Inaonyesha machapisho yaliopangwa kwa tarehe ya hoja Injili. Panga kwa uhusiano Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliopangwa kwa tarehe ya hoja Injili. Panga kwa uhusiano Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 28 Desemba 2019

Kujua madhumuni na Umuhimu wa Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu

(1) Lengo na umuhimu wa kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake. Israeli ni mahali ambapo Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka katika mavumbi ya mahali hapo Yehova alimuumba mwanadamu; mahali hapa pakawa kituo cha kazi Yake duniani. Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa ukoo wa Adamu, walikuwa msingi wa kibinadamu wa kazi ya Yehova duniani.

Jumanne, 24 Desemba 2019

Jua madhumuni ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu

Maneno Husika ya Mungu:

Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.

Jumanne, 17 Desemba 2019

“Kupita Katika Mtego” – Kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China Kinalitesa Kanisa la Mwenyezi Mungu | Filamu za Injili (Movie Clip 6/7)


“Kupita Katika Mtego” – Kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China Kinalitesa Kanisa la Mwenyezi Mungu | Filamu za Injili (Movie Clip 6/7)

Chama cha Kikomunisti cha China ni serikali ya kishetani ambayo huchukia ukweli na Mungu. Kinajua kwamba Mwenyezi Mungu peke Yake katika ulimwengu ndiye Anayeweza kuonyesha ukweli. Mwenyezi Mungu yuko katika mchakato wa kufanya kazi ya wokovu wa siku za mwisho. Neno la Mwenyezi Mungu likienezwa kati ya watu, wale wote wanaopenda ukweli watarejea kwa Mwenyezi Mungu.

Jumapili, 15 Desemba 2019

Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?

Kanisa la Mwenyezi Mungu

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Na itatimia katika siku za mwisho, kwamba mlima wa nyumba ya Yehova utawekwa imara juu ya milima, na utainuliwa juu zaidi ya vilima; na mataifa yote yatamiminika kwenda kwake. Na watu wengi wataenda na kusema, Njoo, na hebu twende juu ya mlima wa Yehova, kwa nyumba ya Mungu wa Yakobo; na atatufunza kuhusu njia zake, nasi tutatembea kwa njia zake: kwani sheria itatoka Zayuni, na neno la Mungu litatoka Yerusalemu. Naye atahukumu miongoni mwa mataifa, na atawakemea watu wengi: nao wata, nao watafua panga zao ili ziwe majembe, na mikuki yao ili iwe mundu: hakuna taifa litakaloinua upanga dhidi ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena. Enyi wa nyumba ya Yakobo, njooni, tutembee katika nuru ya Yehova” (Isaya 2:2-5).

Jumatano, 4 Desemba 2019

The Words the Holy Spirit Says to the Churches | "Sauti Nzuri Ajabu" | Filamu za Injili


The Words the Holy Spirit Says to the Churches | "Sauti Nzuri Ajabu" | Filamu za Injili

Dong Jingxin ni mhubiri katika kanisa la nyumba nchini Uchina. Amemsadiki Bwana kwa miaka thelathini, na anapenda ukweli, mara kwa mara yeye husoma maneno ya Bwana na yanamsisimua. Anajitumia kwa ajili ya Bwana kwa shauku kubwa. Kwa sababu ya kazi yake ya kuhubiri, alikamatwa na polisi wa serikali ya Kikomunisti ya Kichina na akafungwa gerezani ambako alivumilia ukatili na mateso. Maneno ya Bwana ndiyo yaliyomwongoza kwa kustahamili miaka saba ya maisha ya gerezani yasiyokuwa ya kibinadamu .

Alhamisi, 21 Novemba 2019

Swahili Christian Movie Based on True Story "Miaka 17? Hakika!" | The Power of Faith in God


"Kijana! Je, unajua kwamba Chama cha Kikomunisti ni kikana Mungu na kiko kinyume na imani katika Mungu? Katika China, kuna Mungu yupi kwako kuamini? Mungu huyu wako yuko wapi?" "Usifikiri kwamba kwa sababu wewe ni mdogo, tutakuwa wenye huruma kwako! Ukiendelea kumwamini Mungu, utaishia kufa!" Wakiwa na fimbo za umeme mikononi, polisi wa Kikomunisti wa China wanamvamia kijana huyu ambaye amejawa na mavilio ya damu.

Ijumaa, 1 Novemba 2019

Video za Kikristo | "Kaa Mbali na Shughuli Zangu" | Christ Is My Lord and My God


Li Qingxin ni mhubiri katika kanisa la nyumba nchini Uchina ambaye amekuwa mwaminifu kwa Bwana kwa miaka mingi. Siku zote kwa shauku kubwa anaifanya kazi ya Bwana ya kuieneza injili, akisubiri kwa uangalifu kuja kwa Bwana ili amlete hadi kwenye ufalme wa mbinguni. Katika miaka ya hivi majuzi, Li Qingxin amegundua kwamba vikundi na makanisa mbalimbali yamekuwa na ukiwa zaidi. Umeme wa Mashariki, hata hivyo, limekuwa la kusisimua zaidi, licha ya shutuma na mateso mengi yenye mhemko kutoka kwa serikali ya Kikomunisti ya Uchina na jamii ya dini. 

