwasi na utunzaji anao Mungu kwa wanadamu wote, Kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kuruhusu mwanadamu kumwona Mungu aliye mbinguni Akiishi miongoni mwa wanadamu duniani, na kumwezesha mwanadamu kuja kumjua, kumtii, kumheshimu, na kumpenda Mungu. Hii ndiyo maana Amerudi kwa mwili kwa mara ya pili. …

… Yote mliyonayo siku hii ni kwa sababu ya huu mwili. Ni kwa sababu Mungu huishi ndani ya mwili ndiyo mna nafasi ya kuishi. Hii bahati yote nzuri imepatwa kwa sababu ya huyu mwanadamu wa kawaida. Siyo haya tu, lakini mwishowe kila taifa litamwabudu huyu mwanadamu wa kawaida, na pia kumpa shukrani na kumtii huyu mwanadamu asiye muhimu. Kwa sababu ni Yeye aliyeleta ukweli, uhai, na njia ya kuwaokoa wanadamu wote, kutuliza migogoro kati ya Mungu na mwanadamu, kuleta Mungu na mwanadamu pamoja karibu zaidi na kuwasilisha mawazo kati ya Mungu na mwanadamu. Pia ni Yeye ambaye Ameleta hata utukufu zaidi kwa Mungu. Mwanadamu wa kawaida kama huyu hastahili uaminifu na ibada yako? Mwili wa kawaida kama huu haufai kuitwa Kristo? Mwanadamu wa kawaida kama huyu hawezi kuwa maonyesho ya Mungu miongoni mwa wanadamu? Mwanadamu kama huyu anayesaidia wanadamu kuepuka maafa hastahili mapenzi yenu na nyinyi kumshikilia? Mkiukataa ukweli unaotamkwa kutoka mdomo Wake na pia kuchukia kuwepo Kwake miongoni mwenu, basi nini itakuwa majaliwa yenu?

kutoka katika “Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Na bado ni huyu mtu wa kawaida, aliyefichika kati ya watu, ndiye anayefanya kazi hii mpya ya kutuokoa. Yeye hatupi maelezo yoyote, wala Hatuambii kwa nini amerudi, lakini Yeye anafanya tu kazi anayotarajia kufanya kwa hatua zilizopimwa, na kwa mujibu wa mpango Wake. Maneno Yake na matamshi Yake yanazidi kuja kwa wingi. Kuanzia kufariji, kuonya, kukumbusha, na kupeana onyo mpaka kukaripia na kufundisha nidhamu; kuanzia kutumia sauti ya upole na laini mpaka kutumia maneno makali na ya adhimu—lakini hakuna inayompa mwanadamu huruma na kumtia hofu. Kila kitu Anachosema kinatufikia kwetu na kulenga siri zilizofichwa ndani yetu, maneno Yake huchoma mioyo yetu, huchoma nafsi zetu, na hutuacha tukiwa tumejaa aibu isiyovumilika, tusijue pa kujificha. …

