Jumapili, 30 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote II Sehemu ya Nne


Chakula na Kinywaji cha Kila Siku Ambavyo Mungu Anawatayarishia Wanadamu
Kuna chochote ambacho Mungu hufanya, bila kujali iwapo kitu hicho ni kikubwa au kidogo, kisicho na thamani au maana? Kila kitu Afanyacho kina thamani na maana. Tujadili hili kutoka kwa swali ambalo watu mara nyingi hulizungumzia. Watu wengi huuliza: Ni kipi kilitangulia, kuku au yai? (Kuku.) Je, utajibuje hili? Kuku alitangulia, hilo ni hakika! Kwa nini kuku alitangulia? Kwa nini yai halingetangulia? Je, kuku haanguliwi kutoka kwa yai? Mayai huangua kuku, kuku huatamiza mayai. Baada ya kuatamiza mayai kwa siku 21, kuku huangua. Kisha kuku huyo hutaga mayai, na kuku huanguliwa tena kutoka kwa mayai.

Jumamosi, 29 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote II Sehemu ya Tatu


Neno la Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote II Sehemu ya Tatu

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Tatu
Chakula na Kinywaji cha Kila Siku Ambavyo Mungu Anawatayarishia Wanadamu
Tulikuwa tumezungumza sasa hivi kuhusu sehemu ya mazingira ya jumla, yaani, hali zilizo muhimu kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu ambazo Mungu aliwatayarishia wanadamu tangu Alipoumba ulimwengu. Tumezungumza sasa hivi kuhusu vitu vitano, na vitu hivi vitano ndivyo mazingira ya jumla. Tunachoenda kuzungumzia baada ya hapo kinahusiana kwa karibu na kila maisha ya wanadamu katika mwili. Ni hali muhimu inayolingana zaidi na inayokubaliana zaidi na maisha ya mtu katika mwili. Kitu hiki ni chakula.

Ijumaa, 28 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote II Sehemu ya Pili


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Pili

Mazingira ya Kuishi ya Msingi Ambayo Mungu Anawaumbia Wanadamu
3. Sauti
Kitu cha tatu ni nini? Ni kitu ambacho mazingira ya kuishi ya kawaida ya wanadamu yanatakiwa kuwa nacho. Ni kitu ambacho Mungu alishughulikia alipoumba vitu vyote. Hiki ni kitu muhimu sana kwa Mungu na pia kwa kila mtu. Kama Mungu hakushughulikia suala hilo, ingekuwa kizuizi kikubwa kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu. Hiyo ni kusema kwamba ingekuwa na athari yenye maana sana kwa mwili na maisha ya mwanadamu, kiasi kwamba wanadamu hawangeweza kuendelea kuishi katika mazingira kama hayo.

Alhamisi, 27 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Kwanza


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Kwanza

Tuendelee na mada ya mawasiliano ya wakati uliopita. Je, mnaweza kukumbuka ni mada gani tuliwasiliana wakati uliopita? (Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Je, “Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote” ni mada mnayohisi ikiwa mbali sana nanyi? Je, una ufahamu wowote wa juujuu kuhusu jambo hilo? Mtu fulani anaweza kuniambia wazo kuu la mada hii tuliyowasiliana wakati uliopita? (Kupitia kwa uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ninaona kwamba Mungu hulea vitu vyote na hulea wanadamu. Katika siku zilizopita, kila mara nilifikiria kwamba Mungu anapompa mwanadamu, Anawapa tu watu Wake waliochaguliwa neno Lake, lakini kamwe sikuona, kupitia kwa sheria za vitu vyote, kwamba Mungu anawalea wanadamu.

Jumatano, 26 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Sehemu ya Nne Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu VyoteI



Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote(I)
Kusudi la mjadala wetu wa haya mambo ni nini? Je, ni ili kwamba watu waweze kutafiti kanuni zilizopo kwenye uumbaji wa Mungu wa ulimwengu? Je, ni ili kwamba watu wavutiwe na falaki na jiografia? (Hapana.) Sasa ni nini? Ni ili kwamba watu wataelewa matendo ya Mungu. Katika matendo ya Mungu, watu wanaweza kukubali na kuthibitisha kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Kama unaweza kuielewa hoja hii, basi utaweza kuthibitisha kweli nafasi ya moyoni mwako na utaweza kuthibitisha kwamba Mungu ni Mungu Mwenyewe wa kipekee, Muumbaji wa mbingu na nchi na vitu vyote.

