Na Wang Li, Mkoa wa Zhejiang
Nilimwamini Bwana Yesu pamoja na mama yangu tangu nilipokuwa msichana mdogo; katika siku zangu za kumfuata Bwana Yesu, mara nyingi niliguswa na upendo Wake. Nilihisi kwamba Alitupenda sana hata Akasulibiwa na kumwaga kila tone la damu Yake ili kutukomboa. Wakati huo, ndugu katika kanisa letu wote walikuwa wenye upendo na wenye kusaidiana, lakini kwa bahati mbaya imani yetu katika Bwana ilikutana na mateso na kukandamizwa mikononi mwa serikali ya CCP.
CCP hufafanua Ukristo na Ukatoliki kama “xie jiao,” na huibandika mikutano inayofanywa na makanisa ya nyumba kama “mikusanyiko isiyo halali.” Polisi walikuwa wakivamia maeneo yetu ya mikutano mara kwa mara, wakituambia kwamba lazima tupate kibali kutoka kwa serikali kwanza na kupata ruhusa kabla ya kufanya mikutano, vinginevyo tungekamatwa na kutozwa faini au kupelekwa gerezani. Wakati mmoja, mama yangu na ndugu wengine watano au sita walikamatwa na kuhojiwa kwa siku nzima. Mwishowe, uchunguzi wa polisi ulithibitisha kwamba wote walikuwa tu Wakristo wa kawaida, na waliachiliwa. Kuanzia wakati huo, hata hivyo, tulilazimika kukutana kwa siri ili kuzuia mashambulizi ya serikali; licha ya haya yote, imani yetu haikuwahi kudhoofika. Mwishoni mwa 1998, jamaa yangu alinihubiria kwamba Bwana Yesu alikuwa amerudi kama Mwenyezi Mungu ambaye alikuwa amekuwa mwili katika siku za mwisho. Jamaa huyu pia alinisomea maneno mengi ya Mwenyezi Mungu, ambayo yalinifurahisha sana. Nilikuwa na hakika kuwa maneno ya Mwenyezi Mungu ni matamko ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi. Kufikiria kwamba ningeweza kuunganishwa tena na Bwana wakati wa maisha yangu kulinigusa zaidi ya uwezo wangu wa kuelezea, nikalia machozi ya furaha. Kuanzia wakati huo na kuendelea, niliyala maneno ya Mungu kwa shauku kila siku, na kutoka kwayo nilielewa ukweli na siri nyingi—roho yangu yenye kiu ilipata unyunyizaji na lishe. Nikistarehe katika raha na faraja iliyoletwa kwetu na kazi kubwa ya Roho Mtakatifu, mimi na mume wangu tulijizamisha katika furaha na raha ya kuunganishwa tena na Bwana. Mara nyingi tungejifunza kuimba nyimbo na kucheza ngoma katika sifa kwa Mungu pamoja na ndugu wengine, na mara nyingi tulikusanyika pamoja ili kushirikiana kuhusu maneno ya Mungu. Roho yangu ilihisi kuburudishwa na kupata nguvu mpya, na nilihisi kana kwamba nilikuwa tayari naona mbele ya macho yangu tukio zuri la ufalme uliojitokeza duniani na kila mtu akifurahia. Hakuna vile ambayo ningetarajia, hata hivyo, kwamba tulipokuwa tukimfuata Mungu na kutembea katika njia sahihi maishani kwa imani inayoongezeka, serikali ya CCP ingeanza kututesa kwa ukatili.
Mnamo Oktoba 28, 2002, mimi na dada wengine kadhaa tulikuwa tukifanya mkutano. Wakati wa mkutano huo, mimi na dada mwingine tulitoka kwenda kufanya shughuli ya safari fupi, lakini kabla hatujafika mbali, nilimsikia akisema nyuma yangu, “Unanikamata kwa sababu ya nini?” Kabla sijapata nafasi ya kujibu, afisa wa polisi asiye na sare rasmi alinikaribia na kunishika, akisema, “Unaandamana nami hadi kituo cha polisi!” kabla ya kunipeleka kwenye gari la polisi. Tulipelekwa katika kituo cha polisi na mara tu nilipotoka ndani ya gari, niliona kuwa wale dada wengine sita ambao walikuwa kwenye mkutano walikuwa wamekamatwa na kuletwa kituoni. Polisi walituamuru tuvue nguo na kujisalimisha kwa upekuaji wa mwili. Walinipata na peja mbili, na kwa hivyo wakanitambulisha kama kiongozi wa kanisa, na kwa hivyo, walinianisha kama mlengwa wa kipaumbele wa kuhojiwa. Polisi mmoja alinifokea, “Ulianza kumwamini Mwenyezi Mungu lini? Ni nani aliyekuhubiria? Umekutana na nani? Cheo chako ni kipi kanisani?” Kuhojiwa kwa nguvu sana na yeye kulinitia woga sana, na sikujua jinsi ya kutenda. Kila nilichoweza kufanya kilikuwa tu kumwomba Mungu kwa kimya, nikimwomba Anilinde ili nisije nikamsaliti. Baada ya kuomba, nilijituliza polepole na kuamua kunyamaza. Kuona kwamba nilikuwa siongei, polisi huyo alikasirika na akanipiga vibaya kichwani. Mara moja nilichanganyikiwa na kuhisi kizunguzungu, na masikio yangu yakaanza kuwangwa. Kisha wakamleta mmoja wa akina dada na kutuambia tutambulishane. Walipoona kwamba hatungefanya kile walichosema, hata hivyo, walikasirika na kuniamuru nivue viatu vyangu vyenye laini ya pamba na nisimame bila viatu kwenye sakafu ya saruji iliyoganda. Walinifanya pia nisimame wima mgongo wangu ukiwa dhidi ya ukuta, na wangenipiga kwa nguvu ikiwa mkao wangu ungeharibika hata kidogo. Ilikuwa katikati ya msimu wa kupukutika kwa majani wakati huo; hali ya joto ilikuwa ikishuka na kulikuwa kunanyesha kidogo. Nilikuwa nahisi baridi sana kwamba mwili wangu wote ulikuwa ukitetemeka, na meno yangu yalitatarika mfululizo. Yule polisi alitembea huku na kule, akiigonga meza, na kunitishia, “Tumekuwa tukikufuata kwa muda mrefu. Tuna njia nyingi za kukufanya uongee leo, na ikiwa hutazungumza basi tutakuacha ugande hadi ufe, au tutakunyima chakula hadi ufe njaa, au tutakupiga hadi ufe! Acha tuone utasimama kwa muda gani!” Nilihisi hofu kidogo nilipomsikia akisema hivi, na kwa hivyo nikamlilia Mungu moyoni mwangu: “Ee Mungu! Sitaki kuwa Yuda na kukusaliti. Tafadhali nilinde na Unipe ujasiri na imani ninayohitaji kupigana na Shetani, ili niweze kuwa shahidi Kwako.” Baada ya kuomba, nilifikiria juu ya maneno ya Mungu ambayo yanasema: “Tabia Yake ni ishara ya mamlaka, ishara ya kila kitu kilicho cha haki, cha kuvutia, ishara ya kila kitu kilicho chema na kizuri. Aidha, ni ishara ya Yeye ambaye hawezi[a] kushindwa au kushambuliwa na giza na nguvu yoyote ya adui, pamoja na ishara ya Yeye ambaye hawezi kukosewa(wala Hatavumilia kukosewa)[b] na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Tabia Yake ni ishara ya nguvu za kiwango cha juu zaidi” (“Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Ndiyo,” niliwaza. “Mungu ana mamlaka na nguvu, na mamlaka Yake na nguvu haviwezi kuangushwa na nguvu yoyote ya adui au giza. Haijalishi vibaraka wa CCP walivyo katili, wote wapo mikononi mwa Mungu, na mradi namtegemea Mungu na kushirikiana naye, basi hakika nitawashinda.” Nikiwa na mwongozo wazi uliotolewa na maneno ya Mungu, ghafla nilipata imani na ujasiri, na sikuhisi baridi tena. Baada ya kusimama pale kwa zaidi ya saa tatu, polisi walinirudisha kwenye gari la polisi na kunipeleka kizuizini.
