Jumanne, 30 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III Sehemu ya Pili

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Tumezungumza tu kuhusu kazi yote ambayo Mungu amekamilisha, misururu ya mambo Aliyoyafanya kwa mara ya kwanza. Kila mojawapo ya mambo haya yanahusiana na mpango wa Mungu wa usimamizi na mapenzi ya Mungu. Yanahusiana pia na tabia binafsi ya Mungu na kiini Chake. Kama tunataka kuelewa bora zaidi kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho, hatuwezi kukoma katika Agano la Kale au katika Enzi ya Sheria, lakini tunahitaji kusonga mbele pamoja na hatua ambazo Mungu alichukua katika kazi Yake. Hivyo basi, Mungu alipotamatisha Enzi ya Sheria na kuanza Enzi ya Neema, hatua zetu binafsi zimefika katika Enzi ya Neema—enzi iliyojaa neema na ukombozi. Katika enzi hii, Mungu tena Alifanya kitu cha muhimu sana kwa mara ya kwanza.

Jumatatu, 29 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Kwanza)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Vikao hivi kadhaa vya ushirika vimekuwa na athari kubwa kwa kila mmoja wa watu. Kwa sasa, watu wanaweza hatimaye kuhisi uwepo wa kweli wa Mungu na kwamba Mungu kwa hakika yuko karibu sana na wao. Ingawa watu wamemwani Mungu kwa miaka mingi, hawajawahi kuelewa kwa kweli mawazo na fikira Zake kama wanavyozielewa sasa, wala hawajawahi kupata kwa kweli uzoefu wa matendo Yake halisi kama walio nao kwa sasa. Kama ni maarifa au matendo halisi, watu wengi wamejifunza kitu kipya na kutimiza ufahamu wa juu zaidi, na wametambua kosa lililopo katika ufuatiliaji wao wa kale, wametambua hali yao waliyopitia ya juujuu na kwamba mambo mengi sana hayaambatani na mapenzi ya Mungu, na wametambua kwamba kile ambacho binadamu amepungukiwa nacho zaidi ni maarifa ya tabia ya Mungu.

Jumapili, 28 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Sehemu ya Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Msiwe na Wasiwasi Wowote Kuhusu Majaribio ya Mungu
Baada ya kuupokea ushuhuda kutoka kwa Ayubu kufuatia mwisho wa majaribio yake, Mungu aliamua kwamba angepata kundi au zaidi ya kundi—la watu kama Ayubu, ilhali aliamua kutowahi tena kumruhusu Shetani kushambulia au kunyanyasa mtu yeyote mwingine kwa kutumia mbinu ambazo kwazo alimjaribu, kumshambulia na kumnyanyasa Ayubu, kwa kufanya mzaha na Mungu; Mungu hakumruhusu Shetani tena kufanya mambo kama hayo kwa binadamu ambaye ni mnyonge, mjinga, na asiyejua—ilikuwa tosha kwamba Shetani alikuwa amemjaribu Ayubu!

Jumamosi, 27 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II (Sehemu ya Tano)


Kuhusu Ayubu
Baada ya kusikia namna Ayubu alivyopitia majaribio, kunao uwezekano kwamba wengi wenu watataka kujua maelezo zaidi kuhusu Ayubu mwenyewe, hasa kuhusiana na siri iliyomfanya akapata sifa za Mungu. Hivyo basi leo, hebu tuzungumzie kuhusu Ayubu!
Katika Maisha ya Kila Siku ya Ayubu Tunaona Utimilifu, Unyofu, Kumcha Mungu, na Kujiepusha na Maovu Kwake
Kama tutazungumzia Ayubu, basi lazima tuanze na namna ambavyo alitathminiwa kwa mujibu wa matamshi kutoka kwa kinywa cha Mungu mwenyewe: "hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu."

Ijumaa, 26 Aprili 2019

"Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Sehemu ya Tatu"


Kuanzia mwanzo hadi leo, ni binadamu tu ambaye ameweza kuzungumza na Mungu. Yaani, miongoni mwa viumbe wote walio hai na viumbe wa Mungu, hakuna yeyote isipokuwa binadamu ameweza kuzungumza na Mungu. Binadamu anayo masikio yanayomwezesha kusikia, na macho yanayomwezesha kuona, anayo lugha na fikira zake binafsi, na pia anao uhuru wa kuamua chochote. Anamiliki kila kitu kinachohitajika kusikia Mungu akiongea, na kuelewa mapenzi ya Mungu, na kukubali agizo la Mungu, na hivyo basi Mungu anayaweka matamanio yake yote kwake binadamu, Akitaka kumfanya binadamu kuwa mwandani Wake ambaye anayo akili sawa na Yeye na ambaye anaweza kutembea na Yeye.

Alhamisi, 25 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II (Sehemu ya Pili)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Katika kipindi sawa na kile cha Ibrahimu, Mungu pia aliliangamiza jiji. Jiji hili liliitwa Sodoma. Bila shaka, watu wengi wanaijua hadithi ya Sodoma, lakini hakuna yeyote aliyejua fikira za Mungu zilikuwa usuli wa kuangamiza Kwake jiji hili.
Na hivyo leo, kupitia mazungumzo yake Mungu na Ibrahimu hapa chini, tutajifunza fikira Zake wakati huo, huku pia tukijifunza kuhusu tabia Yake. Kinachofuata, hebu tusome vifungu vya maandiko.
B. Mungu Lazima Aangamize Sodoma

Jumatano, 24 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II (Sehemu ya Kwanza)



Katika mkutano wetu wa mwisho tuliweza kuzungumzia mada muhimu sana. Je, mnakumbuka mada hiyo ilikuwa kuhusu nini? Hebu Niirudie. Mada ya ushirika wetu wa mwisho ilikuwa: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Je, mada hii ni muhimu kwenu? Ni sehemu gani katika mada hii ni muhimu kwenu? Kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, au Mungu Mwenyewe? Ni sehemu ipi inawavutia zaidi? Ni sehemu ipi mnayotaka kusikiliza kuhusu zaidi? Najua ni vigumu kwenu ninyi kulijibu swali hilo, kwa sababu tabia ya Mungu inaweza kuonekana katika kila kipengele cha kazi Yake, na tabia Yake inafichuliwa katika kazi Yake siku zote na pahali pote, na, kutokana na hayo, inawakilisha Mungu Mwenyewe; kwenye mpango wa usimamizi wa ujumla wa Mungu, kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe vyote hivi haviwezi kutenganishwa.