Kutatua Asili na Kutenda Ukweli
1. Uhusiano Kati ya Ubinadamu na Uwezo wa Kutenda Ukweli
Mwenyezi Mungu alisema, Watu husema kuwa kutenda ukweli ni vigumu kabisa. Basi mbona watu wengine wanaweza kutenda ukweli? Watu wengine husema ni kwa sababu kwa asili wanaipokea kazi ya Roho Mtakatifu ikifanya kazi juu yao, na pia kwa sababu ni wazuri kiasili. Hoja hii ina kiwango fulani cha mantiki. Watu wengine ni wazuri kiasili; wana uwezo wa kutenda ukweli. Ubinadamu wa watu wengine ni mnyonge, hivyo ni vigumu kwao kutenda ukweli; hii inamaanisha kuwa watakumbana na matatizo fulani. Je, mnaweza kusema kuwa yule ambaye hatendi ukweli amewahi kuutafuta ukweli? Hajautafuta kabisa! Fikira zake binafsi hutokea: “Njia hii ni nzuri, ni kwa faida yangu.” Mwishowe, bado anatenda kulingana na mawazo yake binafsi. Hatafuti ukweli kwa sababu kuna kitu kisicho sawa na moyo wake, moyo wake hauko sawa.