Adhuhuri ya siku baada ya kufika kwangu katika nyumba ya uzuiliaji, maafisa wawili wa polisi, mwanamume na mwanamke, walikuja kunihoji. Katika lafudhi ya mji wangu mwenyewe, waliniita kwa jina langu na kujaribu kusikika kama kwamba walikuwa upande wangu. Mwanamume huyo alijitambulisha kama mkuu wa Kitengo cha Dini cha Ofisi ya Usalama wa Umma, na akasema, “Maafisa wa polisi kituoni tayari wamekusanya habari juu yako. Kile ambacho umefanya kweli si kitu kikubwa, na tumetembea safari maalum kuja hapa kukurudisha nyumbani. Ikiwa utatuambia kila kitu tunapofika huko, basi utakuwa sawa.” Sikujua ni ujanja gani ambao walikuwa nao, lakini nilipomsikia akisema hivi, mwanga wa tumaini uliingia moyoni mwangu. Niliwaza: “Wenyeji wa mahali ninakotoka ni watu wazuri, kwa hiyo labda wataniachilia hata nisipowaambia chochote.” Kinyume na matarajio yangu, hata hivyo, tulipokuwa tukirudi mji wa nyumbani kwangu, polisi walifunua asili zao kama za wanyama na kujaribu kunilazimisha niwape funguo za nyumba yangu. Nilijua kuwa wanataka kuipekua nyumba yangu, na nilifikiria juu ya vitabu vyote vya maneno ya Mungu na orodha za majina ya ndugu ambazo nilikuwa nazo humo. Na kwa hivyo, nilitoa ombi la dhati kwa Mungu: “Ee Mwenyezi Mungu! Tafadhali vilinde vitabu vya maneno ya Mungu na orodha nilizo nazo nyumbani ili zisianguke mikononi mwa Shetani….” Nilikataa kuwakabidhi funguo zangu. Polisi walinipeleka kwenye jengo langu na wakanifungia ndani ya gari huku wakiingi kwa fujo kwenye nyumba yangu ya orofa. Nikiwa nimeketi ndani ya gari, nilimwomba Mungu bila kukoma, na kila sekunde iliyopita ilikuwa mateso. Baada ya muda mrefu, polisi walirudi na kusema kwa hasira, “Wewe ni mjinga kweli, unajua hivyo? Hakuna kitabu hata kioja nyumbani mwako, na bado unajaribu sana kuwasaidia watu hao wa kanisa.” Nilipowasikia wakisema hivi, moyo wangu wenye wasiwasi ulianza kupumzika, na nikamshukuru Mungu kwa ulinzi Wake kutoka moyoni mwangu. Ilikuwa ni baadaye tu ndipo nilipata habari kuwa polisi hawakupata vitabu vyovyote nyumbani kwangu, na walichukua tu Yuani 4,000 pesa taslimu, simu ya rununu, na picha zote za mimi na familia yangu. Kwa bahati nzuri, dada yangu mdogo alikuwepo wakati polisi walifika na mara walipoondoka, alikimbia kulikabidhi kanisa vitabu vyote vya maneno ya Mungu na vifaa vya imani vilivyobaki. Siku iliyofuata, polisi walirudi kutafuta mahali hapo tena, lakini wakaondoka tena mikono mitupu.