Pasipo sisi kujua, huyu mtu asiye muhimu ametuelekeza katika hatua moja baada yanyingine ya kazi ya Mungu. Sisi hupitia majaribu tele, kuvumilia kurudi kusikohesabika, na tunajaribiwa na kifo. Tunapata kujua kuhusu tabia ya Mungu ya haki na uadhama, kufurahia, pia, upendo na huruma Zake, tunakuja kufahamu nguvu za Mungu ambazo ni kubwa na hekima Yake, tunashuhudia uzuri wa Mungu, na kutazama hamu Yake ya kumwokoa mwanadamu. Kwa maneno ya huyu mtu wa kawaida, tunakuja kujua tabia na kiini cha Mungu, kufahamu mapenzi ya Mungu, kujua asili ya mwanadamu na kiini cha mwanadamu, na tunapata kuona njia ya wokovu na ukamilifu. Maneno Yake hutufanya sisi “tufe,” na tena hutufanya “kuzaliwa upya”; maneno Yake hutufariji, na ilhali pia hutuacha tukiwa tumejawa na hatia na hisia ya kuwa wadeni; maneno Yake hutuletea furaha na amani, lakini pia maumivu makubwa sana. Wakati mwingine sisi ni kama wanakondoo wa kuchinjwa mikononi Mwake; wakati mwingine sisi ni kama kipenzi cha roho Yake na kufurahia upendo Wake wenye upole; wakati mwingine sisi ni kama adui Yake, na chini ya macho Yake tunageuzwa majivu na ghadhabu Yake. Sisi ni jamii ya wanadamu waliookolewa Naye, sisi ni funza machoni Pake, na sisi ni wanakondoo waliopotea ambao, usiku na mchana, Yeye hunuia kuwapata. Yeye ni mwenye huruma kwetu, hutudharau, Yeye hutuinua, Yeye hutufariji na kutuhimiza, Yeye hutuongoza, yeye hututia nuru, yeye huturudi na kutufundisha nidhamu, na Yeye hata hutulaani. Usiku na mchana, Yeye hakomi kamwe kuwa na wasiwasi nasi na hutulinda na kututunza usiku na mchana, Asiwache upande wetu kamwe, bali humwaga damu ya moyo Wake kwa ajili yetu na hulipia gharama yoyote kwa ajili yetu. Miongoni mwa matamshi ya mwili huu mdogo na wa kawaida wa nyama, tumefurahia ukamilifu wa Mungu na kuona hatima ambayo Mungu ametupa. …

Mungu huendelea na matamshi Yake, akitumia mbinu mbalimbali na mitazamo kutuonya kuhusu kile tunachofaa kufanya na wakati uo huo akipea moyo Wake sauti Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, hutuonyesha njia tunayopasa kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Tunaanza kuvutiwa na maneno Yake, tunaanza kuzingatia sauti Yake na jinsi Anavyoongea, na bila hiari tunaanza kuvutiwa na hisia za ndani kabisa za mwanadamu huyu asiye wa ajabu. Yeye hutema damu ya moyo Wake kwa niaba yetu, hupoteza usingizi na hamu ya chakula kwa ajili yetu, analia kwa ajili yetu, anashusha pumzi kwa ajili yetu, anaugua magonjwa akigumia kwa ajili yetu, anadhalilishwa kwa ajili ya wokovu na hatima yetu, na uasi wetu na kufa ganzi kwetu kunatoa machozi na damu kutoka kwa moyo Wake. Njia hii ya kuwa na kumiliki si ya mtu wa kawaida, wala haiwezi kumilikiwwa au kufikiwa na mtu yeyote aliyepotoka. Anaonyesha uvumilivu na subira isiyomilikiwa na mtu wa kawaida, na upendo Wake si kitu ambacho kiumbe chochote kimepewa. Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu na kiini chetu kwa dhahiri na ukamilifu, ama kuhukumu uasi na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu aliye mbinguni. Hakuna mtu isipokuwa Yeye ambaye amepewa mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Mungu Anacho na alicho yanatoka, kwa ukamilifu wao, ndani Yake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana na utumwa wa Shetani na tabia yetu potovu. Yeye humwakilisha Mungu. Yeye huonyesha moyo wa ndani zaidi wa Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya Mungu kwa wanadamu wote. Ameanzisha enzi mpya, nyakati mpya, na kuleta mbingu na nchi mpya na kazi mpya, na ametuletea matumaini, akimaliza maisha ambayo tuliishi katika hali isiyo dhahiri, na kuwezesha nafsi yetu nzima kuona njia ya wokovu kwa udhahiri kamili. Ameshinda ubinadamu wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili zetu zimepata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na ambaye amekataliwa na sisi zamani—Je, huyu si ni Bwana Yesu, ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, tukiwa tumeamka au kuota, na ambaye tunamtamani usiku na mchana? Ni Yeye! Ni Yeye kweli! Yeye ni Mungu wetu! Yeye ndiye ukweli, njia, na uzima! Yeye ametuwezesha kuishi tena na kuona nuru, na amekomesha mioyo yetu kuhangaika. Tumerudi nyumbani mwa Mungu, tumerejea mbele ya kiti Chake cha enzi, tuko uso kwa uso pamoja na Yeye, tumeshuhudia uso Wake, na tumeona njia iliyo mbele.

