Umeme wa Mashariki | Sababu ya Kweli ya Kazi Isiyofaa
Xinyi Mji wa Xi’an, Mkoa wa Shaanxi
Katika ziara zangu za karibuni kwa makanisa, mara nyingi niliwasikia viongozi na wafanyakazi wakisema kwamba watu wengine, baada ya kuhudhuria ushirika na mimi, waligeuka hasi, wanyonge na walikosa motisha ya kuendelea kutafuta. Wengine walisema ilikuwa vigumu sana kumwamini Mungu na walimwelewa Mungu visivyo. Wengine walisema kwamba hali zao zilikuwa nzuri kabla ya wao kukutana na mimi, lakini punde tu waliponiona, walihisi shinikizo kubwa mno na wasio na raha. ...Niliposikia haya yote, nilihuzunika, na nilihisi kukosewa vibaya—kila wakati nilipokuja kushiriki na wao ningeishi kwa baadhi ya siku, na, ili kutatua shida zao, nilipitia na kudondoa kama mifano vifungu vingi vya neno la Mungu, nikizungumza hadi nilipokauka mdomo, na wakati huo wote nikifikiri kwamba juhudi zangu zilikuwa zimetoa matokeo mazuri. Sikuwahi kufikiri kwamba mambo yangegeuka kuwa hivi. Mbona hili lilifanyika. Niliweka swali hili katika mawazo yangu nilipomwomba Mungu, “Ee Mungu, hakika mimi ni mwenye makosa kwa ajili ya yote ambayo yamefanyika, lakini sijui nilikosea wapi. Naomba mwongozo Wako, ili niweze kutambua zaidi makosa yangu. Niko tayari kusubiri kupokea nuru Yako.”