Jioni ilipofika, polisi walinipeleka kwenye kituo cha polisi kilicho karibu na kwangu na wakaniuliza maswali yale yale ambayo nilikuwa nimeulizwa hapo awali. Kuona kwamba bado nilikuwa siongei, walimwita mchungaji kutoka katika Kanisa la Kanuni Tatu za Binafsi kujaribu kunishawishi. “Ikiwa wewe sio Mkristo katika Kanisa la Kanuni Tatu za Binafsi, basi unafuata njia ya uwongo,” alisema. Nilimpuuza, na nikaomba kimya kwa Mungu aulinde moyo wangu. Kadiri alivyozungumza, ndivyo madai yake yalivyozidi kuwa ya kukasirisha, hadi akaanza kumkashifu na kumkufuru Mungu kwa ukorofi. Nikiwa nimejawa na hasira, nilimjibu vikali, “Mchungaji, unamshutumu Mwenyezi Mungu kiholela, lakini si kitabu cha Ufunuo kinasema wazi ‘ambaye yuko, na ambaye alikuweko, na ambaye atakuja, Mwenyezi’ (Ufunuo 1:8)? Je! Huogopi kumkosea Roho Mtakatifu kwa kumhukumu Mungu bila kujali namna hiyo? Bwana Yesu aliwahi kusema, ‘yeyote ambaye atasema neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa: ila yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja’ (Mathayo 12:32). Huogopi?” Mchungaji aliachwa bila kuongea na aliweza tu kuondoka baada ya kukemewa vile. Moyoni mwangu, nilimshukuru Mungu kwa kunielekeza katika ushindi juu ya kizuizi hiki. Walipoona kwamba ujanja wao haukufaulu, polisi waliniambia niandike kitu kwenye karatasi. Sikuweza kujua kwa nini waliniambia nifanye hivi, na kwa hivyo nilimwomba Mungu kimya kimya; kisha niligundua kuwa hii ilikuwa ni mojawapo ya ujanja wa hila za Shetani na nikataa kuandika chochote, nikisema kwamba sikujua kuandika. Baadaye niligundua kutoka kwa mazungumzo kati ya maafisa hao wa polisi kuwa waliniuliza niandike kitu ili waweze kukagua mwandiko wangu na kwa hivyo kuthibitisha kwamba daftari walizopata katika eneo letu la mkutano zilikuwa zimeandikwa na mimi, na kisha kutumia hili kuleta mashtaka dhidi yangu. Hili lilinionyesha kuwa maafisa hao hawakuwa kitu zaidi ya mbwa na vikaragosi wa kukimbia waliofunzwa na CCP, ambao walikuwa na uwezo wa kufanya lolote na kujihusisha na njia zozote mbovu ambazo wangefikira ili kuwatesa waumini—kweli walikuwa wa kudhuru kwa siri, wajanja, waovu na wenye chuki! Mara nilipoona wazi sura mbaya za mbwa wa kukimbia wa CCP ambao huwatesa wale wanaomwamini Mungu, nilifanya uamuzi kimya kimya: Sitawahi kumtii au kumsujudia Shetani!
Waliniuliza bila kukoma kwa masaa hadi karibu saa sita usiku, lakini mkuu wa Kitengo cha Dini hakuweza kupata chochote kutoka kwangu. Ghafla, alionekana kugeuka kuwa mnyama mwenye njaa na kunifokea kwa hasira, “Al-la! Napaswa kuondoka saa 5 usiku. Umekuwa mwiba kwangu hivi kwamba imenibidi nisalie hapa, na ikiwa sitokufanya uumie kwa sababu hiyo basi hutaelewa hali ilivyo kikamilifu!” Alipokuwa akisema haya, alivuta mkono wangu wa kulia na kuuweka juu ya meza na kuufinya chini juu ya meza kwa nguvu. Kisha akachukua fimbo nene kama sentimita tano au sita na akaugonga mkono wangu kwa nguvu. Baada ya kunigonga mara ya kwanza, mishipa mikubwa kwenye mkono wangu ilianza kuvimba, kisha misuli yote iliyozunguka ilianza kuvimba pia. Nililia kwa uchungu na kujaribu kuuvuta mkono wangu nyuma, lakini akaushikilia kwa uthabiti. Huku akinigonga alinipigia kelele, “Hii ni kwa sababu ya kukataa kuandika! Hii ni kwa sababu ya kukataa kuongea! Nitakugonga kwa nguvu sana hata hutawahi kuandika neno lingine kamwe!” Aliendelea kuugonga mkono wangu hivyo kwa dakika tano au sita kabla ya kukoma hatimaye. Kufikia wakati huo, mkono wangu ulikuwa umevimba kama balungi, na aliponiachilia, mara moja niliuvuta mkono wangu na kuuweka mgongoni. Lakini yule polisi mwovu alienda nyuma yangu, akashika mikono yangu na kuanza kuipiga yote kwa nguvu ikining’inia hewani huku akisema, “Wewe hutumia mikono hii kumfanyia Mungu wako vitu, sivyo? Nitaivunja, nitailemaza, kisha tutaona jinsi utakavyofanya chochote! Halafu tutaona ikiwa wale waumini katika Mwenyezi Mungu watakutaka tena!” Kumsikia akisema hivi kulinaniacha nimejawa na chuki kwa genge hili la polisi waovu. Wanatendaa kwa ukaidi sana na kutenda kinyume na Mbingu; wanawaruhusu watu kuwa watumwa wa CCP tu na kujitumikia hadi wanyauke kwa ajili ya CCP, lakini hawawaruhusu watu wamwamini Mungu au kumwabudu Muumba. Katika jitihada ya kunilazimisha nimsaliti Mungu, polisi huyo hakuwa na shaka yoyote wakati huo juu ya kunitesa kwa mateso ya kikatili—kwa kweli wao ni kundi la wanyama na pepo katika umbo la binadamu, na ni waovu na wanaopinga maendeleo sana. Yule polisi alinipiga mara tatu namna hiyo; mikono yangu ilikuwa imepigwa na kujeruhiwa vibaya, na vifundo vya mikono yangu na nyuma ya mikono yangu ilikuwa imevimba sana ilionekana karibu kulipuka—maumivu yalikuwa makali sana. Nilipokuwa tu nikipitia maumivu makali, mistari michache kutoka katika wimbo wa maneno ya Mungu ilinijia: “Hivyo lazima utoe ushuhuda wako kila wakati katika siku za mwisho. Haijalishi unavyoteseka, mradi tu bado unapumua, ubaki mwaminifu kwa Mungu, uusujudie mkono Wake. Huu ni upendo wa kweli kwa Mungu, ushuhuda wa kweli” (“Tafuta Kumpenda Mungu Bila Kujali Mateso Yako Ni Makubwa Vipi” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Maneno ya Mungu yaliuchochea moyo wangu, na nikawaza: “Hiyo ni kweli. Mungu hufanya kazi bila kuchoka usiku na mchana kutuokoa. Yeye hutulinda na hukaa nasi kila wakati, na Hutuonyesha upendo na huruma isiyo na mipaka. Sasa, Shetani anapojaribu kunilazimisha nimsaliti Mungu na kuwasaliti ndugu zangu, Mungu anatumai kwa ari kuwa nitatoa ushuhuda imara na mkubwa kwa ajili Yake. Ningewezaje kumsikitisha au kumdhuru?” Huku nikifikiria hili, nilishikilia machozi yangu na nikajiambia niwe hodari, nisiwe mwoga au mwenye kutishwa. Serikali ya CCP haikuwa ikinitesa na kuniumiza kikatili kwa sababu ilinichukia binafsi, lakini kwa sababu ya asili yake ya kumpinga Mungu, ya kumchukia Mungu. Kusudi lake la kunitendea kwa njia hiyo lilikuwa kunifanya nimsaliti na kumkataa Mungu, na kunifanya nikubali udhibiti wake na utumwa wangu milele. Nilijua, hata hivyo, kwamba singeweza kamwe kuitii, lakini kwamba nilipaswa kusimama kidete upande wa Mungu na kumwaibisha Shetani. Niliimba wimbo huo tena na tena mawazoni mwangu na nilihisi roho yangu ikizidi kuwa yenye nguvu polepole. Yule polisi mwovu aliishia kunifanya nikeshe usiku kucha baada ya kunipiga. Angeniona hata naanza kufunga macho yangu, angenifokea au kunipiga teke. Lakini nikiwa nimeguswa na upendo wa Mungu kama nilivyokuwa, sikujisalimisha kwake.
