Jumanne, 30 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III Sehemu ya Pili

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Tumezungumza tu kuhusu kazi yote ambayo Mungu amekamilisha, misururu ya mambo Aliyoyafanya kwa mara ya kwanza. Kila mojawapo ya mambo haya yanahusiana na mpango wa Mungu wa usimamizi na mapenzi ya Mungu. Yanahusiana pia na tabia binafsi ya Mungu na kiini Chake. Kama tunataka kuelewa bora zaidi kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho, hatuwezi kukoma katika Agano la Kale au katika Enzi ya Sheria, lakini tunahitaji kusonga mbele pamoja na hatua ambazo Mungu alichukua katika kazi Yake. Hivyo basi, Mungu alipotamatisha Enzi ya Sheria na kuanza Enzi ya Neema, hatua zetu binafsi zimefika katika Enzi ya Neema—enzi iliyojaa neema na ukombozi. Katika enzi hii, Mungu tena Alifanya kitu cha muhimu sana kwa mara ya kwanza.

Jumatatu, 29 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Kwanza)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Vikao hivi kadhaa vya ushirika vimekuwa na athari kubwa kwa kila mmoja wa watu. Kwa sasa, watu wanaweza hatimaye kuhisi uwepo wa kweli wa Mungu na kwamba Mungu kwa hakika yuko karibu sana na wao. Ingawa watu wamemwani Mungu kwa miaka mingi, hawajawahi kuelewa kwa kweli mawazo na fikira Zake kama wanavyozielewa sasa, wala hawajawahi kupata kwa kweli uzoefu wa matendo Yake halisi kama walio nao kwa sasa. Kama ni maarifa au matendo halisi, watu wengi wamejifunza kitu kipya na kutimiza ufahamu wa juu zaidi, na wametambua kosa lililopo katika ufuatiliaji wao wa kale, wametambua hali yao waliyopitia ya juujuu na kwamba mambo mengi sana hayaambatani na mapenzi ya Mungu, na wametambua kwamba kile ambacho binadamu amepungukiwa nacho zaidi ni maarifa ya tabia ya Mungu.

Jumapili, 28 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Sehemu ya Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Msiwe na Wasiwasi Wowote Kuhusu Majaribio ya Mungu
Baada ya kuupokea ushuhuda kutoka kwa Ayubu kufuatia mwisho wa majaribio yake, Mungu aliamua kwamba angepata kundi au zaidi ya kundi—la watu kama Ayubu, ilhali aliamua kutowahi tena kumruhusu Shetani kushambulia au kunyanyasa mtu yeyote mwingine kwa kutumia mbinu ambazo kwazo alimjaribu, kumshambulia na kumnyanyasa Ayubu, kwa kufanya mzaha na Mungu; Mungu hakumruhusu Shetani tena kufanya mambo kama hayo kwa binadamu ambaye ni mnyonge, mjinga, na asiyejua—ilikuwa tosha kwamba Shetani alikuwa amemjaribu Ayubu!

Jumamosi, 27 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II (Sehemu ya Tano)


Kuhusu Ayubu
Baada ya kusikia namna Ayubu alivyopitia majaribio, kunao uwezekano kwamba wengi wenu watataka kujua maelezo zaidi kuhusu Ayubu mwenyewe, hasa kuhusiana na siri iliyomfanya akapata sifa za Mungu. Hivyo basi leo, hebu tuzungumzie kuhusu Ayubu!
Katika Maisha ya Kila Siku ya Ayubu Tunaona Utimilifu, Unyofu, Kumcha Mungu, na Kujiepusha na Maovu Kwake
Kama tutazungumzia Ayubu, basi lazima tuanze na namna ambavyo alitathminiwa kwa mujibu wa matamshi kutoka kwa kinywa cha Mungu mwenyewe: "hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu."

Ijumaa, 26 Aprili 2019

"Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Sehemu ya Tatu"


Kuanzia mwanzo hadi leo, ni binadamu tu ambaye ameweza kuzungumza na Mungu. Yaani, miongoni mwa viumbe wote walio hai na viumbe wa Mungu, hakuna yeyote isipokuwa binadamu ameweza kuzungumza na Mungu. Binadamu anayo masikio yanayomwezesha kusikia, na macho yanayomwezesha kuona, anayo lugha na fikira zake binafsi, na pia anao uhuru wa kuamua chochote. Anamiliki kila kitu kinachohitajika kusikia Mungu akiongea, na kuelewa mapenzi ya Mungu, na kukubali agizo la Mungu, na hivyo basi Mungu anayaweka matamanio yake yote kwake binadamu, Akitaka kumfanya binadamu kuwa mwandani Wake ambaye anayo akili sawa na Yeye na ambaye anaweza kutembea na Yeye.