Jumanne, 22 Oktoba 2019

Kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho ni hukumu ya kiti cha enzi kikubwa, cheupe, kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo

Aya za Biblia za Kurejelea:
Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17).
Na nikaona kiti kikubwa cha enzi, cheupe, na yeye akiketiye, ambaye kutoka kwa uso wake nchi na mbingu zilitoroka; na hapakupatikana mahali pao. Na nikawaona waliokufa, wakubwa na wadogo, wakiwa wamesimama mbele ya Mungu; na vitabu vilifunguliwa: na kitabu kingine pia kikafunguliwa, ambacho ni kitabu cha uhai: na waliokufa walihukumiwa kwa mambo yale yaliyokuwa yameandikwa katika vitabu hivyo, kulingana na vitendo vyao. Nayo bahari ikawatoa waliofariki ambao walikuwa ndani yake; na kifo na kuzimu zikawatoa waliofariki ambao walikuwa ndani zao: na kila mtu alihukumiwa kulingana na vitendo vyake. Na kifo na kuzimu zikarushwa katika ziwa la moto. Hiki ndicho kifo cha pili. Na yeyote ambaye hakupatikana ameandikwa ndani ya kitabu cha uzima alirushwa katika ziwa la moto” (Ufunuo 20:11-15).
Maneno Husika ya Mungu:
“Hukumu” katika maneno yaliyonenwa awali—hukumu itaanza na nyumba ya Mungu—inarejelea hukumu ambayo Mungu anatoa leo kwa wale wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi katika siku za mwisho.

Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu


Tumesikia sauti ya Mungu na kurudi nyumbani Kwake.
Mikutanoni tunakula na kunywa maneno ya Mungu, tunahudhuria karamu.
Sisi tunaaga huzuni na vifungo vyetu, tunaishi maisha mapya.
Maneno ya Mungu yako nasi kila siku, tunastarehe ndani yake.
Tunapofungua mioyo yetu katika ushirika wa kweli, mioyo yetu inaangazwa sana.

Jumapili, 20 Oktoba 2019

“Sauti Nzuri Ajabu” – Hukumu ya Mungu ya Siku za Mwisho Ni Wokovu kwa Mwanadamu | Filamu za Injili (Movie Clip 5/5)

“Sauti Nzuri Ajabu” – Hukumu ya Mungu ya Siku za Mwisho Ni Wokovu kwa Mwanadamu | Filamu za Injili (Movie Clip 5/5)


Baadhi ya watu husoma maneno ya Mungu na kuona kwamba kunayo mambo makali ambayo ni hukumu ya wanadamu, na shutuma na laana. Wanafikiria kwamba kama Mungu huhukumu na kulaani watu, nao pia hawatashutumiwa na kuadhibiwa? Inawezaje kusemekana kwamba aina hii ya hukumu ni ya kutakasa na kuokoa wanadamu?

Jumanne, 15 Oktoba 2019

Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani” | Mtazamo Kimbele Uliorefushwa

Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani” | Mtazamo Kimbele Uliorefushwa


Wimbo wa kusisimua wa ufalme umevuma, ukitangazia ulimwengu wote kuwasili kwa Mungu kati ya mwanadamu! Ufalme wa Mungu umefika! Watu wote washangilia, vitu vyote vyafurahi! Kila kitu mbinguni kote kina furaha tele. Mandhari haya yanayopendeza mno ya shangwe ni yapi?

Alhamisi, 10 Oktoba 2019

14. Kujihusisha katika sherehe ya kidini ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:

Maisha ya kawaida ya kiroho hayakomi tukwa ombi, wimbo, maisha ya kanisa, kula na kunywa maneno ya Mungu, na matendo mengine kama haya, bali yana maana ya kuishi maisha ya kiroho yaliyo mapya na ya kusisimua. Siyo kuhusu mbinu, lakini matokeo. Watu wengi sana wanafikiri kwamba ili kuwa na maisha ya kawaida ya kiroho lazima mtu asali, aombe, ale na anywe maneno ya Mungu, au kujaribu kuelewa maneno ya Mungu. Bila kujali kama kuna matokeo yoyote, au kama kuna kuelewa kwa kweli, watu hawa hulenga tu kufanya mambo yasiyo ya dhati kwa nje, na hawalengi matokeo ni watu wanaoishi ndani ya mila za dini, na si watu wanaoishi ndani ya kanisa, na hata zaidi wao si watu wa ufalme. 