Siku iliyofuata, mkuu wa Kitengo cha Dini alikuja kunihoji tena. Kuona kwamba nilikuwa bado siongei, alichukua fimbo na kuipiga kwa nguvu kwenye mapaja yangu. Baada ya vichapo kadhaa, miguu yangu ilianza kuvimba hadi nikawa naweza kuhisi suruali yangu ikianza kujikaza ikiishika miguu yangu iliyovimba. Polisi mwingine mwovu akasimama upande mmoja akinidhihaki, akisema, “Ikiwa Mungu unayemwamini ni mkubwa sana, kwa nini Asije kukusaidia sasa tunapokutesa?” Pia alisema mambo mengine kadhaa ya kumkashifu na kumkufuru Mungu. Nilikuwa naumia na mwenye hasira, na moyoni mwangu nilijibu kukufuru kwake kwa kuwaza: “Wewe askari wa pepo, Mungu atakupa adhabu kulingana na matendo yako maovu! Sasa ndio wakati ambao Mungu anakufunua na kukusanya ukweli wa matendo yako maovu!” Kisha nikayafikiria maneno haya kutoka kwa Mungu: “Maelfu ya miaka ya chuki ikiwa imejaa kifuani, milenia ya dhambi imeandikwa katika moyo—inawezekanaje hii isichochee chuki? Kumlipiza Mungu, kuuondoa kabisa uadui wake, usimwache kutangatanga tena, na usimruhusu kufanya fujo zaidi kama anavyotaka! Sasa ndio wakati: Mwanadamu ana muda mrefu tangu akusanye nguvu zake zote, amejitolea nguvu zake zote, amelipa kila gharama, kwa hili, kuchana uso uliojificha wa pepo hili na kuwafanya watu, ambao wamepofushwa na kuvumilia kila aina ya mateso na taabu, kuinuka kutoka katika maumivu na kurudi kwa ibilisi huyu wa zamani” (“Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kutoka katika maneno ya Mungu, niliona mapenzi Yake muhimu na wito Wake motomoto, na nilielewa kuwa CCP haina budi kuangamizwa na Mungu. Ingawa nilikuwa nikipitia mateso ya kikatili ya CCP wakati huo, hekima ya Mungu inatekelezwa kwa kutegemezwa kwa ujanja wa hila wa Shetani, na Mungu alikuwa akitumia kile kilichokuwa kinanipata ili niweze kuona wazi kiini cha mapepo ya CCP, na ili niweze kutambua mema kutoka kwa mabaya. Hivyo, upendo wa kweli na chuki ya kweli vingeweza kuibuka ndani yangu; kisha ningeweza kuiacha na kuikataa CCP mara moja na kuugeuza moyo wangu kwa Mungu, ili nipate kumshuhudia Mungu na kumwaibisha Shetani. Mara nilipoelewa mapenzi ya Mungu, hisia kubwa za nguvu ziliongezeka ndani yangu, na niliazimia kuapa kwa mwaaminifu kwa Mungu na kumwacha Shetani. Ingawa nilikuwa nikipigwa kila wakati kwa mateso ya kikatili, na ingawa mwili wangu wote ulikuwa umetolewa nguvu na miguu yangu ilikuwa katika maumivu yasiyoweza kustahimilika, kwa kutegemea nguvu ambayo Mungu alinipa, bado niliweza kutosema chochote (niligundua baadaye kwamba miguu yangu ilikuwa imepigwa ikapata majeraha mabaya, na hata sasa moja ya misuli katika mguu wangu wa kulia bado imefifia. Mwishowe, mkuu wa Kitengo cha Dini hakuweza kufanya chochote isipokuwa kuondoka kwa kishindo kwa kuudhika.
Siku ya tatu, polisi waovu walinihoji na kunipiga tena, wakiacha tu baada ya kunikaripia vya kutosha na kuchoka kutokana na kunipiga. Baada ya hapo, afisa wa polisi wa kike alinijia na, akijifanya kujali, akasema, “Tulikuwa na mtu aliyemwamini Mwenyezi Mungu aliyeletwa hapa awali. Hakutuambia chochote na alihukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani. Je, kukaa kimya kunakusaidiaje? Unaweza kupoteza miaka 10 mahali hapa, halafu ukitoka Mungu wako hatakutaka tena hata hivyo, na itakuwa umechelewa sana kuwa na majuto….” Alisema mambo kadhaa kujaribu kunihadaa nizungumze, lakini niliendelea kuomba kimya kimya, nikimwomba Mungu aulinde moyo wangu ili nisije nikaanguka katika mtego wa ujanja wa hila za Shetani. Baada ya kuomba, sehemu ya wimbo iliingia akilini mwangu: “Mimi mwenyewe niko radhi kumfuatilia Mungu na kumfuata Yeye. Sasa Mungu anataka kuniacha lakini bado nataka kumfuata Yeye. Iwapo Ananitaka au la, bado nitampenda Yeye, na mwishowe lazima nimpate Yeye. Ninatoa moyo wangu kwa Mungu, na haijalishi kile Yeye hufanya, nitamfuata Yeye kwa maisha yangu yote. Lolote litokealo, lazima nimpende Mungu na lazima nimpate Yeye; sitapumzika mpaka nimpate Yeye” (“Nimeamua Kumpenda Mungu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). “Ndiyo,” niliwaza. “Sasa namwamini Mungu na namfuata Mungu kwa sababu ndicho ninachotaka kufanya. Haijalishi ikiwa Mungu ananitaka au la—nitamfuata Mungu mpaka mwisho kabisa!” Maneno ya Mungu yalileta ufahamu akilini mwangu na nikagundua kuwa Shetani alikuwa akifanya yote awezayo kupanda chuki kati yangu na Mungu ili nife moyo, nimkane Mungu, na mwishowe nikamsaliti Mungu kama Yuda. Wakati huo huo, njia pekee ambayo ningemshinda Shetani na kuwa na ushuhuda kwa ushindi wa Mungu juu ya Shetani ilikuwa kuweka imani Kwake na kuendelea kuwa mwaminifu Kwake. “Kama napelekwa gerezani au la, na matokeo yangu yawe yapi yote yako mikononi mwa Mungu,” Nilijiwazia. “Vyovyote ambavyo Mungu anaamua kupanga na kupangilia maisha yangu, sina usemi katika jambo hilo, na naamini kwa undani kwamba kila kitu anachofanya Mungu kinafanywa ili kuniokoa. Ijapokuwa naweza kulazimika kuwa bila starehe za mwili gerezani, kile ningepata kingekuwa kuridhika kwa kiroho. Aidha, kwenda gerezani kwa niaba ya Mungu kungekuwa heshima yangu, ilhali ningemsaliti Mungu kwa sababu ya tamaa zangu za starehe za mwili, basi ningepoteza heshima na uadilifu wote, na dhamiri yangu haingekuwa na amani tena.” Kwa hivyo niliazimia kimya kimya: Hata nikipelekwa gerezani, nitabaki mwaminifu kwa Mungu hadi mwisho; najitolea upendo wangu wa kweli kwa Mungu ili Shetani aaibike na kushindwa mara moja! Polisi waovu walijaribu mbinu za polisi mzuri na polisi mbaya kwangu, na walinipitishia katika mateso ya kikatili kwa muda wa siku tatu na usiku tatu, lakini hawakupata mwelekeo wowote kutoka kwangu. Wakikosa chaguzi, walichoweza kufanya kilikuwa kunichukua, nikiwa nimepigwa na kujeruhiwa nilivyokuwa, na kunifunga kizuizini. Walipokuwa wakinifungia, mmoja wa polisi alisema kwa chuki, “Tutakuacha uvute pumzi kidogo kisha tutakuhoji tena!”
Siku tano baadaye, polisi hao waovu walikuja kunihoji mara nyingine tena, ila wakati huu walichukua zamu kunichosha. Waliniamuru niketi kwenye kiti cha chuma kilichokuwa baridi kama barafu na kisha wakaufunga pingu mkono wangu wa kulia kwenye kitu hicho. Waliweka mhimili wa chuma mbele ya kifua changu kunizuia kusonga, miguu yangu ikining'inia juu ya sakafu. Walifanya hivyo ili nisiweze kusonga hata msuli mmoja, na kabla ya muda, mikono na miguu yangu yote ilikuwa imekufa ganzi. Polisi waovu waliniambia, “Kila mtu aliyefungwa kwenye kiti hiki huishia kutuambia kila kitu anachojua. Usipozungumza kwa siku moja, basi utafungwa hapa kwa siku mbili. Usipoanza kuzungumza baada siku mbili, basi itakuwa siku tatu. Sitaki mengi kutoka kwako. Nataka tu uniambie viongozi katika kanisa lako ni akina nani.” Shukrani kwa Mungu kwa kunipa nguvu, kwa kuwa wakati wote huo nilishikilia wazo moja tu: Sitawahi kumsaliti mtu yeyote! Walinihoji kwa kurudia, hawakunipa chochote cha kula wala kitu chochote cha kunywa, na hawangeniruhusu niende chooni. Jioni hiyo, ili kunizuia kulala, walifunga pingu mkono mmoja kwenye kiti hicho, lakini walinifanya nisimame karibu nacho wakiendelea kunihoji. Nilikuwa nimechoka sana na nilikuwa na njaa, na mwili wangu wote ulikuwa umekufa ganzi. Singeweza kusimama peke yangu na ningeweza kusalia nimesimama wakati wote kwa kuegemea kiti. Lakini punde nilipokiegemea kiti hicho au hata kufikiria kulala, polisi angepunga kijiti kirefu cha mwanzi usoni mwangu na kunichapa nacho, na hawakuniacha nifunge macho yangu hata mara moja usiku kucha. Hili liliendelea kwa siku mbili na nikawa dhaifu sana hadi mwili wangu wote ukawa dhaifu na mnyonge. Sikujua hata wangeendelea kunipitisha katika haya kwa muda gani; niliogopa kwamba singeweza kustahimili, kwamba ningemsaliti Mungu na kuwa Yuda, na kwa hivyo nikamlilia Mungu tena na tena: “Ee Mungu! Mwili wangu ni dhaifu sana na kimo changu ni kidogo. Tafadhali nikinnge nisiwe Yuda.” Nilipokuwa tu nikimwita Mungu kwa haraka, mmoja wa polisi waovu alitoa kitabu cha maneno ya Mungu na kusoma: “Sitawahurumia tena wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Sipendi kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali huyo mtu ni nani, hii ndiyo tabia Yangu. Ni lazima Niwaambie hili: Yeyote atakayeuhuzunisha moyo Wangu hatapokea huruma kutoka Kwangu mara ya pili, na yeyote ambaye amekuwa mwaminifu Kwangu atadumu moyoni Mwangu milele” (“Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako” katika Neno Laonekana katika Mwili). Nuru iliujaza moyo wangu—Mungu hakuwa ananionyesha njia? Niliona kwamba Mungu kweli amejawa na tumaini na kunijali na, kunifanya niendelee kuwa imara, Alikuwa amemtumia polisi huyu mwovu hapa kwenye kiota hiki cha mapepo kunisomea maneno ya Mungu. Kupitia hili, Mungu alikuwa akiniambia wazi kuwa anawapenda na anawabariki wale wanaosalia waaminifu Kwake kupitia katika dhiki, na kwamba Anawachukia na kuwakataa wale wanyonge sana kuweza kumsaliti. Ningewezaje kushindwa kutimiza matarajio ya Mungu mbele ya upendo na huruma Yake? Yule polisi mwovu alipokuwa amemaliza kusoma, aliniuliza, “Je, hili ndilo Mungu wako anakufanya ufanye? Yaani, kukaa kimya?” Sikujibu na, kwa kushangaza, polisi alifikiria kuwa sikumsikia, na kwa hivyo alisoma kifungu hicho tena mara nyingi, akaniuliza swali lile lile kwa kurudia. Niliona jinsi Mungu alivyo mwenye hekima na mwenye uweza: Kadiri yule polisi mwovu alivyosoma maneno ya Mungu zaidi, ndivyo kila neno lilivyoandikwa ndani ya moyo wangu, na vivyo hivyo, ndivyo imani yangu ilivyoongezeka. Niliamua kwamba haijalishi jinsi wale pepo wangejaribu kunifanya nikiri, kamwe sitakuwa Yuda!
Siku ya tatu, polisi waovu walinifanya nitembee juu na chini ngazi, nikitoka kwenye chumba kimoja cha mahojiano kwenda kingine, ili kumaliza nguvu yangu yote iliyobaki. Mateso haya yaliendelea hadi mwili wangu ulikuwa umemalizika kabisa na miguu yangu ilikuwa ikitetemeka, ikawa vigumu sana kuinyanyua ili kupanda ngazi. Kwa sababu ya imani na nguvu ambayp maneno ya Mungu yalikuwa yamenipa, hata hivyo, nilikataa kufungua mdomo wangu. Walinihoji hadi machweo lakini bado hawakuwa na chochote, na kwa hivyo walinitishia, wakisema, “Hata usiposema neno, bado tunaweza kukutia hatiani. Tutakusingizia!” Kuwasikia wakisema jambo hilo kuliibua hofu kiasi ndani mwangu na niliwaza moyoni: “Je, wanaweza kunitesa kwa namna gani nuyingine? Nimeisha kabisa na siwezi kuendelea muda mrefu zaidi….” Kisha nikamlilia Mungu, nikisema: “Ee Mungu! Naomba Unisaidie. Nahofu sana kuwa siwezi kustahimili tena. Tafadhali nilinde na Uniongoze ili nijue jinsi ya kushirikiana na Wewe.” Nilihisi nguvu ikiongezeka ndani yangu baada ya ombi hili, na sikuhisi maumivu yakiwa mengi sana. Na kwa hivyo, katika wakati wangu mchungu na mgumu zaidi, kupitia maombi bila kukoma, Mungu alinipa imani na nguvu ya kuendelea.
Asubuhi na mapema siku ya nne, walipoona kwamba siku tatu za kunihoji hazikutoa matokeo, polisi waovu walinifungua pingu zangu kwa hasira na kunisukuma chini. Kisha waliniamuru nipige magoti na nisinyanyuke. Kwa kutumia fursa kwamba nilikuwa tayari nimepiga magoti, nilianza sala ya kimya kwa Mungu: “Ee Mungu! Najua kuwa ulinzi Wako umeniruhusu nishinde siku hizi chache za mateso, kuhojiwa na majaribio ya kunifanya nikiri na sina maneno ya kukushukuru kwa ajili ya upendo na rehema Zako. Ee Mungu! Ingawa sijui jinsi polisi waovu watakavyonitesa kwa kufuatia, haijalishi kitakachotokea sitakusaliti kamwe, wala sitawasaliti ndugu zangu kamwe. Naomba Uendelee kunipa imani na nguvu na unifanye nisimame imara.” Mara ombi langu lilipomalizika, nilihisi wimbi la nguvu kubwa ikiinuka ndani yangu, na nikajua sana kuwa nilikuwa nikishikiliwa katika upendo wa Mungu. Haijalishi jinsi mapepo hao wanavyoweza kunitesa, nilijua kuwa Mungu angenielekeza kuyashinda yote. Baada ya muda, polisi waovu labda walikisia kwamba nilikuwa nikimwomba Mungu, na wakibwata kwa hasira, walinipigia kelele na kunifokea laana. Mmoja wao alichukua gazeti, akalizungusha kuwa aina ya kirungu na kunipiga kikatili kichwani. Kila kitu kilikuwa giza na nikaanguka chini na kupoteza fahamu. Walinitupia maji baridi ili waniamshe na, katika ukungu ulioziba akili yangu, nilimsikia mmoja wa polisi waovu akinitishia. “Usipotuambia kila kitu unachojua, nitakupiga hadi ufe au hadi ulemae! Hakuna atakayejua kamwe nikikupiga hadi ufe, na hakuna ndugu yako au dada yako ambaye anaweza kuthubutu kuja hapa.” Nilimsikia pia mmoja wao akisema, “Achana na hili jambo. Ukiendelea kumpiga namna hiyo basi hakika atakufa. Yeye ni kazi bure. Hatutapata chochote kutoka kwake.” Sikuweza kujizuia ila kutanafusi kwa kupata nafuu niliposikia hivyo, kwa maana nilijua kuwa ilikuwa ni Mungu anayeonyesha kuelewa kuhusu udhaifu wangu, na kwamba kwa mara nyingine alinifungulia njia. Polisi waovu bado hawakuwa tayari kukubali kushindwa, hata hivyo, na kwa hivyo walimleta dada yangu mdogo na mwanangu, wote ambao hawakuwa waumini wa Mungu, wajaribu kunifanya niongee niongee. Dada yangu alipoona macho yangu meusi na mikono yangu iliyovimba na kujeruhiwa, sio tu kwamba hakujaribu kunifanya niongee kama polisi walivyotaka, lakini badala yake alilia na kusema, “Li, ninaamini kuwa huwezi kufanya kitu chochote kibaya. Kaa imara.” Alipomwona dada yangu akinitia moyo, yule polisi akamgeukia mwanangu na kumwambia, “Afadhali uzungumze na mama yako na umfanye ashirikiane na sisi, na kisha anaweza kwenda nyumbani na akutunze.” Mwanangu alinitazama na hakumjibu afisa huyo. Alipokuwa karibu kuondoka, alinisogelea kisha akasema ghafla, “Mama, usijali kunihusu mimi. Wewe jichunge, na mimi nitajichunga.” Kuona jinsi mwanangu alivyokomaa na mwenye busara, niliguswa kiasi kisichoelezeka, lakini nikatikisa kichwa changu kwa nguvu na kulia walipomwelekeza yeye na dada yangu kutoka chumbani. Tukio hili liliniruhusu kupata upendo na kujali kwa Mungu tena. Mungu alikuwa anaonyesha kuelewa kuhusu udhaifu wangu kwani, katika siku hizo chache zilizopita, yule ambaye nilikuwa na wasiwasi zaidi kumhusu alikuwa mwanangu. Nilihofu kuwa, bila mimi hapo, hangeweza peke yake. Kilichokuwa kimehofisha zaidi ni kwamba, kwa kuwa ni mdogo sana, alipokuja katika kituo cha polisi kuniona, angetiwa kasumba mpaka anichukie kwa kumwamini Mungu. Kwa mshangao wangu, hata hivyo, sio tu kwamba hakudanganywa na mazungumzo ya kejeli na yenye sumu ya polisi waovu, lakini kinyume chake alinifariji badala yake. Kisha nikaona kweli jinsi Mungu alivyo wa ajabu na mwenye uweza kweli! Moyo na roho ya mwanadamu kweli vimepangwa na Mungu. Baada ya mwanangu na dadangu kuondoka, polisi waovu walinitishia tena kwa kuniambia, “Bado usipoongea, amini usiamini, tutakutesa kwa siku kadhaa zaidi usiku na mchana. Na hata ikiwa bado hutazungumza, bado tunaweza kukufanya uhukumiwe kifungo cha miaka mitatu hadi mitano gerezani….” Nikiwa nimepitia matendo mengi ya Mungu, nilijawa na imani kwa Mungu na kwa hivyo nikasema kwa uamuzi na ujasiri, “Kibaya zaidi kinachoweza kutokea ni kwamba nakufa mikononi mwenu! Mnaweza kuumiza mwili wangu, lakini kamwe hamwezi kuuyumbisha moyo wangu. Hata mwili wangu ukifa, Mungu bado atakuwa na roho yangu.” Kuona kwamba nimekaa kidete, hakuna kitu ambacho polisi waovu wangeweza kufanya isipokuwa kutamatisha kuhoji kwao na kunirudisha katika seli yangu. Kushuhudia umbo la kusikitisha la Shetani akishindwa kabisa kuliniletea furaha isiyo na kifani, na nilielewa kweli kuwa Mungu ndiye Mkuu wa vitu vyote na kwamba maisha yetu na vifo viko mikononi Mwake. Ingawa sikuruhusiwa kupata chakula chochote au maji kwa siku nyingi na mwili wangu ulikuwa umedhoofika, upendo wa Mungu ulikuwa na mimi siku zote. Maneno Yake yalikuwa chanzo cha imani na nguvu kisichokoma, yakiniwezesha kushinda kwa ushupavu majaribio ya Shetani ya kunifanya nikiri kwa polisi kuchukua zamu kunichosha. Hili liliniruhusu kufahamu kweli jinsi nguvu ya maisha ya Mungu ilivyo kuu na ya kuzidi uwezo mwanadamu—nguvu ambayo Mungu hutupa haiishi na haiwekewi mipaka na mwili.
Siku kadhaa baadaye, serikali ya CCP ilibuni shtaka la kuvuruga utaratibu wa umma, na baada ya kunihukumu miaka mitatu ya masomo upya kupitia kazi, polisi walinipeleka hadi katika kambi ya kazi. Niliishi maisha mabaya huko, nikifanya kazi bila kukoma tangu alfajiri hadi machweo. Kwa sababu mikono yangu ilikuwa imelemazwa na kupigwa huko, misuli nyuma ya mikono yangu ilikuwa imekazika sana kwa miezi sita ya kwanza ya kifungo changu hata sikuwa na nguvu ya kuosha nguo zangu. Kila kulipokuwa kukinyesha, mikono yangu ingeuma na kuvimba kwa sababu mishipa ya damu haingeweza kuzungusha damu yangu vizuri. Licha ya haya, walinzi wa gereza wangenilazimisha nizidi kiwango changu cha siku kila siku, vinginevyo kifungo changu kingeongezeka. Zaidi ya hayo, waliwachunga kwa ukali zaidi wale kati yetu ambao tuliwamini Mungu; kila mara kulikuwa na mtu anayetutazama tukila milo yetu, tulipoosha, na hata tulipoenda chooni…. Maumivu mwilini mwangu, kuzidishiwa kazi, pamoja na mateso ya kisaikolojia yote yalinisababisha niteseke kwa kiasi kisichotajika. Nilihisi kama miaka mitatu mahali hapo ingekuwa mingi sana kwangu na kwamba singeweza kuendelea. Mara nyingi nilifikiria juu ya kujitia kitanzi kama njia ya kumaliza mateso yangu. Katika uchungu mwingi, nilimwomba Mungu: “Ee Mungu, Unajua jinsi mwili wangu ulivyo dhaifu. Nateseka sana hivi sasa na kwa kweli siwezi kustahimili zaidi. Hata nataka kufa. Tafadhali nipe nuru na uniongoze, unipe nguvu ya utashi, na Unipe imani ninayohitaji kuendelea….” Mungu alinionyeshea fadhila wakati huo, kwa kuwa Alinifanya nifikirie wimbo wa maneno ya Mungu: “Mungu amefanyika kuwa mwili wakati huu kufanya kazi hii, kukamilisha kazi ambayo bado Hajaikamilisha, kuifunga enzi hii, kuihukumu enzi hii, kuwaokoa waliozama kabisa dhambini kutoka katika ulimwengu wa bahari ya mateso na kuwabadilisha kabisa. Mungu amevumilia sana kulala bila kupata usingizi kwa ajili ya kazi ya binadamu. Kutoka vina vya juu hadi vya chini, Amepanda kwenda katika kuzimu ambapo mwanadamu anaishi kupitisha siku Zake na mwanadamu, hajawahi kulalamikia uchakavu walionao wanadamu, hajawahi kumlaumu kwa ukaidi wake, lakini Anavumilia mateso makuu kadri Anavyofanya kazi Yake. … Lakini kwa ajili ya binadamu wote, ili binadamu wote waweze kupata pumziko mapema zaidi, Amestahimili fedheha na kupitia udhalimu kuja duniani, na Aliingia mwenyewe ‘jahanamu’ na ‘kuzimu,’ katika tundu la duma, kumwokoa mwanadamu” (“Kila Hatua ya Kazi ya Mungu ni Kwa Ajili ya Uzima wa Mwanadamu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Nilipokuwa nikitafakari maneno haya, moyo wangu ulitiwa msukumo na kubadilishwa na upendo wa Mungu. Nilifikiria juu ya jinsi, ili kuwaokoa wanadamu, ambao ni wapotovu sana, Mungu alikua mwili na kushuka kutoka urefu wa juu hadi chini kabisa, Akajiweka katika hatari kubwa ya kuja nchini China—tundu hili la ibilisi—kutekeleza kazi Yake. Amepitia aibu na uchungu, mateso na shida nyingi, na bado Mungu huwa Akijitumia Mwenyewe kimya kimya, bila