Jumapili, 30 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote II Sehemu ya Nne


Chakula na Kinywaji cha Kila Siku Ambavyo Mungu Anawatayarishia Wanadamu
Kuna chochote ambacho Mungu hufanya, bila kujali iwapo kitu hicho ni kikubwa au kidogo, kisicho na thamani au maana? Kila kitu Afanyacho kina thamani na maana. Tujadili hili kutoka kwa swali ambalo watu mara nyingi hulizungumzia. Watu wengi huuliza: Ni kipi kilitangulia, kuku au yai? (Kuku.) Je, utajibuje hili? Kuku alitangulia, hilo ni hakika! Kwa nini kuku alitangulia? Kwa nini yai halingetangulia? Je, kuku haanguliwi kutoka kwa yai? Mayai huangua kuku, kuku huatamiza mayai. Baada ya kuatamiza mayai kwa siku 21, kuku huangua. Kisha kuku huyo hutaga mayai, na kuku huanguliwa tena kutoka kwa mayai.

Jumamosi, 29 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote II Sehemu ya Tatu


Neno la Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote II Sehemu ya Tatu

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Tatu
Chakula na Kinywaji cha Kila Siku Ambavyo Mungu Anawatayarishia Wanadamu
Tulikuwa tumezungumza sasa hivi kuhusu sehemu ya mazingira ya jumla, yaani, hali zilizo muhimu kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu ambazo Mungu aliwatayarishia wanadamu tangu Alipoumba ulimwengu. Tumezungumza sasa hivi kuhusu vitu vitano, na vitu hivi vitano ndivyo mazingira ya jumla. Tunachoenda kuzungumzia baada ya hapo kinahusiana kwa karibu na kila maisha ya wanadamu katika mwili. Ni hali muhimu inayolingana zaidi na inayokubaliana zaidi na maisha ya mtu katika mwili. Kitu hiki ni chakula.

Ijumaa, 28 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote II Sehemu ya Pili


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Pili

Mazingira ya Kuishi ya Msingi Ambayo Mungu Anawaumbia Wanadamu
3. Sauti
Kitu cha tatu ni nini? Ni kitu ambacho mazingira ya kuishi ya kawaida ya wanadamu yanatakiwa kuwa nacho. Ni kitu ambacho Mungu alishughulikia alipoumba vitu vyote. Hiki ni kitu muhimu sana kwa Mungu na pia kwa kila mtu. Kama Mungu hakushughulikia suala hilo, ingekuwa kizuizi kikubwa kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu. Hiyo ni kusema kwamba ingekuwa na athari yenye maana sana kwa mwili na maisha ya mwanadamu, kiasi kwamba wanadamu hawangeweza kuendelea kuishi katika mazingira kama hayo.

Alhamisi, 27 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Kwanza


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Kwanza

Tuendelee na mada ya mawasiliano ya wakati uliopita. Je, mnaweza kukumbuka ni mada gani tuliwasiliana wakati uliopita? (Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Je, “Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote” ni mada mnayohisi ikiwa mbali sana nanyi? Je, una ufahamu wowote wa juujuu kuhusu jambo hilo? Mtu fulani anaweza kuniambia wazo kuu la mada hii tuliyowasiliana wakati uliopita? (Kupitia kwa uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ninaona kwamba Mungu hulea vitu vyote na hulea wanadamu. Katika siku zilizopita, kila mara nilifikiria kwamba Mungu anapompa mwanadamu, Anawapa tu watu Wake waliochaguliwa neno Lake, lakini kamwe sikuona, kupitia kwa sheria za vitu vyote, kwamba Mungu anawalea wanadamu.

Jumatano, 26 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Sehemu ya Nne Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu VyoteI



Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote(I)
Kusudi la mjadala wetu wa haya mambo ni nini? Je, ni ili kwamba watu waweze kutafiti kanuni zilizopo kwenye uumbaji wa Mungu wa ulimwengu? Je, ni ili kwamba watu wavutiwe na falaki na jiografia? (Hapana.) Sasa ni nini? Ni ili kwamba watu wataelewa matendo ya Mungu. Katika matendo ya Mungu, watu wanaweza kukubali na kuthibitisha kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Kama unaweza kuielewa hoja hii, basi utaweza kuthibitisha kweli nafasi ya moyoni mwako na utaweza kuthibitisha kwamba Mungu ni Mungu Mwenyewe wa kipekee, Muumbaji wa mbingu na nchi na vitu vyote.

Jumanne, 25 Juni 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu”



Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili, angalau, ni lazima liwe ukweli. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu. ...

Jumatatu, 24 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Sehemu ya Tatu Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu VyoteI


Kwa mara nyingine tena Nitatumia njia ya kusimulia hadithi, ambayo ninyi nyote mnaweza kusikiliza mkiwa kimya na kutafakari juu ya kile Ninachokizungumzia. Baada ya kumaliza kusimulia hadithi, nitawauliza maswali kuona mmeelewa kiasi gani. Wahusika wakuu katika hadithi ni mlima mkubwa, kijito kidogo, upepo mkali, na wimbi kubwa.

Hadithi ya 2. Mlima Mkubwa, Kijito Kidogo, Upepo Mkali, na Wimbi Kubwa
Kulikuwa na kijito kidogo kilichotiririka kwa kuzungukazunguka, hatimaye kikawasili chini ya mlima mkubwa.