kutoka katika “Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumkamilisha binadamu, na kumwondoa binadamu. Hii ndiyo maana ya kweli ya kutumia neno ili kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia katika neno, binadamu anajua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha binadamu, na kile ambacho binadamu anastahili kuingia ndani yake. Kupitia katika neno, kazi yote ambayo Mungu angependa kufanya katika Enzi ya Neno inatimizwa. Kupitia katika neno, binadamu anafichuliwa, anaondolewa, na kujaribiwa. Binadamu ameliona neno, amelisikia neno, na akapata habari ya uwepo wa neno. Kutokana na haya, binadamu anaamini katika uwepo wa Mungu; binadamu anaamini katika uwezo na hekima za Mungu, pamoja na moyo wa upendo wa Mungu kwa binadamu na tamanio Lake la kumwokoa binadamu. Ingawa neno “neno” ni rahisi na la kawaida, neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu mwenye mwili hutikisa dunia nzima; neno Lake hubadilisha moyo wa binadamu, fikira na tabia zee za binadamu, na sura nzee ya ulimwengu mzima. Kupitia enzi nyingi, Mungu pekee wa leo ndiye anayefanya kazi katika njia kama hiyo, na ni Yeye tu Anayeongea na kumwokoa binadamu hivyo. Kuanzia wakati huu kuendelea, binadamu huishi katika mwongozo wa neno, wakichungwa na kuruzukiwa na neno. Binadamu wote wanaishi katika ulimwengu wa neno, wanaishi katika laana na baraka za neno la Mungu, na hata kuna binadamu zaidi wanaoishi chini ya hukumu na kuadibu kwa neno. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa minajili ya wokovu wa binadamu, kwa minajili ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa minajili ya kubadilisha sura asilia ya ulimwengu wa uumbaji wa kale. Mungu aliuumba ulimwengu kwa neno, huwaongoza wanadamu kote ulimwenguni kwa neno, na pia hushinda na kuwaokoa binadamu kwa neno. Hatimaye, Yeye atatumia neno ili kuutamatisha ulimwengu mzima wa kale. Ni hapo tu ndipo mpango wa usimamizi unapokuwa mkamilifu kabisa.

kutoka katika “Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno” katika Neno Laonekana katika Mwili