malalamiko na bila majuto, kwa ajili ya wanadamu. Mungu hutekeleza kazi hii yote ili Apate tu kundi la watu ambao wanaweza kudhukuru mapenzi Yake, ambao ni wenye haki, na ambao hawajisalimishi kamwe. Nilikuwa nimejikuta katika hali hiyo kwa sababu Mungu alitaka kuitumia kuyachovya mapenzi yangu, na kuikamilisha imani yangu na utiifu wangu kwa Mungu; Alikuwa ameruhusu hali hii inipate ili kunifanya nielewe na kuingia katika ukweli. Kiasi kidogo cha mateso ambayo nilikuwa nikipitia hayakufaa hata kutajwa karibu na maumivu na aibu ambayo Mungu amepitia. Ikiwa singeweza hata kustahimili kiasi kidogo cha mateso kama hicho gerezani, singekuwa nikijithibitisha kuwa asiyestahili juhudi za kujitolea ambazo Mungu amefanya kwa sababu yangu? Aidha, mwongozo wa Mungu ulikuwa umeniwezesha kushinda mateso yote ya ukatili ambayo polisi waovu walinipitishia nilipokamatwa mara ya kwanza. Kwa muda mrefu Mungu alikuwa ameniruhusu kuona vitendo Vyake vya ajabu Akifanya kazi, kwa hivyo sipaswi kuwa na imani thabiti na kuendelea kutoa ushahidi mzuri kwa ajili Yake? Kwa kufikiria haya, nguvu zangu zilirudi, na niliamua kumwiga Kristo: Haijalishi jinsi vitu vitakavyokuwa vigumu au vichungu, ningeendelea kuishi kwa ukakamavu. Baada ya hapo, kila wakati nilipohisi kuwa maisha yangu katika kambi ya kazi yalikuwa yananizidi mimi, ningeimba wimbo huo, na kila wakati nilipoimba, maneno ya Mungu yalinipa imani na nguvu isiyoisha, na nikatiwa moyo kuendelea. Wakati huo, kulikuwa na dada wengine kadhaa kutoka kanisa hilo pia waliokuwa wakizuiliwa katika kambi ya kazi. Kwa kutegemea hekima ambayo Mungu alitupa, kila tulipopata nafasi, tungeandika maneno ya Mungu kwa maelezo mafupi na kuyapitisha kwa kila mmoja au kushirikiana maneno machache na kila mmoja wakati muda uliporuhusu—tulisaidiana na kutiana moyo. Licha ya ukweli kwamba sote tulikuwa tukizuiliwa katika tundu la pepo wa serikali ya CCP, tukifungiwa ndani ya kuta hizo ndefu na kutengwa kabisa na ulimwengu wa nje, ni kwa sababu ya hili hasa ndiyo tulipata kuthamini kila moja la maneno ya Mungu zaidi, na kuthamini hata zaidi msukumo ambao Mungu alimpa kila mmoja wetu, na ilikuwa kwa sababu ya hili kwamba mioyo yetu iliungana kwa karibu sana ilivyofanya.
Mnamo Oktoba 29, 2005, hukumu yangu ilitekelezwa kikamilifu na niliachiliwa mwishowe. Licha ya kuruhusiwa kuwa nje ya gereza, hata hivyo, bado sikuweza kupata uhuru wangu. Polisi walikuwa wakiwatuma watu kila wakati kufuatilia mienendo yangu, na waliniamuru niripoti binafsi katika kituo cha polisi kila mwezi. Ingawa nilikuwa nyumbani kwangu binafsi, ilionekana kama kwamba nilikuwa nimezuiliwa ndani ya gereza lisiloonekana, na ilinibidi niwe macho kila wakati dhidi ya wapigaji ripoti wa CCP. Hata ingawa nilikuwa nyumbani, bado ilinilazimu niwe mwangalifu sana wakati wa kusoma maneno ya Mungu, nikiogopa kwamba polisi wangeingia ghafla wakati wowote. Aidha, kwa sababu nilikuwa nikifuatiliwa kwa karibu sana, sikuwa na njia ya kuwaona ndugu zangu au kuishi maisha ya kanisa. Hili lilikuwa jambo la kutia wazimu kwangu, na kila siku ilihisi kama mwaka. Mwishowe, singeweza kuishi maisha ya kufuatiliwa na kukandamizwa, ya kulazimika kuliacha kanisa na ndugu zangu wote, na kwa hivyo niliuhama mji wangu na kutafuta kazi mahali pengine. Mwishowe niliweza kuwasiliana na kanisa na kwa mara nyingine tena nilianza kuishi maisha ya kanisa.
Nikiwa nimepitia mateso mikononi mwa serikali ya CCP, niliona waziwazi na dhahiri kiini chake cha unafiki na kishetani ambacho kinadanganya umma ili kujipatia sifa, na nikawa na hakika kuwa sio kitu kingine ila genge la mashetani ambalo linakufuru dhidi ya Mbingu na kujiweka dhidi ya Mungu. Kwa kweli CCP ni mfano wa Shetani, kupata mwili kwa ibilisi mwenyewe; chuki yangu kwa CCP inaenea sana na ninaapa kubaki adui wake hadi kufa. Katika ugumu huu wote, pia nilikuja kuthamini uweza na ukuu wa Mungu na vitendo Vyake vya ajabu, nilipitia mamlaka na nguvu ya maneno ya Mungu, na hakika nilihisi upendo wa Mungu na wokovu Wake mkubwa: Nilipokuwa hatarini, ni Mungu ndiye Aliyekuwa kando yangu kila wakati, Akinipa nuru na kuniangazia kupitia katika maneno Yake, akinijalia imani na nguvu, Akinielekeza kushinda mateso ya ukatili moja baada ya lingine na kunipitisha katika miaka mitatu mirefu, ya giza utumwani Nikikabiliwa na wokovu mkubwa wa Mungu, najawa na shukrani, imani yangu inajazwa mara dufu, na nimeamua: Haijalishi ugumu ambao lazima nipitie ulivyo mkubwa katika siku za usoni, nitategemea mwongozo na uongozi wa maneno ya Mungu daima kutupa ushawishi wote wa giza, nami nitamfuata Mungu kwa uthabiti hadi mwisho kabisa!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni