Jumanne, 31 Desemba 2019

“Kutamani Sana” – Je, Ufalme wa Mbinguni uko Mbinguni au Ulimwenguni? | Swahili Christian Movie Clip 4/5


Watu wengi walio na imani kwa Bwana wanasadiki kwamba ufalme wa mbinguni uko mbinguni. Je, hivyo ndivyo ilivyo kwa kweli? Sala ya Bwana inasema: "Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe. Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni" (Mathayo 6:9-10). Kitabu cha Ufunuo kinasema, "Falme za dunia zimekuwa falme za Bwana wetu, na za Kristo wake" (Ufunuo 11:15). "Mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni, … maskani ya Mungu yako pamoja na wanadamu" (Ufunuo 21:2-3). Hivyo, ufalme wa mbinguni uko mbinguni au ulimwenguni?

Jumatatu, 30 Desemba 2019

Wimbo wa Kusifu na Kuabudu | “Matendo Ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu” | Kenyan gospel music


I

Mungu anatazama chini juu ya vitu vyote kutoka juu,
na Anatawala vitu vyote kutoka juu.
Wakati huo huo, Mungu ametuma wokovu Wake juu ya dunia.
Mungu anaangalia kutoka mahali Pake pa siri kila wakati,
kila hatua ya mwanadamu, kila kitu anachosema na kufanya.
Mungu anamjua mwanadamu kama kiganja cha mkono Wake.
Mahali pa siri ni makao ya Mungu, anga ndicho kitanda Mungu akilaliacho.
Nguvu ya Shetani haiwezi kumfikia Mungu,
kwani Yeye amejawa na utukufu, haki, na hukumu.

Jumapili, 29 Desemba 2019

Sura ya 22


Mwanadamu anaishi katikati ya mwanga, ilhali hana habari kuhusu thamani ya mwanga huo. Hana ufahamu kuhusu kiini cha mwanga huo, na chanzo cha mwanga huo, na, zaidi ya hayo, hajui mmiliki wake ni nani. Ninapotuza mwanga huo miongoni mwa binadamu, papo hapo Ninachunguza hali ilivyo miongoni mwa wanadamu: Kwa sababu ya mwanga huo, watu wote wanabadilika, na wanakua, na wametoka gizani. Ninaangalia kila pembe ya ulimwengu, na Ninaona kuwa milima yote imefunikwa na ukungu, kwamba maji yameganda kwa ajili ya baridi, na kwamba, kwa sababu ya kuja kwa mwanga, watu wanatazama Mashariki ili wapate kuona kitu kilicho na thamani zaidi—ilhali mwanadamu bado hana uwezo wa kutambua njia ya wazi kwenye ukungu huo. Kwa sababu dunia nzima imefunikwa kwa ukungu, Ninapotazama kutoka mawinguni, kuwepo Kwangu hakujawahi kutambuliwa na mwanadamu;

Jumamosi, 28 Desemba 2019

Kujua madhumuni na Umuhimu wa Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu

(1) Lengo na umuhimu wa kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake. Israeli ni mahali ambapo Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka katika mavumbi ya mahali hapo Yehova alimuumba mwanadamu; mahali hapa pakawa kituo cha kazi Yake duniani. Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa ukoo wa Adamu, walikuwa msingi wa kibinadamu wa kazi ya Yehova duniani.

Ijumaa, 27 Desemba 2019

Sura ya 21

Mwanadamu huanguka katikati ya mwanga Wangu, na anasimama imara kwa sababu ya wokovu Wangu. Niletapo wokovu ulimwenguni kote, mwanadamu hujaribu kutafuta njia za kuingia miongoni mwa mtiririko wa urejesho Wangu, ilhali kuna watu wengi ambao huoshwa wasijulikane waliko na gharika hili la urejesho; kuna watu wengi ambao wamezama na kumezwa na mafuriko haya ya maji; na kuna watu wengi pia ambao husimama imara huku kukiwa na mafuriko, ambao hawajawahi kupoteza hisia zao za mwelekeo, na ambao basi wamefuata mafuriko mpaka sasa. Ninaenda hatua kwa hatua na mwanadamu, lakini yeye hajawahi kunitambua; yeye anajua tu nguo Ninazovaa kwa nje, na hajui utajiri uliofichika ndani Mwangu. Ingawa Mimi humruzuku mwanadamu na kumpa kila siku, hana uwezo wa kukubali kwa kweli, hana uwezo wa kupokea utajiri wote niliompa. Hakuna jambo lolote kuhusu upotovu wa mwanadamu ambalo huniepuka;

Alhamisi, 26 Desemba 2019

Latest Swahili Gospel Song 2019 "Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa" (Lyrics)



I

Kwa kuwa Mungu alimuumba mwanadamu, Atamwongoza;
kwa kuwa Anamwokoa mwanadamu, Atamwokoa na kumpata kabisa;
kwa kuwa anamwongoza mwanadamu, Atamfikisha katika hatima sahihi.
Kwa kuwa Alimuumba mwanadamu na Anamsimamia,
ni lazima awajibikie matarajio na jalaa ya mwanadamu.
Ni hii ndiyo kazi inayofanywa na Muumba.
Ingawa kazi ya ushindi inafanikishwa ikiondoa matarajio ya jamii ya wanadamu,
mwishowe, mwanadamu bado ataletwa katika hatima sahihi ambayo Mungu amemwandalia.

Jumatano, 25 Desemba 2019

“Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni ni Yenye Hatari” – Umeme wa Mashariki Laitikisa Dunia ya Kidini | Swahili Gospel Film Clip 1/6


Umeme wa Mashariki—kuonekana na kazi ya Mungu katika siku za mwisho limetikisa makundi na madhehebu yote, na kila aina ya wanadamu wamefichuliwa. Kondoo wengi wazuri katika kanisa wangependelea kuteseka kukamatwa kusikodhibitiwa na kuteswa na Chama cha Kikomunisti cha China ili tu kutafuta na kuchunguza Umeme wa Mashariki. Watu wengine, hata hivyo, wanaamini maneno ya wachungaji na wazee wa  vna wanasisitiza kutochunguza Umeme wa Mashariki, huku wengine, licha ya kujua kikamilifu kwamba Umeme wa Mashariki linashuhudia ukweli, hawathubutu kutafuta wala kulichunguza kwa hofu ya kuteswa na Chama cha Kikomunisti cha China.