Alhamisi, 31 Oktoba 2019

Sura ya 5

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu
Wakati Roho Wangu anatoa sauti, Anaonyesha hali nzima ya tabia Yangu. Je, wewe unalifahamu hili? Kutolifahamu hili katika hatua hii itakuwa sawa na kunipinga moja kwa moja. Je umeona umuhimu ulioko humu? Je, unajua juhudi kiasi gani, kiasi gani cha nguvu, Ninatumia juu yako? 

Jumatano, 30 Oktoba 2019

Sura ya 4

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Watu Wangu wote wanaohudumu mbele Zangu wanapaswa kutafakari kuhusu siku zilizopita: Je, upendo wenu Kwangu ulikuwa umetiwa doa na uchafu? Je, uaminifu wenu Kwangu ulikuwa safi na wa moyo wako wote? Je, ufahamu wenu kunihusu ulikuwa wa kweli? Je, Nilikuwa na nafasi kiasi gani katika nyoyo zenu? Je, Nilikuwa Nimejaza nyoyo zenu zote? Je, maneno Yangu yalitimiza kiasi gani ndani yenu?

Jumanne, 29 Oktoba 2019

Gospel Music | "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu" | Musical Documentary (Swahili Subtitles)

Gospel Music | "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu" | Musical Documentary (Swahili Subtitles)


Kote katika ulimwengu mkubwa mno, sayari zote ya mbingu husogea kwa usahihi katika mizunguko yazo zenyewe. Chini ya mbingu, milima, mito, na maziwa vyote vina mipaka yavyo, na viumbe vyote huishi na kuzaana wakati wa misimu yote minne kulingana na sheria za maisha…. Hili lote limepangwa vizuri sana—je, kuna Mwenye Uwezo Mmoja anayepanga na kutawala yote haya?

Jumatatu, 28 Oktoba 2019

Swahili Christian Musical Drama "Hadithi ya Xiaozhen" | Mungu ni upendo


Xiaozhen alikuwa Mkristo mwenye moyo safi, ulio na huruma, ambaye kila wakati alikuwa akiwashughulikia wenzake kwa uaminifu. Hata hivyo, ilipokuwa ni kwa manufaa yao, marafiki wake wa awali waligeuka na kuwa maadui wake. Baada ya kuteseka kutokana na msiba huu, Xiaozhen alilazimika kuuacha moyo wake wa kweli na kanuni zake za awali. Alianza kuisaliti dhamiri yake mwenyewe iliyo nzuri na roho safi, na kugaagaa katika kinamasi cha ulimwengu mbaya. … Huku akianguka kutoka kwa rehema na kutembea katika njia ya upotovu, alikanyagwa na ulimwengu na kukung'utwa na makovu na vilio. Alikuwa amefika mwisho kabisa, na katika wakati wa kukata tamaa wakati alikuwa amepoteza matumaini yote, mwishowe mwito wa kuaminika wa Mwenyezi Mungu ukauamsha moyo na roho ya Xiaozhen …

Jumapili, 27 Oktoba 2019

Utofautishaji Kati ya Kazi ya Mungu na Ile ya Mwanadamu

1. Utofautishaji Kati ya Kazi ya Mungu na Ile ya Mwanadamu

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Mungu Mwenyewe inahusisha kazi ya wanadamu wote, na pia inawakilisha kazi ya enzi nzima. Hii ni kusema kwamba, kazi ya Mungu mwenyewe inawakilisha harakati na mwelekeo wa kazi yote ya Roho Mtakatifu, ilhali kazi ya mitume inafuata kazi ya Mungu na wala haiongozi enzi, na wala haiwakilishi mwelekeo wa kufanya kazi wa Roho Mtakatifu katika enzi nzima.

Jumamosi, 26 Oktoba 2019

Kwa Nini Mungu Hutajwa Majina, na Jina Moja Linaweza Kuwakilisha Uzima wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sura ya 2 Ukweli wa Majina ya Mungu

1. Kwa Nini Mungu Hutajwa Majina, na Jina Moja Linaweza Kuwakilisha Uzima wa Mungu?

Maneno Husika ya Mungu:
Je, Jina la Yesu “Mungu pamoja nasi,” linaweza kuwakilisha tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake? Je, linaweza kueleza Mungu kwa ukamilifu? Kama mwanadamu atasema ya kwamba Mungu Ataitwa tu Yesu, na hawezi kuwa na jina lingine kwa sababu Mungu hawezi kubadilisha tabia yake, basi maneno hayo ni kufuru! Je, unaamini kwamba jina la Yesu, Mungu pamoja nasi, linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu? 

Ijumaa, 25 Oktoba 2019

Wimbo Mpya wa Kusifu na Kuabudu 2019 | “Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu” | MV

Wimbo Mpya wa Kusifu na Kuabudu 2019 | “Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu” | MV


Mandhari iliyochorwa katika Biblia “Amri ya Mungu kwa Adamu”
ni ya kugusa na yenye kutia moyo.
Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu,
uhusiano kati ya hao wawili ni wa ndani sana tunaanza kuhisi mshangao.
Upendo wa Mungu unaofurika umepewa mwanadamu bure;
Mwanadamu, maasumu na safi, bila ya wajibu wa kumnyima uhuru,
huishi kwa furaha kamili machoni mwa Mungu.
Mungu humtunza mtu, na mtu huishi chini ya mabawa Yake.
Yote ambayo mtu hufanya, maneno yake yote na matendo,
yamefungwa pamoja na Mungu, hayawezi kujitenga.

Alhamisi, 24 Oktoba 2019

Wimbo wa Kanisa Niko Tayari Kutekeleza Wajibu Wangu kwa Uaminifu


Wimbo wa Kanisa 

Niko Tayari Kutekeleza Wajibu Wangu kwa Uaminifu


  • Mpendwa Mwenyezi Mungu, ni Wewe ndiye Unayenipenda,
    uliniinua kutoka kwa rundo la kinyesi hadi kwa mazoezi ya ufalme.
    Maneno Yako yamenitakasa,
    yakanifanya nianze kuishi maisha ya furaha.
    Moyoni mwangu nahisi, kwa kweli, ni upendo Wako mkuu.
    Aa … aa … aa … aa … Mpendwa Mwenyezi Mungu!
    Maneno Yako yote ni ukweli.
    Unastahili upendo wa binadamu.
    Ee Mungu! Ukipuuza uasi wangu wa zamani,
    Unanijali na kufanya kazi kuniokoa.
    Unaniongoza katika njia ya kweli,
    Ukitazama kila wakati katika upande wangu,
    natarajia tu nitakua na kuwa mtu mpya.
    Aa … aa … aa … aa … Mpendwa Mwenyezi Mungu!
    Nitafuatilia kukupenda Wewe, mwaminifu kwa wajibu ili kukufurahisha Wewe.

Jumatano, 23 Oktoba 2019

Wimbo wa Kanisa Wewe tu Unaweza Kuniokoa Mimi


Wimbo wa Kanisa 

Wewe tu Unaweza Kuniokoa Mimi

  • I
  • Mnyenyekevu na Uliyejificha,
  • Waambatana na watu katika matatizo yao,
  • Ukiwapa njia ya uzima wa milele.
  • Unawapenda binadamu kama mwili Wako mwenyewe.
  • Na Wastahili upendo wao.
  • Afadhali Uteseke Mwenyewe,
  • ili Umwezeshe mwanadamu apate faida.
  • Na Wanyesha uzima juu yao.

Jumanne, 22 Oktoba 2019

Kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho ni hukumu ya kiti cha enzi kikubwa, cheupe, kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo

Aya za Biblia za Kurejelea:
Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17).
Na nikaona kiti kikubwa cha enzi, cheupe, na yeye akiketiye, ambaye kutoka kwa uso wake nchi na mbingu zilitoroka; na hapakupatikana mahali pao. Na nikawaona waliokufa, wakubwa na wadogo, wakiwa wamesimama mbele ya Mungu; na vitabu vilifunguliwa: na kitabu kingine pia kikafunguliwa, ambacho ni kitabu cha uhai: na waliokufa walihukumiwa kwa mambo yale yaliyokuwa yameandikwa katika vitabu hivyo, kulingana na vitendo vyao. Nayo bahari ikawatoa waliofariki ambao walikuwa ndani yake; na kifo na kuzimu zikawatoa waliofariki ambao walikuwa ndani zao: na kila mtu alihukumiwa kulingana na vitendo vyake. Na kifo na kuzimu zikarushwa katika ziwa la moto. Hiki ndicho kifo cha pili. Na yeyote ambaye hakupatikana ameandikwa ndani ya kitabu cha uzima alirushwa katika ziwa la moto” (Ufunuo 20:11-15).
Maneno Husika ya Mungu:
“Hukumu” katika maneno yaliyonenwa awali—hukumu itaanza na nyumba ya Mungu—inarejelea hukumu ambayo Mungu anatoa leo kwa wale wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi katika siku za mwisho.

Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu


Tumesikia sauti ya Mungu na kurudi nyumbani Kwake.
Mikutanoni tunakula na kunywa maneno ya Mungu, tunahudhuria karamu.
Sisi tunaaga huzuni na vifungo vyetu, tunaishi maisha mapya.
Maneno ya Mungu yako nasi kila siku, tunastarehe ndani yake.
Tunapofungua mioyo yetu katika ushirika wa kweli, mioyo yetu inaangazwa sana.

Jumatatu, 21 Oktoba 2019

ungu aliwakomboa wanadamu katika Enzi ya Neema, hivyo kwa nini bado anahitaji kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho?

Aya za Biblia za Kurejelea:
Kwa hivyo mtakuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu” (Walawi 11:45).
“Utakatifu, bila huu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana” (Waebrania 12:14).
Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:47-48).
Maneno Husika ya Mungu:
Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani.

Jumapili, 20 Oktoba 2019

“Sauti Nzuri Ajabu” – Hukumu ya Mungu ya Siku za Mwisho Ni Wokovu kwa Mwanadamu | Filamu za Injili (Movie Clip 5/5)

“Sauti Nzuri Ajabu” – Hukumu ya Mungu ya Siku za Mwisho Ni Wokovu kwa Mwanadamu | Filamu za Injili (Movie Clip 5/5)


Baadhi ya watu husoma maneno ya Mungu na kuona kwamba kunayo mambo makali ambayo ni hukumu ya wanadamu, na shutuma na laana. Wanafikiria kwamba kama Mungu huhukumu na kulaani watu, nao pia hawatashutumiwa na kuadhibiwa? Inawezaje kusemekana kwamba aina hii ya hukumu ni ya kutakasa na kuokoa wanadamu?

Jumamosi, 19 Oktoba 2019

Ni jinsi gani hatua tatu za kazi ya Mungu kwa pole pole huongeza uketo ili watu waokolewe na kukamilishwa?

4. Ni jinsi gani hatua tatu za kazi ya Mungu kwa pole pole huongeza uketo ili watu waokolewe na kukamilishwa?

Maneno Husika ya Mungu:
Usimamizi mzima wa Mungu umegawika katika hatua tatu, na katika kila hatua, mahitaji yanayofaa yanatakiwa kutoka kwa mwanadamu. Aidha, kadri enzi zinavyopita na kuendelea, mahitaji ya Mungu kwa wanadamu wote huwa ya juu hata zaidi. Kwa hiyo, hatua kwa hatua, kazi hii ya usimamizi wa Mungu hufikia kilele chake, hadi mwanadamu aamini ukweli wa “kuonekana kwa Neno katika mwili,”

Ijumaa, 18 Oktoba 2019

Best Swahili Christian Movie "Kubisha Hodi Mlangoni" | Je, Umesikia Sauti ya Mungu?

Best Swahili Christian Movie "Kubisha Hodi Mlangoni" | Je, Umesikia Sauti ya Mungu?


Miaka elfu mbili iliyopita, Bwana Yesu alitabiri, "Na usiku wa manane pakawa na kelele, Tazama, bwana harusi anakuja; tokeni nje mwende kumlaki" (Mathayo 25:6).“Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi” (Ufunuo 3:20).

Alhamisi, 17 Oktoba 2019

“Siri ya Utauwa: Mfuatano” – Bwana Yesu ni Mwana wa Mungu au Mungu Mwenyewe | Swahili Gospel Movie Clip 6/6

“Siri ya Utauwa: Mfuatano” – Bwana Yesu ni Mwana wa Mungu au Mungu Mwenyewe | Swahili Gospel Movie Clip 6/6


Imeandikwa waziwazi katika Biblia kwamba Bwana Yesu ni Kristo, kwamba Yeye ni Mwana wa Mungu. Lakini Umeme wa Mashariki unashuhudia kwamba Kristo aliyepata mwili ni dhihirisho la Mungu, kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe. Kwa hiyo Kristo aliyepata mwili ni Mwana wa Mungu?Au Yeye ni Mungu Mwenyewe? 

Jumatano, 16 Oktoba 2019

“Wimbo wa Ushindi” – Kwa nini Bwana Anarudi Kufanya Kazi ya Hukumu katika Siku za Mwisho | Swahili Gospel Movie Clip 5/7

“Wimbo wa Ushindi” – Kwa nini Bwana Anarudi Kufanya Kazi ya Hukumu katika Siku za Mwisho | Swahili Gospel Movie Clip 5/7


Watu wengi wanaamini kwamba tayari dhambi zetu zimesamehewa na kupata wokovu kwa sababu tulitangaza imani yetu kwa Bwana, basi kwa nini Bwana anakuja kutuchukua moja kwa moja hadi kwenye ufalme wa mbinguni? Kwa nini bado Anahitaji kuwahukumu na kuwatakasa? Je, hukumu ya Mungu kwa wanadamu katika siku za mwisho ni utakaso na wokovu, au ni shutuma na uharibifu wa wanadamu? Kipande hiki kitakufunulia siri hizo.

Jumanne, 15 Oktoba 2019

Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani” | Mtazamo Kimbele Uliorefushwa

Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani” | Mtazamo Kimbele Uliorefushwa


Wimbo wa kusisimua wa ufalme umevuma, ukitangazia ulimwengu wote kuwasili kwa Mungu kati ya mwanadamu! Ufalme wa Mungu umefika! Watu wote washangilia, vitu vyote vyafurahi! Kila kitu mbinguni kote kina furaha tele. Mandhari haya yanayopendeza mno ya shangwe ni yapi?

Jumatatu, 14 Oktoba 2019

Je, Utatu Mtakatifu Upo?

Baada ya ukweli wa Yesu aliyepata mwili kutokea, mwanadamu aliamini hili: Si Baba pekee aliye mbinguni, bali pia Mwana, na hata Roho Mtakatifu. Hii ndiyo dhana ya kawaida aliyonayo mwanadamu, kwamba kuna Mungu wa aina hii mbinguni: Utatu ambao ni Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, wote katika nafsi moja. 

Jumapili, 13 Oktoba 2019

Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Huenda ikawa safari yako ya imani katika Mungu imekuwa ndefu zaidi ya mwaka mmoja au miwili, na labda kwa maisha yako umestahimili ugumu mwingi miaka hii yote; au labda haujapitia ugumu na badala yake umepokea neema nyingi. 

Jumamosi, 12 Oktoba 2019

Dhambi Zitampeleka Mwanadamu Jahanamu

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Nimewapa maonyo mengi na kuwapa ukweli mwingi ili kuwashinda. Leo mnajihisi kustawishwa zaidi kuliko mlivyohisi hapo zamani, kuelewa kanuni nyingi za jinsi mtu anavyopaswa kuwa, na kumiliki kiasi kikubwa cha maarifa ya kawaida ambayo watu waaminifu wanapaswa kuwa nayo. 

Ijumaa, 11 Oktoba 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini”


Mwenyezi Mungu anasema, “Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako? Ni mara ngapi umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake? Lielewe neno la Mungu na uliweke katika vitendo. Kuwa mwenye maadili katika vitendo na matendo yako; huku si kutii sheria au kufanya hivyo shingo upande kwa ajili ya kujionyesha. Badala yake, huku ni kutenda ukweli na kuishi kulingana na neno la Mungu. Vitendo kama hivi pekee ndivyo humridhisha Mungu. Desturi yoyote inayompendeza Mungu si kanuni bali ni kutenda ukweli.”

Alhamisi, 10 Oktoba 2019

14. Kujihusisha katika sherehe ya kidini ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:

Maisha ya kawaida ya kiroho hayakomi tukwa ombi, wimbo, maisha ya kanisa, kula na kunywa maneno ya Mungu, na matendo mengine kama haya, bali yana maana ya kuishi maisha ya kiroho yaliyo mapya na ya kusisimua. Siyo kuhusu mbinu, lakini matokeo. Watu wengi sana wanafikiri kwamba ili kuwa na maisha ya kawaida ya kiroho lazima mtu asali, aombe, ale na anywe maneno ya Mungu, au kujaribu kuelewa maneno ya Mungu. Bila kujali kama kuna matokeo yoyote, au kama kuna kuelewa kwa kweli, watu hawa hulenga tu kufanya mambo yasiyo ya dhati kwa nje, na hawalengi matokeo ni watu wanaoishi ndani ya mila za dini, na si watu wanaoishi ndani ya kanisa, na hata zaidi wao si watu wa ufalme. 

Jumanne, 8 Oktoba 2019

2. Kuna tofauti ipi kati ya jinsi ambavyo Bwana Yesu alifanya kazi katika Enzi ya Neema na jinsi Mwenyezi Mungu anavyofanya katika Enzi ya Ufalme?

V. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu ya Hukumu Katika Siku za Mwisho na Kazi Yake ya Ukombozi Katika Enzi ya Neema

2. Kuna tofauti ipi kati ya jinsi ambavyo Bwana Yesu alifanya kazi katika Enzi ya Neema na jinsi Mwenyezi Mungu anavyofanya katika Enzi ya Ufalme?

Maneno Husika ya Mungu:
Wakati wa kupata mwili Kwake mara ya kwanza, ilikuwa muhimu kwa Mungu kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo kwa sababu kazi Yake ilikuwa ni kukomboa. Ili kulikomboa kabila lote la mwanadamu, Alipaswa kuwa mwenye upendo na mwenye kusamehe. Kazi Aliyoifanya kabla ya kusulubiwa ilikuwa kuponya watu na kufukuza mapepo, ambayo iliashiria wokovu Wake wa mwanadamu kutoka katika dhambi na uchafu. Kwa sababu ilikuwa ni Enzi ya Neema, ilikuwa muhimu Kwake kuponya wagonjwa, na kwa njia hiyo Alionyesha ishara na miujiza, mambo ambayo yalikuwa kiwakilishi cha neema katika hiyo enzi; kwani Enzi ya Neema ilikitwa katika kutolewa kwa neema, ikiashiriwa na amani, furaha, na baraka ya vitu, vyote vikiwa zawadi za imani ya watu kwa Yesu.

Jumatatu, 7 Oktoba 2019

3. Kuna tofauti ipi kati ya maisha ya kanisa katika Enzi ya neema na maisha ya kanisa katika Enzi ya Ufalme?

V. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu ya Hukumu Katika Siku za Mwisho na Kazi Yake ya Ukombozi Katika Enzi ya Neema

3. Kuna tofauti ipi kati ya maisha ya kanisa katika Enzi ya neema na maisha ya kanisa katika Enzi ya Ufalme?

Aya za Biblia za Kurejelea:
“Na wakati walipokuwa wakila, Yesu alichukua mkate, na akaubariki, na kuumega, na akawapa wanafunzi wake, na kusema, Chukueni, kuleni; huu ni mwili wangu. 

1. Kuna tofauti ipi kati ya maneno yaliyoonyeshwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme?

V. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu ya Hukumu Katika Siku za Mwisho na Kazi Yake ya Ukombozi Katika Enzi ya Neema

1. Kuna tofauti ipi kati ya maneno yaliyoonyeshwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme?

Aya za Biblia za Kurejelea:
Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu” (Mathayo 4:17).
Na kwamba toba na msamaha wa dhambi vinapaswa kuhubiriwa katika jina lake miongoni mwa mataifa yote, kuanzia Yerusalemu” (Luka 24:47).
Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13).

Jumapili, 6 Oktoba 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu I” Sehemu ya Pili


Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu (I)” Sehemu ya Pili
Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu anafanya kazi, Mungu anamtunza mtu, anamwangalia mtu, na Shetani anafuata hatua Yake yote. Yeyote anayefadhiliwa na Mungu, Shetani pia anatazama, akifuata nyuma. Iwapo Mungu anamtaka mtu huyu, Shetani atafanya kila kitu kwa uwezo wake kumzuia Mungu, akitumia mbinu mbalimbali mbovu kujaribu, kusumbua na kuharibu kazi anayofanya Mungu ili kufikia lengo lake lililofichwa. Lengo lake ni nini? Hataki Mungu awe na mtu yeyote; anataka wale wote ambao Mungu anataka, kuwamiliki, kuwatawala, kuwaelekeza ili wamwabudu, ili watende maovu pamoja naye. Je, hii siyo nia ya husuda ya Shetani?... Shetani yuko vitani na Mungu, akifuata nyuma Yake. Lengo lake ni kubomoa kazi yote ambayo Mungu anataka Kufanya, kuwamiliki na kudhibiti wale wote ambao Mungu anawataka, kuwafisha kabisa wale ambao Mungu anataka. Kama hawajafishwa, basi wanakuja kwa milki ya Shetani kutumiwa naye—hili ndilo lengo lake.”

Zaidi: Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu
Tazama Video: Wimbo wa Kuabudu | "Tabia ya Haki ya Mungu ni ya Pekee" | How to Know God

Jumamosi, 5 Oktoba 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Nne



Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Nne
Mwenyezi Mungu anasema, “Wakati Ayubu alipopitia majaribio yake kwa mara ya kwanza, alinyang’anywa mali yake yote na watoto wake wote, lakini hakujisujudia na kusema chochote ambacho kilikuwa dhambi dhidi ya Mungu kutokana na hayo. ... Kwenye jaribio la pili, Shetani aliunyosha mbele mkono wake ili kumdhuru Ayubu, na ingawaje Ayubu alipitia maumivu yaliyokuwa makubwa zaidi kuliko yale aliyokuwa amepitia awali, bado ushuhuda wake ulikuwa wa kutosha wa kuacha watu wakiwa wameshangazwa. Alitumia ujasiri wake, imani yake, na utiifu kwa Mungu, pamoja na kumcha Mungu kwake, kwa mara nyingine tena kumshinda Shetani, na mwenendo wake na ushuhuda wake viliweza kwa mara nyingine tena kuidhinishwa na kupata kibali cha Mungu.

Ijumaa, 4 Oktoba 2019

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kazi ya Mungu

Kila mtu anahisi kuwa usimamizi wa Mungu ni wa ajabu, kwa sababu watu wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu hauna uhusiano wowote na mwanadamu. Wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu ni kazi ya Mungu pekee, shughuli za Mungu, na hivyo wanadamu hawajali kuhusu usimamizi wa Mungu. Kwa njia hii, kuokolewa kwa wanadamu kumekuwa kusiko yakini na kusiko dhahiri, na kumebaki tu maneno matupu. Hata kama mwanadamu anamfuata Mungu ili aokolewe na aingie katika hatima inayopendeza, mwanadamu hajishughulishi na jinsi ambavyo Mungu Hutekeleza kazi Yake. Mwanadamu hashughulishwi na Anachokipanga Mungu na anachopaswa kufanya ili aokolewe.

Alhamisi, 3 Oktoba 2019

Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, Mapenzi ya Mungu

Kunayo siri kubwa moyoni mwako. Huifahamu kamwe kwa sababu umekuwa ukiishi katika ulimwengu usio na mwanga unaoangaza. Moyo wako na roho yako vimechukuliwa mateka na yule mwovu. Macho yako yamefunikwa na giza; huwezi kuliona jua angani, wala nyota ikimetameta wakati wa usiku. Masikio yako yamezibwa na maneno ya udanganyifu na husikii sauti ya Yehova ingurumayo kama radi, wala sauti ya maji yatiririkayo kutoka katika kiti cha enzi. Umepoteza kila kitu ambacho kilipaswa kuwa chako na kila kitu ambacho mwenye Uweza alikupa. Umeingia katika bahari ya uchungu isiyokuwa na mwisho, pasipo uwezo wa kukuokoa, hukuna matumaini ya kuishi, umeachwa ukipambana na kuzunguka zunguka tu.…

Jumatano, 2 Oktoba 2019

Maneno ya Mungu | Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, neno la Mungu,

Kulingana na vitendo na matendo katika maisha yenu, nyote mnahitaji kurasa za maneno ya kuwajaza na kuwajenga kila siku, kwani mko na upungufu mno, na ujuzi na maarifa yenu ya kupokea ni ya hali ya chini sana. Katika maisha yenu ya kila siku, mnaishi katika hali na mazingira yasiyo na ukweli ama fahamu nzuri. Hamna rasilimali ya uwepo na pia hamna msingi wa Kunijua au kujua ukweli. Imani yenu imejengwa tu juu ya ujasiri usio dhahiri au kwenye ibada za kidini na ujuzi kulingana na mafundisho ya kidini kabisa. Kila siku Ninatazama mienendo yenu na kuchunguza nia yenu na matunda yenu maovu.

Jumanne, 1 Oktoba 2019

Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, Kumjua Mungu,

Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani


Nyinyi nyote mna furaha kupokea tuzo mbele ya Mungu na kutambuliwa na Mungu. Haya ni matakwa ya kila mtu baada ya yeye kuanza kuwa na imani kwa Mungu, kwani mwanadamu kwa moyo wake wote hutafuta mambo yaliyo juu na hakuna aliye tayari kubaki nyuma ya wengine. Hii ndiyo njia ya mwanadamu. Kwa sababu hii, wengi kati yenu wanajaribu daima kupata neema ya Mungu mbinguni, lakini kwa kweli, uaminifu wenu na uwazi kwa Mungu ni wa kiasi kidogo sana ukilinganishwa na uaminifu na uwazi wenu kwenu wenyewe. Mbona Nasema hivi? Kwa sababu Sikiri uaminifu wenu kwa Mungu kabisa, na zaidi Nakana kuwepo kwa Mungu ndani ya mioyo yenu.