Alhamisi, 25 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II (Sehemu ya Pili)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Katika kipindi sawa na kile cha Ibrahimu, Mungu pia aliliangamiza jiji. Jiji hili liliitwa Sodoma. Bila shaka, watu wengi wanaijua hadithi ya Sodoma, lakini hakuna yeyote aliyejua fikira za Mungu zilikuwa usuli wa kuangamiza Kwake jiji hili.
Na hivyo leo, kupitia mazungumzo yake Mungu na Ibrahimu hapa chini, tutajifunza fikira Zake wakati huo, huku pia tukijifunza kuhusu tabia Yake. Kinachofuata, hebu tusome vifungu vya maandiko.
B. Mungu Lazima Aangamize Sodoma

Jumatano, 24 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II (Sehemu ya Kwanza)



Katika mkutano wetu wa mwisho tuliweza kuzungumzia mada muhimu sana. Je, mnakumbuka mada hiyo ilikuwa kuhusu nini? Hebu Niirudie. Mada ya ushirika wetu wa mwisho ilikuwa: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Je, mada hii ni muhimu kwenu? Ni sehemu gani katika mada hii ni muhimu kwenu? Kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, au Mungu Mwenyewe? Ni sehemu ipi inawavutia zaidi? Ni sehemu ipi mnayotaka kusikiliza kuhusu zaidi? Najua ni vigumu kwenu ninyi kulijibu swali hilo, kwa sababu tabia ya Mungu inaweza kuonekana katika kila kipengele cha kazi Yake, na tabia Yake inafichuliwa katika kazi Yake siku zote na pahali pote, na, kutokana na hayo, inawakilisha Mungu Mwenyewe; kwenye mpango wa usimamizi wa ujumla wa Mungu, kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe vyote hivi haviwezi kutenganishwa.

Jumanne, 23 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Uendelezo wa Sehemu ya Kwanza

Kazi ya Usimamizi wa Mungu na Wokovu wa Wanadamu Yaanza na Ibrahimu Kumtoa Isaka
Baada ya kumpa mtoto Ibrahimu, maneno ambayo Mungu alikuwa ametamka kwa Ibrahimu yakawa yametimizwa. Hii haimaanishi kwamba mpango wa Mungu ulifikia mwisho hapa; kinyume cha mambo ni kwamba, mpango wa ajabu wa Mungu wa usimamizi na wokovu wa wanadamu ndipo ulikuwa tu umeanza, na baraka Yake ya mwana kwa Ibrahimu ilikuwa tu ni utangulizi wa mpango wa usimamizi Wake kwa ujumla. Wakati huo, ni nani aliyejua kwamba vita vya Mungu na Shetani vilikuwa vimeanza kimya kimya wakati Ibrahimu alipomtoa Isaka?

Jumatatu, 22 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I Uendelezo wa Sehemu ya Nne



Mungu aliwaumba wanadamu; licha ya kama wamepotoka au kama wanamfuata Yeye, Mungu hushughulikia binadamu kama wapendwa Wake—au kama vile binadamu wangesema, watu walio wapenzi Wake sana—na wala si makaragosi Yake. Ingawaje Mungu anasema Yeye ndiye muumba na kwamba binadamu ni uumbaji Wake, hali ambayo inaweza kuonekana ni kana kwamba kuna tofauti kiasi katika mpangilio wa cheo, uhalisia ni kwamba kila kitu ambacho Mungu amefanya kwa mwanadamu kinazidi kabisa uhusiano wa asili hii. Mungu anampenda mwanadamu, anamtunza mwanadamu, na anaonyesha kwamba anamjali mwanadamu, pamoja na kumkimu mwanadamu bila kuacha na bila ya kusita.

Jumapili, 21 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I Sehemu ya Nne


3) Mungu Atumia Upinde wa Mvua Kama Ishara ya Agano Lake na mwanadamu.
Mwa 9:11-13 Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia. Naye Mungu akasema, Hii ni alama ya agano ambayo naifanya kati ya Mimi na ninyi na viumbe vyote vyenye uhai vilivyo nanyi, kwa vizazi vya kudumu: naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.