Neno limepata mwili na Roho wa kweli amepatikana katika mwili—kwamba ukweli wote, uzima, na njia umekuja katika mwili, na Roho amewasili duniani na katika mwili kwa kweli. Ingawa, kijuujuu, hili linaonekana ni tofauti na utungaji mimba kwa Roho Mtakatifu, katika kazi hii mnaweza kuona kwa dhahiri zaidi kwamba Roho tayari amepatikana katika mwili, na, zaidi ya hayo, kwamba Neno limepata mwili, na Neno limeonekana katika mwili, na unaweza kufahamu maana ya kweli ya maneno haya: Hapo mwanzo kulikuwako na Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Zaidi ya hayo, lazima ufahamu maneno ya leo ni Mungu, na lazima utazame maneno yakipata mwili. Huu ni ushuhuda bora zaidi unaoweza kuwa nao. Hili linathibitisha kwamba una ufahamu wa kweli wa Mungu kupata mwili—wewe huwezi tu kumjua na kumchambua Yeye, lakini pia unajua kwamba njia unayoifuata leo ni njia ya uzima, na njia ya ukweli. Yesu alifanya hatua ya kazi ambayo ilitimiza tu kiini cha “Neno alikuwako kwa Mungu”: Ukweli wa Mungu ulikuwako kwa Mungu, na Roho wa Mungu alikuwa na mwili na alikuwa asiyetenganishwa kutoka Kwake, yaani, mwili wa Mungu mwenye mwili ulikuwa na Roho wa Mungu, ambalo ni thibitisho kuu zaidi kwamba Yesu mwenye mwili alikuwa aliyepata mwili wa kwanza wa Mungu. Hatua hii ya kazi ilitimiza maana ya ndani ya “Neno lapata mwili,” ilichangia kwenye maana ya kina zaidi ya “naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu,” na inakuruhusu wewe uamini kwa uthabiti maneno haya kwamba “Hapo mwanzo kulikuwako na Neno.” Ambalo ni kusema, wakati wa uumbaji Mungu alikuwa na maneno, Maneno Yake yalikuwa na Yeye na yasiyotenganishwa kutoka Kwake, na enzi ya mwisho inafanya nguvu na mamlaka ya maneno Yake yawe hata wazi zaidi, na kumkubalia mwanadamu kuyaona maneno Yake yote—kuyasikia maneno Yake yote. Hiyo ndiyo kazi ya enzi ya mwisho. Lazima uyajue mambo haya yote kabisa. Si suala la kuujua mwili, bali la kuujua mwili na Neno. Hiki ndicho kile unachotakiwa kushuhudia, kile ambacho kila mtu lazima akijue.

kutoka katika “Utendaji (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

span style="background-color: white;">Maneno yangu ndio ukweli usiobadilika milele. Mimi Ndiye msambazaji wa binadamu na kiongozi wa pekee wa mwanadamu. Thamani na maana ya maneno Yangu haibainishwi na kama yanakubaliwa au kutambuliwa na mwanadamu, ila ni kwa kiini cha maneno yenyewe. Hata kama hakuna mtu hata mmoja duniani anaweza kupokea maneno Yangu, thamani ya maneno Yangu na usaidizi wake kwa mwanadamu hayapimiki na mwanadamu yeyote. Kwa hivyo, Ninapokumbwa na wanadamu wengi wanaoasi, kukataa au kudharau kabisa maneno Yangu, msimamo Wangu ni huu tu: Wacha wakati na ukweli uwe shahidi Wangu na uonyeshe kuwa maneno Yangu ndiyo ukweli, njia na uhai. Wacha vionyeshe kuwa yote Niliyosema ni ya ukweli, na kuwa ni yale ambayo mwanadamu lazima apewe, na, zaidi ya yote, yale ambayo mwanadamu anafaa akubali. Nitawaruhusu wote wanaonifuata wajue ukweli huu: Wote wasioyakubali maneno Yangu kikamilifu, wale wasioyaweka maneno Yangu katika vitendo, wale wasiopata sababu ndani ya maneno Yangu, na wale wasiopata wokovu kwa sababu ya maneno Yangu, ni wale ambao wamehukumiwa na maneno Yangu na, zaidi ya hayo, wamepoteza wokovu Wangu, na fimbo Yangu haitaondoka kamwe miongoni mwao.

kutoka katika “Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu” katika Neno Laonekana katika Mwili

(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)

Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote. Kutoka Alipoumba dunia, Mungu amefanya kazi kubwa inayoshirikisha uhai wa maisha, Amefanya kazi kubwa ambayo huletea mwanadamu maisha, na Amelipa gharama kubwa ili mtu aweze kupata uzima, kwa kuwa Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele, na Mungu Mwenyewe ni njia ambayo kwayo mtu hufufuliwa. Mungu kamwe hajawahi kosa kwa moyo wa mwanadamu, na Anaishi miongoni mwa binadamu wakati wote. Amekuwa nguvu ya kuendesha maisha ya mwanadamu, chanzo cha kuwepo kwa binadamu, na amana ya fahari ya kuwepo kwa binadamu baada ya kuzaliwa. Husababisha binadamu kuzaliwa upya, na kumwezesha kwa ushupavu kuishi kwa kila jukumu lake. Kwa sababu ya uwezo Wake, na nguvu ya maisha Yake yasiyopungua, binadamu ameishi kwa kizazi baada ya kizazi, ambapo nguvu ya uhai wa Mungu umekuwa uti wa mgongo wa kuwepo kwa binadamu, na ambayo Mungu amelipia gharama ambayo hakuna mtu wa kawaida amewahi kulipa. Nguvu za Mungu za maisha zinaweza kutawala juu ya nguvu zozote; zaidi ya hayo, inazidi mamlaka yoyote. Maisha Yake ni ya milele, nguvu zake za ajabu, na nguvu Zake za maisha si rahisi kuzidiwa na kiumbe yeyote au nguvu za adui. Nguvu za maisha ya Mungu zipo, na hung’aa mwangaza wake ulio mzuri sana, bila ya kujali muda au mahali. Maisha ya Mungu, huishi milele bila kubadilika katika kusumbuka kwa mbingu na nchi. Mambo yote hupita, lakini maisha ya Mungu hubaki, kwa maana Mungu ni chanzo cha kuwepo kwa mambo yote, na mizizi ya kuwepo kwao. Asili ya maisha ya mwanadamu hutoka kwa Mungu, kuwepo kwa mbingu ni kwa sababu ya Mungu, na kuwepo kwa ardhi kunatokana na nguvu ya uhai wa Mungu. Hakuna kitu kinachomiliki nguvu kinachoweza kuzidi ukuu wa Mungu, na hakuna kitu chenye nguvu kinachoweza kuvunja mipaka ya mamlaka ya Mungu. Kwa njia hii, bila kujali wao ni nani, kila mtu lazima ajiwasilishe kwa utawala wa Mungu, kila mtu lazima aishi chini ya amri za Mungu, na hakuna mtu anayeweza kutoroka kutoka katika utawala Wake.

Pengine, sasa, unataka kupokea maisha, au labda unataka kupata ukweli. Vyovyote vilivyo, unataka kumpata Mungu, kumpata Mungu unayeweza kutegemea, na ambaye anaweza kukupa uzima wa milele. Ukitaka kupata uzima wa milele, lazima kwanza uelewe chanzo cha uzima wa milele, na lazima kwanza ujue Mungu yuko wapi. Tayari nilishasema Mungu pekee ndiye maisha yasiyobadilika, na Mungu tu ndiye aliye na njia ya maisha. Kwa kuwa maisha Yake ni imara, hivyo ni ya milele; kwa kuwa Mungu tu ndiye njia ya maisha, basi Mungu Mwenyewe ni njia ya uzima wa milele. Kwa hivyo, lazima kwanza uelewe aliko Mungu, na jinsi ya kupata njia hii ya uzima wa milele. Hebu sasa tushiriki kwa masuala haya mawili tofauti.