Jumatatu, 7 Oktoba 2019

1. Kuna tofauti ipi kati ya maneno yaliyoonyeshwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme?

V. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu ya Hukumu Katika Siku za Mwisho na Kazi Yake ya Ukombozi Katika Enzi ya Neema

1. Kuna tofauti ipi kati ya maneno yaliyoonyeshwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme?

Aya za Biblia za Kurejelea:
Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu” (Mathayo 4:17).
Na kwamba toba na msamaha wa dhambi vinapaswa kuhubiriwa katika jina lake miongoni mwa mataifa yote, kuanzia Yerusalemu” (Luka 24:47).
Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13).

Jumanne, 24 Septemba 2019

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi.

Jumamosi, 21 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Pili

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Ingawaje Hasira ya Mungu ni Fiche na Haijulikani kwa Binadamu, Haivumilii Kosa Lolote
Hasira ya Mungu Ni Usalama wa Nguvu Zote za Haki na Mambo Yote Mazuri
Mtu Hafai Kutegemea Uzoefu na Fikira Ili Kujua Tabia ya Haki ya Mungu
Ingawa Shetani Anaonekana Mwenye Utu, Haki na Maadili, Ni Mkatili na Mwovu katika Kiini Chake

Jumapili, 15 Septemba 2019

Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, Kikristo

Punde tu Shetani anaposhindwa, hivyo ni kusema, punde tu mwanadamu anaposhindwa kabisa, mwanadamu ataelewa kwamba kazi yake yote ni kwa ajili ya wokovu, na kuwa mbinu ya wokovu huu ni kurejesha kutoka kwa mikono ya Shetani. Miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi imegawanywa katika awamu tatu: Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Awamu hizi zote tatu za kazi ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, ambayo ni kusema, ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu ambaye ameharibiwa na Shetani kwa kiasi kikubwa. Wakati huo huo, hata hivyo, pia ni ili kwamba Mungu afanye vita na Shetani.

Alhamisi, 12 Septemba 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)” Sehemu ya Pili
Mwenyezi Mungu anasema, “Tofauti kubwa kabisa kati ya Mungu na wanadamu ni kwamba Mungu hutawala vitu vyote na hupeana vitu vyote. Mungu ni chanzo cha vitu vyote, na wanadamu hufurahia vitu vyote wakati Mungu anawapa. Hiyo ni kusema, mwanadamu hufurahia vitu vyote anapokubali maisha ambayo Mungu anatoa kwa vitu vyote. Wanadamu hufurahia matokeo ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ilhali Mungu ni Bwana. Kisha kutokana na mtazamo wa vitu vyote, ni nini tofauti kati ya Mungu na wanadamu? Mungu anaweza kuona vizuri mipangilio ya ukuaji wa vitu vyote, na kudhibiti na kutawala mipangilio ya ukuaji wa vitu vyote.

Jumatano, 11 Septemba 2019

Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Pili)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, Kazi-ya-Mungu

Wakati kazi ya Mungu inafikia hatua fulani, na usimamizi Wake kufikia hatua fulani, wale wanaoutafuta moyo Wake wote huwa na uwezo wa kutimiza matakwa yake. Mungu humwekea mwanadamu matakwa kulingana na viwango Vyake mwenyewe, na kulingana na kile ambacho mwanadamu anaweza kufanikisha. Akiwa anazungumzia usimamizi Wake, Yeye humwonyesha njia mwanadamu , na kumpa mwanadamu namna ya kudumu. Usimamizi wa Mungu na vitendo vya mwanadamu vipo katika hatua sawia kikazi, na yote yanafanyika kwa wakati mmoja. Mazungumzo kuhusu usimamizi wa Mungu yanagusia mabadiliko katika tabia ya mwanadamu, na yanazungumzia kuhusu yale yafaayo kufanywa na mwanadamu, na mabadiliko katika tabia ya mwanadamu, hugusia kazi ya Mungu; hakuna wakati ambao haya mawili yanaweza kutenganishwa. Vitendo vya mwanadamu vinabadilika, hatua kwa hatua.

Jumapili, 8 Septemba 2019

Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Pili)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Kazi Yake katika mwili ni ya umuhimu mkubwa, ambao umezungumzwa kuhusiana na kazi, na Yule ambaye hatimaye anahitimisha kazi ni Mungu mwenye mwili, na sio Roho. Baadhi ya watu wanaamini kwamba Mungu wakati fulani anaweza kuja duniani na kumtokea mwanadamu, ambapo atawahukumu wanadamu wote, akimjaribu mmoja baada ya mwingine bila mtu yeyote kupitwa. Wale wanaofikiri kwa namna hii hawafahamu hatua hii ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu hamhukumu mwanadamu mmoja baada ya mwingine, na hamjaribu mwanadamu mmoja baada ya mwingine; kufanya hivyo sio kazi ya hukumu.

Alhamisi, 5 Septemba 2019

Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Kwanza)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Kazi ya Mungu,kumjua mungu

Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu.