Jumanne, 31 Desemba 2019

“Kutamani Sana” – Je, Ufalme wa Mbinguni uko Mbinguni au Ulimwenguni? | Swahili Christian Movie Clip 4/5


Watu wengi walio na imani kwa Bwana wanasadiki kwamba ufalme wa mbinguni uko mbinguni. Je, hivyo ndivyo ilivyo kwa kweli? Sala ya Bwana inasema: "Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe. Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni" (Mathayo 6:9-10). Kitabu cha Ufunuo kinasema, "Falme za dunia zimekuwa falme za Bwana wetu, na za Kristo wake" (Ufunuo 11:15). "Mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni, … maskani ya Mungu yako pamoja na wanadamu" (Ufunuo 21:2-3). Hivyo, ufalme wa mbinguni uko mbinguni au ulimwenguni?

Jumatatu, 30 Desemba 2019

Wimbo wa Kusifu na Kuabudu | “Matendo Ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu” | Kenyan gospel music


I

Mungu anatazama chini juu ya vitu vyote kutoka juu,
na Anatawala vitu vyote kutoka juu.
Wakati huo huo, Mungu ametuma wokovu Wake juu ya dunia.
Mungu anaangalia kutoka mahali Pake pa siri kila wakati,
kila hatua ya mwanadamu, kila kitu anachosema na kufanya.
Mungu anamjua mwanadamu kama kiganja cha mkono Wake.
Mahali pa siri ni makao ya Mungu, anga ndicho kitanda Mungu akilaliacho.
Nguvu ya Shetani haiwezi kumfikia Mungu,
kwani Yeye amejawa na utukufu, haki, na hukumu.

Jumapili, 29 Desemba 2019

Sura ya 22


Mwanadamu anaishi katikati ya mwanga, ilhali hana habari kuhusu thamani ya mwanga huo. Hana ufahamu kuhusu kiini cha mwanga huo, na chanzo cha mwanga huo, na, zaidi ya hayo, hajui mmiliki wake ni nani. Ninapotuza mwanga huo miongoni mwa binadamu, papo hapo Ninachunguza hali ilivyo miongoni mwa wanadamu: Kwa sababu ya mwanga huo, watu wote wanabadilika, na wanakua, na wametoka gizani. Ninaangalia kila pembe ya ulimwengu, na Ninaona kuwa milima yote imefunikwa na ukungu, kwamba maji yameganda kwa ajili ya baridi, na kwamba, kwa sababu ya kuja kwa mwanga, watu wanatazama Mashariki ili wapate kuona kitu kilicho na thamani zaidi—ilhali mwanadamu bado hana uwezo wa kutambua njia ya wazi kwenye ukungu huo. Kwa sababu dunia nzima imefunikwa kwa ukungu, Ninapotazama kutoka mawinguni, kuwepo Kwangu hakujawahi kutambuliwa na mwanadamu;

Jumamosi, 28 Desemba 2019

Kujua madhumuni na Umuhimu wa Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu

(1) Lengo na umuhimu wa kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake. Israeli ni mahali ambapo Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka katika mavumbi ya mahali hapo Yehova alimuumba mwanadamu; mahali hapa pakawa kituo cha kazi Yake duniani. Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa ukoo wa Adamu, walikuwa msingi wa kibinadamu wa kazi ya Yehova duniani.

Ijumaa, 27 Desemba 2019

Sura ya 21

Mwanadamu huanguka katikati ya mwanga Wangu, na anasimama imara kwa sababu ya wokovu Wangu. Niletapo wokovu ulimwenguni kote, mwanadamu hujaribu kutafuta njia za kuingia miongoni mwa mtiririko wa urejesho Wangu, ilhali kuna watu wengi ambao huoshwa wasijulikane waliko na gharika hili la urejesho; kuna watu wengi ambao wamezama na kumezwa na mafuriko haya ya maji; na kuna watu wengi pia ambao husimama imara huku kukiwa na mafuriko, ambao hawajawahi kupoteza hisia zao za mwelekeo, na ambao basi wamefuata mafuriko mpaka sasa. Ninaenda hatua kwa hatua na mwanadamu, lakini yeye hajawahi kunitambua; yeye anajua tu nguo Ninazovaa kwa nje, na hajui utajiri uliofichika ndani Mwangu. Ingawa Mimi humruzuku mwanadamu na kumpa kila siku, hana uwezo wa kukubali kwa kweli, hana uwezo wa kupokea utajiri wote niliompa. Hakuna jambo lolote kuhusu upotovu wa mwanadamu ambalo huniepuka;

Alhamisi, 26 Desemba 2019

Latest Swahili Gospel Song 2019 "Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa" (Lyrics)



I

Kwa kuwa Mungu alimuumba mwanadamu, Atamwongoza;
kwa kuwa Anamwokoa mwanadamu, Atamwokoa na kumpata kabisa;
kwa kuwa anamwongoza mwanadamu, Atamfikisha katika hatima sahihi.
Kwa kuwa Alimuumba mwanadamu na Anamsimamia,
ni lazima awajibikie matarajio na jalaa ya mwanadamu.
Ni hii ndiyo kazi inayofanywa na Muumba.
Ingawa kazi ya ushindi inafanikishwa ikiondoa matarajio ya jamii ya wanadamu,
mwishowe, mwanadamu bado ataletwa katika hatima sahihi ambayo Mungu amemwandalia.

Jumatano, 25 Desemba 2019

“Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni ni Yenye Hatari” – Umeme wa Mashariki Laitikisa Dunia ya Kidini | Swahili Gospel Film Clip 1/6


Umeme wa Mashariki—kuonekana na kazi ya Mungu katika siku za mwisho limetikisa makundi na madhehebu yote, na kila aina ya wanadamu wamefichuliwa. Kondoo wengi wazuri katika kanisa wangependelea kuteseka kukamatwa kusikodhibitiwa na kuteswa na Chama cha Kikomunisti cha China ili tu kutafuta na kuchunguza Umeme wa Mashariki. Watu wengine, hata hivyo, wanaamini maneno ya wachungaji na wazee wa  vna wanasisitiza kutochunguza Umeme wa Mashariki, huku wengine, licha ya kujua kikamilifu kwamba Umeme wa Mashariki linashuhudia ukweli, hawathubutu kutafuta wala kulichunguza kwa hofu ya kuteswa na Chama cha Kikomunisti cha China.

Jumanne, 24 Desemba 2019

Jua madhumuni ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu

Maneno Husika ya Mungu:

Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.

Jumatatu, 23 Desemba 2019

Sura ya 20

Utajiri wa jumba Langu ni bila idadi na usioeleweka, lakini mwanadamu hajawahi kuja Kwangu kuufurahia. Hana uwezo wa kuufurahia mwenyewe, wala wa kujilinda mwenyewe kwa kutumia juhudi zake mwenyewe; badala yake, yeye daima huweka imani yake kwa wengine. Kati ya wale wote Ninaowatazamia, hakuna mtu aliyewahi kunitafuta kwa makusudi na moja kwa moja. Wao wote huja mbele Zangu kwa kushawishiwa na wengine, wakiwafuata watu wengi, na hawana nia ya kulipa gharama au kutumia muda kustawisha maisha yao. Kwa hivyo, miongoni mwa watu hakuna mtu aliyewahi kuishi katika hali halisi, na watu wote huishi maisha yasiyo na maana.

Jumapili, 22 Desemba 2019

“Kutoka kwa Kiti cha Enzi Hububujika Maji ya Uzima” – Mbona Kuna Ukiwa Ulioenea Pote katika Ulimwengu wa Dini? | Swahili Gospel Movie Clip 2/9


Dunia nzima ya dini kwa sasa inapitia njaa kubwa, hawapo tena pamoja na kazi ya Roho Mtakatifu au uwepo wa Bwana, wanafanya mambo maovu zaidi na zaidi na imani na huruma ya waumini inadhoofika na kuwa baridi. Aidha, maafa yanazidi kuwa mabaya zaidi na zaidi kote duniani, unabii kwamba Bwana angerudi katika siku za mwisho tayari umetimia. Hivyo, tunawezaje kutatua chanzo cha ukiwa wa makanisa kwa njia ambayo inawaruhusu wale ambao kweli wanaamini katika Mungu, ambao wanatamani kuonekana kwa Mungu kwa mara nyingine tena waje mbele za Mungu na kutembea kwenye njia ya wokovu? Hii video fupi itachunguza pamoja nawe jinsi ya kutatua tatizo hili la ukiwa wa makanisa.

Jumamosi, 21 Desemba 2019

Kwa nini husemwa kuwa kupata mwili kwili kwa Mungu hukamilish umuhimu wa kupata mwili?

Kanisa la Mwenyezi Mungu

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Kwa hiyo Kristo alitolewa mara moja kuzichukua dhambi za wengi; na kwa wale wamtazamiao ataonekana mara ya pili bila dhambi kwa wokovu” (Waebrania 9:28).

“Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu” (Yohana 1:1).

Maneno Husika ya Mungu:

Ijumaa, 20 Desemba 2019

Jinsi ya kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima?


Aya za Biblia za Kurejelea:

“Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu. Hivyo ndivyo alivyokuwa mwanzoni na Mungu” (Yohana 1:1-2).

“Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, aliyejawa neema na ukweli” (Yohana 1:14).

“Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu” (Yohana 14:6).

“Maneno ninayoongea kwenu ni roho, na ni uhai” (Yohana 6:63).

Alhamisi, 19 Desemba 2019

Sura ya 19


Ni wajibu wa mwanadamu kuchukua maneno Yangu kama msingi wa maisha yake. Mwanadamu lazima aanzishe fungu lake binafsi katika kila sehemu ya maneno Yangu; kutofanya hivyo kutakuwa kuuliza matata, kutafuta maangamizo yake mwenyewe. Binadamu haunijui, na kwa sababu ya hili, badala ya kuleta maisha yake Kwangu badala, anachofanya ni kujipanga tu mbele Yangu na takataka mikononi mwake, na hivyo kujaribu kuniridhisha. Lakini, mbali na kuridhishwa na mambo yalivyo, Naendelea kutoa matakwa kwa binadamu. Napenda michango ya mwanadamu, lakini Nachukia madai yake.

Jumatano, 18 Desemba 2019

Nitampenda Mungu Maisha Yangu Yote | "Mpendwa Wangu, Tafadhali Nisubiri" (Video Rasmi ya Muziki)


Juu ya miti, nikiukwea mwezi wa amani. Kama mpendwa wangu, wa haki na mzuri.
Ee mpendwa wangu, Uko wapi? Sasa mimi nina machozi. Je, Wanisikia nikilia?
Wewe Ndiwe hunipa upendo. Wewe Ndiwe Unayenitunza.
Wewe Ndiwe unayeniwaza daima, Wewe Ndiwe unayeyatunza maisha yangu.
Mwezi, nyuma ya upande wa pili wa anga. Usimfanye mpendwa wangu asubiri muda mrefu sana.
Tafadhali mwambie Yeye ninamkosa sana.
Usisahau kuubeba pamoja nawe upendo wangu, pamoja nawe upendo wangu.

Jumanne, 17 Desemba 2019

“Kupita Katika Mtego” – Kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China Kinalitesa Kanisa la Mwenyezi Mungu | Filamu za Injili (Movie Clip 6/7)


“Kupita Katika Mtego” – Kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China Kinalitesa Kanisa la Mwenyezi Mungu | Filamu za Injili (Movie Clip 6/7)

Chama cha Kikomunisti cha China ni serikali ya kishetani ambayo huchukia ukweli na Mungu. Kinajua kwamba Mwenyezi Mungu peke Yake katika ulimwengu ndiye Anayeweza kuonyesha ukweli. Mwenyezi Mungu yuko katika mchakato wa kufanya kazi ya wokovu wa siku za mwisho. Neno la Mwenyezi Mungu likienezwa kati ya watu, wale wote wanaopenda ukweli watarejea kwa Mwenyezi Mungu.

Jumatatu, 16 Desemba 2019

Sura ya 18

Katika mwako wa umeme, kila mnyama hufichuliwa katika hali yake halisi. Hivyo pia, kama wameangaziwa na mwanga Wangu, wanadamu wamepata tena utakatifu waliokuwa nao wakati mmoja. Oo, ya kwamba dunia potovu ya zamani mwishowe imeanguka na kutumbukia ndani ya maji ya taka na, kuzama chini ya maji, na kuyeyuka na kuwa tope! Ah, ya kwamba binadamu wote Niliouumba hatimaye umerudiwa na uhai tena katika mwanga, kupata msingi wa kuwepo, na kuacha kupambana katika tope! Ah, Mambo mengi ya uumbaji Ninayoyashikilia mikononi Mwangu! Wanawezaje, kukosa kufanywa upya, kupitia maneno Yangu?

Jumapili, 15 Desemba 2019

Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?

Kanisa la Mwenyezi Mungu

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Na itatimia katika siku za mwisho, kwamba mlima wa nyumba ya Yehova utawekwa imara juu ya milima, na utainuliwa juu zaidi ya vilima; na mataifa yote yatamiminika kwenda kwake. Na watu wengi wataenda na kusema, Njoo, na hebu twende juu ya mlima wa Yehova, kwa nyumba ya Mungu wa Yakobo; na atatufunza kuhusu njia zake, nasi tutatembea kwa njia zake: kwani sheria itatoka Zayuni, na neno la Mungu litatoka Yerusalemu. Naye atahukumu miongoni mwa mataifa, na atawakemea watu wengi: nao wata, nao watafua panga zao ili ziwe majembe, na mikuki yao ili iwe mundu: hakuna taifa litakaloinua upanga dhidi ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena. Enyi wa nyumba ya Yakobo, njooni, tutembee katika nuru ya Yehova” (Isaya 2:2-5).

Jumamosi, 14 Desemba 2019

Kwa nini ni kwa kupitia na kuitii kazi ya Mungu mwenye mwili pekee ndipo mtu anaweza kumjua Mungu?


Aya za Biblia za Kurejelea:

“Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, (nasi tukautazama utukufu wake, utukufu kama ule wa Mwana wa pekee aliyezaliwa na Baba,) aliyejawa neema na ukweli” (Yohana 1:14).

“Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu. Kama ninyi mngelinijua, pia mngelimjua Baba yangu: na kuanzia sasa mnamjua, na mmemwona” (Yohana 14:6-7).

Ijumaa, 13 Desemba 2019

Wimbo wa Maneno ya Mungu Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi

Kanisa la Mwenyezi Mungu

I
Mungu ana mpango wa usimamizi wa miaka 6,000,
uliyogawanywa katika hatua tatu,
kila moja inaitwa enzi.
Kwanza ni Enzi ya Sheria, kisha Enzi ya Neema,
na Enzi ya Ufalme ni awamu ya mwisho.
Ingawa kazi ya Mungu ni tofauti katika kila moja,
yote inalingana na kile ambacho binadamu wanahitaji,
ama hasa inalingana na ujanja ambao Shetani anatumia,
anapopigana na Yeye.

Alhamisi, 12 Desemba 2019

"Mazungumzo" – Kwa nini CCP Huwafuatia na Kuwakandamiza Wakristo Sana? | Swahili Christian Video Clip 1/6


Katiba ya China hutamka kwa dhahiri uhuru wa dini, lakini kisirisiri, serikali hutumia rasilimali nyingi mno za binadamu na za kifedha kwa kuikandamiza imani ya dini na kuwatesa Wakristo kikatili. Hata hawajaacha kununua vifaa vya hali ya juu zaidi kuwafuatia, kuwafuma, na kuwakamata Wakristo. Serikali ya China imewanyang'anya raia wake haki ya uhuru wa imani na imewanyima kwa utundu haki ya kuishi. Kwa hiyo kwa kweli ni nini sababu na lengo la CCP kufanya yote haya?

Sikiliza zaidi: 

Jumatano, 11 Desemba 2019

"Utamu katika Shida" – Mbinu ya Chama cha Kikomunisti cha China ya Kuwashurutisha Wakristo kwa Kutishia Familia Zao | Swahili Christian Testimony Video Clip 1/6


Ili kuwashurutisha Wakristo kulighilibu kanisa, wamsaliti Mungu na kuharibu nafasi zao za kuokolewa na Mungu, Chama cha Kikomunisti cha China kwa ufidhuli kinawatishia wanafamilia wa Wakristo na kutumia hisia za familia za Wakristo kuwashurutisha kumsaliti Mungu. Je, njama za Chama cha Kikomunisti cha China zinaweza kuendelea? Katika mapambano haya kati ya mema na mabaya, Wakristo watawezaje kumtegemea Mungu ili kushinda majaribu ya Shetani na kusimama imara na kuwa na ushuhuda kwa Mungu?

Jumanne, 10 Desemba 2019

Nikiongozwa na Maneno ya Mungu, Nilishinda Ukandamizaji wa Nguvu za Giza

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Na Wang Li, Mkoa wa Zhejiang

Nilimwamini Bwana Yesu pamoja na mama yangu tangu nilipokuwa msichana mdogo; katika siku zangu za kumfuata Bwana Yesu, mara nyingi niliguswa na upendo Wake. Nilihisi kwamba Alitupenda sana hata Akasulibiwa na kumwaga kila tone la damu Yake ili kutukomboa. Wakati huo, ndugu katika kanisa letu wote walikuwa wenye upendo na wenye kusaidiana, lakini kwa bahati mbaya imani yetu katika Bwana ilikutana na mateso na kukandamizwa mikononi mwa serikali ya CCP.

Jumatatu, 9 Desemba 2019

Sura ya 17

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sauti Yangu inatoka kama radi, ikitia nuru roboduara zote nne na dunia nzima, na katikati ya radi na umeme, binadamu wanaangushwa chini. Hakuna mwanadamu aliyewahi kusimama imara katikati ya radi na umeme: Wanadamu wengi wanaogopa sana kuja kwa mwangaza Wangu na hawajui cha kufanya. Wakati mwangaza hafifu unaanza kuonekana Mashariki, watu wengi, wakiongozwa na huu mng’ao dhaifu, wanaamshwa mara moja kutoka kwa njozi zao. Lakini, hakuna aliyewahi kutambua kwamba siku imewadia mwangaza Wangu unaposhuka duniani. 

Jumapili, 8 Desemba 2019

"Utamu katika Shida" – Kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China Kilibuni Tukio la 5/28 la Zhaoyuan? | Swahili Christian Testimony Video Clip 5/6


Baada ya kesi ya hadharani ya Tukio la Shandong Zhaoyuan, watu wenye utambuzi wote walitambua kuwa kesi hii ilibuniwa kabisa na Chama cha Kikomunisti cha China ili kulisingizia na kuliaibisha Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa makusudi. Ilikuwa kesi ya kuundwa na utumiaji vibaya wa haki. Sababu ya nia mbaya ya Chama cha Kikomunisti cha China kufanya hivi ni nini?

Sikiliza zaidi: Swahili Christian Movie | Nyendo za Mateso ya Kidini | "Kukaribia Hatari na Kurudi"

Jumamosi, 7 Desemba 2019

Sura ya 16

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kuna mengi ambayo Natamani kumwambia mwanadamu, mambo mengi sana ambayo lazima Nimwambie. Lakini uwezo wa mwanadamu wa kukubali una upungufu mwingi: Hana uwezo wa kuyaelewa kabisa maneno Yangu kulingana na kile Ninachokitoa, na anaelewa kipengele kimoja tu lakini haelewi vingine. Lakini Simwangamizi mwanadamu kwa ajili ya ukosefu wake wa nguvu, wala Siudhiki na udhaifu wake. Naifanya kazi Yangu tu, na kuongea jinsi ambavyo Nimefanya, hata kama mwanadamu haelewi matakwa Yangu; siku itakapokuja, watu watanijua ndani kabisa ya nyoyo zao, na watanikumbuka katika mawazo yao.

Ijumaa, 6 Desemba 2019

Swahili Gospel Full Movie "Fichua Siri Kuhusu Biblia" | Kufichua Hadithi ya Kweli ya Biblia


Feng Jiahui na wazazi wake waliamini katika Bwana tangu alipokuwa mdogo. Alipokuwa na umri wa miaka 18 aliingia katika shule ya seminari, na katika miaka yake ya 30 akawa mhubiri katika kanisa la nyumba huko Shanxi, Uchina. Kwa miaka mingi, Feng Jiahui alidumisha imani madhubuti ya kuwa Biblia ilitiwa msukumo na Mungu, na kwamba lazima tuamini katika Mungu kwa mujibu wa Biblia. Aliamini kuwa hakukuwa na maneno yaliyonenwa na Mungu nje ya Biblia, na kwamba kuondoka kutoka kwa Biblia kutakuwa uzushi.

Alhamisi, 5 Desemba 2019

Best Swahili Worship Song "Nitampenda Mungu Milele" | Kusogea Mbele na Upendo wa Mungu



Best Swahili Worship Song "Nitampenda Mungu Milele" | Kusogea Mbele na Upendo wa Mungu (Swahili Dubbed)
I
Ee Mungu! Maneno Yako yameniongoza kukurudia Wewe.
Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku.
Mara nyingi nilitoa machozi na kuhuzunika sana,
mara nyingi nimeanguka katika mtego wa Shetani.
Lakini hujaniacha kamwe.
Uliniongoza kupitia taabu nyingi, Ukanilinda katika hatari nyingi.
Sasa najua kuwa Umenipenda.

Jumatano, 4 Desemba 2019

The Words the Holy Spirit Says to the Churches | "Sauti Nzuri Ajabu" | Filamu za Injili


The Words the Holy Spirit Says to the Churches | "Sauti Nzuri Ajabu" | Filamu za Injili

Dong Jingxin ni mhubiri katika kanisa la nyumba nchini Uchina. Amemsadiki Bwana kwa miaka thelathini, na anapenda ukweli, mara kwa mara yeye husoma maneno ya Bwana na yanamsisimua. Anajitumia kwa ajili ya Bwana kwa shauku kubwa. Kwa sababu ya kazi yake ya kuhubiri, alikamatwa na polisi wa serikali ya Kikomunisti ya Kichina na akafungwa gerezani ambako alivumilia ukatili na mateso. Maneno ya Bwana ndiyo yaliyomwongoza kwa kustahamili miaka saba ya maisha ya gerezani yasiyokuwa ya kibinadamu .

Jumanne, 3 Desemba 2019

Sura ya 15

Mwanadamu ni kiumbe asiyejifahamu. Hata ingawa hawezi kujijua mwenyewe, yeye hata hivyo anajua kila mwanadamu mwingine kama kiganja cha mkono wake, kana kwamba watu wengine wote wamepitia ukaguzi wake na kupokea kibali chake kabla waseme au kufanya chochote, na hivyo ionekane kama yeye amewapima kikamilifu wengine wote mpaka katika hali yao ya kisaikolojia. Binadamu wote wako namna hii. Mwanadamu ameingia katika Enzi ya Ufalme leo hii, lakini asili yake bado haijabadilika.

Jumatatu, 2 Desemba 2019

Filamu za Kikristo "Chama Hakijamaliza Kuzungumza" | Concrete Proof of the CCP Persecuting Christians


Filamu za Kikristo "Chama Hakijamaliza Kuzungumza" | Concrete Proof of the CCP Persecuting Christians

Li Ming’ai ni Mkristo nchini China Bara. Yeye ni mwanamke mwadilifu ambaye anawaheshimu wakweze, humsaidia mumewe na kumuelimisha mtoto wake, na ana familia ya furaha na patanifu. Katika China, ambako ukanaji Mungu unatawala, hata hivyo, serikali ya Kikomunisti ya China daima huwakamata na kuwatesa ovyo ovyo watu wanaomwamini Mungu. Katika mwaka wa 2006, Li Ming'ai alikamatwa na kutozwa faini kwa sababu ya imani yake kwa Mungu. 

Jumapili, 1 Desemba 2019

Wimbo wa Maneno ya Mungu Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

I
Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia,
unaanza kutenda wajibu wako.
Katika mpango na utaratibu wa Mungu,
unachukua nafasi yako,
na unaanza safari ya maisha.
Vyovyote vilivyo msingi wako
ama safari iliyo mbele yako,
hakuna anayeweza kuepuka utaratibu
na mpango ambao Mbingu imeweka,
na hakuna aliye na amri juu ya hatima yake,
kwani ni Yule tu anayetawala juu ya vitu vyote
ndiye ana uwezo wa kazi kama hii.