Jumanne, 25 Juni 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu”



Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili, angalau, ni lazima liwe ukweli. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu. ...

Jumatatu, 24 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Sehemu ya Tatu Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu VyoteI


Kwa mara nyingine tena Nitatumia njia ya kusimulia hadithi, ambayo ninyi nyote mnaweza kusikiliza mkiwa kimya na kutafakari juu ya kile Ninachokizungumzia. Baada ya kumaliza kusimulia hadithi, nitawauliza maswali kuona mmeelewa kiasi gani. Wahusika wakuu katika hadithi ni mlima mkubwa, kijito kidogo, upepo mkali, na wimbi kubwa.

Hadithi ya 2. Mlima Mkubwa, Kijito Kidogo, Upepo Mkali, na Wimbi Kubwa
Kulikuwa na kijito kidogo kilichotiririka kwa kuzungukazunguka, hatimaye kikawasili chini ya mlima mkubwa.

Jumapili, 23 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Sehemu ya Pili Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu VyoteI


Leo Nitashiriki nawe mada mpya. Mada itakuwa ni nini? Kichwa cha mada kitakuwa "Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote." Je, hii siyo mada kubwa kidogo kuweza kuijadili? Je, inaonekana kama kitu ambacho kidogo hakiwezi kufikika? Mungu kuwa chanzo cha uhai kwa vitu vyote inaweza kuonekana ni mada ambayo watu wanahisi kutohusika nayo, lakini wote wanaomfuata Mungu wanapaswa kuielewa. Hii ni kwa sababu mada hii haihusiani kwa kuchanganulika na kila mtu anayemjua Mungu, kuweza kumridhisha na kumheshimu. Hivyo, mada hii inapaswa kuwasilishwa. Awali, pengine baadhi ya watu walikuwa na ufahamu wa msingi wa mada hii, au pengine baadhi ya watu waliifahamu.

Jumamosi, 22 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Sehemu ya Kwanza Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu


Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu

Mnapomaliza maombi yenu, je, mioyo yenu inahisi utulivu katika uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Ikiwa moyo wa mtu unaweza kutulizwa, ataweza kusikia na kuelewa neno la Mungu na ataweza kusikia na kuuelewa ukweli. Ikiwa moyo wako hauwezi kutulizwa, ikiwa moyo wako siku zote unayoyoma, au siku zote unafikiria juu ya mambo mengine, utaathiri kuja kwako pamoja kusikia neno la Mungu. Sasa, ni kitu gani cha msingi tunachokijadili wakati huu? Hebu sote turudi nyuma kidogo katika hoja kuu.

Ijumaa, 21 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu III Sehemu ya Nne


     Hebu turudi kuzungumza kuhusu mbinu ambazo Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu. Tumeongea karibuni kuhusu mbinu mbalimbali ambazo Mungu anafanya kazi kwa mwanadamu na ambazo kila mmoja wenu mnaweza kupitia nyinyi wenyewe, kwa hivyo sitatoa maelezo zaidi. Lakini katika mioyo yenu pengine mmechanganyikiwa kuhusu mbinu ambazo Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu, ama kwa kiwango cha chini zaidi ana upungufu wa maelezo. Ni ya manufaa kwenu kwa Mimi kuzungumzia hili tena? (Ndiyo.) Je, mnataka kumwelewa? (Ndiyo.) Pengine wengine wenu watauliza: "Mbona tuzungumze kuhusu Shetani tena? Punde tunapoongea kuhusu Shetani, tunakuwa na hasira, na tunaposikia jina lake tunahisi kutotulia kila mahali."