Jumamosi, 20 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I (Sehemu ya Tatu)


Kisha, tutazungumzia hadithi ya Nuhu na namna ambavyo inahusiana na mada ya kazi ya Mungu, tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe.
Mnaona Mungu akimfanya nini Nuhu kwenye sehemu hii ya maandiko? Pengine kila mmoja aliyeketi hapa anajua kitu kuhusu hayo baada ya kusoma maandiko: Mungu alimfanya Nuhu kujenga safina, kisha Mungu akatumia gharika kuangamiza ulimwengu.

Ijumaa, 19 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I (Sehemu ya Pili)

Ili kuelewa tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe lazima muanzie na jambo dogo sana. Jambo hilo dogo sana mnalopaswa kuanzia ni nini? Kwanza kabisa, Nimezikusanya baadhi ya sura kutoka kwenye Biblia. Taarifa iliyo hapa chini inayo mistari ya Biblia, ambayo yote inahusiana na mada ya tabia ya Mungu, kazi ya Mungu na Mungu Mwenyewe. Nilipata dondoo hizi mahususi kama nyenzo za marejeleo ili kuwasaidia kujua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Hapa Nitayashiriki nanyi ili muweze kuona ni aina gani ya tabia na kiini cha Mungu ambacho kimefichuliwa kupitia kwa kazi Yake ya kitambo lakini watu hawajui kukihusu.

Alhamisi, 18 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I (Sehemu ya Kwanza)


Leo tunawasiliana kuhusu mada muhimu. Hii ni mada ambayo imezungumziwa tangu kuanza kwa kazi ya Mungu mpaka sasa, na inayo umuhimu mkuu kwa kila mtu. Kwa maneno mengine, hili ni suala ambalo kila mmoja atakutana nalo kwenye mchakato wote wa kusadiki kwake katika Mungu na suala ambalo lazima lizungumziwe. Ni suala muhimu, lisiloepukika ambalo mwanadamu hawezi kujitenganisha nalo. Tukizungumzia umuhimu, ni nini kitu muhimu zaidi kwa kila muumini katika Mungu? Baadhi ya watu wanafikiri kwamba kitu muhimu zaidi ni kuyaelewa mapenzi ya Mungu; baadhi wanasadiki ni muhimu zaidi kula na kunywa maneno ya Mungu; baadhi wanahisi kitu muhimu zaidi ni kujijua wenyewe; wengine wanayo maoni kwamba kitu muhimu zaidi ni kujua namna ya kupata wokovu kupitia kwa Mungu, namna ya kumfuata Mungu, na namna ya kuyatimiza mapenzi ya Mungu.

Jumatano, 17 Aprili 2019

Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu

Kila mmoja anapaswa kuchunguza maisha yake upya ya kumwamini Mungu ili kuona iwapo, katika kumtafuta Mungu, ameelewa kwa dhati, amefahamukwa dhati, na kuja kumjua Mungu kwa dhati, iwapo anajua kweli ni mawazo gani Mungu Anayo kwa aina tofauti za binadamu, na iwapo kweli anaelewa kile ambacho Mungu Anafanya juu yake na jinsi Mungu Anaeleza kila tendo lake. Huyu Mungu, Ambaye yuko kando yako, Akiongoza mwelekeo wa kuendelea kwako, Akiamuru hatima yako, na kukupa mahitaji yako—ni kiasi gani ambacho, katika uchambuzi wako, unaelewa nani kiasi gani ambacho kweli unajua kumhusu Yeye? Je, unajua Anachofanyia kazi kwako kila siku? Je, unajua kanuni na makusudi Anayozingatia katika matendo Yake yote? Unajua jinsi Anavyokuongoza?

Jumanne, 16 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Kwanza



Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Kwanza

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Uzito wa Matokeo katika Mioyo ya Watu Imani za Watu Haziwezi Kubadilishwa na Ukweli Kunayo Maoni Mengi Yanayohusu Kiwango Ambacho Mungu Hutumia Kuasisi Matokeo ya Binadamu

Jumatatu, 15 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)” Sehemu ya Tano



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)” Sehemu ya Tano

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Shetani Hajawahi Kuthubutu Kukiuka Mamlaka ya Muumba, na Kwa Sababu Hiyo, Vitu Vyote Vinaishi kwa Mpangilio Mungu Pekee, Ambaye Anao Utambulisho wa Muumba, Anamiliki Mamlaka ya Kipekee Utambulisho wa Muumba ni wa Kipekee, na Hufai Kufuata lile Wazo la Imani ya Kuabudu Miungu Wengi

Jumapili, 14 Aprili 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza



Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza

Mwenyezi Mungu anasema, “Kuingia rahani hakumaanishi kwamba mambo yote yatakoma kusonga, ama kwamba mambo yote yatakoma kuendelea, wala hakumaanishi kwamba Mungu atakoma kufanya kazi ama mwanadamu atakoma kuishi. Ishara ya kuingia rahani ni kama hii: Shetani ameangamizwa; wale watu waovu wanaomuunga mkono Shetani kwa kufanya maovu wameadhibiwa na kuondolewa; nguvu zote za uhasama kwa Mungu zimekoma kuwepo.

Jumamosi, 13 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Moja”


Matamshi ya Mungu | “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Moja”

Mwenyezi Mungu anasema, “Je, nani kati ya wanadamu wote hatunzwi mbele ya macho ya Mwenyezi? Nani haishi maisha kati ya majaaliwa ya Mwenyezi? Kuzaliwa na kufa kwa nani kulitokana na kuchagua kwao? Je, mwanadamu anadhibiti hatima yake? Wanadamu wengi wanalilia kifo, lakini kiko mbali nao; watu wengi wanataka kuwa watu wenye nguvu maishani na wanahofia kifo, lakini bila kujua kwao, siku ya kufa kwao inasongea karibu, ikiwatumbukiza ndani ya dimbwi la kifo; watu wengi wanatazama angani na kutoa pumzi kwa undani; watu wengi wanalia sana, wakiomboleza; watu wengi wanaanguka kuwapo majaribu; na watu wengi wanakuwa wafungwa wa majaribu.”

Ijumaa, 12 Aprili 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote”



Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote”

Mwenyezi Mungu anasema, “Kwa kweli, Mungu ni Bwana wa mambo yote. Yeye ndiye Mungu wa viumbe vyote. Yeye si Mungu wa Waisraeli pekee, na Yeye si Mungu wa Wayahudi pekee; Yeye ni Mungu wa viumbe vyote. … Kazi Yake ya awali ilifanywa Yudea, ndani ya eneo la Israeli; katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi Hakufanya kazi yoyote ya uzinduzi wa enzi hata kidogo.

Alhamisi, 11 Aprili 2019

Wimbo wa Kuabudu | “Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu” | Kids Dance


Wimbo wa Kuabudu | “Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu” | Kids Dance
Safi na mwaminifu, kama mtoto bila hatia, mchangamfu na mwenye nguvu za ujana, wao ni kama malaika wanaokuja ulimwenguni. Bila udanganyifu, na mioyo iliyo wazi tu, wao ni waadilifu. Wanatoa mioyo yao kwa Mungu na kupata imani Yake. Wao ni watu waaminifu ambao Mungu anapenda. Kuacha maneno ya Mungu yatuongoze kila siku, tumebarikiwa na Roho Mtakatifu anatuongoza.

Jumatano, 10 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima



Matamshi ya Mungu | “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele”

Mwenyezi Mungu anasema, “Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia.

Jumanne, 9 Aprili 2019

Wimbo wa kuabudu | Mtazamo wa Mungu kwa Mwanadamu

Wimbo wa kuabudu | Mtazamo wa Mungu kwa Mwanadamu

I
Matendo maovu ya wanadamu yanapomchukiza Mungu,
Ataiteremsha hasira Yake juu yao,
ila wanapotubu kwa kweli mbele Yake.
Watu wanapoendelea kumpinga Mungu,
Ghadhabu Yake haitakoma, hata watakapoangamizwa.
Hii ni tabia ya Mungu.

Jumatatu, 8 Aprili 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” (Sehemu ya Kwanza)



Maneno ya Roho Mtakatifu | “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” (Sehemu ya Kwanza)
Mwenyezi Mungu anasema, "Katika kila aina ya kazi ya Mungu kuna maono yanayofahamika na mwanadamu; maono yanayofuatwa na matarajio mwafaka ya Mungu kwa mwanadamu. Bila haya maono kama msingi, mwanadamu hawezi kuwa na uwezo wa utendaji na pia hangeweza kumfuata Mungu bila kuyumbayumba. Ikiwa mwanadamu hamjui Mungu au hayaelewi mapenzi ya Mungu, basi yote ayafanyayo ni bure na yasiyoweza kukubalika na Mungu. Hata mwanadamu awe na vipawa vingi kiasi gani, bado hawezi kujitenga na kazi ya Mungu na uongozi wa Mungu.

Jumapili, 7 Aprili 2019

Wimbo wa kuabudu | Shetani Hawezi Kubadili Chochote Chini ya Mamlaka ya Mungu

Wimbo wa kuabudu Shetani Hawezi Kubadili Chochote Chini ya Mamlaka ya Mungu

I
Ni kwa miaka ngapi, maelfu ya miaka,
Shetani amekuwa akimpotosha mwanadamu, akifanya mabaya mengi sana.
Vizazi, kimoja baada ya kingine vimedanganywa naye.
Oh, ni uhalifu kiasi kipi, uhalifu wa kuogofya
ambao Shetani amefanya katika dunia hii yote.
Alimchangamsha mwanadamu kupigana na Mungu, akamnyanyasa, na kumdanganya mwanadamu,
akatafuta kuuharibu mpango wa usimamizi wa Mungu.

Jumamosi, 6 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Tatu



Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu anasema, “Wakati Mungu alipofanya kazi katika ubinadamu, mbinu, maneno, na ukweli Wake mwingi vyote vilionyeshwa kwa njia ya kibinadamu. Lakini wakati uo huo tabia ya Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, na mapenzi Yake vyote vilionyeshwa kwa watu kuweza kujua na kuvielewa. Kile walichojua na kuelewa kilikuwa hasa kiini Chake na Alicho nacho na kile Alicho, vyote ambavyo vinawakilisha utambulisho na hadhi ya asili ya Mungu Mwenyewe.

Ijumaa, 5 Aprili 2019

Wimbo wa kuabudu | 79. Kazi na Maonyesho Huamua Kiini Chake


Wimbo wa kuabudu | 79. Kazi na Maonyesho Huamua Kiini Chake

I


Kiini cha Kriso kinaamuliwa na kazi Yake na maonyesho.

Na moyo ulio wa kweli, Anatimiza kile ambacho ameaminiwa nacho,

Anamwabudu Mungu aliye mbinguni na anatafuta mapenzi ya Baba Yake.

Haya yote yanaamuliwa na kiini Chake, na hivyo pia ufunuo Wake wa asili.

Alhamisi, 4 Aprili 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII” Sehemu ya Pili
Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu ni Bwana wa kanuni zinazoudhibiti ulimwengu, Anadhibiti kanuni zinazoongoza kuishi kwa vitu vyote, na pia Anadhibiti ulimwengu na vitu vyote kiasi kwamba vinaweza kuishi pamoja; Anaifanya ili kwamba visikwishe au kutoweka ili kwamba binadamu aendelee kuishi, binadamu anaweza kuishi katika mazingira hayo kupitia uongozi wa Mungu. Kanuni hizi zinazoongoza vitu vyote zipo chini ya utawala wa Mungu, na binadamu hawawezi kuingilia na hawawezi kuzibadilisha; ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anajua kanuni hizi na ni Yeye pekee ndiye anazisimamia.”

Tazama zaidi: Maonyesho ya Mungu | "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu"




Jumatano, 3 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)” Sehemu ya Kwanza



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)” Sehemu ya Kwanza
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Kwenye Siku ya Kwanza, Mchana na Usiku wa Mwanadamu Vinazaliwa na Kujitokeza Waziwazi kwa Msaada wa Mamlaka ya Mungu Kwenye Siku ya Pili, Mamlaka ya Mungu Yalipangilia Maji, na Kufanya Mbingu, na Anga za Mbinu za Kimsingi Zaidi za Kuishi kwa Binadamu Kuonekana

Jumanne, 2 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 38

Matamshi ya Mwenyezi MunguSura ya 38

Si kwamba imani yako ni nzuri au safi, lakini badala yake, kazi Yangu ni ya ajabu! Kila kitu ni kwa sababu ya rehema Zangu! Hupaswi kuwa na tabia potovu ya ubinafsi au kiburi hata kidogo, vinginevyo kazi Yangu kwako haitaendelea. Lazima uelewe wazi kwamba iwapo watu wanaanguka au kusimama imara si kwa sababu yao, ni kwa sababu Yangu. Leo, kama huelewi vizuri hatua hii, hutaweza kuingia katika ufalme! 

Jumatatu, 1 Aprili 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku”



Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku”

Mwenyezi Mungu anasema, “Kuanzia leo, Mungu ataweza kuwafanya watu wasiokuwa na fikira za kidini kuwa watimilifu kwa njia rasmi, ambao wako tayari kuweka pembeni nafsi zao za kale, na ambao wanamtii tu Mungu, pamoja na kuwafanya kuwa watimilifu wale wanaotamani neno la Mungu. Watu hawa wanafaa kusimama na kumhudumia Mungu. Kwake Mungu kunayo na hekima nyingi na isiyoisha. Kazi yake ya kustaajabisha na matamshi yake yenye thamani ni vitu ambavyo vipo ili watu wengi zaidi kuweza kufurahia.