Kama kweli unataka kupata njia ya uzima wa milele, na kama wewe unayo tamaa katika utafutaji wako kwa ajili yake, basi kwanza ulijibu swali hili: Mungu yuko wapi leo? Labda utajibu kwamba Mungu anaishi mbinguni, bila shaka—Hangeishi katika nyumba yako? Labda unaweza kusema, kawaida Mungu anaishi kati ya mambo yote. Au unaweza kusema kwamba Mungu anaishi katika moyo wa kila mtu, au kwamba Mungu yuko katika ulimwengu wa kiroho. Mimi sipingi lolote kati ya haya, lakini lazima nifafanue suala hilo. Sio sahihi kabisa kusema kwamba Mungu anaishi katika moyo wa mwanadamu, wala si makosa kabisa. Hiyo ni kwa sababu, miongoni mwa waumini katika Mungu, kuna wale ambao imani yao ni ya kweli na wale ambao imani yao ni uongo, kuna wale ambao Mungu anawakubali na wale ambao hawakubali, kuna wale ambao humfurahisha na wale ambao ni chukizo, na kuna wale ambao Yeye huwafanya kamili na wale ambao hupunguza. Na hivyo Mimi Nasema kwamba Mungu Anaishi tu katika nyoyo za watu wachache, na watu hawa bila shaka ni wale ambao kweli wanaamini katika Mungu, wale ambao Mungu anawakubali, wale ambao humpendeza, na wale ambao Yeye huwafanya kamili. Wao ni wale wanaoongozwa na Mungu. Kwa kuwa wanaongozwa na Mungu, kwa hivyo ni watu ambao tayari wamesikia na kuona njia ya Mungu ya uzima wa milele. Wale ambao imani yao kwa Mungu ni ya uongo, wale ambao hawajaidhinishwa na Mungu, wale ambao wanadharauliwa na Mungu, wale ambao wamechujwa na Mungu—wamefungwa katika kukataliwa na Mungu, wamefungwa kubaki bila njia ya maisha, na wamefungwa kubaki wajinga wa kujua aliko Mungu. Kwa upande mwingine, wale ambao Mungu anaishi katika nyoyo zao wanajua aliko Mungu. Wao ni watu wale ambao Mungu huwapa njia ya uzima wa milele, na ni wale wanaomfuata Mungu. Je, unajua, sasa, aliko Mungu? Mungu yupo katika moyo wa mtu na upande wa mtu. Hayupo tu katika ulimwengu wa kiroho, na juu ya mambo yote, lakini hata zaidi Yupo duniani ambapo mwanadamu huishi. Na hivyo kufika kwa siku za mwisho kumechukua hatua ya kazi ya Mungu katika sehemu mpya. Mungu ana ukuu juu ya mambo yote katika ulimwengu, na Yeye ni uti wa mgongo wa mwanadamu katika moyo wake, na zaidi ya hayo, Yeye yuko miongoni mwa wanadamu. Ni kwa njia hii pekee Anaweza kuleta njia ya maisha kwa binadamu, na kumleta mwanadamu katika njia ya maisha. Mungu amekuja duniani, na Anaishi kati ya wanadamu, ili wanadamu wanaweza kupata njia ya maisha, na hivyo binadamu anaweza kuwepo. Wakati huo huo, Mungu pia huamuru mambo yote katika ulimwengu, ili wapate kushirikiana na usimamizi Wake miongoni mwa wanadamu. Na hivyo, kama wewe unakiri tu kwamba Mungu yuko mbinguni na katika moyo wa mwanadamu, lakini usikiri ukweli wa kuwepo kwa Mungu miongoni mwa watu, basi kamwe hutapata uzima, na kamwe hutapata njia ya kweli.