Alhamisi, 20 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Nne



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Nne

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Uzao: Awamu ya Tano 1. Mtu Hana Udhibiti wa Hatima ya Uzao Wake 2. Baada ya Kulea Kizazi Kijacho, Watu Hufaidi Ufahamu Mpya wa Hatima Yao 3. Kusadiki Katika Hatima si Kibadala cha Maarifa ya Ukuu wa Muumba 4. Wale tu Wanaonyenyekea Ukuu wa Muumba Ndio Wanaweza Kupata Uhuru wa Kweli

Video Husika: Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII” Sehemu ya Kwanza

Yaliyopendekezwa: APP ya Kanisa la Mwenyezi Mungu


Jumatano, 19 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu III Sehemu ya Tatu


      Najua kwamba sasa watu wengi wananitarajia kusema ni nini hasa utakatifu wa Mungu, lakini Ninapozungumza kuhusu utakatifu wa Mungu Nitaongea kwanza kuhusu matendo ambayo Mungu anafanya. Nyinyi nyote mnapaswa kusikiza kwa makini, kisha nitawauliza utakatifu wa Mungu ni nini hasa. Sitawaeleza moja kwa moja, lakini badala yake nitawaacha mjaribu kuutambua, kuwapa nafasi ya kuutambua. Mnafikiri nini kuhusu mbinu hii? (Ni nzuri.) Kwa hivyo sikizeni kwa makini.
Wakati wowote Shetani anampotosha mwanadamu ama anashughulika na madhara yasiyodhibitiwa, Mungu hasimami bila kazi, wala haweki kando ama kupuuza wale ambao amechagua.

Jumanne, 18 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu III Sehemu ya Pili


Neno la Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu III Sehemu ya Pili

Tumetoka tu kuongea kuhusu jinsi Shetani hutumia maarifa kumpotosha mwanadamu, basi kinachofuata wacha tushiriki kuhusu jinsi Shetani hutumia sayansi kumpotosha mwanadamu. Kwanza, Shetani hutumia jina la sayansi kuridhisha kutaka kujua kwa mwanadamu, kuridhisha hamu ya mwanadamu[a] kutafiti sayansi na kuchunguza siri. Pia, katika jina la sayansi, Shetani huridhisha haja ya mwili na mahitaji ya mwanadamu kuendelea kuinua ubora wao wa maisha. Shetani hivyo, katika jina hili, hutumia njia ya sayansi kumpotosha mwanadamu.

Jumatatu, 17 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu III Sehemu ya Kwanza


Neno la Mwenyezi Mungu|Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu III Sehemu ya Kwanza

Tulishiriki mada ipi wakati uliopita? (Utakatifu wa Mungu.) Na ni kipengele kipi cha Mungu Mwenyewe kinahusisha utakatifu wa Mungu? Je, kinahusisha kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo ni nini mada inayohusiana na kiini cha Mungu katika ushirika wetu? Je, ni utakatifu wa Mungu? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu: hiki ni kiini cha kipekee cha Mungu. Ni nini ilikuwa dhamira kuu tuliyoshiriki wakati uliopita? (Kutambua uovu wa Shetani.) Na ni yapi tuliyoyashiriki wakati uliopita kuhusu uovu wa Shetani? Mnaweza kukumbuka? (Jinsi Shetani anampotosha mwanadamu.

Jumapili, 16 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu II Sehemu ya Nne



  5. Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Mienendo ya Kijamii Kumpotosha Mwanadamu
Mienendo ya kijamii ilianza lini? Je, ni kitu kipya? (La.) Hivyo mtu anaweza kusema kwamba mienendo ya kijamii ilianza wakati Shetani alipoanza kuwapotosha watu? (Ndiyo.) Mienendo ya kijamii inajumuisha nini? (Mtindo wa mavazi na vipodozi.) Hiki ni kitu ambacho watu mara nyingi wanakutana nacho. Mtindo wa mavazi, mtindo wa kisasa na mienendo, hiki ni kipengele kidogo. Kuna kingine zaidi? Je, misemo maarufu ambayo watu wanapenda kusema inahesabika pia? Je, pia mitindo ya maisha ambayo watu wanataka inahesabika? Je, nyota wa muziki, watu mashuhuri, majarida, na riwaya ambazo watu hupenda zinahesabika? (Ndiyo.)

Jumamosi, 15 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Tano



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Tano

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
1. Muumba Pekee Ndiye Anayeshikilia Nguvu za Maisha na Kifo juu ya Binadamu
Maudhui ya video hii: Kifo: Awamu ya Sita 2. Yule Asiyejua Ukuu wa Muumba Atahangaika kwa Woga wa Kifo
3. Maisha ya Kuishi Ukitafuta Umaarufu na Utajiri Yatamwacha Mtu Akiwa na Hasara Akikabiliana na Kifo

Ijumaa, 14 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu (II) Sehemu ya Tatu

Kuhusu utakatifu wa Mungu, hata kama inaweza kuwa mada inayojulikana, katika majadiliano inaweza kuwa dhahania kiasi kwa watu wengine, na maudhui yake yanaweza kuwa ya kina sana. Hii ni kwa sababu zamani, watu hawakushughulika sana na kipengele cha utendaji wa mada hii. Lakini msijali, tutaishughulikia polepole na Nitawasaidia kuelewa maana ya utakatifu wa Mungu. Wacha tuseme hili kwanza: Iwapo unataka kujua mtu, angalia tu kile anachofanya na matokeo ya vitendo vyake, na utaweza kuona kiini cha mtu huyo—hebu tushiriki kuhusu utakatifu wa Mungu kutoka kwa mtazamo huu kwanza.

Alhamisi, 13 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu II Sehemu ya Pili

Kuhusu utakatifu wa kiini cha Mungu, wakati uliopita tulishiriki kidogo kuuhusu na huo ulikuwa msukumo wa maarifa ya watu ya utakatifu wa Mungu, lakini hautoshi. Hauwezi kutosha kusaidia watu kujua kikamilifu utakatifu wa Mungu, wala hautoshi kuwasaidia kuelewa kwamba utakatifu wa Mungu ni wa kipekee. Zaidi, hautoshi kuruhusu watu kuelewa kipengele cha maana ya ukweli ya utakatifu kwani imejumuishwa kabisa kwa Mungu. Kwa hivyo, ni muhimu kwamba tuendelee na ushirika wetu katika mada hii. Hapo nyuma ushirika wetu ulijadili mada tatu, kwa hivyo sasa tunapaswa kujadili mada ya nne, na tutaanza kusoma maandiko.

Jumatano, 12 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu II Sehemu ya Kwanza


Leo, kaka na dada, hebu tuimbe wimbo. Tafuta mmoja ambao mnapenda na ambao mmeimba mara nyingi kabla. (Tungependa kuimba wimbo wa neno la Mungu "Upendo Safi Bila dosari.")
1. "Upendo" unarejelea hisia ambayo ni safi na bila dosari, ambapo mnatumia mioyo yenu kupenda, kuhisi, na kuwa wa kufikiri. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi, na hakuna umbali. Katika upendo hakuna tuhuma, hakuna udanganyifu, na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna umbali na hakuna chochote kichafu. Iwapo una upendo, basi hautadanganya, kulalamika, kusaliti, kuasi, kushurutisha, au kutafuta kupata kitu au kupata kiasi fulani.

Jumanne, 11 Juni 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu “Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli”



Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu “Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli”


Mwenyezi Mungu anasema, “Baada ya kazi ya Yehova, Yesu Alipata mwili ili Afanye kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Kazi Yake haikutekelezwa kivyake, ila ilijengwa juu ya misingi ya kazi ya Yehova. Ilikuwa kazi ya enzi mpya baada ya Mungu kukamilisha Enzi ya Sheria. Vivyo hivyo, baada ya kazi ya Yesu kukamilika, Mungu bado Aliendeleza kazi Yake ya enzi iliyofuata, kwa sababu usimamizi wote wa Mungu huendelea mbele siku zote.

Jumatatu, 10 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu I Sehemu ya Tatu


Kwa sababu sasa tumemaliza kuzungumza kuhusu Shetani, hebu turudie kuzungumza kuhusu Mungu wetu. Wakati wa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita wa Mungu, matamshi machache sana ya moja kwa moja ya Mungu yamerekodiwa katika Biblia, na yale yaliyorekodiwa ni rahisi sana. Hivyo wacha tuanzie mwanzoni. Mungu alimuumba mwanadamu na tangu hapo kamwe Ameongoza maisha ya binadamu. Iwe kwa kuwapa wanadamu baraka, kuwapa sheria na amri Zake, ama kuweka masharti kanuni mbalimbali za maisha, mnajua lengo analonuia Mungu kwa kufanya mambo haya ni nini? Kwanza, mnaweza kusema kwa uhakika kwamba yote anayofanya Mungu ni kwa wema wa binadamu? (Ndiyo, tunaweza.) Mnaweza kufikiria kwamba sentensi hii kwa kulinganishwa ni pana na tupu, lakini kuzungumza hasa, kila kitu anachofanya Mungu ni cha kumwongoza na kumwelekeza mwanadamu kuishi maisha ya kawaida.

Jumapili, 9 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu I Sehemu ya Pili


Hebu sasa tuangalie maneno na maonyesho mengine ya Shetani yanayomruhusu mwanadamu kuona uso wake wenye sura mbaya. Hebu tuendelee kusoma baadhi ya maandiko.
Mazungumzo kati ya Shetani na Yehova Mungu
Ayubu 1:6-11 Sasa kulikuweko na siku ambapo wana wa Mungu walikuja kujidhihirisha mbele za Yehova, naye Shetani akaja pia kati yao. Naye Yehova akasema kwa Shetani, Ni wapi umetoka? Basi Shetani akamjibu Yehova, na kunena, Natoka katika kuenda hapa na pale duniani, na katika kutembea juu chini humo. Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu?

Jumamosi, 8 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu I Sehemu ya Kwanza


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu I Sehemu ya Kwanza

Tumekuwa na ushirika wa ziada wa mamlaka ya Mungu leo, na hatutazungumza kuhusu haki ya Mungu sasa hivi. Leo tutazungumza kuhusu mada nzima mpya—utakatifu wa Mungu. Utakatifu wa Mungu pia ni kipengele kingine cha kiini cha kipekee cha Mungu, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kushiriki mada hii hapa. Hiki kipengele cha kiini cha Mungu ambacho Nitashiriki, pamoja na vile vipengele viwili tulivyoshiriki mbeleni cha tabia ya haki ya Mungu na mamlaka ya Mungu—yote ni ya kipekee? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu pia ni wa kipekee, basi msingi wa upekee huu, mzizi wa upekee huu, ni maudhui ya ushirika wetu wa leo.

Ijumaa, 7 Juni 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III Sehemu ya Nane


    13. Bwana Yesu Ala Mkate na Kuonyesha Maandiko Baada ya Kufufuka Kwake
Luka 24:30-32 Na ikatimia, alipokuwa akikaa na wao ili wale, aliuchukua mkate, na kuubariki, na akaupasua, na kuwapa. Na macho yao yakafunguka, na wakamjua, na akatoweka wasimwone. Na wakaambiana, je, Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu sisi, wakati alipokuwa akituzungumzia njiani, na wakati alipotufungulia maandiko?
14. Wanafunzi Wampa Bwana Yesu Kipande cha Samaki wa Kuokwa Ale
Luka 24:36-43 Na wakati walipokuwa wakinena hayo, Yesu mwenyewe alisimama katikati yao, na akasema kwao, Amani iwe kwenu ninyi. Lakini walikuwa na woga na hofu sana, na wakafikiri kwamba walikuwa wameona roho.

Alhamisi, 6 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Saba



Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Saba

Mwenyezi Mungu anasema, “Kuonekana kwa Bwana Yesu kulifanikisha kujali Kwake kwingi kwa minajili ya wafuasi Wake katika ubinadamu na akakupokeza kwa mwili Wake wa kiroho, au unaweza kusema uungu Wake. Kuonekana Kwake kuliwaruhusu watu kuwa na hali nyingine waliyopitia na hisia walizopitia zinazohusu kujali na utunzaji wa Mungu huku kukithibitisha kwa uthabiti kwamba Mungu Ndiye anayefungua enzi, anayeiendeleza enzi, na Yeye ndiye anayetamatisha enzi.

Jumatano, 5 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Saba



Hakuna Anayeweza Kubadilisha Hoja Kwamba Mungu Anashikilia Ukuu juu ya Hatima ya Binadamu
Baada ya kusikiliza kila kitu Nilichomaliza kusema, je, fikira yenu ya hatima imebadilika? Mnaelewa vipi hoja ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu? Ili kuiweka kwa urahisi, katika mamlaka ya Mungu kila mtu anakubali waziwazi au kimyakimya ukuu Wake na mipangilio Yake, na haijalishi ni vipi ambavyo mtu anashughulika katika mkondo wa maisha yake, haijalishi ni njia ngapi mbovu ambazo mtu ametembelea, mwishowe atarudi tu kwenye mzingo wa hatima ambayo Muumba amempangia yeye. Hii ndiyo hali isiyoshindika ya mamlaka ya Muumba, namna ambavyo mamlaka Yake yanavyodhibiti na kutawala ulimwengu.

Jumanne, 4 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Sita


Kifo: Awamu ya Sita
4. Njoo Chini ya Utawala wa Muumba na Ukabiliane na Kifo kwa Utulivu
Wakati ule ambao mtu anazaliwa, nafsi ya mtu iliyo pweke inaanza kupitia maisha hapa duniani, inapitia mamlaka ya Muumba ambayo Muumba ameipangilia. Ni wazi kwamba, kwa mtu husika, ile nafsi, hii ni fursa nzuri kabisa ya kupata maarifa kuhusu ukuu wa Muumba, kujua mamlaka Yake na kuyapitia binafsi. Watu wanaishi maisha yao kulingana na sheria za hatima zilizowekwa wazi kwao na Muumba, na kwa mtu yeyote mwenye akili razini aliye na dhamiri, kuelewa ukuu wa Muumba na kutambua mamlaka yake kwenye mkondo wa miongo yao mbalimbali hapa nchini si jambo gumu kufanya.

Jumatatu, 3 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Tano



Kifo: Awamu ya Sita
Mwenyezi Mungu anasema, Baada ya mahangaiko mengi na masikitiko mengi, na kuvunjwa moyo kwingi, baada ya furaha nyingi na huzuni nyingi na baada ya misukosuko ya maisha, baada ya miaka mingi sana isiyosahaulika, baada ya kutazama misimu ikipita na kujirudia, mtu hupita kwenye kiungo muhimu sana cha maisha bila ya arifa, na kwa ghafla tu mtu anajipata kwenye miaka yake ya kufifia.

Jumapili, 2 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Nne



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Nne

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Mahitaji ya Mungu kwa Wanadamu 1. Utambulisho na Hadhi ya Mungu Mwenyewe 2. Mielekeo Mbalimbali ya Wanadamu kwa Mungu 3. Mwelekeo Ambao Mungu Anahitaji Mwanadamu Awe Nao Kwake
    Sikiliza zaidi: Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)” Sehemu ya Nne
Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?


Jumamosi, 1 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II) Sehemu ya Nne

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Uzao: Awamu ya Tano
Baada ya kuoa, mtu anaanza kulea kizazi kijacho. Mtu hana uwezo wa kujua atakuwa na watoto wangapi na watoto hawa watakuwa aina gani; hili pia linaamuliwa na hatima ya mtu, iliyoamuliwa kabla na Muumba. Hii ndiyo awamu ya tano ambayo lazima mtu apitie.
Kama mtu amezaliwa ili kutimiza jukumu la mtoto wa mwengine, basi mtu analea kizazi kijacho ili kutimiza jukumu la mzazi wa mwengine. Mabadiliko haya ya majukumu yanamfanya mtu kupitia awamu tofauti za maisha kutoka mitazamo tofauti.