Mungu Mwenyewe ni maisha, na kweli, na uzima Wake na ukweli hutawala. Wale ambao hawana uwezo wa kupata ukweli kamwe hawatapata uzima. Bila mwongozo, msaada, na utoaji wa kweli, nanyi tu mtapata barua, mafundisho, na zaidi sana, kifo. Maisha ya Mungu ni ya milele, na ukweli wake na maisha hupatana. Kama huwezi kupata chanzo cha ukweli, basi huwezi kupata lishe ya maisha; kama huwezi kupata starehe ya maisha, basi utakuwa hakika huna ukweli, na hivyo mbali na mawazo na dhana, ukamilifu wa mwili wako hautakuwa chochote ila mwili, mwili wako unaonuka. Ujue kwamba maneno ya vitabu hayahesabiki kama maisha, kumbukumbu za historia haziwezi kupokelewa kama ukweli, na mafundisho ya siku za nyuma hayawezi kutumika kama sababu ya maneno ya sasa anayosema Mungu. Kinachoonyeshwa tu na Mungu anapokuja duniani na kuishi miongoni mwa binadamu ni ukweli, maisha, mapenzi ya Mungu, na njia Yake ya sasa ya kufanya kazi. Kama wewe utatumia rekodi ya maneno yaliyosemwa na Mungu wakati wa enzi zilizopita leo, basi wewe ni mtafutaji wa mambo ya kale, na njia bora ya kukueleza wewe ni mtaalamu wa urithi wa kihistoria. Kwa sababu wewe daima unaamini katika athari ya kazi ambayo Mungu alifanya katika nyakati zilizopita, amini tu katika kivuli cha Mungu alichowacha awali Alipokuwa Akifanya kazi miongoni mwa wanadamu, na kuamini tu kwa njia ambayo Mungu aliwapa wafuasi wake katika nyakati za zamani. Huamini katika mwelekeo wa kazi ya Mungu leo, huamini katika uso wa utukufu wa Mungu leo, na huamini katika njia ya sasa ya kweli iliyotolewa na Mungu. Na hivyo wewe ni mwotaji wa mchana ambaye hana ufahamu kamwe na hali ya mambo ya sasa. Kama sasa bado wewe unafuata maneno yasiyokuwa na uwezo wa kuleta maisha kwa binadamu, basi wewe ni kipande cha ukuni uliokauka kisicho na matumaini[a], kwa maana wewe ni mwenye kushikilia ukale mno, asiyeweza kutiishwa kwa urahisi, huwezi kusikiza wosia!

Mungu aliyepata mwili Anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye Anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kikuu kuliko hiki, Kwa kuwa Anayo hali ya Mungu, na ana tabia za Mungu, na hekima katika kazi Yake, ambayo haiwezi kupatikana kwa binadamu. Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo wa kweli sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, bali pia, mwili hasa ulioigwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kueleza tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu, na kumpa binadamu maisha. Hivi karibuni au baadaye, wale Kristo bandia wataanguka wote, ingawa wanadai kuwa Kristo, hawana chochote cha hali ya Kristo. Na hivyo Mimi nasema kwamba hali halisi ya Kristo haiwezi kuelezwa na mwanadamu, bali inajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe. Kwa njia hii, kama kweli unataka kutafuta njia ya maisha, lazima kwanza ukiri kuwa ni kwa kuja duniani ndipo Anazirejesha njia za maisha kwa binadamu, na lazima kukiri ni katika siku za mwisho Yeye anakuja duniani kuhifadhia njia ya maisha kwa mwanadamu. Haya sio ya wakati wa nyuma; yanatendeka leo.

Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hayo ni kwa sababu walio nayo ni maji machafu yaliyolala palepale kwa maelfu ya miaka, badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, wala njia inayoweza kukuongoza kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima.

Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote. Nawaambia tena kwamba kama mtampinga Kristo wa siku za mwisho, na kumkanusha, basi hakuna mtu ambaye anaweza kubeba matokeo ya hilo kwa niaba yako. Aidha, tangu siku hii na kuendelea huwezi kuwa na nafasi nyingine ya kupata kibali cha Mungu; hata kama utajaribu kujikomboa mwenyewe, kamwe tena hutautazama uso wa Mungu. Kwa kuwa unachopinga si binadamu, unachokataa si jambo dogo, bali ni Kristo. Je, unafahamu ghadhabu ya matokeo haya? Wewe hujafanya makosa madogo, bali umetenda uhalifu wa kutisha. Na hivyo Nashauri kila mtu kutoweka wazi meno yenu mbele ya ukweli, au kufanya shutuma bila ya kujali, kwa kuwa ni ukweli tu unaoweza kukuletea maisha, na hakuna kitu isipokuwa ukweli kinachoweza kukuruhusu kuzaliwa upya na kutazama uso wa Mungu.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni